Tuesday, 17 July 2012

[wanabidii] BUNGE NA CABINET YETU NI YA COPY AND PASTE

Unapozuia gari ya mwaka 2004 toka Japan isiingie katika nchi yako wakati ile ya 1979 ipo ndani ya nchi yako inatembea na kuvuja moshi mzito unakuwa na lengo lipi? Kwa sheria hii mpya ya kodi ya uchakavu bei ya kuingiza Toyota RAV4 ya mwaka 1997 yenye uchakavu ni kama nusu au theluthi ya bei ya kuingiza Toyota RAV4 ya mwaka 2005. Hoja yangu ni je, hii sheria kweli ina lengo lile la kupunguza magari chakavu kuingia au ni kuongeza rate ya kununua hayo magari yetu ya miaka ya nyuma? Ilipokuwa miaka 10 kweli ilikuwa na mantiki kidogo lakini hii ya miaka minane inatia mashaka.
 
Sera ya kupunguza wimbi la kuingiza magari ya miaka ya nyuma inashika kasi katika mataifa mengi yaliyoendelea ili kulinda mazingira yetu. Mataifa makini hayakomei kupunguza wimbi la kuingiza magari ya miaka ya nyuma tu bali huweka pia zuio la kutumia magari yaliyochakaa katika barabara zao. Sera kama hii ndiyo hutufanya sisi kununua magari kuu kuu kutoka Japan maana kulingana na sheria za matumizi katika nchi ile, hizo gari hazitakiwi tena. Hii sheria ni kali sana katika mataifa kama Singapore n.k. Ukweli ni kwamba hao wanazuia matumizi ya magari yaliyochakaa katika nchi yao.
 
Bunge letu linazidi kupitisha sheria ya kupunguza kuingiza magari ya miaka ya 2004 ambayo ni mazuri ukilinganisha na haya ambayo tayari tunayatumia hapa. Ukiangalia kwa makini hii sheria inapunguza uwezo wa mtu kuagiza coaster ya mwaka 2004 na kuendelea kutumia ile aliyokuwa bayo ambayo ni ya mwaka 1988 japo ni chakavu kuliko ile ambayo angeagiza! Kuwakatisha watu kuingiza magari ya 2004 bila kuweka sheria ya kuzuia kutumia magari ya mwaka 1990 ni sawa na kuchochea matumizi ya gari chakavu zaidi katika taifa lako maana watu tutaona ni bora kuendelea na gari la zamani kuliko kuagiza lingine kwa bai kubwa.
 
Ni ipi gari itakayochafua mazingira kati ya Basi la Komakoma la mwaka 1980 na gari inayoingia toka Singapore ya mwaka 2003? Watu watasema tunataka hizi za zamani zijifute! Jamani hii ni simple math.. hata hili la mwaka 2006 likiingia leo baada ya miaka sita si litakuwa chakavu na kuharibu mazingira?
 
Kwangu mimi hii sheria ina mapungufu mengi na haya yote ni udhaifu wa bunge letu kuongozwa na itikadi kuliko kuangalia vitu kwa undani. Hii sheria imenakiliwa nchi fulani na sasa tunaipaste hapa bila kuifanyia marekebisho sahihi.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment