Yona sasa ndiyo ujue hii Serikali yako ambayo unaitunishia mashavu kuitetea humu kila siku ilivyo ya ajabu. Hii mahakama ilitakiwa ianzishwe na waislam na ifanye kazi katika mazingira ya dini ya kiislam bila kuathiri wala kuingiliana na taratibu za serikali lakini ajabu ni kwamba hata gharama ya kufanya study katika mataifa mengine inaghalimikiwa na serikali yetu. Hapa kuna baadhi yetu tunaona ni sawa lakini kitendo cha kukiuka miiko ya Baba wa taifa na kuiingiza Serikali katika mambo ya kidini tujue tunajijengea mazingira magumu sana hapo mbeleni. Hakuna kitu kibaya kama migogoro ya kiimani na sasa tumeingia huko. Tunakoelekea tutasikia Mahakama nyingi za madhehebu ya dini zikihitaji gharama za Serikali. Lakini kubwa zaidi tungejiepusha na haya hususani katika kipindi hiki ambacho dunia ipo katika ushetani wa ndoa ya jinsia moja. Lakini kwa kuwa Serikali yetu ni sikivu basi tutegemee Serikali isaidie kuanzishwa kwa mahakama za baadhi ya dini zitakazokuwa zikifungisha na kutetea ndoa za jinsia moja na kupiga watu mawe hadi kufa. Hapo ndipo kazi itakuwa kubwa maana tayari tumeingia mikenge. --- On Tue, 17/7/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
|
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment