Wednesday, 29 October 2014

Re: [wanabidii] Shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu kuibeba CCM 2015

Mfa maji haachi kutapatapa

2014-10-28 21:10 GMT+03:00 <mchunguzihuru@gmail.com>:

Shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu kuibeba CCM 2015
SWALI: Kwa nini CCM wameanzisha Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania huku ilhali ndani ya Chama kuna Jumuiya zake?
JIBU : Shirikisho la Wanafunzi wa Tanzania wa vyuo vya elimu ya juu,umeanzishwa kwa kuzingatia umuhimu wa Chama kuungwa mkono na kundi la Vijana Wasomi waliopo katika Taasisi za Elimu ya Juu hapa nchini. Lengo kuu likiwa ni kuwapatia wanafunzi wa elimu ya juu fursa ya kukutana na kubadilisha mawazo na uzoefu juu ya maswala ya Itikadi ya chama,maadili na uzalendo wa nchi pamoja na kujenga fikra za kujitegemea na ubunifu.Chama cha Siasa kikomavu hakitaacha kuunda Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kuufanya uhusiano wake kuwa wa chanda na pete. Umadhubuti wa chama chochote cha siasa, ufanisi wake na uhai wake, unategemea vijana wake na hasa vijana waliopo katika vyuo vya elimu ya juu. Hivyo, Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu unapaswa kuwa imara kimuundo,kimaadili na kimkakati. Umadhubuti huo hutoa msaada mkubwa katika kufanikisha azma na malengo ya chama cha siasa.Shirikisho la Wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania tunatambua kuwa harakati za kuleta mapinduzi ya kiuchumi,kisayansi na kitekinolojia na kujenga jamii ya watu iliyo sawa nchini Tanzania, tunahitaji chombo madhubuti kinachounganisha fikra na vitendo vya vijana wote wakiwemo vijana wasomi.Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu tunaounda,unakusudia kushiriki katika kutatua changamoto za wanavyuo zinazohusu elimu, mikopo ya elimu ya juu, siasa, namna bora ya kujiajiri na uwezeshaji.
SWALI: NEC imepitisha Kanuni za Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, Je, una kauli gani katika hili na mipango yako kulisaidia Shirikisho kufika mbali zaidi.
JIBU: Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Mwenyekiti wa CCM,Ndg. Dkt.J.M.Kikwete kwa kuridhia kuundwa kwa Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, pia shukrani kwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwa kupitisha rasmi Kanuni za Shirikisho mnamo tarehe 16/10/2014.
Kuhusu mipango yangu juu ya kulisaidia Shirikisho kufika mbali zaidi ni pamoja na kufanya mambo ya msingi yaliyopelekea kuanzishwa kwa Shirikisho hili. Aidha,kutokana na kuwepo kwa upinzani mkubwa kutoka kwa vyama vya upinzani vyuoni, mtazamo wa vijana kutokuwa na imani na CCM, vijana kugeuzwa kuwa daraja kwa wanasiasa, kupungua kwa moyo wa uzalendo wa Taifa na maadili hasa kwa vijana wasomi, kutokuwa na utashi wa kufanya kazi kwa kujitolea hasa kazi za kijamii, kuibuka kwa vijana wenye mtazamo hasi juu ya CCM, na kutokuwa na taarifa sahihi zinazohusu baadhi ya makundi ya kijamii. Kutokana na hisia hizo zilizopo katika kundi kubwa la vijana na hasa vijana wasomi Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania limeweka programu ya kazi zake kwa kipindi cha 2014 – 2015 ili kuyaoandoa na yasiendelee kuwepo tukielekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa dola.
Programu hii ya Kazi za Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu tatu:- Kutoa mafunzo ya kina kwa wanavyuo kuhusu kazi ya Itikadi ndani ya chama.Kuwajenga wanavyuo katika maadili ya uzalendo, umoja na utaifa.Kujenga fikra "mind set" na kuwashirikisha kikamilifu wanafunzi wa vyuo katika ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na taaluma za wasomi kwa lengo la kuimarisha elimu ya kujitegemea.
SWALI: Umezungumza mambo mengi, lakini wapo watu wanaoamini Shirikisho lenu 'linadeal' na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, ambao ni wanafunzi, Je hamuoni mnavunja sheria kwa kuwa mtakuwa mnafanya siasa ndani ya vyuo.
JIBU: Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini unaundwa na Vyuo Vikuu vyote ambavyo vinatambuliwa na T.C.U. pamoja na Vyuo vya Elimu ya Juu ambavyo vinatambuliwa na NACTE, ambapo huko ndiko wanachama wake watakapopatikana. Wanachama hawa ambao ni Wanazuoni tutawafundisha Itikadi ya Chama ili waielewe vyema na wawe na uwezo wa kuizungumzia ndani ya Chama na nje ya Chama ndani ya Umma.Kuwafundisha wasomi hawa itikadi ya Chama hasa katika mfumo wa vyama vingi utasaidia kupatikana kwa wanachama bora watakaokisaidia Chama kuleta mawazo na Fikra mpya. Ikumbukwe kuwa sheria za nchi yetu hairuhusu kufanya siasa za vyama ndani ya wigo wa vyuo na si nje ya vyuo kama sisi Shirikisho tunavyofanya. Kuna siasa za wanafunzi "students politics" na ndiyo maana kuna Serikali za wanafunzi na sisi tunawafundisha makada wetu siasa za vyama " party politics".
SWALI: Nchini Tanzania hakuna sheria inayoruhusu kufanyika kwa siasa vyuoni. Sasa ujio wa Shirikisho na kuonyesha kabisa wanachama wake ni wanafunzi, huoni itachochea maandamano?
JIBU: Ni vema kufahamu kuwa maandamano hayaletwi na siasa kufanyika vyuoni. Kama nilivyosema hapo awali kuwa kuna siasa ya wanafunzi inayotambulika kama "students politics". Hii inawafanya wanafunzi kujifunza uongozi katika ngazi yao ya chuo. Siasa za vyama na hasa zinazotokana na kuwajenga vijana katika mtazamo hasi ndizo wakati mwingine husababisha maandamano na fujo kutokea na hizi huwa haziletwi na CCM bali vyama vingine kwa kuwatumia wanafunzi hawa kama chambo kwa kuvulia samaki wao.
Shirikisho halifanyi siasa zake katika maeneo ya chuo. Wakati mwingine maandamano na ukosefu wa amani husababishwa na menejimenti za vyuo husika,mfano kuna tatizo la upatikanaji wa maji chuoni na wanafunzi wametoa taarifa kwa menejimenti ya chuo,kuchelewa kupatikana kwa suluhisho na bila kuwepo kwa taarifa sahihi kwa ucheleweshaji wa upatikananji wa maji kunaweza kukaleta fujo chuoni,nk.
SWALI: Kumekuwepo na sintiofahamu hasa kutokana na taarifa zinazosambazwa katika vyombo vya habari kuwa Shirikisho lenu tayari lina mgombea wa Urais. Je kauli hii ni kweli?
JIBU: Ndugu mwandishi, nafikiri nimeeleza kwa kina madhumuni na malengo ya kuanzishwa kwa Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, na hakuna hata sehemu moja nimesema kuhusu kuwa na mgombea wa ngazi yeyote hata urais.CCM kina utaratibu wa Uchaguzi kwa ajili ya kuwapata Viongozi wake wa dola ikiwemo na Rais ambaye kwa mujibu wa Katiba yetu ndiye atakuwa Mwenyekiti wa CCM. Hivyo basi sisi kama wasomi tunaheshimu sana kanuni na taraatibu ambazo chama kimeziweka ili kuwapata viongozi wetu wa chama na dola. Kwa ufupi Shirikisho halina mgombea wa nafasi yeyote kwa sasa mpaka Chama kitakapomtangaza .

SWALI; Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu linazungumziaje juu ya Katiba Inayopendekezwa iliyotolewa na Bunge Maalumu la Katiba.
JIBU : Kwanza ni vema tukafahamu kuhusu Katiba ni kitu gani; Katiba ya nchi yeyote duniani ni andiko mahsusi lenye sura mbili: Sura ya kisheria na sura ya kisiasa . Sura yake ya kisheria inaelezwa kwa kigezo kuwa Katiba ndiyo sheria mama ya nchi: na sura yake ya kisiasa inaelezwa kwa kigezo kuwa Katiba ndiyo inayoweka wazi utaratibu mzima wa utawala wa nchi ulivyo. 
Kwa ujumla sisi kama wasomi vijana tunampongeza Ndg. J.M.Kiwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia mchakato huu mpaka hapa ilipofika tukiwa na hatua moja mbele ya Kura za Maoni,nasi tunaahidi kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa kwa sababu za msingi kabisa. Leo nitagusia suala moja tu inayohusu Serikali mbili. Hoja ya serikali 3 siyo hoja nyepesi. Kiukweli ni hoja ngumu yenye majibu magumu pia. Lakini cha ajabu ni kuwa baadhi ya watanzania wanaipa majibu rahisi ya kushauri kuwe na serikali tatu. Kwa upande wetu tunaiona hoja hii haina uzito wa kuwa na mustakabali mzuri na taifa letu. Haiwezi kuwa rahisi kiasi hicho kwani ni mjadala mkubwa unaohusisha usalama na uhai wa taifa hili. Waasisi wa taifa hili waliouna mfumo wa serikali 3 kuwa haufai kabisa. Mawazo mengi huwa yanapitwa na wakati lakini kwa suala hili mawazo yao tunauhakika wa asilimia 100 kuwa hayapitwa na wakati. Marekani ina muungano wa nchi 50 kwa karne kadhaa na kuwa Rais mmoja tu.Muungano wao haujapitwa na wakati ila wa kwetu ndio umepitwa na wakati.
Mjadala huu si mpya ulishakuwepo tangu hapo kama mwaka 1983 na 1984 na bahati nzuri hata hotuba za Mwalimu Julius kambarage Nyerere, Baba wa Taifa letu bado zipo na zinaweka wazi jambo hili. Mwalimu alikuwa na uwezo wa kujieleza kwa utashi hali ya juu. Serikali ya Tanganyika ilizikwa 1964 na asilimia kubwa ya watanzania wa leo hawakuwepo, hawako tayari kurudishwa kule ambako hawakujui. 
Watanzania walio wengi wanahitaji kupata utumishi unaowajali kwa kusaidia harakati za kupunguza umaskini kama si kuuondoa. Je kuleta serikali tatu itaondoa umasikini tulionao? Sisi kama vijana tunawaomba watanzania kusimama imara ili kuondoa uzushi huu ambao si kwanza kuwepo katika historia ya taifa letu kwani mwaka 1993 uzushi kama huu wa kundi la G55 ulisambaratishwa.
Tunachotaka kama makada wa Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini ni kuweka wazi kwamba hakuna mfumo wa serikali 3 uliodumu katika historia ya dunia. Mfano Singapore na Malaysia 1964; Senegal na Gambia‚ uliojulikana kama Senegambia' 1982-1989; Misri Syria, China Taiwani miungano hii yote ya serikali 3 haikudumu hata mara moja. Tunachoamini sisi na wataalamu wengine wa siasa na mambo ya kiuchumi ni kuwa hii ni njia ya kistaarabu ya kuuvunja mungano huu wa Serikali ya Tanganyika na Zanzibar.
Kwanza lazima tuelewe kuwa heshima ya Tanzania itashuka sana nje ya muungano huu. Je tutaingia vipi kwenye Shirikisho la EAC Tukiwa na serikali 3 Zbr, Tanganyika na ile ya Jamhuri ya Muungano? Tutakuwaje na nguvu tukiwa tumemegeka megeka?
Tuna uhakika kama Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu uwezo wa kiuchumi ya Jamhuri mbili ya Zanzibar na Tanganyika utadumu bila ya matatizo kwenye mfumo huu tulionao wa serikali mbili. Hasa tukiangalia hali halisi ya takwimu za makusanyo ya kodi kutoka sehemu zote mbili za Jamhuri yetu, yaani Zanzibar na Tanzania Bara. Mashaka ya kuvunjika muungano unatokana na ukweli kuwa serikali ya Zanzibar ina tax base ndogo. Wakati hii serikali ya Tanganyika inajiweza kabisa kujiendesha na kuiendesha ile ya Jamhuri ya Muungano bila shaka yeyote kwa sababu tax base yake ni kubwa (yaani makusanyo ya kodi ni makubwa). 
Lakini kwa kuwa tunaingia kwenye mfumo wa serikali 3, kila nchi itakuwa inawajibika kutoa fungu sawasawa kwa ajili ya kuichangia serikali ya Shirikisho yaani ya Jamhuri ya Muungano. Zanzibar ambayo itakuwa inajiendesha kwa tabu sana kwa kuwa uchumi wake ni mdogo haitoweza kuichangia Serikali ya Jamhuri ipasavyo. Hapo ndipo patatokea matatizo kwani serikali ya Tanganyika haitokuwa tayari kulifidia pengo la mchango wa Zanzibar katika kuiendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano. Na wala Watumishi wake kuanzia Rais wa Tanganyika, na wasaidizi wake pamoja na wafanyakazi wa kada mbalimbali hatudhani kama watakubali kukatwa kodi zao kwa ajili ya kufidia pengo la mchango wa Zanzibar kwa ajili ya kuiendesha Serikali ya Shirikisho.
Hii ina maana kama Zanzibar ingekuwa na Effective Tax Base ambayo ingeipatia kodi kubwa kama ya upande wa TZ Bara basi Muungano kidogo ungekuwa Alhamdulillah salama. Lakini kwa kuwa uwezo wa Zanzibar kiuchumi ni mdogo migogoro hiyo ya michango inaweza kumuacha Rais wa Jamhuri ya Muungano hana kazi ya kufanya kwa kuwa atakuwa hana kitu kwenye Account za Serikali, kitu ambacho ni hatari sana. Ndio maana watu kama sisi tunasema Serikali 3 ni ufunguo wa kuuvunja Muungano kwa kuwa nguzo zake zimelegezwa, kugongwa na kutikiswa.
SWALI:Mmejiandaa vipi sasa kukisaidia Chama katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na huu wa serikali za mitaa mwaka huu?
JIBU: Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini,tumejiandaa vema kwa kutimiza wajibu wetu katika kufikiri kwa makini, kuchambua kwa makini na mwisho kuchagua sera makini kwa ajili ya mustakabali makini wa taifa letu linalomjali kila mtu bila kumbagua kwa ukoo wake, kabila lake, dini yake au kwa eneo analotoka kama wenzetu wengine wa vyama pinzani wanavyofanya.
Shirikisho letu ni vema likatumika katika kutoa taarifa sahihi ya serikali ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi chote ili wananchi ambao wametupatia dhamana ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano waweze kuona nini kimetekelezeka katika kipindi hiki. Tupimwe kwa hayo. Aidha,vijana tutafute njia mbadala ya kuwasiliana kama vile kuwa ndani ya FaceBook ili tuweze kutoa majawabu dhidi ya hoja zilizojaa kila aina ya uongo. 
Lazima tuwe na uwezo wa kufikiri, kuchambua, na kufanya uchaguzi makini na uliotukuka kwa mustakabali wa uhai wa taifa hili utakaomjali mtanzania bila kujali rangi, kabila, na dini yake. Na uchaguzi huu hauwezi kupatikana nje ya CCM.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment