Sunday 12 October 2014

Re: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA

N vibaya kunyamazia kama ilivyo vibaya kutamka lakini Hilder uhuru wa kuabudu nao utaleta sokomoko. Bukoba mjini kuna shule fulani ambayo kila mtu aliyeitembelea ana wasiwasi kwa mafunzo yanayotolewa pale (Nshambya). Eneo limegeuzwa 'Jangwa' au Uarabuni kwa kufugia pale kondoo. Hiyo si kitu lakini aina ya mafunzo yakiwemo ya'viungo' kila anayeona haelewi. Watu wanaishia kunong'ona kuwa huensa maandalizi ya IS yanaendelea pale. Ndio uhuru wa kuabudu uliomaanisha katika jibu lako hapo chini?
--------------------------------------------
On Sun, 10/12/14, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, October 12, 2014, 12:27 PM

 Ubaguzi
wa dini haukuanza leo ni miaka mingi ila kwa sasa media ndio
ipo inauonyesha. Nikiwa umri mdogo nimeuona, kanisani
wakiingia wenzetu wasilamu na kufanya fujo; kujaribu kupokea
sakramenti na kupiga kelele yesu si Mungu. Ikafika siku za
sikukuu lazima kanisa liombe askari kwani walinzi wazee wa
kanisa hawakufaa kitu. Sanamu ya Bikira Maria ikiondolewa
pangoni na kukojolewa, kunyewa mavi, misalaba kuondolewa;
kanisa kuibiwa vikombe vyake na vitu vingine kwa sasa ni
kuajiri makampuni ya ulinzi. Bado tukitoka shule ya mzingi
ya mission kwenda ya serikali na nguo zetu ndefu na mwendo
wa kiumini tukitwa madukuo-kusukumwa kichwa, kupiga makwenzi
kichwani tukiitwa -makombo ya masista au Masea, wala nguruwe
na majina mengi. Ikifika siku-Maurid au kumepikwa ubwabwa
msikitini-about turn shuleni hapo ambapo ktk watoto 700 in
1960s (shule kubwa ya serikali zile za awali sana) wakristu
walikuwa 15 tu. Tuliipata. Lakini, ikifika miradi ya kulea
na kutunza wakoma, watoto yatima na wale wanaookotwa,
albino, miradi ya maji, vibarua, kukwea minazi kuangua nazi
kanisa halikubagua ajira au needy person wa kumtunza katika
vituo vyake budi awe mkristu. Shule zake ilipokea dini zote
sisi tukisali kila mwalimu akiingia darasani wao hukaa
chini. Wakigawa unga wa uji wa purenda wakati wa njaa au
nguo za mitumba kwa masikini-hugawa bila kigezo cha dini
mradi tu mtu anatambuliwa ni masikini katika eneo. Wakoma
walitunzwa na pia wazee baadae serikali kuja kuvichukua
vituo hivyo na vimeishia. Shule zinazopeta za kidini wote
wakihudhuria  isipokuwa ya masista au seminary ambapo budi
uwe mkristu. Kwa kifupi- huu ubaguzi wa sasa sio mpya ila
sasa unaongelewa kwa uwazi zaidi.
Bukoba au
Mkoa wa Kagera mtu hawezi kuamini kwamba yaliyotokea Uganda
wakati wa Kabaka Mutesa kuwachoma waitwao-'Mashahidi wa
Uganda' ndio yatakuwa yanaendelea sasa kwani huko dini
zote mbili ni strong sana na makardinari wakwanza wametoka
huko. Kinachotakiwa kwa sasa kila mtu awe na uhuru wake wa
kuabudu. Sali sana katika hekalu lako hata kama ikibidi
usali sana mpaka usijue kuwa nguo imekuvuka. Kuna uhuru wa
kuabudu-ugomvi wa nini mwenzako akisali wewe ukasirike? Kuna
siri gani hapo-anakuharibia nini mpaka uchukie? Mbona wewe
ukisali haji kukuharibia vyako au kukudhuru? Ni juzi tu
viongozi wa dini pande zote wamekaa kuungana na kuwa na
maamuzi ya bapoja ya kudumisha amani wanalipiga ball
kuonyesha upendo na ushirikiano. Kwa nini tena tuanze kurudi
nyuma? kuna nini hapa? Tujiangalie yasije kama yale
yatokeayo Jamuhuri ya kati ya wadini kuchinjana nyumba hadi
nyumba. Tumeoleana, tumechanganya dini na makabila-tujikanye
yasitukute hayo. Uhuru wa kuabudu upo kwa nini uchomee
wengine mahekalu yao na kuwaua? ISIS ndio imeshaingia? Mungu
atusaidie tuuone ukweli wa Uhuru sa Kuabudu tuliopewa na
Katiba ya Nchi.



On Saturday, 11
October 2014, 23:23, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:



Udini utalitesa taifa
hili madhali hatuko tayari kuuongelea kwa uhuru. Tunatambua
sana makemeo ya viongozi wetu wa siasa huku wakihisiwa
kuushiriki, na hapa ndipo palipo na tatizo. Nimesikiliza kwa
makini kusikia jina la mshukiwa. Nikahisi ni mwanzo mzuri
kupita kandoni mwa tatizo.
Mazishi ya
Mchungaji Kabuga yalihuzuliwa na Police wengi na habari juu
ya mjahidina aliyejifanya kujiunga na kanisa lake na baadaye
kumpa sumu tulifikiri zitafuatiliwa. Uamuzi wa familia na
waumini kusamehe haikuwa sababu ya serikali kunyamaza. Ni
makosa kuyafumbia macho matukio na badala yake kuwafuatilia
wanaotoa maoni kama ninayoyatoa hapa na hili natamani
kulisema tena
--------------------------------------------
On Sat, 10/11/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
wrote:

Subject:
[wanabidii] TAMKO LA WAKRISTO BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI
PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, October 11, 2014, 9:32 PM

TAMKO LA WAKRISTO
BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI
MAKANISA
TAREHE 11/10/2014.

Baada ya tukio la kutisha
la kushambuliwa kwa washirika na
hatimaye kuuawa kwa mshirika na kujeruhiwa
vibaya kwa
mwingine kanisani Kagemu
PAG; Wachungaji na viongozi wa kiroho wa
Bukoba tumepokea
taarifa hizi kwa
mshtuko mkubwa. Tumekutana tarehe 10 Oct 2014
na kutafakari
hatima ya wakristo
katika eneo hili. 

Matukio rejea

tuliyojikumbusha ni kama ifuatavyo:

1.      
Kanisa
la Living water pale Buyekera mlimani
limechomwa moto mara
2


2.      
Kanisa
la Hofan ministries limechomwa moto pale
Rugambwa. 


3.      
Kanisa
la
la International assemblies of God lilipo Magoti
lilichomwa moto na

kuteketea. 


4.      
Kanisa
la
TAG Kihwa lilichomwa moto na kuteketea

5.      
Makanisa
mengine maeneo ya vijijini kuchomwa moto nayo
ni pamoja na
Ruhanga TAG, Kakindo
PAG na Kasharu EAGT.

6.      
Vitisho
na Kushambuliwa kwa mawe wakati ibada
zikiendelea mara kwa
mara Kanisa la PAG
Buyekera.


7.      
Kanisa
la
EAGT Kibeta kushambuliwa kwa mawe baada ya kundi la watu
kuvamia kanisani
miezi 3
iliyopita


8.      
Kanisa
la
Harvest kushambuliwa kwa mawe usiku na kundi la watu.



9.      
Jaribio
la
kuchomwa kisu Askofu Sesse Lazaro wakati akiwa
kanisani.


10.   Kifo
cha kutatanisha cha Mch
Jackson Kabuga wa TAG Kashabo. 

Mengi ya matukio haya

yameripotiwa
katika vyombo vya usalama
ingawa hatujapata mrejesho wowote
toka
vyombo hivi.

Kwa mtazamo
wetu huu ni mpango
uliolasimishwa wa
kujenga hofu na hatimaye kukomesha uhuru

wetu katika
kumwabudu Mungu. Matukio haya
japo yanaonekana hayahusiani
lakini
yamebeba
maudhui inayofanana na
yanatekelezwa kwa mbinu zinazofanana
na
inawezekana na
kundi moja lenye mtandao
mpana. 

Kwa tamko hili
tunataka yafuatayo
yazingatiwe:

a.       Kwa
hali hii wakristo tutaweka mtandao
unaojitegemea wa ki
ulinzi wa nyumba za
ibada, viongozi wa kiroho, na washirika wetu
pamoja na hatua
nyingine zozote za
kiusalama tutakazoona zinafaa.

b.      Tunaitaka
serkali ifanye uchunguzi wa kina juu ya tukio
hili na
mengine yaliyotangulia na
kutupatia taarifa ndani ya muda mfupi juu ya
mafanikio au
kukwama kwa

uchunguzi.  


c.      
Kwa wakristo wote walioguswa
na kuumizwa na
tukio hili maneno la Mungu
toka Rumi 8:37-39 yawe faraja
yetu:

 "Lakini katika mambo
hayo yote
tunashinda, na zaidi ya kushinda,
kwa yeye aliyetupenda. Kwa
maana
nimekwisha
kujua hakika ya kwamba, wala
mauti, wala uzima, wala
malaika, wala
wenye
mamlaka, wala yaliyopo, wala
yatakayokuwapo, wala wenye
uwezo, wala
yaliyo juu, wala yaliyo chini,
wala kiumbe
kinginecho
chote hakitaweza kututenga na
upendo wa Mungu ulio katika
Kristo Yesu
Bwana
wetu." Amen 


 

Tamko
hili limetolewa na
wachungaji 35 waliokaa katika kikao cha
dhararula PAG tarehe
10/10/2014 na
kutiwa sahihi kwa niaba yao na:-

   

Mch Crodward Edward.

Mwenyekiti wa Umoja wa wachungaji
Bukoba.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda


wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:


Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.


---

You received this
message because you are subscribed to the

Google Groups "Wanabidii" group.


To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment