Monday, 11 November 2013

Re: [wanabidii] Maelezo ya Kitila Mkumbo kuhusu “Taarifa ya siri ya CHADEMA”

Ukichunguza kwa kina nadhani kuna haja ya kuliangalia jambo hili kwa mtazamo mpana zaidi kwani tuhuma hizi ni nzito sana.chadema makao makuu mna kila sababu ya kujiangalia upya bila shaka ninyi si wamoja na humo ndani kuna sumu baridi inayoweza kuuwa taratibu kabisa.Me nakubaliana na Dr Mkumbo kuwa ndani ya chama ambacho si tawala kuna siri gani za kununuliwa kwa bilioni mbili ?

Rgrds
Magora

On Nov 11, 2013 12:49 PM, "Juma Mzuri" <jumamzuri@gmail.com> wrote:
ni vema kama Dr. Kitila kwenye hili tamko lake angetuambia kama alishawahi kufanya mawasiliano na idara ya habari na uenezi ya chama na kueleza kile walichomjibu ili hata kama ni lawama basi yeye awepo kwenye upande salama kwa kuzingatia utaratibu pamoja na itifiki ya kichama, ila hii ya kuingia moja kwa moja kwenye vita ya mtandaoni (kuchafuana) sidhani kama na yeye atakuwa salama, kwa sababu ukiufuatilia kwa makini huu mgogoro ni kama kuna hila/njama/hujuma za kutaka kuwadhoofisha watu na au kikundi cha watu flani kwa makusudi na kama hao watu/hicho kikundi cha watu hakitakuwa makini zaidi basi malengo/ dhamira yao ovu itafanikiwa tena kwa kiasi kikubwa, so ni vema kama dr.kitila angelitazama hili kwa undani na athari zake kwake na chama chake kabla ya kukimbilia mitandaoni japo ilikuwa ni muhimu sisi tujue amelichukuliaje hili

On Monday, November 11, 2013 12:01:52 PM UTC+3, paul lawala wrote:
Kwa jinsi ile taarifa ilvyokaa kama ni uongo basi kuna watu ni wazuri wa kutunga uongo,mbaya zaidi inaonekana imetoka makao makuu ya CHADEMA

2013/11/11 Francis Kasili <Francis...@nmbtz.com>

Big up Kitila, Kweli I admire this stand. Tunahitaji watanzania wazalendo namna hii pasipo kujali maslahi makubwa ya kipesa bali mapambano dhidi ya ufedhuli wa mafisadi lazima yaendelee na kutokomeza ukandamizaji wowote and wizi unaoangamiza taifa at any cost. 

God bless you Kitila and all Patriotic Tanzanians.

Regards

F.Kasili

Mob: 0784850583 or 0755850583

Always darkness will never comprehend light

From: wana...@googlegroups.com [wana...@googlegroups.com] on behalf of Abdalah Hamis [hami...@gmail.com]
Sent: Monday, November 11, 2013 11:11 AM
To: Wanabidii
Subject: [wanabidii] Maelezo ya Kitila Mkumbo kuhusu "Taarifa ya siri ya CHADEMA"

Kufuatia taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuhongwa kwa Zitto naye kuhonga watu wengine, nikiwemo mimi, ili kutoa siri za chama chetu (CHADEMA) kwa lengo ya kukivuraga watu, wengi sana wameniandikia email, sms na hapa fb ili nitoe ufafanuzi kuhusu ukweli wa mimi kuhongwa na Zitto na mahusiano yangu na mwanasiasa huyu nguli. 

Mwanzoni nilipuuzia na sikutaka kabisa nitoe maoni kuhusu jambo hili kutokana na kiwango cha ujinga kilichomo ndani ya waraka huo unaosambazwa. Hata hivyo kwa kuwa watu wengi wamenitaka nitoe ufafanuzi, napenda kueleza haya yafuatayo:
i) Mimi Kitila Mkumbo, pamoja na umaskini wangu, sijawahi kuhongwa popote na sitarajii kuhongwa. Taarifa zinazosambazwa juu yangu ni za uwongo wa kijinga na uzushi wa kitoto kwa malengo ya siasa nyepesi. Ni wazi kwamba wanaosambaza habari chafu juu yangu hawanijui na ndiyo maana wanaweza kudiriki kuzusha kwamba mie Kitila Mkumbo naweza kuhongwa sh. 200,000/=. Hakuna namna nyingine ya kuthibitisha kwamba waraka huu na maudhui yake ni mambo ya kutunga zaidi ya hilo la kuzusha kwamba nami ni miongoni mwa watu waliohongwa. 

ii) Kuhusu mahusiano yangu na Zitto ni kwamba kijana huyu ni rafiki yangu wa miaka mingi tuliyejuana na kuanza urafiki kabla ya hata mie kuijua CHADEMA. Urafiki wetu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo ndani na/au nje ya siasa. Wasiopenda hili poleni sana. Mie ni mtu mzima na hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kunichagulia marafiki na/au maadui. 

iii) Wanaosambaza waraka huu ni watu woga wa demokrasia na wasioijua CHADEMA. Chama hiki kimejipambanua kwa miaka mingi kwamba ni chama kinachopigania demokrasia ndani na nje ya chama. Matatizo yetu hushughulikiwa kikamilifu ndani ya vikao ambapo huwa tunajadili mambo kwa upana. Watu wenye makosa husutwa, huonywa na ikibidi huadhibiwa. Kama kweli haya yanayosambazwa yangekuwa na hata chembe ya ukweli, na kama kweli waraka huu umetoka makao makuu ya chama, sioni ni kwa nini jambo hili zito kiasi hiki haliletwi kwenye vikao vya chama na sisi tunaotuhumiwa kukivuruga chama tushughulikiwe kwa mujibu wa taratibu kama ambavyo watu wengi wamewahi kushughulikiwa ndani ya chama chetu kwa makosa waliyotenda. 

iv) Ni vizuri tukajenga utamaduni wa kuhoji mambo badala ya kuyameza kana kwamba tunasoma msaafu. Hivi huyo mtu anayemhonga Zitto bilioni mbili (2,000,000,000) ili atoe siri za chama, ni siri gani hizo ambacho chama cha siasa kinazo ambazo ni za hatari hata itolewe hongo kama hiyo? 

v) Ninasikitishwa na idara ya uenezi wa chama chetu kukaa kimya bila kutoa maelezo juu ya jambo hili, hasa pale ambapo tumeambiwa waraka huu umetoka makao makuu. Hii si kawaida kwa idara yetu hii nyeti iliyosheheni watu mahiri. Mara zote huwa wepesi kabisa kwa vijana wetu katika idara hii kutoa ufafanuzi, tena kwa mambo mepesi kabisa yanayokigusa chama, vipi makamanda kwenye jambo hili imekuwaje?

v) Mwisho kama kuna watu walidhani kwamba kwa uzushi huu watanikatisha tamaa na kunirudisha nyuma katika kutoa mchango wangu wa kuimarisha siasa ya vyama vingi hapa nchini, na kuijenga CHADEMA kama chama mbadala imara wamekosea. Nipo imara na nitaendelea kutoa mchango wangu kikamilifu. Poleni sana wote mliokwazwa na jambo na ufafanuzi wangu ndio huo.

--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
*************************************************************************************** *************************************************************************************** This e-mail and any attachments are proprietary to NMB PLC. Any unauthorized use or interception is illegal. The views and opinions expressed are those of the sender, unless clearly stated as being those of NMB PLC. This e-mail is only addressed to the addressee and NMB PLC shall not be responsible for any further publication of the contents of this e-mail. If this e-mail is not addressed to you, you may not copy, distribute or disclose the contents to anyone nor act on its contents. If you received this in error, please inform the sender and delete this e-mail from your computer.

--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

0 comments:

Post a Comment