Wednesday, 9 December 2015

Re: [wanabidii] Kamati Za Bunge Nazo Zilishindwaje Kubaini Madudu Haya?

Hakuna mfugaji anayeonewa au atakayeonewa akifuga kisasa. Hachukiwi mfugaji hapa ila wazungu na wasomi wengine wanaojipendeleza kwao kutumia nafasi wapatazo na kulinda mahusiano na scholarship zao kuonyesha kuwa wafugaji wanaonewa. Mtazamo huu hausaidii maendeleo ya nchi. Hata mkoloni alipowaweka ndani ya wildlife conservation area hakutegemea kuwa watabadilika na kuanza kulima mazao, kujenga nyumba za kisasa za matofari na maghorofa humo. Sasa wanalima na majumba yamo. Tembea na safiri uone.

Ranch za mifugo kuwa sio solution. Kenya wameweka mpaka ranches za wildlife na wanachinja nyama ya wanyamapori-swala etc kutoka ranch zao na watu wanakula mpaka nyama ya mamba aliyefugwa pia.

Mbona nchi za ulaya na USA na hata nchi nyingine za Africa na jirani zetu wanaweza kufuga kisasa kwa mafanikio. Wapo wafugaji tata mfano Kenya waliwapa maeneo kuanzisha Group livestock Ranches. Lakini baadhi ya wafugaji wakayakodisha kwa wapanda maua na wauza maharage mabichi na mazao mengine ya mboga wanaosafirisha kupeleka UK-ulaya? Matatizo hayatakosa. Group ranches zikaishia kuwa mashamba na mifugo yao inakuja kuchungiwa Loliondo inajazana.

Ng'ombe mmoja (one livestock unit) in a semi-arid area anatakiwa kula square acre 5. Sasa matajiri wachache (say 20) kati ya kaya 2,000 wana ng'ombe elfu 10 kila moja, kondoi 400, mbuzi 2,000 kwa vile mbuzi wanauzwa sana. Mbuzi au kondoo 5 ni sawa na ng'ombe mmoja hivyo ana ng'ombe 10,480 anahitaji ekari 52,400. atazitoa wapi? Zidisha kwa idadi ya matajiri wote 20 uone ni ekari ngapi zitahitajika kama mmoja tu atahitaji hizi. Ndio maana wanawagawia wachungaji wanaolipwa inkind watembee nao mikoa mingine. Fika Terrat uone ukubwa wa Kata na vijiji. Fika vijiji vya Loliondo uone mfano wa degradation kutokana na mifugo. Sina haja ya kukulundikia picha hapa lakini haitowezekana tuendelee kufuga kizamani bila ya sisi wananchi kuuana.

Sasa hivi livelihood za wananchi wengi zimebadilika. Ukifika kwa wafugaji NCAA-wanalima; Loliondo wanalima kwa plau ya kukokotwa na ng'ombe na kwa trekta na vijiji pipo ndani ya wildlife conservation area. Vijiji vilivyozunguka Tarangire NP ni hivyo hata mito (terrat, Sirret) imekauka mifugo inapata tabu. Wazee wa mila nao wameshindwa kuzuia uharibifu wa vyanzo vya maji wamama wanatembea na punda mwendo mrefu kutafuta maji na tena machafu. Kama ni development hata ya kuchimba mabwawa na borehole-wafugaji wanauwezo wa pesa na wanaweza kuchangia mifugo wakachimba binafsi au ya jamii. Mtu kuchangia mbuzi 5 au wawili au ng'ombe mmoja. Pia miradi ya modren ranching wao wenyewe katika ushirika inawezekana. Mifano mizuri ipo-Botswana na baadhi wamepelekwa study tour lakini tukirudi kama kawa. Botwana wamewezaje na wanalisha nyama ile mbaya na wanategemea ng'ombe? Huwezi ukaingia hovyo ardhi ya mwenzako kuharibu na mifugo. Kama kiwanda cha nyama kinaanzishwa huko maeneo ya viwanda na bandari bagamoyo-modrrn ranching itapata soko sana na Sokoine University kupata maeneo ya field work na vijana wanaomaliza degree zao kupata ajira. Hii ya kuhamahama italeta vita kubwa sana. Mbona hatuoni Msukuma anayelima ardhi yake kupanda mpunga na Mfugaji Loliondo, NCAA, Simanjiro na Monduli anapolima mahindi na maharage-ngwara kulishia mazao yake mifugo au wakapigana kutokana na mifugo kula mashamba ya wengine. Ila wakifika Ruvu, Kilosa, Chalinze, Rufiji, Tunduru, Kilombero, Ngerengere hilo ni tatizo kubwa? Fika Irrigation system japanese financed ya Kisanga-Malolo na ya Ruvu Bagamoyo ukaone mifugo ilivyojaa na kuathiri uzalishaji halafu utetee migratory livestock keeping. Pita Morogoro uangalie milima inavyolimwa isivyo endelevu bila makinga maji na kuchoma misitu kupasua mawe, kujengwa majumba utetee kilimo kisicho endelevu cha kuhamahama na kuchoma moto. Lazima tufike mahala tubadilike.

Kama si wakoloni na serikali ya TZ kuanzisha protected forests na wildlife protected areas hii nchi ingekuwa jangwa kuliko Ethiopia na Somalia. Na sasa uchimbaji madini unaofanyika maeneo ya wafugaji na wakulima na kufanya degradation na pollution ya mito na maji yake isiposhughulikiwa taifa litakuwa na zombies wengi. Madini yanayoingia ndani ya maji na kuingia ziwa victoria na mito ya maji inayotegemewa na binadamu na mifugo italeta madhara kiafya kwani bio-accumulation ya madini ya madhara inafanyika katika maziwa ya mbuzi, ng'ombe, samaki, dagaa, nyama tulayo TZ.

Ranching ya mifugo TZ ilianza zamani na elimu kutolewa an zonal ranching units kuanzishwa ili kusaidia wafugaji. Hizo zimebaki kuuza mifugo ya kisasa kwa wenye uwezo lakini waliobaki hawataki kuiga for social cultural reasons tu. Ukiwa na wengi hata wawe wamekonda wewe kiutamaduni ndio unapata heshima ndio tajiri. Fuga wachache wawe bora na ranches zitalisha viwanda maziwa na nyama. Mbona Ulaya wanalisha dunia nzima nyama za makopo za misaada na wanalisha nchi yao na ardhi wao ni ndogo kulinganisha na ya TZ. Mbona Ranches za Serikali zinaweza mtu binafsi mwenye ardhi ya kimila yake pekee, ya ukoo ya kijiji kikubwa kama Terrat, Loiborsirret au Naitolia, Kitwai watashindwaje? Village Land Use Planning and Certification ndio itakuwa mwisho wa tatizo la uharibifu mazingira na mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanayozidi kukua.

Hakuna mfugaji anayechukiwa hapa ni mawazo ya maendeleo.
Mbona hata huko wanakopigana wafugaji na wakulima wameoana? Mkwere au Mnguu, Mkutu kaolewa na Ilparakuyo, unamkuta Msambaa, Mpare kaolewa na Mmasai na kavaa kama mwanamke wa Kimasai. Huko Morogoro rural wanadada wamewageuza wafugaji banki yao. Mfugaji amezaa kila kijiji huko ngerengere kutokana na wadada kuwafuata kujipatia kipato, maziwa na nyama. Pia nao wafugaji kutumia kuzaa kama mbinu ya kurasimisha makazi. Wakiambiwa wahame na mifugo wanaharimu vyanzo vya maji na mashamba pia wetlands za kipato kwa mazao wanasema- "sasa ikihama ile toto tatunza nani?"

Ukiwakuta wafugaji wahamaji na mifugo na wenyeji wa hapo wakwere, wakutu etc kilabuni wanakunywa pombe kwa pamoja na wameshikana mikono wanatembea kurudi home wanaanguka wote wawili huwezi kuamini kama yatatokea mapigano ya kugombea ardhi na kulishia mashamba. Maeneo mengine hawagombani hata mfano Gonja na wanakaa vitongoji vya wafugaji na kutembea pamoja kwenda na kurudi magulioni. Lakini land degradation ni issue ambayo sheria mfano Upareni inasimamia sana na adhabu yake ya kimila kali na husikii mapigano Upareni, Uchagani, Lushoto kama yanavyotokea mkoa wa Morogoro na mikoa mingine ambapo ni cultural ethnocentrism (uonevu ufanywao na wafugaji kudharau wengine). Mbona hawapigani na jirani zao(wachaga, wapare) lakini wafikapo mbali na hao jirani zao niliowataja huko mbali (Moro, Tunduru, Mbeya, Rufiji, Ruvu Bagamoyo, Kisarawe etc) bakora nyingi na uharibifu mahindi kuwa nyasi za mifugo? Tuyaangalie positively kisha tusaidie jamii zetu kuona nakutumia fursa zilizoto na sasa ni Kazi tu ya maendeleo!!

Issue kuu ni ufugaji na kilimo endelevu-sote tutaishi salama kwa pamoja na kuboresha kipato. Mfugaji tajiri wa wilaya ya Simanjiro, Monduli, Arusha ana mifugo na utajiri mwingi-magari ya utalii, landrover ya mama kuchotea maji hachotei na kubebesha punda, ana lodging na restaurant au hoteli, ana nyumba ya kisasa kabisa na wengine ni vijana waliosoma wana degree; ana machimbo Mererani au kijijini kwao wamegundua machimbo. Alichovaa mkononi si shaba bali bangili ya dhahamu, kiatu cha bei pia mgolole wake na material ya bei akitembea kukagua mifugo porini anakwenda kwa pikipiki na ana Nissan poa ya kutembelea. Dunia ya sasa sio ile ya zamani hivyo ranchin ya livestock itaturudisha kule kwa Nyerere masuala haya yalikoanzia na viwanda vinafufuliwa na kujengwa vya maziwa na nyama. Mabwawa ya samaki yarudishwe tena kuwa mradi kwa wakulima na kuelimisha watu kutokukomoana kwa kutia sumu kwenye bwawa la mwenzako kutokana na wivu au kuiba mifugo yake ya kisasa anapofanya zero grazing na kuwa na migombe na mbuzi wakubwa wa kisasa. Inawezekana.

Kama Kawa

--------------------------------------------
On Wed, 9/12/15, 'margeryalex' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Kamati Za Bunge Nazo Zilishindwaje Kubaini Madudu Haya?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, 9 December, 2015, 13:52

Hahahaaaaa kama ni ranch, Hugo ni
ndoto ya mchana kweupeee. Uzeni tu nchi, wajukuu
watairudisha hata kwa mawe.

AM
Send from Minolta PN 995.

'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Margeryalex;Nyama
inatakiwa kutoka katika mashamba (Ranch) ya mifugo kama
ilivyo kongwa.
Reuben




On Wednesday,
December 9, 2015 11:47 AM, 'margeryalex' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Tuseme ukweli
wapendwa, hawa wafugaji tunawaonea sana. Ndugu zangu wakiuza
mifugo yote na waanze ufugaji wa kisasa kuna mlala hoi
atakula nyama? Hiyo nyama itatoka wapi? Wakati wote wafugaji
wamebaki na ng'ombe 10 na wote wa  maziwa tu. Au
tutaanza kuingia hifadhi na kula nyama za Nyumbu na 
Nyati. Ukweli tunauficha, wakati kiongozi mmoja tu au
mwekezaji anahodhi ekari pori eka 10,000. Eneo lililobakia
tunawapa hifadhi za mbuga zetu wageni kwa mgongo wa
uwekezaji. Maelfu ya mbuga pori zimeuzwa kwa watu binafsi,
na wala hakuna kinachoendelezwa. Mapori yote yaliouzwa
kifisadi yamepewa hati miliki na mawaziri husika, na
yanalindwa na bunduki/mizinga usiku na mchana. Wafugaji
wazawa wana nyanyasika na kuuawa kwenye ardhi ya nchi yao
mama. Hili swala la kuuza mifugo ili kupisha mapori na
misitu, hifadhi zilizouzwa kifisadi kwa watu binafsi
mafisadi sio ufumbuzi. Ni kuenzi ufisadi na udhalilishaji
kwa wananchi wazawa. Suluhisho ni kurudisha mapori yaliouzwa
kwa maelfu ya ekari yote. Tanzania haina shida ya malisho
kwa mifugo yetu. Tatizo ni maelfu ya ekari za misitu kuuzwa
kifisadi kwa viongozi na wawekezaji uchwara. Unataka
wafugaji wahamie nchi gani? Mbinguni kama wanavyoahidi? Ina
maana wameshaamua kufa kuliko kunyanyasika kwa sera za
kibaguzi na kinyanyasaji.

AM.
Send from Minolta PN 995.

'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

>
>
>Mashaka ni gharama kubwa sana kutunga kamati ambazo
zinatumia mabilioni na mabadiliko hakuna wala ufanisi.
>
>Pia zile safari za study tours ambapo wakirudi hata
majimboni kwao hakuna tofauti. Wamefanya manunuzi na kuona
nchi za watu wakafurahia mataa.
>
>Hata wakirudi jimboni kwao kunaweza kuwa na chuo cha
kilimo lakini vijiji vyote kuzunguka chuo hakuna anayelima
sustainably na waka hawahoji. Kunaweza kuwa na shamba la
serikali la mifugo na wana mbegu za kuzalisha mifugo ya
kisasa ya kuishi mazingira yetu na wanayo ya mfano na majani
ya lishe na chakula cha lishe cha mifugo wanatengeneza.
Lakini wafugaji waliozunguka shamba hili wana mifugo mingi
ya kienyeji kuliko uwezo wa ardhi yao na wanavamia shamba la
serikali na kusababisha vurugu. Diwani, mbunge wapo na
watumishi ugani wa sekta za kilimo, mifugo wapo pia.
>
>Na hata mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme yanavamiwa na
kuwa degraded mpaka hata Nyumba ya Mungu na Mtera Dam. Hivi
tupoje sisi watanzania?!
>
>Tuache siasa tufanye kazi za ufanisi. Hebu ona photo
attached ya Mto ng'ombe Jangwani ukishuka kinondoni
Mkwajuni. Hizo nyumba zitajengwaje kwenye hizo wetlands kama
Ofisi ya Ardhi, Bwana Mazingira, DC, Maendeleo na Ustawi wa
Jamii na DMO wapo serious na kazi yao. Worse-NEMC haipo
plan. Wanajua ugonjwa wa matende na mabusha na dengue.
Lakini tunatazama hayo ya kujenga na kuishi hapo kuvamia
wetlands yanaendelea na umwagaji taka kujenga nyumba. Nani
haoni hayo? Wote tunaona na waliondolewa wamerudi tena.
>
>Tunataka kuwe na Fagia, Fagia vunja na bomoa kuanzia
Buguruni Mnyamani, Tabata, Ilala Mchikichini, Kigogo hadi
Jangwani Sunna na safisha hadi Salander bridge. Jenga nyumba
za juu za hoteli na madaraja ya kuingiza hela na weka nyumba
za boat za utalii na boat za mafunzo na mashindano watu
wapate ajira na hela ya wanaopenda starehe iingie kusaidia
maendeleo. Connect hizo hoteli za kitalii na utalii Mafia,
ZNZ, Saadan-Bagamoyo, Rufiji na Mikindani na Arusha.
Hamishia wakazi hao pimia viwanja, wajengee masoko, zahanati
na shule huko nj



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment