Thursday, 12 July 2012

Re: [wanabidii] Re: MKUTANO WA MHE BERNARD MEMBE NA MABALOZI PAMOJA NA WANAHABARI KUHUSU SAKATA LA MELI ZA IRAN

Naomba kujua: Ni/si hatari kwa Tanzania Marekani kuwa na silaha za nuclea? Ni/si hatari kwa Tanzania kwa Iran kuwa na silaha za nuclea?
Tunawasaidia wamarekani kuwabana waIran kwa manufaa gani kwetu?
 
Tunastahili kumuogopa nani anayedhaniwa anaweza kutumia silaha za atomic au aliyewhi kuzitumia?


--- On Fri, 7/6/12, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Re: MKUTANO WA MHE BERNARD MEMBE NA MABALOZI PAMOJA NA WANAHABARI KUHUSU SAKATA LA MELI ZA IRAN
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, July 6, 2012, 9:33 AM

TAARIFA KUHUSU MKUTANO WA MHE. BERNARD MEMBE (MB), WAZIRI WA MAMBO YA
NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA MABALOZI WA NCHI ZA UMOJA WA ULAYA
NA MAREKANI PPAMOJA NA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 05 JULAI 2012
Jana tarehe 05 Julai 2012, Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb),Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amekutana na Waandishi wa
Habari pamoja na Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani hapa
nchini kwa lengo la kutoa msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuhusu kuwepo kwa uvumi kwamba Meli za Iran zimesajiliwa
na kupeperusha bendera ya Tanzania kama ilivyotangazwa katika vyombo
vya habari ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo yake na Waandishi wa Habari na baadaye Mabalozi,
Mhe. Waziri alieleza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ilipata taarifa kuhusu meli za Iran kusajiliwa na kupeperusha
bendera ya Tanzania kupitia kwenye vyombo vya habari.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilichukua hatua ya kuitaka
Mamlaka ya Usafiri wa Baharini ya Zanzibar – Zanzibar Marine Authority
(ZMA) ambayo kwa Sheria Na. 3 ya mwaka 2009 ina mamlaka ya kusajili
meli za Kimataifa kuchuguza tuhuma hizo na kutoa taarifa.

Aidha, aliwatanabaisha Waandishi na Mabalozi kwamba Mamlaka ya Usafiri
wa Baharini Zanzibar ilichukua hatua za kumtaka Wakala wake wa
kusajili meli, Kampuni ya PHILTEX yenye makao yake makuu Dubai, Falme
za Kiarabu (UAE) kutoa taarifa kama kati ya meli 399 zilizosajiliwa
kuna meli za Iran.

Nayo Kampuni ya PHILTEX ilitoa taarifa kuwa kati ya meli
zilizosajiliwa hakuna meli hata moja ya Iran. Hata hivyo, waliongeza
kuwa meli zilizosajiliwa hivi karibuni zilikuwa na usajili wa Cyprus
na Malta.

Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilimwita
Balozi wa Iran nchini ili kujua kama kuna ukweli kuwa baadhi ya meli
zilizosajiliwa ni za Iran. Balozi alikataa kabisa kuwa hakuna meli za
Iran zilizosajiliwa Zanzibar na zinazopeperusha bendera ya Tanzania.

Taarifa hizi kutoka kwenye vyombo vya habari, Kampuni ya PHILTEX na
Ubalozi wa Iran nchini zimepelekea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kufanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha kama kweli kuna
meli za Iran zilizosajiliwa Zanzibar na zinazopeperusha bendera ya
Tanzania.

Ili kupata ukweli wa tuhuma hizo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imeomba nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani kusaidia katika
uchunguzi. Mhe. Waziri, aliwakabidhi Barua za Kibalozi kuwasilisha
rasmi ombi hilo.

Mhe. Waziri Membe aliwahidi waandishi wa Habari na Mabalozi hao kwamba
kuwa baada ya uchunguzi kukamilika na ukweli kubainika, serikali ya
Jamhuri ya Muungano itachukuwa hatua za haraka ikiwemo kufuta usajili
wa meli zote zitakazogundulika kuwa ni za Iran.

On Jul 6, 2:05 pm, Abdalah Hamis <hamis...@gmail.com> wrote:
> Serikali imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha
> bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo. Serikali ya Jamhuri ya
> Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili
> zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha. Tanzania imewaarifu nchi
> zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na
> kushirikiana kuthibitisha taarifa hii. Tumefanya hivyo kwa kuzingatia
> uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa
> kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa. Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala
> wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran,
> Balozi wa Iran nchini aliitwa akakanusha. Tutakapopata matokeo ya
> utafiti na ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara
> moja. Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli
> hizo. Tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio
> 1920 la UN Security Council.Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani.
> Tunafurahia mahusiano yetu na nchi zote duniani. Hili ni jambo
> linalogusa maslahi ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani
> (Muungano), tujihadhari na namna tunavyolizungumzia. Tusimame pamoja
> kama taifa. Nchi kwanza!
>
> Chanzo :http://www.facebook.com/pages/Bernard-Kamilius-Membe/204958252852114

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment