Sunday, 18 November 2012

Re: [wanabidii] MPIGANIA UKOMBOZI WA KWELI Ndg. MAKWETTA AFARIKI DUNIA

Prof. Lwaitama na Wote Mlioguswa na Msiba huu mkubwa!!!

Kwetu sisi, Wapigania Ukombozi na wapenda Mabadiliko, na Maendeleo tumepata PIGO KUBWA kuondokewa na mtetezi wa Elimu ya Ukombozi kupitia katika Lugha ya Kiswahili.

Kama ulivyosema kwa usahihi, Mwalimu Nyerere alipounda tume hiyo chini ya Ndg. Jackson Makweta, alitarajia kuwa matokeo ya utafiti wa tume hiyo, yatainufaisha Tanzania na kuiletea mabadiliko.
Hakuna kitu kilichomsononesha Waziri Makweta, kama kudharauliwa kwa matokeo ya utafiti wake huo (kulikofanywa kwa makusudi na mtu aliyepewa dhamana ya kuupitia na kutoa ushauri wa kitaalamu)

Katika makala aliyoiandika mwishoni mwa mwaka jana ili kuiwasilisha katika Mkutano ulioandaliwa na Haki Elimu na Shule Kuu ya Eimu hapa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Ulifanyika katika Ukumbi wa Mihadhara Yombo), Mzee Makweta alisema maneno ya uchungu kabisa kuhusiana na mwenendo wa Elimu Tanzania na jinsi ambavyo mawazo yake yalipuuzwa na kusababisha mporomoko huu wote. Hakuweza kuwepo kuiwasilisha mwenyewe, lakini makala ilitumwa kwa waandaaji na kutolewa hadharani.

NITAITAFUTA NA KUIWEKA MAKALA YAKE YOTE katika Mtandao huu.

(Dr. Mkumbo ukiwa unayo unaweza kuiweka pia maana wewe ulikuwa mmoja wa waandaaji wa mkutano huo)

Katika makala hiyo naomba sasa ninukuu mistari michache aliyoiandika kwa uchungu mwishoni mwa makala hiyo:

"...sasa ninakubaliana na Karl Max aliyesema kuwa "utumiaji nguvu, ni mkunga wa kila jamii iliyo na mimba ambapo ni lazima mtoto azaliwe... [katika hali hiyo] nguvu hiyo ni ile ya kiuchumi....  inafikia wakati uamuzi mgumu ni lazima ufanyike katika maisha ya mjamzito ambaye muda wa kujifungua umefika, na yeye hajifungui, kinachofuata ni upasuaji, ili kuokoa maisha ama yake na mtoto au yake mwenyewe.... Wakati kama huu, umefika kwa Tanzania sasa, ikiwa tunataka kuwa na maendeleo ya kweli ....."  Mwisho wa kunukuu.

Kwa mkosi mkubwa, mawazo ya Ndg. Makweta kuhusu elimu YALIPINGWA NA PROFESA MMOJA WA ELIMU  ambaye KWA SABABU ZA UBINAFSI NA ZA KUPATA PESA, alionesha kuwa kungelikuwa na matokeo tofauti ikiwa mawazo ya Mzee  Makweta yangelifuatwa. BAADAYE PROFESA HUYO ALIITWA MSALITI WA UMMA WA WATANZANIA - jambo ambalo hajaweza kukanusha hadi leo. Huu ulikuwa mkosi. Na katika makala hiyo, Mzee Makweta anaandika kwa kusononeka kuwa hakuona ni kwanini utafiti wake ulipingwa bila kuonesha mawazo mbadala wa maendeleo ya elimu Tanzania.

Wanaojua kisa hiki, wanaelewa ninachokiandika.

Mungu amlaze Mzee Makweta mahali pa raha ya kiroho. Ajue kuwa bado kuna baadhi ya watu - na labda ni wengi, ambao wanayaenzi, kuyaheshimu na kuyapigania mawazo yake kuhusu elimu ya ukombozi.

Aldin

Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
Mkurugenzi                                                  Director
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day time-Office)
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>

From: Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, November 18, 2012 10:39 AM
Subject: RE: [wanabidii] MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA

Ulale Panapostahili Mzee Makweta,
Labda sasa watu watasoma Ripoti ya Makweta ya 1982 iliyopendekeza kutumia Lugha ya Kiswahili kama  Lugha ya Kufundishia masomo yote  tangu elimu ya wali hadi chuo kikuu huku Kiingereza kikifundishwa vizuri kama somo kwenye Taasisi ya Lugha za Kigeni ( Institute of Foreign Languages) na matawi yake nchi nzima...Ripoti ilipuuzwa na leo tunavuna matunda ya ukaidi huu dhidi ya kazi nzuri ya utafiti wa miaka miwili uliyoisimamia vizuri. Mimi nitakukumbuka pia kwa sura yangu kufaninishawa na  ya kwako!!!Ulale Panapostahili Mzee Makweta!! Nabubujikwa na machozi nikiona jinsi mfumo  wa elimu wa enzi zako  ulivyovurugwa na wanasisa wenye kutojali matokeo ya kutowekeza vyakutosha katika elimu  na kung'ang'ania  sera ya lugha ya kufundishia  ya kimamuluki inayofuatwa sasa ya kudhani eti eleimu ni kujua Kiingereza  tu basi....matokeo  ambayo kati ya viashiria vyake ni wahitimu mbumbu mzungu wa reli wa amabo  yote ya kisayansi wenye imani potovu za kishirikina kama zilivyojitokeza  katika  matukio ya Mbangala  yaliyozaa kuchomwa moto  makanisa...Mfumo  wa  elimu  unaozidi kuwagawa Watanzania kitabaka, kikanda,  kikabila,  na kidini. Mungu hatunusuru na matokeo mengine  hasi mbele ya safari...Kifo chako kizinduie Watanzania zaidi na zaidi wenye dhamira ya kuthubutu kupigania utekelezaji wa Ripoti ya Makweta  katika mazingira ya sasa kwa kuunda Tume ya Makweta ya miaka hii.
Ulale Panapostahili Mzee Makweta,
Mwl. Lwaitama

Date: Sun, 18 Nov 2012 09:46:25 +0300
Subject: Re: [wanabidii] MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA
From: smkina@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Ulale Panapostahili Mzee Makweta,

Nakumbuka mara ya mwisho ulinialika kwako kwa chakula cha mchana pamoja na mtoto wako wa kike aliyekuja nyumbani Njombe kumtambulisha mumewe, Mchina pamoja na watoto wenu.

Tulizungumza mengi juu ya maendeleo ya nchi na hasa suala zima la elimu.

Nitakukumbuka sana Mzee Makweta

Lala salama.

Simon

2012/11/17 sharon sauwa <antisharo@yahoo.co.uk>
Ninakumbuka mzee huyu mara nyingi nilikuwa nikipanda naye daladala za kutoka Mwenge kwenda Posta. Huyu ni mfano wa wazee wachache ambao waliitumikia nchi hii kwa uaminifu na uadilifu wakiamini katika siasa za ujamaa na kujitegemea ambazo kwa sasa tumeziweka hazijulikani kama zipo. Mungu akupokee kwenye ufalme wake.

From: Deogratias Kawonga <deogratias.kawonga@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA
To: "Deogratias Kawonga" <deogratias.kawonga@gmail.com>
Cc: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 17 November, 2012, 21:27

Aaah Sorry ni Mzee Makweta, Kumradhi

Sent wirelessly from my iPhone device on the Airtel Network

On Nov 17, 2012, at 22:24, Deogratias Kawonga <deogratias.kawonga@gmail.com> wrote:

RIP mzee Mangula

Sent wirelessly from my iPhone device on the Airtel Network

On Nov 17, 2012, at 21:48, Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com> wrote:

Oh! R.I.P mzee. Mwendo umeumaliza.
Vin

2012/11/17 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA

SERIKALI inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta
kilichotokea leo saa 11 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya
jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango
ya mazishi zitatolewa baadaye.

Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo
Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi.

Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Simon Martha Mkina
Executive Chairman  & Founder
Tanzania Journalists Alliance (Tajoa)
Author/Columnist/Editor/Publisher
Tanzania

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment