Wednesday, 9 December 2015

Re: [wanabidii] Kamati Za Bunge Nazo Zilishindwaje Kubaini Madudu Haya?

Margeryalex;
Nyama inatakiwa kutoka katika mashamba (Ranch) ya mifugo kama ilivyo kongwa.
Reuben




On Wednesday, December 9, 2015 11:47 AM, 'margeryalex' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Tuseme ukweli wapendwa, hawa wafugaji tunawaonea sana. Ndugu zangu wakiuza mifugo yote na waanze ufugaji wa kisasa kuna mlala hoi atakula nyama? Hiyo nyama itatoka wapi? Wakati wote wafugaji wamebaki na ng'ombe 10 na wote wa  maziwa tu. Au tutaanza kuingia hifadhi na kula nyama za Nyumbu na  Nyati. Ukweli tunauficha, wakati kiongozi mmoja tu au mwekezaji anahodhi ekari pori eka 10,000. Eneo lililobakia tunawapa hifadhi za mbuga zetu wageni kwa mgongo wa uwekezaji. Maelfu ya mbuga pori zimeuzwa kwa watu binafsi, na wala hakuna kinachoendelezwa. Mapori yote yaliouzwa kifisadi yamepewa hati miliki na mawaziri husika, na yanalindwa na bunduki/mizinga usiku na mchana. Wafugaji wazawa wana nyanyasika na kuuawa kwenye ardhi ya nchi yao mama. Hili swala la kuuza mifugo ili kupisha mapori na misitu, hifadhi zilizouzwa kifisadi kwa watu binafsi mafisadi sio ufumbuzi. Ni kuenzi ufisadi na udhalilishaji kwa wananchi wazawa. Suluhisho ni kurudisha mapori yaliouzwa kwa maelfu ya ekari yote. Tanzania haina shida ya malisho kwa mifugo yetu. Tatizo ni maelfu ya ekari za misitu kuuzwa kifisadi kwa viongozi na wawekezaji uchwara. Unataka wafugaji wahamie nchi gani? Mbinguni kama wanavyoahidi? Ina maana wameshaamua kufa kuliko kunyanyasika kwa sera za kibaguzi na kinyanyasaji.

AM.
Send from Minolta PN 995.

'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>
>
>Mashaka ni gharama kubwa sana kutunga kamati ambazo zinatumia mabilioni na mabadiliko hakuna wala ufanisi.
>
>Pia zile safari za study tours ambapo wakirudi hata majimboni kwao hakuna tofauti. Wamefanya manunuzi na kuona nchi za watu wakafurahia mataa.
>
>Hata wakirudi jimboni kwao kunaweza kuwa na chuo cha kilimo lakini vijiji vyote kuzunguka chuo hakuna anayelima sustainably na waka hawahoji. Kunaweza kuwa na shamba la serikali la mifugo na wana mbegu za kuzalisha mifugo ya kisasa ya kuishi mazingira yetu na wanayo ya mfano na majani ya lishe na chakula cha lishe cha mifugo wanatengeneza. Lakini wafugaji waliozunguka shamba hili wana mifugo mingi ya kienyeji kuliko uwezo wa ardhi yao na wanavamia shamba la serikali na kusababisha vurugu. Diwani, mbunge wapo na watumishi ugani wa sekta za kilimo, mifugo wapo pia.
>
>Na hata mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme yanavamiwa na kuwa degraded mpaka hata Nyumba ya Mungu na Mtera Dam. Hivi tupoje sisi watanzania?!
>
>Tuache siasa tufanye kazi za ufanisi. Hebu ona photo attached ya Mto ng'ombe Jangwani ukishuka kinondoni Mkwajuni. Hizo nyumba zitajengwaje kwenye hizo wetlands kama Ofisi ya Ardhi, Bwana Mazingira, DC, Maendeleo na Ustawi wa Jamii na DMO wapo serious na kazi yao. Worse-NEMC haipo plan. Wanajua ugonjwa wa matende na mabusha na dengue. Lakini tunatazama hayo ya kujenga na kuishi hapo kuvamia wetlands yanaendelea na umwagaji taka kujenga nyumba. Nani haoni hayo? Wote tunaona na waliondolewa wamerudi tena.
>
>Tunataka kuwe na Fagia, Fagia vunja na bomoa kuanzia Buguruni Mnyamani, Tabata, Ilala Mchikichini, Kigogo hadi Jangwani Sunna na safisha hadi Salander bridge. Jenga nyumba za juu za hoteli na madaraja ya kuingiza hela na weka nyumba za boat za utalii na boat za mafunzo na mashindano watu wapate ajira na hela ya wanaopenda starehe iingie kusaidia maendeleo. Connect hizo hoteli za kitalii na utalii Mafia, ZNZ, Saadan-Bagamoyo, Rufiji na Mikindani na Arusha. Hamishia wakazi hao pimia viwanja, wajengee masoko, zahanati na shule huko nje ya mji na hati miliki zao weka alama nyekundu-Haati haihamishiki na ukimkuta nayo mtu mwingine-weka ndani kwani wananchi wanauza maeneo yao hovyo na kuvamia ya watu wengine, wawekezaji na right of way za barabara. Lile suala la uhuru kuhamahama kwenda popote linaongeza uzembe, uvamizi ardhi, uuzaji ardhi hovyo na wanafamilia kuoneana. sasa iwe mwisho na ifanikishwe na donors kutusaidia kufanya upimaji ardhi na land use planning. Kila mmoja akae penye ardhi yake na aitimie sustainably. Hii itapunguza moaka uhamaji hamaji na malundo ya mifugo, uhamaji na ukataji misitu. kusiwe na leseni ya mbao au kukata magogo na kuuza kama mtu hana shamba la miti ya mbao. Mwisho wa leseni za magogo bila ya kuwa na shamba la miti!!
>
>Pamoja na kurahisisha manunuzi kwa wapita njia-ondoa wafanya biashara wote wakae panapohitajika. Ndani ya Kituo cha Mawasiliano kuna eneo la biashara-Hawakai wapo barabarani kwenye vumbi. Tususe kula vyakula vyao hapo penye vumbi. Lakini tunajazana tunakula na mainzi na mavumbi tunayaona sisi wanunuzi. Tugomee kula vyakula vilivyojaa mainzi, vinavyouzwa barabarani kwenye mavumbi, kula usiku kucha near mitaro yenye kinyesi na maji machafu yazalishayo mbu wa matende. Kununua maji ya visima ambavyo vimechoimwa maeneo ya vyoo vya shimo na barabarani kunakopita uchafu. Tunayafanya yenyewe.  Hapo Mawasiliano-Hao waliozuia soko kwa kununua hizo meza ili waziuze kwa bei ya juu wakamatwe hi hao hao maofisa wa serikali. Wanapopima viwanja Afisa Ardhi anachukua viwanja mwenyewe vingi na kuandika majina mbali mbali halafu kuviuza kwa mamilioni. Hili nalo tunalolisikia lichunguzwe. Ndivyo inavyotokea masokoni wafanya biashara kushindwa kukaa sokoni kutokana na hizo meza kuwa zimenunuliwa na washikaji wao wa maofisa wa soko wanazipangisha kwa bei ghali kwa siku. Manejiment ya Soko inakuwa haina maana kama umoja wa wafanyabiashara hapo sokoni nao unakuwa na uongozi wa rushwa tupu. Ndio maana unaona baadhi ya masoko yapo kama mabanda ya mbwa. Mabati yamechoka, mvua ikinyesha wananyeshewa wao na vyakula vyao, vitu vinaoza hakuna modern storage facilities including cold storage room.
>
>Yote inawezekana ila tumboni street tumeiweka mbele katika utendaji wetu. Government system ilikuwa better na ushirika kuliko sasa under PPP. Ila world Bank hawakujua tu akili zetu waafrika kuwa private sector hjuku nji wezi na vibaka kuliko public setor. Kwamba ubinafsi na udugu, tumboni na chupi street ni kansa ambazo ni challenges katika maendeleo yetu. Bado kuogopana kutokana na visasi ambavyo hufanya watendaji kuogopa kuchukua sheria zinazotakiwa. Watakufuata kwa utendaji wa kutumia sheria mpaka wakumalize. Hili nalo ni tatizo. Bwana Afya atamkamata huyo  lakini anakaa mtaa huo nyumba ya kupanga-anatishiwa nae. Viongozi na watumishi wa umma zamani wakikaa maeneo maalum tumetaka kujenga umoja lakini uswahili wetu ndio tatizo-Visasi hata kiongozi wa mtaa ambaye tu

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment