| Ndugu Watanzania sasa umefika wakati kila mtu ajue CCM hawajatulia na wala hawajui kuwa nchi ni ya Watanzania wote wanadhanishia nchi ni mali yao. Mimi nadhani kila Mtanzania anayo haki ya kikatiba kuwa Kiongozi wa Nyumba kumi, Tawi, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, na hata kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ukiona wa Zanzibari wanachachamaa kujitenga ni kwa ajili ya uovu unaofanyika bara. Mbona enzi za Karume na Mwalimu Nyerere hakuna Muunguja au Mpemba alikuwa anataka kuuvunja Muungano.
Leo hawa wanaotaka Muungano uvunjike wamezaliwa toka nchi gani si kwa sababu ya kuona hawafaidiki na utawala mbovu uliopo madarakani. Unguja na Pemba hakuna Mafisadi huku Bara tunawafuga wa kazi gani?. Unguja na Pemba hakuna wala Rushwa watajeni kama wapo sasa bara tunaendekeza Rushwa kuanzia Ikulu mpaka kwenye shina. Au mnataka kuniambia Dr Shein anakula rushwa au ni Fisadi. Sasa huwa najiuliza hawa ndugu zangu wa CCM tuliowakabidhi nchi tutawahoji lipi kati ya haya yafuatayo. Hata tukiwahoji tutegemee majibu gani haswa kutoka kwao. Majibu dhahiri au majibu ya siasa?. -Rushwa katika kila sekta wao -Kutorosha fedha nje wao -Ufisadi wao -Wizi wa mali za Umma wao -Kujiuzia viwanda wao -Kujiuzia mashirika ya umma wao -Kujiuzia nyumba za umma wao -Kuuza magogo nje ya nchi wao -Kuuza ndege wanaotuamsha alfajiri tukasali nba kuswali wao -Kuuza Vitalu vya uwindaji wao -Kuuza Wanyama nje ya nchi wao -Mikataba mibovu ya madini wao -Kusafirisha madawa ya kulevya wao -Kuua shirika la ndege Tanzania wao -Kuua shirika la reli Tanzania wao -Kuuza pembe za ndovu wao -Kuua Faru kule Serengeti wao -Kamilikisha ardhi kwa wageni wao -Kuua Elimu na mashule Tanzania wao -Kusababisha migogoro ya mipaka na majirani zetu wao -Kupunguza ajira nchini wao -Kuzuia uhuru wa vyombo vya habari wao -Udini na Ukabila wao -Kuua michezo Tanzania wao -Kuua Kilimo cha mazao ya biashara wao -Kumilikisha viwanda kwa wageni wao -Kijilipa mishahara minono wao -Kulimbikizia vyeo vikubwa vikubwa wao -Kujilipa mara mbili mbili wao -Kuua Demokrasia nchini wao -Kuwaua wapinzani wao -Madeni makubwa ya nje wao -Kuwasingizia watu makosa wao Ndugu Watanzania naombeni mnisaidie kutaja maovu ya hawa watu wa CCM mimi hata nashikwa na hasira. Mtu anadiriki kusema sentensi za kejeli kwa Watanzania walio na elimu. Eti Shehe wa Msikiti, au Mchungaji wa Kanisa au Askofu akishikwa amebaka je waumini mtaacha kwenda kusali, kuswali au mnachagua mtu mwingine kuendesha ibada?. Huyo ni Mzee tena mheshimiwa Steven Wassira. Mwingine anashika kidedea Watanzania tuchangie Elimu sawa hatukatai lakini je tukichanga mkazila itakuaje?. Mama Mary Nagu sio hatutaki kuchangia elimu Tanzania ila tukueleze wazi hatuna imani na nyie?. Tunahofia hata hizi 1,000/= zetu tukichanga mtazila.
Watanzania tuendelee kuwaangali mkibaka nchi kwa kuwa mnapokezana vijiti?. Mchanga wa madini unapakiliwa kwenda kuchambuliwa Canada sisi tuwaangalie tu. Twiga, Simba, Punda Milia, Chui, Duma, wanapakiliwa kwenye ndege tuwaangalie tu, Meno ya Tembo yanapakiliwa kwenda nje na kukamatwa Ulaya tuwaangalie tu. Nyie bandarini na Airport kinawashinda nini kuzikamata. Au wenzenu wanatumia uchawi kukamata?. Au mazingaumbwe?. Mnataka watoto wetu na wajukuu wetu tuwarithishe kitu gani?. Yani mnataka wasikute kitu si ndio. Tukubali siasa zenu majukwaani. za ubakaji kila siku kwa kuwa sisi tumekuwa Mazuzu ama?. Tumevumila tumechoka. Ubakaji wenu sasa umefikia kikomo. Mkereketwa. Lengai Ole Letipipi |
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment