Ni vema kufahamu saikolojia ya Mbongoland kisha kuifanyia kazi ibadilike:
-Hupenda kulaumu ila utendaji kwake yeye mwenyewe pungufu. hapo ndio utaona desturi ya uchafuzi mazingira, kuunganisha bomba ta maji taka katika mtaro funikwa au wazi lakini hapo nje yake kuna sewerline hataki kuunganisha ili asilipie kodi ya majitaka anayozalisha au kuchangia uzoaji. atatuma masanduku ya taka kutupwa barabarani ili asichangie usafi shs 1000-5,000/= kwa mwezi kulinganisha na uzalishaji taka wake. Apange biashara barabarani Msimbazi kote na magari yashindwe kupita, alaumu serikali hata kama kuna soko la majinga, Ilala, Buguruni, mabibo, (20 manzese, tandale, Tegeta you name it na aandamane asilipe kodi. lawama tu. Mitaro ya ubungo mikukwa kiasi gani for stormwater drainage na imejaa uchafu wa mganga njaa kiwango gani?
-Akalete maembe Mombasa, sudan, asiende Mtwara, Lindi, Ulanga, Kilosa, tabora, Mkuranga yanakooza. Akalete samaki China zilizooza lakini asiende Mafia ambako Samaki hazina soko, ndio kwasa gati na bandari zimejengwa lakini kuna boat na ngalawa kubwa mchuuzi asiende kuleta toka Mafia ila alete mbovu zinakuja kuangamizwa tunaangalia. Ikifika jioni wauzaji maziwa Mafia Island huyamwaga-hayana soko. lakini tunaletewa na wafanyabiashara maziwa toka China ambayo yanaprotein ya plastic inayoua.
-Mheshimiwa anasifika kwa ufisadi au kaingia biashara za hasara serikalini-kesi mahakamani na sifa za ufisadi-huyo atapokewa kwa shangwe jimboni kwake, watampigia KURA atashinda na kila kona watamkaribisha kufungua kikao, sherehe hii na ile kuchangia hiki na kile-kisha kulalama na ufisadi. Cheza na mbongo wewe!! Hata mbakaji atatetewa atoke kama innocent; muuaji atawekewa dhamana na wakili na amekamatwa vitu vya marehemu vilivyoibwa. Unataka nini tena kesi ichukue miaka? Mfungwa au jambazi aliyepewa hukumu akae jela miaka saba, leo anakamatwa katika team ya majambazi wauaji na police wanamtambua yeye na wenzake-ametokaje jela kabla ya kifungo kuisha (katolewa kijanja wakati wa Msamaha wa Rais kwa wafungwa, ndugu wamehonga hela)-Cheza na Mbongoland wewe-mtendaji yeye na mlaumu yeye!! haki gani anaitaka anapomtoa mhalifu jela kijanja na kumtetea mume, ndugu mbakaji, muuaji albino, mkataji viganja, mleta mali mbovu-
atasifia Kenya, China (ambako atanyongwa) na akikamatwa huko kwa madawa ya kulevya atataka serikali imtetee.
-haki gani za binadamu wakati topic ya gazeti ni tofauti na andiko lililo ndani lakini topic inahamasisha kitu fulani cha chungi au ushabiki utakaoleta madhara. halafu ndio vyombo vya kuelimisha jamii ambavyo vinadai haki huku vinahamasisha chuki. Ona kesi ya Kapuya binti anavyoonyeshwa kuwa tapeli. Vitoto vinakwenda kubakwa kuanzia 2012 na kimoja kinasimama kumwambia mwenzake avumilie mchungaji atawapa hela ya matumizi. unabakwa kwa kwenda mwenyewe daily, unajua ni uovu, husemi nyumbani ila unaendelea mpaka mnagombana wenyewe ndio siri inatoka!! Useseme home au kwa mwalimu au unayemwona msiri wako-kisha tutaweka dhamana, mbakaji atoke na huku tunasali bsana. Amwagiaye watu tindikali mjomba; aliyejaza magari na pikipiki za wizi-mume, ndugu, baba; mwenye danguro auzae vitoto vichanga na wasenge-mama, shangazi, bibi na tunamuangalia-Serikali ina macho ya kinyonga? Tunaona hatuoni na tunaweka siri kwa kuogopana au bora mkono uende tumboni?
-Video za matusi majumbani, vijijini kibao watoto wanaangalia-kuganga njaa!! Kisha kulaumu 'Serikali'. Mbona mabonde ya kilimo mengi, mashamba estate za GVt hazilimwi watu wanavamia na kujenga, kuuza ya kibao (easy come, easy go).
Kwa nini matajiri pamoja na investment kwende viwanda vya soda, viwanja vya mpira, kusaidia development groups kwa capital- wasijiunge kutengeneza a National/international company; wakachukua former GVt estate farms kuzalisha mazao na kutoa ajira kwa vijana kwa kujenga nyumba za vijana wakakae walime, weka malori ya kusafirisha mazao well packaged, kuwaekea huko kiwanja cha mkichezo, canteen, TV room etc-Serikali mbaya. Ila akija mchina kuwekeza huko-tunavamia tunadai haki. Tunaisifu kenya yenye private land tenure sio hapa customary 50% plus ambapo una hata uhuru wa kulima utakacho. Ila tija ni kufyeka misitu kuuza mkaa mbao; kuzurula na mifugo (biogas inatembea haitumiki kama alternative energy) na mapigano yasiyoisha, kusababisha food insecurity na vilema sisi wenyewe; kila mtu akae kwake atumie resources sustainably while considering caring capacity ya ardhi-tatizo. Ila Kenya, Uganda etc tunakokusifia hawaruhusu haya. Na ndio maana hata mifugo yao wanaileta kwetu sisi WAJINGA, tunawapokea, tunawapa ardhi, wanatutuma kukata miti tunakata kama vibarua-kisha tunalalamika 'Wageni wameingia wanatunyanyasa!!' Hebu nenda Moshi na Upareni uone kama utaingiza hata mfugo wako mwenyewe shambani kwako au kwa mwenzako. lakini ukifika Kilombero, Kilosa, Ngerengere, Ruvu donor financed irrigated farms, Kilwa, Mkuranga-ingiza, lishia, piga, kata mikono akifukuza ng'ombe asile mahindi-akale wapi? Kisha-SERIKALI.
-Media/Blogi zinamuonyesha kiongozi Uchi kwa kutumia ICT-ni utamaduni wa kabila lipi la Afrika na ndio haki dani hiyo ktk utandawazi na kulinda utamaduni wetu. Tupo tunaojipeleka kwa viongozi tunaowalaumu kumsifu ili ujipatie mafao au cheo-wewe nawe ufanyweje.
-Una uhuru wa dance unapata jukwaani unavua nguo-suruali chini chupi nje, kukata viouno matusi ya nguoni-serikali ikiamua mkamatwe muwekwe ndani mnaofanya hivyo kuiga utamaduni wa kigeni-hakuna haki, lawama. Ila mnaaibisha taifa na vyombo husika pamoja na NGOs vinakula jiwe kwa kuogopa lawama.
-Vijana wadogo wasomi nao vibaka kisha lawama nchi mbaya-mbagala nyumba iliofanyiwa valuation 30million unampa mzee kibabu au kibibi 30,000/= una utu gani? unatumia uzee na ufahamu wake mdogo kumdhulumu? Utalaumu nani-kipato duni? Malezi duni-uduni wako ukutie huruma kwa mtu duni kama wewe sio kumdhulumu.
-Fika chuo vitoavyo degree uone kama kuna kijana msomi wa hapo anayefanya kazi ya kupata kipato hapo cafeteria, library ili apate hela za ada. Hawezi na akimaliza shule harudi nyumbani. Ni mfano mmoja tu mzuri genge la Survey area darajani lilianzishwa na kijana akajilipia ada, akaosomesha nduguze na akaongeza lingine near mlimani city na sasa anasomea PhD. na hata ukifika vyuo vya masomo na degree za kodi-utakuta canteen, secretarial services, maduka yaliopo hapo chuoni oposite school of commerce hayana mashine za kodi wala hayatoi risiti kwa mauzo yoyote. Ukifika school of medicine and public health engineering-ndio vyoo vinakofurika. Construction engineering-ndio ceiling board za engineering lab zinakoning'ingia na kudondoka na ngazi zote chuoni zimebomoka ukikanyaga uwe mwangalifu utadondoka tu.Ni kutokana na kutokupenda kuchezea uchafu wa kuchanganya zege na kujenga kwa mfano na kwa mazoezi na mfano ni hapo shuleni vyoo visifurike na ngazi zote kubomoka bila ya fungu la consultancies kuingia katika practical training kufanya repair katika mazingira ya chuo cha degree za ujenzi. Ukiwalimisha shule wazazi watasema wanaonewa, ukiwalazimisha waingie vumbini-uonevu. Akiwa manager-hashiki vumbi hata akifungua mradi, kuweka jiwe la msingi mahala-anawekewa mkeka wa kupigia magoti akipanda mti au kuchanganya zege. Hili ndio taifa letu. Ila Mchina-manager ni dreva, ni kuli wa kupakia mchanga, ni desk worker pia kavaa overall gown. wetu sisi wananenepa tu na hata brief case abebewe na mlango wa gari afunguliwe. Wengine ni vijana hasa-Lawama ni kwetu sote tunavyokilea ktk uzembe.
-Tuna vilema wa kila aina-design ya wasanifu majengo mbona hawaangilii mahitaji ya vilema hawa ktk kuingia na kupanda majengo. kama ni barabara ya kupita na miguu vilena na wengineo-mbona wananchi mijini wanapanga biashara na wakiondolewa wanaleta zari. Huko pia wanapitisha pikipiki na bajaji. Vituo vya basi ndio pale pa kukaa watu wanapanga biashara na sahani za kuuza chakula. Waondoe wakupige mawe. lakini wanauwezo wa kuungana, kuchukua mkopo SACCOS yao, VICOBA, Bank kujenga restaurant ya kigenge chao. Mbongo-haiingii akilini suala hili. Kuungana ni tatizo vyama kudumu kwani kila mtu anataka uongozi ili afaidike binafsi-Wote ni inherently mafisadi au fisadi watarajiwa.
-Wangapi wa indigenous minority groups wamepewa favours kwenda nje kusoma lakini lakini hawakurudi kubosha maisha ktk jamii zao. Wamebaki huko-wameoa wazungu akija bongo mara moja moja tu. Nafasi haitumiki vizuri na mzungu hataki extended family issues. Sasa kupata ardhi nchini wageni wameona bora KUOA. Nasi tunataka dual citizenship-tutakuja kuuzaardhi. bado yapo mashamba ya wakoloni wajukuu zao wanarudi sasa kuyalima, tutamezwa zaidi. Absentee land Lords kibao-Kaangalie mashamba makubwa ya Minazi Lindi na Bagamoyo na maeneo mengine-waliokaa hapo wazalendo masuria ni walinzi tu, wenyewe wapo Oman, Dubai maana nao ni watanzania. Dual citizenship itatumalizia ardhi.
-Walionje si nao waanzishe a multinational company waje wachimbe Gas; au kuanzisha A Development Fund kama ya Bill and Melinda gates kuleta maendeleo mikoa na wilaya vijiji vyao. Lawama bila matendo inasaidia nini? Kwanza wengi ya walio nje wanafanya kazi duni sio professional work. Una degree unafagia mabweni pamoja na kuwa mshahara ni mkubwa.
-Inapokuja mob ya wananchi na mawe ambao wanaoondolewa barabarani kuuza bidhaa; au, kutaka kupora lori lililoanguka polisi mwenye silaha atajihami daima. Tunaona hii inatokea nchi nyingi duniani na raia na polisi hufa. Kwa nini iwe ngeni TZ? Inafika eneo limepimwa viwanja na kuwekwa miundo mbinu, lakini wananchi wameziba kila kona na kuweka biashara, mapishi yanayotumia moto kila nyumba na kuna mabanano wa nyumba. Moto ukiwaka fire car ikija haina pa kupina. Miundombinu ya mambomba ya fire brigade tumeng'oa mabomba, maji kupata tabu; foleni ya magari kutokana na njia nyingi za mkato kuzibwa na structures na familia zenye gari kila mmoja kutoka na gari waonekane hivyo foleni ni kubwa hata gari la zimamoto kuchelewa inakuwa kawaida. Ila, wamepika na moto kila barasa wenyewe bila kuzingatia tahadhari, watarusha mawe kuvunja gari eti usalama wa Raia haujaliwi-raia yupi ambaye mtaa mzima unawaka moto kila baraza. Kujenga kwenye wayleave ya barabara ambapo ukiangalia majengo ya GVT yapo mbali na barabara hata wakibomoa kupanua barabara hayaguswi. Unayaona Morogoro, bagamoyo road yapo mbali na njia-wamezingatia sheria-wewe unalitafuta mwenyewe kisha unaitukana serikali. Hata unapopanga biashara barabarani kisha Straabag lorry linapina na greda kubomoa njia/kufanyakazi yake na wewe upo unapika njiani hapo na kuuza biashara katikati ya njia-upuuzi huu huuoni ila unaona GVT ndio mbaya. Umeuziwa ekari moha au nusu eka ya GVT plots na Mzee Mkapa kupunguza gharama za majengo na umeuziwa gari ili uje kazini. Gari ni ya kukodisha, bado ubebwe na ya GVT peke yako toka Tegeta, Bunju hadi Posta. Plot umejenga 100% majengo mbanano ya ghorofa beyond estimate za maji na umeme unaongeza mzigo wa utilities. hapo unapangisha kwa $ na shule imo humo interational; unajaza mifugo unamaliza maji vijijini mito ya kukupa umeme inakauka. Wanao wanasoma malaysia na hao ni wasomi wanaojua masuala ya environment lakini baba ndio mkiukaji mkuu. Bongoland ndio hii-tunajimaliza wenyewe na kisha kuilaumu serikali.
Tuitukane tu nchi yetu lakini wapo wanaoinyemelea kutaka ardhi na hiyo Gas. Kama hatutaleta cultural revolution sasa kubadili mitazamo yetu na kufanya kweli ktk kuzalisha mali, kuunda kampuni za kujiajiri na kuajiri vijana kufaidika na gas, madini na natural resource kwa kuwekeza wenyewe-tutarudi ukoloni mambo leo, tutatawaliwa na kuajiriwa na makampuni toka Kenya, Uganda, Nigeria, Rwanda (hata kama tuna ugomvi nae mbona wamo) na nchi nyinginezo. Akina Mh Mengi, Abood, Bakhresa, Hood, matajiri wa madini na malori, viwanda walioni hili wagangamale. Huko ndiko yatima watapata ajira na SACCOS za wakulina na wafugaji, wavuvu, VICOBA vitapata soko la kuuza bidhaa zao.
Hata aje Rais mwenye mikono ya pweza na macho ya kinyonga yanayozunguka degree 360 na kuona kila kona-bila kubadilika kisaikolojia ktk mitazamo yetu kuondoa uswahili mentality-hatufiki popote.
On Saturday, 23 November 2013, 19:37, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:
Heri,
Umeniwahi. Asante sana.
em
Umeniwahi. Asante sana.
em
2013/11/23 heri rashid <herirashid@yahoo.com>
Rushwa.UfisadiKutetea maovu ya wakubwa.Hata tukiwa wazalendo kiasi gani ni vigumu kutetea mambo haya na mengine.Ni mambo ambayo hayakubaliki!
On Saturday, November 23, 2013 7:08 PM, ananilea nkya <ananilea_nkya@yahoo.com> wrote:
--Hapa Rais wetu kasema vizuri-tuitangaze vema nchi yetu. Hakikamuhimu kila mmoja wetu aipende nchi yetu kwa moyo wote.Lakini pia kulinda heshima ya nchi yetu katika uso wa mataifa watawala wetu wawe waangalifu kuhakikisha kuwa kiwango cha uvunjaji wa haki za binadamu nchini kinadhibitiwa, maana matukio hayo kwa mfano Dr Sengondo Mvungi, Mhadhiri wa wa sheria Chuo Kikuu kuuwawa kikatili kwa mapanga, Daudi Mwangosi kuuwawa na polisi mchana kweupe, matukio hayo yanasambaa kama moto wa nyika katika zama hizi ya mawasiliano huru na hivyo kuiweka nchi yetu katika kundi la nchi chache ovu duniani.Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.comFrom: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, November 23, 2013 3:29 PM
Subject: [wanabidii] Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu, Rais Kikwete awaambia Watanzania
--TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Watanzania waishio nje Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema wajibu mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri, kuihangaikia na kuitetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wakiiponda, kuibeza na kulalamika.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kuishi kwa Watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazozipata ugenini kusaidia kubadilisha hali na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania.
Rais Kikwete pia amewaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za
kigeni kupita kiasi.
Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Watanzania waishio nchini Poland usiku wa jana, Alhamisi, Novemba 21, 2013, kwenye Hoteli ya Bristol mjini Warsaw ambako alifikia wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Poland.
Aliwaambia Watanzania hao na familia zao: "Matumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea
vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yenu, mtaihangaikia nchi na kuleta faida nyumbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi
yenu mnaweza kuishi hapa na kazi yenu ikawa ni kushinda kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya,
viongozi hawafai..mnapata faida gani. Mnazo nchi ngapi?"
Aliongeza Rais Kikwete: "Kuhangaikia nchi yetu ni wajibu wenu ambao hamwezi kuukwepa. Matumaini yetu ni kwamba
mtasukuma mbele maslahi ya nchi yenu, mtatetea ustawi wa nchi yenu na ndugu zenu. Fursa zilizoko hapa mnazijua
wenyewe, sisi hatuzijui. Nyie ndio mnaishi hapa, sisi tuko mbali na hatuwezi sisi kutegemewa na kutarajiwa tufanye
mambo ya hapa ambayo hatuyajui."
Alisisitiza Rais Kikwete: "Mbona kazi za ma-Ngo's mnazifanya vizuri bila kusukumwa ama kushawishiwa lakini
kazi za kusaidia ndugu zenu hamfanyi? Kama hata hamwezi kusaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu?"
Rais amesema kuwa kwa Watanzania waishio nje kuonekana wanajali na kutetea nchi yao kutasaidia kujenga hoja ya msingi kuhusu umuhimu wa kuanzishwa kwa uraia pacha (dual citizenship) ambao Watanzania waishio nje wanaulilia. "Mnaweza kuhalalisha hoja ya uraia pacha kwa kuwa watu wenye faida kwa nchi."
Kuhusu ombi lao la uraia pacha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Watanzania waishio nje kuongeza kasi ya kuchangia mjadala kuhusu suala hilo ili likubaliwe kuingizwa kwenye Katiba Mpya.
"Rasimu ya kwanza ya Katiba ililikataa jambo hilo kwa sababu hili ni jambo lisilokuwa na ushabiki na upenzi mwingi
nyumbani. Ujumbe wangu kwenu ni jipangeni vizuri kutetea hoja yenu hii. Saidieni mjadala wa jambo hilo badala ya
kushinda kwenye mablogu mkijadili siasa na hivyo kusahau yenye maslahi kwenu."
Kuhusu kuiga tamaduni za nchi nyingine na kusahau za nyumbani, Rais Kikwete aliwaambia kuwa inaelekea kuwa baadhi
wachache wanaoishi nje ya nchi, wamejichanganya na kuchanganyikiwa kiasi cha kusahau mambo ya kwao.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa Watanzania kudai kuwa suala zima la mahari limepitwa na wakati na kuwa kutoa mahari ni sawa ni kuwauza watoto wa kike.
Rais ambaye alionyesha kushangazwa na kauli hiyo, alijibu: "Msiige mambo ya kigeni kiasi cha kuanza kuchanganyikiwa."
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Novemba, 2013
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment