Tukumbuke Dr Slaa amefunguliwa kesi na mkewe wa zamani Rose Kamili - Moja anataka kuzuia ndoa hiyo kwa kuwa ana ndoa nyingine , pili anatakiwa kulipa gharama za malezi alizokimbia baada ya kumpata josephine .
Sasa hili linahusiana vipi na Jacob Zuma kuwa na Wake zaidi ya 3 ? Kwani wamepelekana mahakamani ? si wameshakubaliana wenyewe .
Huyu slaa amefikishwa mahakamani maana yake walishindwa kusuluhisha nyumbani na mahakama ni chombo cha umma , wote tunalipa kodi kuhudumia mahamana na matumishi wake .
2012/7/17 Mbeso Society <mbeso_2000@yahoo.com>
--
Ndugu umenene, mfano mzuri ni Raisi wa Africa kusini, mke wake wa kwanza waliachana haikumzuia kuoa tena au kuwa Raisi na jamii ya Afrika kusini waliona haya ni maisha ya ndani ya nyumba. Mama akawa waziri wakati ameachana na mume wake na sasa Kiongozi mku wa Halmashauri ya utendaji ya AU. Kitu muhimu ni uwezo wa kuwa kiongozi wa jamii mwenye upeo mkubwa. Niliwaona wabunge fulani wanawake kwenye Gazeti wanamkumbatia Rose kamili kwa ajili ya maisha yake ya ndani- Je! wao waume zao wako wapi? Kila binadamu aliyeko chini ya jua ana changamoto katika maisha yake kwa namna moja au nyingine.
Swali la kijinga! Je! kuwa mbunge mahili wa CCMlazima ujitahidi kutoa tusi au kutukana wapinzani au vipi?
--- On Tue, 7/17/12, Chacha Wambura <wamburacm@yahoo.com> wrote:
From: Chacha Wambura <wamburacm@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia naKutaka Kufunga Ndoa
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, July 17, 2012, 1:40 AM--
Wandugu,Kwa hili la Dk. Slaa na nikitathmini kiwango cha ukweli katika maadili miongoni mwetu napata shida kidogo kwa nini iwe hivi. Kwa Taifa lolote Afrika kwa sasa, wengi tulishajiondoa katika kuzingatia maadili na uadilifu kama kigezo mojawapo cha kumpatia mtu uongozi. Uadilifu kwangu ni pamoja na kuishi uzingativu wa misingi halisi ya mila na desturi za jamii ya kila mmoja wetu, UchaMungu na utayari wa kuiogopa na kuitunza ipasavyo mali ya Umma.Hapa kuisha kwa maadili yetu kunadhihirika wazi katika maeneo hayo, nikimaanisha kuwa hata nafsi zetu sasa zinaogopwa na wazazi wetu kwa sababu tumejiwekea vizingiti vya kutoingiliwa maisha yetu kwa sababu tumesoma sana, tuna kazi kubwa mijini n.k. kwa hiyo hatutaki mtu atuchokonoe chokonoe kuwa tunaishi ishije.Uzingativu wa mila na Ucha Mungu kwetu ni vitu vinavyohojiwa kwa sababu wengi hatuko katika mstari na Mwenyezi Mungu Anajua zaidi. Kama anatusamehe ama kutusubiria dakika ya mwisho, basi ndio maana tunaonekana kuendelea kubweka na kujitapa kuwa nasi tumo.Ninayo kumbukumbu ya viongozi wengi wanaowekwa madarakani kwa sasa bila kuhoji mambo katika maeneo hayo mawili. Ingawa nasikia zamani hizo ili upewe madaraka ilikuwa lazima ijulikane kama una wajibu wowote wa kiutamaduni, mfano kama umeoa au umeolewa. Kiserikali, najua pia sio lazima mambo ya kiimani yahojiwe. Laiti kama yangehojiwa, huenda ingekuwa na huko nako rushwa inatembea kama nini, ili tupite na kustahili kuingia katika mchakato. Mchakato rasmi huwa unaishia kujua kama mhusika alikopitia katika utekelezaji wa weledi wake amekuwa mwenye historia tulivu na isiyo mashaka, mintarafu kukiuka sheria za nchi, sheria za ajira n.k.Hoja yangu hapa sasa ni hii. Kwa hili la Dk. Slaa, kuacha mke na kutaka kuoa mwingine sioni ni kwanini inakuwa kichwa cha habari cha kushadidiwa na kupigiwa kelele hivi. Kama ninavyoona, tukiamua kujizatiti kikwelikweli kuhesabu maovu yetu, hamna atakayesimama. Wengi ni watu wakubw akatika jamii lakini majumbani mwao wanalala vitanda tofauti na wenzi wao wa ndoa. Wengine walishatengana hata hawakai nyumba moja. Hili nafikiri Dk. Slaa aachwe peke yake. Asiingiliwe. Naamini ana maelezo ya kutosha kuilewesha jamii na wafuasi wake wakaelewa. Tusimlishe maneno.Hao watoto aliozaa na Mhe. Kamili, sidhani kama wako prone to very same situations kama watoto wanaozaliwa na wazazi wasiotaka kuwajibikia matunda ya viuno vyao, wakawatelekeza. Siamini kama watakosa au wamekuwa wakikosa kula na kulala muda wote mama yao alipokuwa hakai na baba yao. Hawa si wa kuingia katika kundi hilo na wala siamini kama Dk. Slaa ndo amekata mguu kabisa kwamba hatoi ushirikiano wa kimalezi kwa watoto hao. Sidhani.Ya Dk. Slaa yabaki kwake kama binadamu, Ya kwetu nasi yabaki kwetu kama binadamu. Lakini kwa sifa binafsi ya mtu, ibaki kuwa hivyo kuwa kwayo atafanikisha ndoto zake za kutaka kuingia katika orodha ya wagombea safari ya Ikulu.Asanteni.
From: Dahlia Majid <dahliamajid@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia naKutaka Kufunga Ndoa
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, July 16, 2012, 1:05 PM
--Yona,Kazi kwenu mnaopenda kushoboka na UPEPO, mkatupa kura zenu kishabiki, mnalo hilo, limewaganda mtalinywa.Mlishaambiwa mara kibao, wengine hawana sifa za uongozi, mkajitia shetani aso mpungaji wake, sasa mwalia majiani hovyo.Wengine mwathubutu kutetea uozo, akina Rottson,Lutgard na wengine, tukuulizeni nyie mso na haya kutetea upuuzi mnalipwa na nani?! "shame on you all plus the one you are defending much... kwli kupenda kubaya, ukipenda-chongo utaita kengezaYaani jamaa kaaibisha Jamii, Chama chake, Familia yake and above all KANISA bado mnafurukuta??!!Mie simo... ila ntawaletea maji huko motoni mtakapokuwa, au mnasemaje?im outNamastee...From: Lutgard Kokulinda Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, July 15, 2012 5:41 AM
Subject: RE: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia naKutaka Kufunga Ndoa
--From: Yona MaroYona huwa unalipwa kiasi gani kwa hii kazi unayotumwa kufanya?
Sent: 15/7/2012 13:03
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia naKutaka Kufunga Ndoa
Dr Slaa mwenyewe alivyohojiwa alisema ameyazoea , Hakukaa kimya kama wengi wanavyotaka wenzao wakae kimya , hili suala lingekuwa la watu 2 yaani rose kamili na dr slaa pekee tungeweza kukaa kimya lakini kuna huyo rose kamili , dr slaa , josephine mushumbusi , watoto wao , maisha ya dr slaa kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani na maslahi ya chama chake katika suala hili .Sasa kwa wale wasioelewa suala hili vizuri na kwa mapana kaeni kimya au chokozeni tutaendelea kuwaelewesha hata viziwi wasikie na vipofu waone hali halisi , huyu angekuwa rais sasa hivi nchi ingekuwa anajadili ndoa yake badala ya kunyanyua maisha ya watanzania na labda tungeumizwa na mengi zaidi ya hili .Sasa yeye binafsi ajisafishe hata baada ya suala hili kumalizwa na mahakama aiweke jamii sawa ielewe .
2012/7/15 Rottson Kabalika <rotts76@yahoo.co.uk>
YonaKama humwamini mkeo hata kazini au kwenye shughuli yoyote hawezi kwenda. Tuache unazi watu wengi tu wa staus yake wachafu kuliko yeye ambaye ameamua kuishi na mtu mwingine baada ya kushindwana na wa kwanza. Elewa 'there is a very thing line btn love n hate'. Kuachwa kimapenzi kunauma sana, huyo anayelalamika kuwa jamaa katekeleza familia ana uwezo wa kulea pia na anaongea hivyo may b kwa hatred au kutaka kumfanya jamaa aonekane vibaya mbele ya jamii. Mume wa huyo anayetaka kuolewa hujatwambia kama naye kaweka pingamizi. Tunaomba tupashe pia kuhusu hilo ili nasi tuanze kufuatilia mambo haya ya watu binafsi.From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, 14 July 2012, 16:19
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia na Kutaka Kufunga Ndoa
Ndugu Jonas na Wengine tukumbuke pia huyu ni kiongozi wa Chama tena chama kikuu cha Upinzani kwahiyo maisha yake na mambo yake hata yakiwa binafsi tunategemea yawe natofauti na wengine kwa tukio kama hili na dr slaa na wale wanaomtetea wengine tunajiuliza ni lipi tofauti analoweza kuleta kwenye jamii kama yeye mwenyewe amechafuka ?Utafauti sio katika kumwaga sera majukwaani tu hata kama maisha ya watu wanayoishi , hivi umeshamsikia freeman mbowe na kashfa yoyote ? Mnataka tuogope hata kuachia wake zetu kwenda kwenye kampeni .
2012/7/14 denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
Dr Slaa needs to get his private life sorted out and he needs to do that pretty soon!!Hawezi ku-afford all these distractions.....................2012/7/14 Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
All men boil to the same thing, including you BARAKA!! LKKFrom: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, July 13, 2012 10:41 PM
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia na Kutaka Kufunga Ndoa
Rugambwa can u try to be fair please??? just try please......wapi mimi nimehukumu? naomba usome tena posting yangu halafu utoe kauli iliyojaa haki na usawa. Nilichokisema ni kwamba, kwangu mimi sioni sababu ya kuwazuia watu kumjadili Dkt. Slaa kwani jambo kama hili hata kama halilingani lakini linashabihana na sakata la Ndg. Simbachawene ingawa mazingira ni tofauti. Kilichofanyika katika sakata la Mh. Naibu Waziri lilikuwa ni kujadili maisha binafsi na hapa kinachojadiliwa ni maisha binafsi. Ni vema kukawa na uwanja sawa na siyo akiwa mtu ni Mserikali au MCCM basi huyo ni mdhambi kuliko wanadamu wengine.
Kiongozi haijalishi ni wa Serikali ama siyo, atajadiliwa tu kwasababu anayodhamana pia. Kuna kundi kubwa la watu nyuma yake hivyo ni lazima awe kioo hasa katika maadili yetu ya Kitanzania. Wengi ni wadhaifu hilo halifichiki ndiyo maana kule Dodoma wako wao wenyewe bila hata wake zao isipokuwa wachache tu. Leo hii mimi siyo kiongozi lakini miaka 3 ijayo ntakuwa kiongozi. Ndiyo maana hata kuna kitu cha Upekuzi/Vetting hufanywa kwa ajili ya watumishi kwa sababu ya kuchunguza mtu alivyo kabla ya kukasimiwa madaraka makubwa kwake
2012/7/13 Laurean Rugambwa B. <rugambwa@hotmail.com>
Bariki na Yona,
Kwa nini mna hukumu mtu kuwa katekeleza familia?
Aliye serikalini ndo anajadiliwa kwa sababu kapewa dhamana na watanzania kuwatumikia, story is more juicy, nyie msiwe na jazba kutetea watumishi na wanasiasa au mawaziri wa chama tawala.
Wananchi, nikiwemo mimi, tunawaangalia hao viongozi watatue matatizo,kero na shida nyingi tulizo wachagua wafanye.
Remember, they have power, privileges and prerogatives, but it comes at the cost. Kuwajadili exclusively and subjectively deeply are one of those costs. Hili ni jambo la kawaida kwenye nchi yoyote.
Dr. Slaa has privilege of being a popular opposition leader. Most Tanzanians, feel connected with him because he talk hope while others talk of fear and despair!
Hivo msichangae, kwanini watu wanakuwa softer kwa dr. Slaa!
Kila la heri,
LR
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
-----Original Message-----
From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
Date: Fri, 13 Jul 2012 15:20:23
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia na
Kutaka Kufunga Ndoa
Hii haina tofauti sana na issue iliyojitokeza mwezi uliopita ikimhusisha Naibu Waziri - Nishati. Wengi walilazimisha kwamba katenda na kumnyooshe vidole lakini kwa sababu tu anayejadiliwa ni mtu wa mrengo huu kwa kweli kwa nilivyoisoma hii mitandao ya kijamii hakika hili haliwezi kujadiliwa. Hii ingemtokea kiongozi wa Serikali iliyoko madarakani hakika mengi yangesemwa (NAOMBA NIJINUKUU....WATANZANIA TUMEJAA UNAFIKI). Mungu atusaidie tu katika yote
2012/7/13 hancy obothe <hanssy84@yahoo.com <mailto:hanssy84@yahoo.com> >
Binafs nimeikubali hoja yako lakini nivizuri tukiwa na masuala ya kubeba katika mjadala wa katiba
--- On Fri, 7/13/12, Daniel Minja <minjartd@yahoo.com <mailto:minjartd@yahoo.com> > wrote:
From: Daniel Minja <minjartd@yahoo.com <mailto:minjartd@yahoo.com> >
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia na Kutaka Kufunga Ndoa
To: "wanabidii@googlegroups.com <mailto:wanabidii@googlegroups.com> " <wanabidii@googlegroups.com <mailto:wanabidii@googlegroups.com> >
Date: Friday, July 13, 2012, 3:18 AM
Hivi maslahi ya watoto huwa yanakuja pindi tu mtu anapotaka kuvunja na kufunga ndoa nyengine? Je kama watoto walitelekezwa, iweje mahitaji yao yasipelekwe ustawi wa jamii au mahakamani hadi ndoa itangazwe ndo court injunction ifanyike? Naelewa fika kwa wanandoa kama wataamua kupeana talaka ama kuachana kwa namna moja ama nyengine kuna issue za kusort out, mojawapo likiwa ni mgawanyo walichochumia wakati wa ndoa, matunzo ya watoto na kadhalika. Mimi kwa maoni yangu, sidhani kama hii issue ya kutelekeza ina mashiko kwa wakati huu, ingetakiwa kuwepo kabla hata ya hili pingamizi lililowekwa sasa ivi. By the way, nani najua responsibilities alizo nazo huyo bwana kwa wanawe? Je bado wanaishi na mamayao? au wako shule na kama wako shule ama popote pale, nani anawatimizia mahitaji? tusipende kurush kwenye conclusions na pia nadhani Slaa siyo wa kwanza kuingia kwenye saga kama hizi, lets let the court discuss this issue, muda huu ni wa kujikita kujua je, tuko tayari kweli kujadili katiba mpya? kujua mapungufu yake kwenye haki za wanandoa na kutalikiana, haki za watoto na kadhalika. mfano kuna vipeperushi vya kutosha ili hata wale walioko Nyarugusu na maeneo ya karibu wavipate, au nikihitaji hata katiba ya zamani au rasimu ya katiba mpya nitaipatia wapi nikiwa Mbezi Temboni ama Nangaru huko Lindi? Lets be serious and discuss ideas zenye mashiko kwa mustakabali wa taifa letu na siyo bedroom politics!
----------------
From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com <mailto:oldmoshi@gmail.com> >
To: wanabidii@googlegroups.com <mailto:wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, July 13, 2012 12:24 PM
Subject: Re: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia na Kutaka Kufunga Ndoa
Ndugu Elisa
Hebu angalia watoto wa mitaani wanavyoendelea kujaa hawana baba wala mama , lakini wengi wao wazazi wao ni miongoni mwetu lakini wametelekezwa kwa sababu ya visa vya wazazi , angalia wale watoto wanaoenda kutumikishwa sehemu mbalimbali , hawa wote wakitendewa vyema sheria zikiwa vizuri ziwatetee na wazazi wao watafutwe wawajibishwe wanaweza kufanya vizuri zaidi na wanaweza kulitumikia taifa vizuri zaidi , tukirudi kwenye suala la dr slaa , hapo ametuhumiwa kutelekeza familia , hatujui hao waliotelekezwa maisha yao yaliharibikaje au walikimbilia wapi na sheria inawalinda vipi labda ni kama wale wengine wanaolalanjiani bila kujua mama wala baba yao au labda wanakosa huduma muhimu kwa ajili ya maisha yao .
Mwisho ni
2012/7/13 ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com <http://mc/compose?to=elisamuhingo@yahoo.com> >
Kama tukivipa kipaumbele vitu vya namna hii basi watu wanaotuangalia wataanza kututilia mashaka hasa kwa kuangalia maswala yanayolikabili taifa letu.Haya ni mambo ya kutungiwa sheria. Tanzania ni Maskini afya mbovu na wajinga toka uhuru si kwa sababu ya mambo yanayotendeka vyumbani mwa watu. Tuna ukubwa wa ajabu wa serikali na magereza yana vibaka wakati wezi wakubwa haya ndiyo ya msingi kwenye katiba. Lakini waliopendana wakitendana waamuliweje si lazima kuyapa kipaumbele kwenye katiba.
--- On Fri, 7/13/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com <http://mc/compose?to=oldmoshi@gmail.com> > wrote:
From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com <http://mc/compose?to=oldmoshi@gmail.com> >
Subject: [wanabidii] Re: Dr Slaa Kushitakiwa kwa Kutelekeza Familia na Kutaka Kufunga Ndoa
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com <http://mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com> >
Date: Friday, July 13, 2012, 12:10 AM
Mada hii inaweza kujadiliwa tu .
Tuangalie sasa hivi tulivyokwenye mchakato wa katiba mpya wananchi
wanatakiwa kutoa maoni yao kuhusu viongozi wanaowataka na hata sheria
za ndoa ziweze kujadiliwa zaidi , haki za wanandoa wanapoachana au
mmoja kuwa mbali na mwenzake na vitu kama hivyo sasa tunaweza kutumia
mjadala wa dr slaa kama sample ya mijadala kama hiyo .
Kama wengi walivyotangulia kusema kwamba kuna viongozi wengi
wanawatoto wa nje na wengine wanandoa zisizoeleweka lakini tumekaa
kimya . Hapana si kweli pengine hatuna taarifa nao na hata vyombo vya
habari havijawahi kugusia masuala hayo ili wengine tupate kujua kama
nyie mnajua kwanini msilete kwenye mitandao ya kijamii watu wajadili
na wabadilishane mawazo ?
Nisiende mbali sana lakini tujue tuko kwenye mchakato wa katiba , kuna
watu wanaimba nyimbo za usawa , nyimbo za kubadilisha sheria za ndoa
na nyingine nyingi matukio kama haya yasiachwe nyuma tunayajadili kwa
uwazi na bila kumwogopa mtu ili tuweze kujenga taifa bora .
On Jul 13, 9:15 am, method francis ngonge <mngo...@gmail.com <http://us.mc1604.mail.yahoo.com/mc/compose?to=mngo...@gmail.com> > wrote:
> Nakuunga mkono Jonas binafsi pia sioni cha kujadili katika hili, Slaa
> kufikishwa mahakamani kwa sababu ya mambo ya kifamilia ni jambo la
> kawaida na la kwake binafsi, sioni kama inatuhusu sisi kama
> watanganyika. Mara nyingi tumeona akina mama wenye uhusiano au
> waliowahi kuwa na uhusiano au wanaowabambikia viongozi wa vyama vya
> upinzani wakitumiwa kwenye kampeini na hili yawezekana ikawa ni
> maandalizi ya uchaguzi wa 2015. Ingekuwa kuna mapenzi yanayoendelea
> kati ya Slaa na huyo Rose basi isingekuwa rahisi kwa Slaa kutembea
> nchi nzima akipiga Kampeini za uchaguzi uliopita akiwa na mwanamke
> mwingine bila kificho. Kuna Kesi aliyokwishafunguliwa ya kumpora mke
> wa mtu hatujui ilikoishia na hii pia ni ya aina hiyo hiyo. Labda
> tumuombe wakili Kitururu atwambie kesi aliyomfungulia Slaa ilivyoisha
> au inavyoendelea
>
> 2012/7/13 <tiko...@yahoo.com <http://us.mc1604.mail.yahoo.com/mc/compose?to=tiko...@yahoo.com> >:
>
>
>
>
>
>
>
> > Mwalimu wangu,
>
> > Mimi huwa natamani watu wote wangemchunia akileta hoja isiyokuwa na mshiko
> > au yenye maslahi binafsi yake. Toka uchaguzi mkuu 2010 umeisha inaonyesha
> > Yona Maro anamaslahi binafsi na Dr Slaa.
>
> > Kimsingi nchi yetu ilipofika kwa rushwa na ufisadi tunahitaji rais ambaye
> > ana ujasiri wa kutosha na bila kumung'unya maneno atuambie nani ni fisadi na
> > hatua za hapo hapo. Ndo faida ambayo watanzania wengi wanasubiri.
>
> > Kwasasa ili ufisadi tuuzike ni raisi pekee anatakiwa aanze kuukana na kuwa
> > mwiko, ndipo wengine wafuate. Ndo maana Dr. Slaa ameweza kuwavuta watanzania
> > walio wengi. Si utakatifu wa familia yake bali ni jinsi ambavyo anaweza
> > kushughulikia ufisadi katika nchi hii. Watanzania tuliowengi tunaamini
> > rushwa na ufisadi ndio kikwazo kuu cha maendeleo ya taifa letu. Kama kuna
> > mtu halioni hili kuna tatizo kubwa na safari yetu itakuwa ndefu sana au
> > analiona tatizo lakini ananufaika na mfumo huu.
>
> > Tutafika tu tusonge.
>
> > Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
> > ________________________________
> > From: Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukaluga...@hotmail.com <http://us.mc1604.mail.yahoo.com/mc/compose?to=kerezesia_mukaluga...@hotmail.com> >
> > Sender: wanabidii@googlegroups.com <
[The entire original message is not included.]
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment