Waz,
Kuna Mz alijibu ujumbe wangu bila kunakili kwa wote, na nimeona
niwanakilie nilivyomjibu bila kuonyesha jina lake. Hii ni kwa sababu
inelekea kwake sikusomeka kama nilivyokusudia, na inawezekana ikawa hivi
kwa wengine. Hivyo nawatumia hii kuonyesha nilichomaanisha.
+++++++++
Mungu Ibariki Tanzania.
Nashukuru kwa majibu yako.
Kama nimesomeka nashutumu viongozi wote wa CCM au wa serikali, haikuwa nia
yangu hata kidogo. Natambua kuwa kuna watu wengi ndani ya CCM na
serikalini wenye nia nzuri na Taifa hili na ambao wanajitahidi sana
kuijenga kwa mwelekeo mzuri. Tume ya Katiba kwa sehemu kubwa ni viongozi
wakongwe wa CCM, na naamini maneno yako kuwa ndani ya chama na serikali
wapo waliochangia na kutetea mambo mazuri.
Lakini pia kuanzia mwanzo, kuna kila ishara kuwa kuna nguvu kubwa ya
wanaolinda maslahi ya muda mfupi na wana nguvu kubwa. Ndio maana hata
swala la kuandika katiba mpya lilikubalika kwa mbinde. Lengo lilikuwa
kuweka viraka hapa na pale. Hivyo wako miongoni mwetu (na si wachache)
ambao tunaangalia maslahi yetu ya muda mfupi.
Mimi mwenyewe siwezi inyoshea serikali kwa ujumla mkono wa lawama
kwa sababu nashirikishwa kwa kwenye baadhi ya mipango kama mshauri. Tuna
mifano ya wana TPN ambao wameteuliwa nafasi muhimu bila hata wao kugombea
uongozi - bila shaka ni kwa kuona wanavyoweza kuchangia uongozi mzuri na
tunapaswa kuwapa moyo watu kama yeye. Habari tulizozipata ni kwamba sasa
hivi hata wageni/wawekezaji wakifika Wizara ya Nishati na Madini
wanatembea na kuzungumza kwa adabu maana wanajua hakuna mchezo pale. Ila
hili halipaswi kutuzuia kutoa ushauri pale tunapoona kuna haja na ndio
maana mijadala ya TPN ina maana sana.
Ukweli ni kuwa mimi ni shabiki wa mfumo unaofaa/upinzani imara kuliko
chama. Kama ingekuwa nina uwezo, ningegawa CCM litokee kundi litakalotoa
ushindani wa kutosha kwa mwenzake. Na nitasikitika sana endapo itafika
siku chama kilichoko upinzani sasa kikashika madaraka na kukawa hakuna
upinzani imara. Tutakuwa hatujapiga hatua ya maana, maana tusidanganyike
kuwa viongozi wote wa upinzani wana nia njema na taifa au serikali yao
itakuwa haina madudu.
Ndivyo nilivyomaanisha!
% Rose,
%
% Hongera kwa mchango mkubwa unaotoa katika mjadala wa Katiba. Hatima ya
% vizazi vyetu na nchi yetu inategemea sana mfumo wa uongozi chini ya
% Katiba.
%
% Mahali popote, wananchi hufika mahali wakauchoka uongozi, hata kama
% matatizo yaliyopo hayatokani na uongozi ule. Katika dunia ya sasa na
% kesho, wananchi wakiona hawawezi kubadili uongozi kwa njia ya kura,
% wanabomoa. Kuwapa wananchi nafasi ya kubadili uongozi kwa njia halali na
% ya amani ni jambo ambalo sote, bila kujali itikadi zetu - tunatakiwa
% kulitafuta kwa kupitia katiba.
%
% Hii si kazi ya kuwaachia walioko kwenye upinzani leo! Wako watu wanasema,
% wapinzani tulio nao wenyewe wana maana basi? (Hata wakoloni walisema,
% wapigania uhuru wenyewe ndio hao?). Katika mjadala wa katiba, tusiangalie
% upinzani kama fulani na fulani. Tuiangalie kama sehemu muhimu ya mfumo
% ambapo Mtanzania yeyote, hata Waziri Mkuu wa sasa, anaweza akaja kujikuta
% humo. Jukumu la kuweka mazingira mazuri ya kujengeka upinzani imara si la
% upinzani peke yake. Ni letu wote.
%
% Katika mjadala wa katiba kuna watu wanaangalia karibu sana
% - maslahi yao ya sasa na jinsi ya kuhakikisha chama hakitoki madarakani.
% Ajabu katika hawa, wako wanataaluma wenzetu wengi.
%
% Nimeshangaa kwa nini TPN imekuwa kimya kabisa siku hizi?
%
% % ---------- Forwarded message ----------
% % From: Rosemary Mwakitwange <rosemarymwakitwange@gmail.com>
% % Date: Sat, Nov 9, 2013 at 8:50 AM
% % Subject:
% % To: Gaston Kikuwi <kikuwigg@gmail.com>
% %
% %
% % [image: Inline image 1]
% %
% % --
% % Rosemary Mwakitwange
% % *B.com (hons), MBA *
% % *Executive Chair*
% % East Africa Business & Media Training Institute
% % *P.O Box*: 5659
% % Dar Es Salaam, Tanzania
% % *Tel: *+255 222 602408
% % *Cel:*+255 717 190 856/755 019 284
% % *website*: www.eabmti.co.tz
% %
% %
% %
% % --
% % Rosemary Mwakitwange
% % *B.com (hons), MBA *
% % *Executive Chair*
% % East Africa Business & Media Training Institute
% % *P.O Box*: 5659
% % Dar Es Salaam, Tanzania
% % *Tel: *+255 222 602408
% % *Cel:*+255 717 190 856/755 019 284
% % *website*: www.eabmti.co.tz
% %
%
%
% --
% "Give your energy to things that give you energy.",
%
% "Learn enough to begin and then learn as you go."
%
%
% Dr. Donath R.Olomi
% Chief Executive Officer
% Institute of Management and Entrepreneurship Development (IMED)
% Mwalimu House 7th Floor, Ilala
% P.O. Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania E-mail: info@imedtz.org, website:
% www.imedtz.org
% Mobile +255-754-296660
%
% Publications available on the Internet
%
% http://www.repoa.or.tz/documents/RR_12-2.pdf
%
% http://www.businessenvironment.org/dyn/be/docs/31/BETanzania02.pdf
%
%
http://www.tanzaniagateway.org/docs/EnhancingSMEcontributiontoempandpovertyreduction.pdf
%
%
http://econpapers.repec.org/article/wsijecxxx/v_3a17_3ay_3a2009_3ai_3a01_3ap_3a103-125.htm
%
% http://www.fek.umu.se/forskning/pub/Business.Studies/babsonpaperversion.pdf
%
% http://www.sbaer.uca.edu/research/icsb/2011/763.pdf
%
% http://fusionmx.babson.edu/entrep/fer/babson2001/I/I-R/I-R/i-r.htm
%
% http://www.theigc.org/sites/default/files/EnterpriseMapofTanzania.pdf
%
%
--
"Give your energy to things that give you energy.",
"Learn enough to begin and then learn as you go."
Dr. Donath R.Olomi
Chief Executive Officer
Institute of Management and Entrepreneurship Development (IMED)
Mwalimu House 7th Floor, Ilala
P.O. Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania E-mail: info@imedtz.org, website:
www.imedtz.org
Mobile +255-754-296660
Publications available on the Internet
http://www.repoa.or.tz/documents/RR_12-2.pdf
http://www.businessenvironment.org/dyn/be/docs/31/BETanzania02.pdf
http://www.tanzaniagateway.org/docs/EnhancingSMEcontributiontoempandpovertyreduction.pdf
http://econpapers.repec.org/article/wsijecxxx/v_3a17_3ay_3a2009_3ai_3a01_3ap_3a103-125.htm
http://www.fek.umu.se/forskning/pub/Business.Studies/babsonpaperversion.pdf
http://www.sbaer.uca.edu/research/icsb/2011/763.pdf
http://fusionmx.babson.edu/entrep/fer/babson2001/I/I-R/I-R/i-r.htm
http://www.theigc.org/sites/default/files/EnterpriseMapofTanzania.pdf
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment