Thursday 28 November 2013

[wanabidii] Re: [Wanazuoni] MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WATANZANIA NCHINI KENYA

well said. Nilianza kuwa na wasiwasi Kenya kumeanza kuwa na xenophobia ya kichini chini, lakini nakubaliana na ulichokisema. 

Kwa mfano, mauaji ya Jerry pamoja bado uchunguzi unaendelea, ukifuatilia habari za mwanzo, alikuwa akitoka club usiku, hivyo inawezekana alikutana na vibaka on his way home. 

After all, bado sijaona sababu ya msingi kwanini Wakenya watuchukie mpaka kufikia sehemu ya kutuuwa. Kama ni chuki, inaleta maana zaidi wao kuwa na chuki zaidi na Wasomali na sio sisi Watanzania. 

Kama ulivyosema, "tusijenge chuki mbazo hazipo" na ninakubaliana na  wewe kabisa.  


On Thursday, November 28, 2013 2:36 PM, Nipael Mrutu <n_mrutu@hotmail.com> wrote:
 
Mimi sidhani kama watanzania ndio wanalengwa, ila ninacho ona kinatokea ni kwamba hali ya usalama nchini kenya ni tete, vitendo vya ujangili na ujambazi vimeshamiri wakati huo huo wana nchi wake (ninao wafahamu) wamekuwa wakilalamika kuhusu bidhaa kupanda bei na kufanya masiha kuwa magumu.

Sidhani kama kuna tofauti kubwa kati ya hali ya usalama Kenya na hali ya usalama Tanzania, vitendo vya ujangili, na mauajii pia kwentu Tanzania vimeongezeka, na kufanya wengi kulala usingizi wa mangamungamu.

Pamoja na hayo yote ni vyema uchunguzi ufanyike ili tupate jibu la uhakika kuhusu kinacho endelea. Balozi wa Tanzania nchini kenya natumai yuko mstari wa mbele katika zoezi la kufanikisha hili.  Hili litatusaidia tusije jenga chuki ambazo hazipo na kuingiza umoja wa nchi za Africa mashariki katika hali mbaya.


To: wanabidii@googlegroups.com; wanakenya@googlegroups.com; wanazuoni@yahoogroups.com; youngprofessionals_ke@googlegroups.com; wanataaluma@googlegroups.com
From: oldmoshi@gmail.com
Date: Mon, 25 Nov 2013 09:34:29 +0300
Subject: [Wanazuoni] MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WATANZANIA NCHINI KENYA

 

MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WATANZANIA NCHINI KENYA

Ndugu zangu ,

Kumekuwa na matukio ya kutisha dhidi ya raia wa watanzania wanaosoma , kuishi Kenya au kwenda tu kwa ajili ya safari zao mbalimbali za kikazi nchini humo matukio haya ni ya kutisha kama sio ya kuogofya na ukizingatia hali ilivyo afrika mashariki kwa sasa ya usalama ndio matukio haya yanaongezeka .

Binafsi niliwahi kupoteza ndugu yangu miaka 3 iliyopita kule Mombasa , huyu ndugu yangu alikuwa anaishi huko na wazazi wake kwenye biashara ya mahoteli basi wakamvizia usiku wakaenda wakanyonga mpaka leo kesi yake haijulikani ilivyoisha isha .

Wiki iliyopita kuna mtanzania ameuwawa kinyama alipokuwa anatoka kwenye ukumbi wa disko , kutokana na maelezo ya awali wanasema alishawasiliana na rafiki zake kwamba ndio anatoka ukumbini kurudi nyumbani lakini hakufika mpaka alipokuja kuokotwa akiwa ameshafariki dunia .

Weekend hii ya kuamkia leo kuna mtanzania amepatikana hospitali Fulani huko jijini Nairobi akiwa hajitambui kabisa ikagundulika ni daktari na mfanyakazi wa wizara ya afya huko Zanzibar mpaka naandika hivi mkewe ameshaenda huko lakini hajitambui inaonekana walimpiga na kitu kizito usoni upande wa jicho .Hatujui baada ya uhalifu huu wamemwibia taarifa gani au nini .

Inaonyesha watanzania wamekuwa target ya uhalifu wa kikenya haswa jijini Nairobi na Mombasa na muda wote huko serikali yetu kupitia balozi wetu huko Kenya hajawahi kutoa tamko lolote wala chochote hata hii habari ya huyu daktari pia watu wako kimya sijui wanataka sasa watu wafanye nini ? wajilinde wenyewe ?

Hali hii inanikumbusha kipindi Fulani wakati wa machafuko ya kibaguzi huko afrika kusini dhidi ya watu wasiokuwa raia wa afrika kusini , siku moja makundi ya vijana wa afrika kusini walikuwa wanaenda kuvamia kwenye sehemu walizokuwa wanakaa raia wa afrika magharibi haswa naigeria hawa jamaa wa naigeria walikuwa wamejiandaa na silaha zao bastoli , bunduki na nyingine mbalimbali wakawa wanawangoja hawa vijana wa zuma .

Wale vijana wa zuma kuona vile na jeshi la polisi kuona vile ndio mzozo ukaishia hapo .

Tusingependa itokee hivi kwa ndugu zetu na jirani zetu hapo Kenya pale ambapo watanzania watachoka kuumizwa na kuuwawa kwa kunyongwa kila mara .

Naomba serikali kupitia waziri mhusika wa mambo ya nje au wa afrika mashariki na balozi wetu hapo Kenya watoe tamko la kuhusu kile kinachoendelea huko Kenya na kuhakikishia watanzania hao usalama wao huko Kenya .

--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya


.

__,_._,___


0 comments:

Post a Comment