'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Upinzani wa kweli nchi za Africa bado maana wapinzani wengi ni tonge kama chama tawala tu. Mtu akikosa cheo upinzani anahamia chama tawala au kuunda chama chake. ujue nia hapa ni tonge.
Kuna kumbukumbu huko nyuma waliungana (1995) hisi sikumbuki uchaguzi wa kwanza au wa pili ila waliungana isipokuwa tamaa ya kila mmojawao kugombea Urais ikawasambaratisha. Tatizo ni mtu mwenye tamaa kuweza kukubali kuiacha ampe nafasi mwingine.
Wanawake nao corrupt kama wanaume. Nilisaidia kesi ya mama mmoja Mkomazi ya kuchukuliwa ardhi yake ambayo mume aligawiwa na kijiji enzi za ujamaa mashamba makubwa kuchukuliwa. Lakini sera ilipobadilika waliokuwa na cutomary land zilizochukuliwa na vijiji wakaanza kuzivamia kuzichukua. Vidhibiti vyote vya mume kupewa na barua za kijiji kumtetea vilikwama na shamba likachukuliwa na huyo mwenye uwezo, kabila moja, koo zinafahamiana. Kuliundwa NGO na mzungu volunteer ya kutetea wanawake hapo vijiji vya kata na alikarabati majumba ya zamani ya Kisiwani sisal Estate wakawa na ofisi nzuri ya NGO kuliko ya Kata. Nikivaa joho la msikilizaji na rafiki kumbe mpelelezi akina mama hao wa NGO waliotakiwa kumsaidia wakimshauri akubali kupokea hela toka huyo mtu ili afute kesi hatoshinda ana uwezo atamkomesha. Ilipofika mahakamani Afisa/karani mahakamani mtetezi wa masuala ya Jamii wa Idara ya Ustawi Jamii (mwanamke) alikuja kumfuata mama tulipokaa kuchukua kitu kidogo/hela ili amsaidie kusaka na file lake. Picha niliyoipata si nzuri. wanawake nao pamoja na matatizo wayapatayo-sio clean ni corrupt wana tamaa hata wale waliopo ktk siasa-rushwa nao inawatawala. Mtoto umleavyo...Wanawake wanatetea fisadi, jambazi, mbakaji. Wanaume corruption na tamaa ya kudumu madarakani pamoja na uzee ndio donda sugu.
Kama hatuwajibiki hata ndani ya familia, kudhulumu mali ya yatima; kumpora mfiwa (ke) mali za urithi na unashuhudia hata kwa msomi aliyepewa dhamana ya kusimamia mirathi-anadhulumu. Nani atatetea uchumi wa nchi? Tujitakase pande zote!!
Wanaungana kijijini wazee wa mila wanatoa ardhi kisiri na watu wa kijijini hapo wanawaogopa wao ni wengi, wazee wa mila ni wawili watatu tu unategemea nini? na hao wanaoingiza wahamiaji haram, wageni wenye bunduki na mabomu kuja kuuza wanaokutwa na garage yenye magari na pikipiki zilizoibiwa ndani ya kuta zao mume, mke na watoto wakibadilisha magari ya ufahari wakati wanajua wamiliki waliuawa yamo uwani kwao wanabadili rangi na namba; tunapopigia kura mafisadi na kuwatangaza wema kuficha uovu wao na kampeni zimeanza; tunapokuwa na matajiri ambao hawaungani kuunda makampuni international yakamiliki mali na kuendesha miradi ya kiuchumi ndani na nje ya nchi kama Dangote bali kugharimia Iftah, Miss Tanzania, Mpira, mlo wa kristmas kila mkoa-vijana bodaboda nguvu kazi zijazane mtaani-unategemea nani ataushika uchumi kama sio wageni wajao. Waungane wachukue mashamba ya mamlaka mbali mbali yanayoota magugu kwa sasa, wakajenge nyumba na godown na processing industries huko, walete wakufunzi wafunze vijana na watoe ajira kwa vijana, omba omba mtaani wakae huko wazuke mapambo yauzwe ndani na nje ya nchi. hata ulaya tunanunua nguo za kutoka nchi mbali mbali-vitenge, tie and dye; unga wa muhogo, mihogo na viazi vibichi, dagaa na samaki hongwe, papa, mbaazi etc vinatoka nje ya nchi hizo nasi Tanzania tunaweza. lakini tupo katika Soda na Juice za rangi maembe, machungwa, mananazi yanaoza vijijini. Nani ataushika uchumi kama sio wageni na makampuni ya kitapeli kununua mazao kwa bei ya kuwaibia wananchi. na makampuni hayo na madalali wao ni ya waafrika, watanzania; ni waume na ndugu zetu. Tunajila wenyewe.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment