Ukweli ulionyooka majid. umekaribia japo hukutaja kuwa Sankara aliuawa na akina Kompaure na kwa kweli mpaka anaondolewa kwa nguvu ya umma mimi sikuwahi kumtambua kompaore na ni kwa sababu sikuwa mkuu wa nchi la sivyo asingekuja kwangu.
Huu ni ukweli mwingine wa mabadiliko aNAYOYAFANYA Mgufuli. Wengine wanafikiri atangaze tu. kwani sikutangaza watu wakapata ulaji! Kumbe mwenzetu licha ya kuwaonyesha kuwa hawakuwepo na mambo yalianza lakini hata kuandaa wizara kuanza kazi chini ya Makatibu wakuu na zikaenda kama anavyoelekeza ili 'kuwarahisishia' mawaziri kazi. Mtu hawezi kuja kusema 'sikujua'. lakini kuna hili kuwa wizara zinatarajia kupungua. Kuhakikisha kuwa hakuna idara inayoachwa katika mabadiliko hayo ya kupunguza wizara inatosha kuchelewesha uamuzi.
Bado una swala la nani. Bibi yangu aliwahi kuniambia wakati natafuta mchumba kuwa 'kuna tofauti kati ya Mwanamke na mke'. Huenda magufuli anatafuta kati ya 'wanawake' wengi nani 'wake'.
Alisema na wengiine walianza, aliposema wakati ule alipochukua form ya kuwania ndani ya chama. amekuwa akisema na sasa na walioona ugumu wa kazi ya mabadiliko anayofanya wameanza kusema-KUMUOMBEA. ambaye hajaanza aanze kumuombea.
Lazima anao maadui wengi.
1) Wapo waliotaka kuleta mabadiliko.
2) Wapo waliozoea kutolipa kodi.
3) Wapo waliozoea kuhujumu na kufisadi.
na makundi mengine mengi. Kumbuka alizoea kusema tumtangulize \Mungu.
TUMUOMBEE KWELI.
--------------------------------------------
On Mon, 11/30/15, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Inavyoonekana; Magufuli Ana Uwezo Wa Kumwona Bata Na Sungura Kwa Wakati Mmoja..!
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, Wanazuoni@yahoogroups.com
Date: Monday, November 30, 2015, 9:53 PM
Ndugu
zangu,Hii ni
dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo
wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye
kufanana. Hivyo, inahusu uwezo kuliona jambo hilo hilo
katika sura tofauti.
Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa
mtazamo tofauti.Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye
anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali
ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye
kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile
tulilokuwa na mazoea nalo.Captain Thomas Sankara, kiongozi mwanapinduzi
aliyeuawa wa Burkina Faso, katika wakati wake, alizungumzia
umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya
kale.Sankara aliacha hiba
njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani.
Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na
wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.Sankara alipata kukaririwa akisema:
"Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama
tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni,
basi, tunastahili ushindi.Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya
kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana
na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri
wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha
mustakabali. Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya
tuyafanyao leo. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao."
(Hayati, Kapteni Thomas Sankara)Yumkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni
Magufuli's paradigm shift'. Hali ya kuwa na
mabadiliko ya msingi. Kuna wanaoshangaa John Magufuli
kuchelewa kutangaza Baraza lake, yawezekana Magufuli
anaonyesha kwa mawaziri wake wajao, kuwa nchi inaweza kwenda
bila uwepo wa mawaziri miungu watu. Wakifanya mchezo
wanatimuliwa.Na hii ya
Magufuli paradigm shift inaweza kuibadili nchi kwa haraka,
maana kila mmoja atalazimika kubadilika.Maggid
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment