Monday, 25 November 2013

[wanabidii] Re: [YP_Ke] MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WATANZANIA NCHINI KENYA


 Kwa aliyeandika,

Kwa kweli ni huzuni na inasikitisha sana  kuona mambo kama haya yakitokea. Usichukulie jibu langu ki makosa lakini kulingana na matokeo uliyo taja, haionekani kama kuna njama ya kuangamiza watanzania. 

Nikiangalia matokeo uliyonakili na vile hali ya usalama ilivyo nchini inaoneka tu kuwa, matokeo haya ni baadhi ya visa vya mauaji ambayo pia yana tokea kwa wakenya. Ili balozi ihusishwe au uwe mzozo wa mataifa lazima kuwe na msukumo fulani unaochangia mauaji hayo. Hivyo basi kama kuna jambo kuhusa hawa walio uliwa na vile hayo mauaji yalivyo tendeka na polisi waone kuwa kunazaidi ya kuwa mauaji ya uhalifu 'wakawaida' basi hapo ombi au mtizamo wako waweza kuwa na uzito. Hata hivyo uko sawa kuomba ubalozi wa Tanzania kujihusisha lakini sidhani kama haya mauaji ni ya kipekee kufikia kiwango cha kusema ni uhasama baina ya Tanzania na Wakenya haswa ukiangalia hali ya usalama ilivyo nchini Kenya.






On Monday, November 25, 2013 11:24 AM, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WATANZANIA NCHINI KENYA

Ndugu zangu ,

Kumekuwa na matukio ya kutisha dhidi ya raia wa watanzania wanaosoma , kuishi Kenya au kwenda tu kwa ajili ya safari zao mbalimbali za kikazi nchini humo matukio haya ni ya kutisha kama sio ya kuogofya na ukizingatia hali ilivyo afrika mashariki kwa sasa ya usalama ndio matukio haya yanaongezeka .

Binafsi niliwahi kupoteza ndugu yangu miaka 3 iliyopita kule Mombasa , huyu ndugu yangu alikuwa anaishi huko na wazazi wake kwenye biashara ya mahoteli basi wakamvizia usiku wakaenda wakanyonga mpaka leo kesi yake haijulikani ilivyoisha isha .

Wiki iliyopita kuna mtanzania ameuwawa kinyama alipokuwa anatoka kwenye ukumbi wa disko , kutokana na maelezo ya awali wanasema alishawasiliana na rafiki zake kwamba ndio anatoka ukumbini kurudi nyumbani lakini hakufika mpaka alipokuja kuokotwa akiwa ameshafariki dunia .

Weekend hii ya kuamkia leo kuna mtanzania amepatikana hospitali Fulani huko jijini Nairobi akiwa hajitambui kabisa ikagundulika ni daktari na mfanyakazi wa wizara ya afya huko Zanzibar mpaka naandika hivi mkewe ameshaenda huko lakini hajitambui inaonekana walimpiga na kitu kizito usoni upande wa jicho .Hatujui baada ya uhalifu huu wamemwibia taarifa gani au nini .

Inaonyesha watanzania wamekuwa target ya uhalifu wa kikenya haswa jijini Nairobi na Mombasa na muda wote huko serikali yetu kupitia balozi wetu huko Kenya hajawahi kutoa tamko lolote wala chochote hata hii habari ya huyu daktari pia watu wako kimya sijui wanataka sasa watu wafanye nini ? wajilinde wenyewe ?

Hali hii inanikumbusha kipindi Fulani wakati wa machafuko ya kibaguzi huko afrika kusini dhidi ya watu wasiokuwa raia wa afrika kusini , siku moja makundi ya vijana wa afrika kusini walikuwa wanaenda kuvamia kwenye sehemu walizokuwa wanakaa raia wa afrika magharibi haswa naigeria hawa jamaa wa naigeria walikuwa wamejiandaa na silaha zao bastoli , bunduki na nyingine mbalimbali wakawa wanawangoja hawa vijana wa zuma .

Wale vijana wa zuma kuona vile na jeshi la polisi kuona vile ndio mzozo ukaishia hapo .

Tusingependa itokee hivi kwa ndugu zetu na jirani zetu hapo Kenya pale ambapo watanzania watachoka kuumizwa na kuuwawa kwa kunyongwa kila mara .

Naomba serikali kupitia waziri mhusika wa mambo ya nje au wa afrika mashariki na balozi wetu hapo Kenya watoe tamko la kuhusu kile kinachoendelea huko Kenya na kuhakikishia watanzania hao usalama wao huko Kenya .

--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
SINGLE & SEARCHING? Your search ends here https://www.facebook.com/pages/The-Perfect-Partner/216150688540099
 
The Perfect Partners mission is to help people find and maintain successful, loving relationships.We believe that the desire for love and companionship is basic to our nature and fundamental to our well being.

Our service is patterned after the model of an Executive Search Firm. Our personal interview takes place in your home so we can gain a better understanding of who you are, and what you?re looking for. You will meet qualified matches that share your goals, aspirations, lifestyle, activities and intellectual pursuits.
 
Join us on facebook here https://www.facebook.com/pages/The-Perfect-Partner/216150688540099


0 comments:

Post a Comment