Saturday, 19 April 2014

RE: [wanabidii] Re: Slaa Haya Unayosema!

Haya sasa na hapa unakumbuka?


Date: Thu, 12 May 2011 00:01:16 -0700
From: innocentmahedi@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: Slaa Haya Unayosema!
To: wanabidii@googlegroups.com

Wanabidii,
 
Tumechangia vyema. Kuna dhana kuwa magari ya Chadema kwanza hayatumii mafuta mengi na hivyo kuzunguka Tanzania nzima sio gharama kubwa. Tena wanajibana katika kutumia magari machache sana sana mawili na hubeba msafara mzima. Huwa wanabeba mikate na maji na hivyo hawana gharama kubwa ya vyakula wawapo ziarani. Na kwa vile wanauchungu na nchi hii pia wanalala katika magari yao hivyo hawana gharama za malazi wawapo ziarani. Viongozi wetu hawa ni kweli wanauchungu nasi walala hoi kwani shule isiyo bora ni afadhali isifundishe na kuhudhuria mihadhara ya chama chetu hivyo inasaidia sana wanafunzi wa shule za kata kupata angalau somo la siasa bure katika mihadhara. Wakulima katika vijiji vyetu hawapewi kipaumbele hivyo kuwakusanya katika mihadhara inasaidia angalau kuwakutanisha na kuwaelewesha gharama za vitu kama magari na posho za viongozi wao maana hakuna popote watakapopata taarifa hizi.
 
Msituhukumu bure jamani tuna malengo thabiti na taifa hili na tukipewa kuongoza nchi kwanza kwa mwaka wa kwanza tutatanga sera zetu nchi nzima. Mwaka wa pili tutapita kuwashukuru, mwaka wa tatu na wanne tutaimarisha ofisi zetu nchi nzima na mwaka wa tano tutajipanga kwa kampeni na tutashinda. Hivyo endeleeni kutupa usikivu wenu ili nchi hii iwe ya kisisasa zaidi maana haijulikani ni ya kibepari, kisayansi, kiuchumi, kidini au ya aina gani. taifa hili litakuwa la kisiasa na itangozwa kwa mihadhara kama njia kuu ya kujipatia kipato na kujikimu. Tena hata Watz watapata kazi kubwa kusimamia siasa na nchi zingine za Afrika.
 
Nawasilisha.
Innocent


From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thu, May 12, 2011 8:30:47 AM
Subject: [wanabidii] Re: Slaa Haya Unayosema!

Upinzani unatakiwa kubadilika kutoka kuongea kwenda kwenye vitendo
zaidi haswa vya kusaidia jamii mbalimbali zilizopo vijijini kwa mfano
wanapoenda kule sumbawanga kwani kuna ubaya gani hata kuchangisha hela
kwa ajili ya kujenga hata darasa moja la wanafunzi ? au hata kupanga
rangi tu kwenye shule moja ya msingi ? wakati unachukuwa wanafunzi
wale waje wakusikilize jukwaani kwa hali na mali halafu wanarudi
makwao kuendelea na maisha yale yale nathani haikubaliki lazima maneno
yaende kwa vitendo na serikali haitoweza kufanya kila kitu hata kujibu
kila kitu vingine ni kujijibu wenyewe kwa matendo

On May 12, 6:58 am, AMAZIA JUDICA <amaz...@yahoo.co.uk> wrote:
> Ndugu yangu Hildergarda,
> Kuelimisha uma ili ufahamu haki zake ni jambo muhimu sana. Chadema wanachokifanya ndicho sahihi.
>  
> Sawe
>
> From: Hildegarda Kiwasila <khildega...@yahoo.co.uk>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Wednesday, 11 May 2011, 14:00
> Subject: Re: [wanabidii] Slaa Haya Unayosema!
>
> Ama kweli nyani haoni kundule (Ashakum!!).. Unamsema mwenzako kumbe nawewe umo humo humo-misafara, uniform, posho, hutuba zisizo na mwisho, gharama za kujenga zahanati, kununua powertiller ni za kulala lodging na kujenga majukwaa. watu hawalimi, hawajengi ni kupanga maandamano hapa na pale. The maandamano diseases of the ignorant poor instigated by the wealthy intelligensia who have a posho disease.
>
> From: mohammed mgori <mohammed.mg...@gmail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Wed, 11 May, 2011 11:59:22
> Subject: [wanabidii] Slaa Haya Unayosema!
>
> Katibu Haya uliyoyasema ni kweli unauchungu nao au it just a politics?
> kwani wewe mshahara wako wa sasa unaopata bure haufai kujengea Vituo vya Afya?
> Magari na Muda mnaotumia hivi sasa kuzunguka nchi nzima ili mpate
> malupulupu je hizi pesa hazifai kujengea Vituo vya Huduma ya Afya?
> Magari ya Kifahari unayotumia wewe na wenzio je yenyewe hayana thamani
> sawa na vituo vya afya acha kuwaongopea wanaTZ.
> tunahitaji Mtu wa kweli mwenye nia thabiti  ya maendeleo ya Tanzania
> na Watanzania na sio kusema uongo mbele ya majukwaa ya siasa kujenga
> chuki kwa wananchi kwa Serikali yao
> na inaonekana Amani iliyopo hapa nchini inakukera sana  au wanao
> wadhani wawaone mpo busy ili wazidi kuwapeni posho mzidi kujinufaisha
> wenyewe na si kwa watanzania?
>
> Mgori
>
> KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa amechafua hali ya hewa
> katika Jimbo la Katavi lililopo Mkoa mpya wa Katavi ambalo Mbunge wake
> ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwaambia wananchi kuwa:
> "Kiongozi huyo anafurahia anasa za uwaziri mkuu."Dk Slaa alifanya
> mikutano mitatu ya hadhara jimboni humo jana katika vijiji vya
> Majimoto, Mbende na Usevya, alikozaliwa Pinda ikiwa ni mfululizo wa
> maandamano na mikutano inayofanywa na chama hicho katika mikoa ya
> Nyanda za Juu Kusini.
>
> Alisema Pinda anatembelea magari yenye gharama kubwa ambayo thamani
> yake ni Sh500 milioni huku wasaidizi wake nao wakipanda yaliyo na
> thamani ya Sh200 milioni wakati wapiga kura wake wana hali ngumu ya
> maisha.
>
> "Nikiangalia hali ya maisha yenu wananchi wa jimbo hili, Mkoa wa Rukwa
> na Katavi si haki ninyi kuendelea kuishi kwenye nyumba za udongo na
> nyasi wakati kodi zinafujwa kila kukicha kwa matumizi ya anasa ya
> Serikali hii," alisema Dk Slaa.
>
> Dk Slaa alisema mbali na anasa hiyo, semina elekezi kwa mawaziri
> inayoendelea mkoani Dodoma imegharimu fedha nyingi na  kwamba iwapo
> serikali ingekuwa inawajali wananchi wake, ingeweza kujenga shule za
> sekondari katika jimbo zima la Waziri Mkuu kwa kutumia fedha
> zinazotumika katika semina hiyo.
>
> "Leo Pinda na Rais Jakaya Kikwete wako Dodoma kwenye Semina Elekezi,
> wanatumia kodi za wananchi na baadaye wanarudi kuwakamua kwa
> kupandisha gharama za maisha na kutoza kodi kubwa," alisema.
>
> "Kikwete amewateua mawaziri kisha anawaandalia semina za kazi gani?
> Kama hawana uwezo wa kuongoza si angeteua wabunge wengine? Alisema
> mawaziri walioshindwa kufanya kazi wajiondoe wenyewe. Kwani anajua
> mawaziri wake hawafai, lakini badala ya kuwafukuza anawapa ruksa
> wajiondoe wenyewe!"
>
> "Pinda, kwa siku moja akiwa kule bungeni hupata posho ya Sh200,000
> ambayo inazidi mshahara wa mwezi mmoja wa mwalimu, hata polisi
> anayelinda usalama wenu.. Lakini magari anayotumia kwenye msafara wake
> yasiyopungua 30 gharama yake haipungui Sh600 bilioni. Gharama ya gari
> analotembelea mbunge wenu ni sawa na kujenga vituo vitano vya afya."
>
> Dk Slaa aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana
> alisema, inasikitisha kuona Mbunge wa Katavi anakuwa mbinafsi kwa
> kujiwekea umeme wa jua kwenye nyumba yake pekee katika Kijiji cha
> Usevya badala ya kuupeleka kwa wananchi wote.
>
> "Inasikitisha kuona mbunge wenu anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme
> wa jua katika nyumba yake iliyopo Usevya badala ya kupeleka umeme
> ambao ungeweza kutumiwa na wananchi wote. Nyinyi wenyewe mnaona kwenye
> nyumba yake pale kuna umeme wa nguvu ya jua, wakati ninyi wapigakura
> wake mkiwa kwenye dimbwi la giza hamuoni kama ni ukatili mkubwa?
> aliuliza.
>
> Zitto amjibu Waziri Mkulo
> Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema atamthibitishia
> bungeni, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kuwa Serikali
> imefilisika.Zitto alisema jana mjini Sumbawanga kuwa wataweka
> hadharani jinsi Serikali ilivyokopa fedha benki ili Waziri Mkulo aweze
> kuwajibika kutokana na kauli yake aliyoiita ya kukataa kusema ukweli.
>
> Alisisitiza kwamba serikali haina fedha na kudokeza kuwa taarifa ya
> Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mapitio ya uchumi ya mwezi Machi mwaka
> huu, inaonyesha kuwa imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15.
>
> "Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali katika makusanyo ya kodi zote
> imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15 isipokuwa ushuru wa forodha.
> Hivyo haikufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi," alisema Zitto.
>
> Kwa mujibu wa Zitto, Machi, mwaka huu Serikali ilikopa fedha katika
> Benki ya Exim na benki zote za biashara nchini na ilikuwa ikihangaika
> ili iweze kuwalipa wafanyakazi.
>
> "Mkulo atueleze ni serikali gani duniani inakopa kwenye benki za
> biashara kwa kuwa kitendo hicho ni hatari sana kwa nchi," alisema na
> kuongeza:"Bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa ni Sh11 trilioni ambayo
> Serikali ilishindwa kufikia malengo ya Sh 1.6 trilioni kutokana na
> kushindwa kukusanya kodi kwa asilimia hiyo 15 isipokuwa ushuru wa
> forodha."
> Alimtaka Mkulo kuacha kuwaona wanaosema kwamba serikali haina fedha si
> wazalendo kwa kuwa wawekezaji hawatakuja nchini, bali atambue kuwa
> kukosekana kwa fedha si suala la uzalendo.
>
> "Serikali ni kweli haina fedha na hakuna suala la uzalendo katika
> hili. Tatizo la uwekezaji ambalo analizungumzia, linatokana na sera
> mbovu za CCM kwa kuwa tangu mwaka 2007, hakuna uwekezaji wowote wa
> maana uliofanyika hapa nchini," alisema Zitto.
>
> Akiwahutubia wanachama wa Chadema na wananchi wa mji wa Vwawa, Mbozi,
> mkoani Mbeya hivi karibuni, Zitto alisema Serikali ina hali mbaya
> kifedha kwa sasa kiasi cha kukopa ili kulipa mishahara ya wafanyakazi.
> Alidai kuwa hali hiyo mbaya kifedha kwa serikali imesababisha
> watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi Mei 7, 2011.
>
> Alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake
> mishahara ya mwezi Aprili.
> "Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za
> kugharimia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa
> kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.
>
> Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imekwenda kukopa Sh540 bilioni
> kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na
> ukata."Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au
> kugharimia miradi ya maendeleo, bali inakopa ili ilipe mishahara ya
> wafanyakazi," alisema Zitto.
>
> --www.kazibongo.blogspot.comkwa Nafasi za Kazi kila siku
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> --www.kazibongo.blogspot.comkwa Nafasi za Kazi kila siku
>  
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>  
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
www.kazibongo.blogspot.com kwa Nafasi za Kazi kila siku

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
www.kazibongo.blogspot.com kwa Nafasi za Kazi kila siku
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment