Mnyonge mnyongeni, mimi Enzi hizo mwanangu aliuguaga, Dr. Masawe huyohuyo alinisaidia kutambua tatizo na kulitibu kwa wakati.
2013/11/11 Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
--2013/11/11 Mwanahamisi <mishysingano@yahoo.com>
Yes Kisinda mimi niliwaambia pale pale kuwa huduma zao sizifurahii na nikaomba discharge wakanambia kwa ethic za kidaktari hawawezi kunidischarge kwani mtoto bado anaumwa sana unless sign kuwa nimekaidi ushauri, na nikawaambia kwakuwa sio kuimarika kwa huduma zenu na hali ya mtoto wangu inazidi kuwa mbaya am more than happy kusign, and I did. So they know at least from me, sijawahi kwenda tena ever since kwahiyo sijui kama walifanyia kazi list ya malalamiko yangu au la.Mishy
Sent from my iPhoneMwanahamisi na Thomas,
Niwapongeze kwa kuja hadharani na mapungufu katika huduma zinazotolewa kwa Dr. Masawe. Pengine hizi zitasaidia kwa wale wenye ukaribu nao kuwaeleza na wao kujirekebisha.
Kwa upande wangu ninaamini kuwa siku mlipoona hayo mapungufu mliwasiliana na uongozi moja kwa moja. Japo kwa wengi, ushauri wa wateja si kitu kwa kuwa majina yao yapo juu. Hiyo ni changamoto kubwa kwa utendaji na uboreshaji wa huduma.
Binafsi nina imani kuwa ubora hudhoofika endapo mtoa huduma anazidiwa na wateja. Kwa mantiki hiyo, sijawahi kwenda, wala kumshauri mtu kwena huko kwa kuwa ninashakia ubora wa huduma kwa kuzidiwa na wateja na si utaalamu.
Nilifurahia sana huduma ya AMI kwa kuwa unaweza kuweka hata miadi (appointment) kwa simu na muda huo ukakuta mtoa huduma akikusubiria.
Hata hivyo, bado tuna mengi ya kuboresha.KISINDA, Octavius Alex | P O Box 21933 | Dar es Salaam | The United Republic of Tanzania
Mobile: +255 (0) 754 470 321 | +255 (0) 788 937 209.'Ongoza kwa kutenda (Lead by doing).'
On Monday, November 11, 2013 2:40 PM, Mwanahamisi <mishysingano@yahoo.com> wrote:
Na mimi pia namuunga mkono Thomas, 2010 kama February hivi Saleem wangu aliumwa by then alikuwa na miezi Sita. Alianza kutapika na kuharisha kama mchezo tukaambiwa tumpeleke pale. Nilikazwa pale siku tatu na Hali ya mtoto akizidi kuwa mbaya, siku ya nne nikaomba ruksa ya nguvu na kusign fomu kuwa namtoa mgonjwa kinyume cha ushauri wa dr nikampeleka Aga Khan. Na kingine customer service ilikuwa sifuri' mtoto anatapika sana, niliomba shuka kubadilisha nikaambiwa shuka zimeisha tukatandika khanga na hawakujali.
Sent from my iPhoneThomas, unaweza kutueleza kwa nini Dr. Massawe sio mzuri? Je, ni kwa sababu ya wingi wa wagonjwa? Pia wako watatu hao - baba, mama na mtoto - sasa unamzungumzia yupi hasa?
From: Thomas Joseph <nkarangot@yahoo.com>
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Sent: Monday, November 11, 2013 6:09 AM
Subject: Re: [Wanazuoni] Msaada: Mtoto wa miezi 8 anaugua mara kwa mara
Ndugu Elly,Ushauri wa Kisinda unamashiko.Angalizo tu: kwa watoto under five asipeleke kwa daktari asiyekuwa bingwa wa maswala ya watoto. Hawa hawana uzoefu na magonjwa ya watoto. Kuna madaktari bingwa kwenye hosptl zote za wilaya na mkoa. Kwa haraka haraka tu mie naweza kuhisi kinachomsumbua mtoto sio malaria, inaweza kuwa ni UTI au infection kwenye tumbo. Mtoto akiwa na UTI akipimwa malaria inaonekana. kwa dkt asiye mzoefu atamtundika midawa. Kwa ushauri, dkt Prof. Massawe wa Morroco sio mzuri, ila Ibra anafaa.Pole kwa kuuguza.ThomasSocial capital is not depleted by use......
On Monday, 11 November 2013, 13:26, Atuwene Mbelle <atuwene.mbelle@gmail.com> wrote:
Mimi ninakushauri umuone Dr. Kuboja, anapatikana Muhimbili, Aghakhan au TMJ. Lakini pia kwa kudiagnose tatizo kwa watoto wadogo Dr. Mbise Aghakhan na Dr. Massawe Moroco ni wazuri. Kwa uzoefu wangu kidogo motto wa umri huo kama ananyonya fulltime Malaria kurudia mara nne sio rahisi.2013/11/11 Octavius Kisinda <kisindao@yahoo.com>
Elly,Poleni kwa kuuguliwa na kuuguza.Pokea ushauri uliotolewa hapo juu na kisha uanza kuufanyia kazi.
Kama upo Dar, Dr. Koya na Dr.Hameer wa Kariakoo ni wazuri sana kwa under fives. Ila ukiweza kuwahi kwa Dr. Koya kabla ya saa saba mchana huwa anakuwepo mwenyewe hutajilaumu. Gharama ya kuwaona madaktari bingwa wote haipungui: T.Shs21,000.00 tu.
Regency pia yupo Dr. Emmanuel ambaye nimekuwa nikimtumia kwa ajili ya watoto wangu. Yupo flexible japo foleni haiepukiki. Elia Complex, opposite na CBE kuna Dr. Yohana, ni experienced na affordable.Usipotaka foleni kabisa fika Masaki, AMI (Afrincan Medical Institute), baada ya Slip Way, kuna full time Pediatrician (Dr. Aisha) au Dr. Namara Mkopi ambaye hufika kuanzia saa 11 jioni akitokea Muhimbili.Endapo upo mikoani, fika hospitali za Mkoa au Wilaya. Na hakikisha unampata daktari bingwa/anayeshughulika na watoto. Utapata huduma kwa kuwa wana uzoefu wa kutosha katika nyanja hiyo.Tunamwombea Mtoto afya njema.KISINDA, Octavius Alex | P O Box 21933 | Dar es Salaam | The United Republic of Tanzania
Mobile: +255 (0) 754 470 321 | +255 (0) 788 937 209.
'Ongoza kwa kutenda (Lead by doing).'
On Monday, November 11, 2013 10:41 AM, Mwanahamis <mishysingano@yahoo.com> wrote:
Poleni Sana,Kwa uzoefu wangu kama mama wa malaika mawili inaweza kuwa U.T.I hizi diaper tunazovalisha watoto wanakaa nazo asubuhi mpaka jioni imekuwa ni tatizo kubwa sana hasa kama mtoto anayeshinda na wasichana, jaribu kucheki hiyo. Kwa hosp nenda kwa Dr Hameer au kwa Dr Koa wote wako kariakoo ni wazuri sana kwa watoto na niafordable ila foleni ni ndefu mno unaweza kuwajibika kwenda sa kumi na mbili asubuhi ili uwahi namba. Sanitax mikocheni ni wazuri sana ila sijui bei zao nadhani watakuwa juu kidogo manake wako kiulaya zaid. Again poleni kwa kuuguza
Sent from my iPadKwanza nianze kwa kuwaomba radha wanajamii, inawezekana ishu kama hii hili sio jukwaa lake lakini wahenga walisema palipo na wengi haliharibiki neno na pia post hii inaweza kusaidia pia watu wengine hapa jamvini.Bila shaka humu kuna watu wenye watoto au uzoefu na malezi ya watoto. Nina mdogo wangu anamtoto wa miezi 8. Kwa kipindi kama cha miezi 2 iliyopita afya ya huyu mtoto imekua sio nzuri. Mara ya kwanza kabisa mtoto alikua anatapika kila chakula anachopewa.walimpeleka dispensary ya jirani na makazi yao hapo wakampima wakasema ana malaria 2, wakampatia dawa na kumchoma sindano kuzuia kutapika. Mtoto alipata nafuu lakini baada ya muda kama wa wili 2 hivi ile hali ikajirudia. Walienda tena pale dispensary wakampima tena wakasema ana malaria 2 wakafanya kama awali ila safari hii walimbadilishia dawa. sasa hii hali imerudia kama mara 4 hivi na kila wakimpima wanasema ana malaria 2. Wamejitahidi nyumbani kuboresha mazingira ikiwa ni pamoja na kutumia dawa ya mbu, kumvalish nguo mwili mzima hasa jioni n.k bila mafanikio.
Wameniomba ushauri na baada ya kuwasikiliza nikahisi hii inaweza kuwa kuna tatizo lingine pia, baada ya hayo maelezo naomba tusaidiane maswali yafuatayo.
1) Ni hospital/Dispensary gani ambayo ni affordable lakini wanahuduma nzuri sana kwa uzoefu wako hasa mambo yanayosumbua watoto?
2) Kuna Dr yeyote wa watoto unayemfaham au hospital/Dispensary yake ambayo sio ghali sana anaweza kumpeleka huyu mtoto akachekiwe.
Ni hayo tu na samahani kwa usumbufu wowote
Find Jobs in Africa Jobs in AfricaInternational Job Opportunities International Job OpportunitiesJobs in Kenya Jobs in Kenya__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (16) .![]()
__,_._,___
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment