Tuesday, 19 April 2016

Re: [wanabidii] MAGUFULI NA MAJAMBAZI

Ananilea Nkya,
Mama, nimekuondoa kwenye hekima sababu umekuwa shabiki zaidi bila kuangalia ukweli. do not mislead poor Tanzanian with your strong argument and believes on Lowasa, educate and let them decide.
regards,
Paulo.
On Sep 25, 2015, at 7:58 PM, 'Mike Zunzu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Sina tatizo na hatua kali juu ya wavunja sharia kama majambazi, naona Magufuli amekuecifiki kwa kusema majambazi wa kutumia silaha, ninachofahamu hata kabla ya Magufuli kusema, vyombo vya usalama wanapokumbana na majambazi wakutumia silaha njia wanaa ni kuwaua au kuwajeruhi kiasi kwamba wasiweze kujibu mapigo ya vyombo vya usalama.

Tatizo langu ni moja, utawalausifanye utafiti wa uhakika kisa cha watu ushughuli yenye hatari kama hiyo? Siwatetei hao majambazi kuchagua njia ya kukidhi maisha yao kwa haribu  pengine hata kua watu wasio na hatia basi wanaweza wakaua kwa kupata kiasi kidogo sana, kitu ambacho naamini hata wao huwa wanajuta kwa kufanya hivyo.

Kwa maoni yangu, kukibunia njia nzwana uhakika mtu atakula nini atawaa nini, atatatuaje matatizo mbali m pesa ujambazi unaweza ukapungua sana, nafahamu siyo rahisi kuuangamiza kabisa lakini unaweza ukapunzwa, nasema hauwezi kuisha kabisa babu kuna watu waliozalia na upungufu wa kutambua umhimu wa maisha ya bmu wenzao,awajali kuchagua njia hizo ovu za kukidhi maisha yao.

Tazizo kwa viongozi: Mtu anapokuwa jukwaani huwa wanashindwa/husahau mamna ya kuweka kiwango jinsi wanapo stress jambo, anachofuhia ni kuona anashangiliwa nadha motto mdogo anavyofuhia pongezi za wazazi wake, hivyo hujikuta wameongea kupita kiwango anachotakia aongee, na akishakaa ofisi kuwa ashughulikia ahadi zake nyingi hawazi hata kuzikumbuka, na zingine hata akizikumbuka huwa hazitekelezeki.



On Friday, 25 September 2015, 15:57, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


MAGUFULI NA MAJAMBAZI

Ananilea Nkya

Mgombea  Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr  John Magufuli akichaguliwa  huenda  nchi yetu ikashuhudia  mapambano dhidi ya polisi na wananchi yakiongezeka kwa sababu  serikali yake  itaruhusu polisi  kuuwa wananchi kwa kisingizio cha ujambazi.

Dr Magufuli katika kampeni zake kwenye uwanja  wa Mashujaa mkoni Mtwara  02 Septemba 2015 alikaririwa  na  vyombo vya habari akisema kuwa  serikali yake haitamshitaki polisi yoyote atakayemuua  jambazi mwenye silaha.

Dr Magufuli alikaririrwa akisema ''serikali yangu askari akipiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi. Kila mara (majambazi) wanavamia vituo vya polisi, mbona hawavamii kambi za jeshi, jeshi la kujenga taifa au Ukonga FFU maana polisi wana nidhamu sasa wanawaonea na kuwaua''.

Wapiga kura wanajiuliza, kama  kabla  hajachaguliwa Dr Magufuli anaanza kuwaweka wananchi roho juu kiasi hiki,  je akichaguliwa  mapambano  kati ya wananchi na vyombo vya dola  yataongezeka kiasi gani?

Wananchi wanauliza  swali hili kwa sababu ingawa  hivi sasa  hakuna polisi  anayeruhusiwa  kuhukumu  watuhumiwa wa makosa mbali mbali ikiwa ni  pamoja na watuhumiwa wa ujambazi, lakini  umma umeshuhudia  polisi  wakiwauwa  watu  hovyo hovyo kwa tuhuma za ujambazi.

Wanauliza je Dr Magufuli akichaguliwa na polisi wakiruhusiwa rasmi kuwauwa watuhumiwa wa ujambazi—ni wananchi wangapi wasio na hatia  watakaosukiwa zengwe la ujambazi na kuishia  kuuwawa kikatili na polisi? 

Hivi Magufuli  ambaye  amekuwa kiongozi wa serikali  kwa  zaidi ya mika 20 hajui kwamba polisi siyo mahakama na kwamba polisi  haipaswi kutoa hukumu ya kifo kwa raia?

Wakati mgombea Dr Magufuli  akitoa ahadi kwamba kwenye serikali yake polisi ndio watakaotoa hukumu ya kifo kwa watuhumiwa wa ujambazi;  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa  ni mahakama  kuu  ndiyo  yenye mamlaha ya  kutoa hukumu ya kifo.

Zaidi wananchi wanajiuliza,  nchi itakuwa katika hatari kubwa kiasi gani  Dr Magufuli akichaguliwa  ambapo ataruhusu polisi kujichukulia sheria mkononi kuwauwa wananchi  ambao  pengine  maisha  magumu  yametumbukiza kwenye ujambazi? 

Lakini pia wananchi wanajiuliza  je  Dr Magufuli  uchambuzi wake wa masuala ya kijamii  umempa jibu kwamba  polisi wakiwauwa  ''majambazi wenye silaha'' ndio utakuwa mwisho wa mapambano kati ya wananchi na polisi?

Pengine  Dr Magufuli anapaswa kujielimisha kujua  kuwa  chanzo cha ujambazi  siyo  wananchi  na wala siyo  polisi. Kadhalika chanzo cha mapambano katika ya polisi na wananchi siyo polisi wala wananchi
Dr Magufuli anapaswa  mapambano kati  ya polisi na wananchi  wa  ni kiashiria kimoja  cha kuonyesha athari  ya  mfumo  wa  serikali ya CCM  wa kutajirisha watawala na kufukarisha  wananchi wengi.

Anapaswa kufahamu kwamba  CCM  baada ya  kulitupa Azimiao la Arusha  bila kuweka mbadala wake katika zama hizi mpya za utandawazi wizi  ambapo mfumo wa uchumi  unaotamba duniani  baada ya ukomunisti kufa ni  wa upebari ambao unaruhusu mtu uwezo wa  kupata apate hata kama kwa wizi na wa kukosa afie mbali.

Matokeo yake sasa  nchi  yetu Tanzania ina kikundi kidogo cha watawala  waliotajirika vya kutisha kwa kujigawia kibepari  fedha  za wananchi na mali za nchi (kutumia ujambazi wa kalamu na sheria)  huku mamilioni ya wananchi  wakiwepo polisi  ambao  hali zao za maisha ni mbaya  wakitumia mbinu mbali mbali safi na chafu  ukiwepo ujambazi  ili  maisha yaende.

Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu. Lakini cha kushangaza ni kwamba Dr Magufuli hajui kwamba  hata  pale mamilioni ya wananchi walipotaka kuisaidia nchi kuondoa  mfumo  huu  wa utawala unaozalisha makundi mengi ya kihalifu katika jamii—majambazi, panya road, wezi wa kutumia kalamu na sheria na kadhalika, CCM na serikali yake walikataa.

Wananchi walipendekeza Katiba Mpya  CCM na serikali yake  ikakataa kata kata na kuyazika maoni hayo pale Dodoma tena kwa mbwembwe na kutukana wananchi mwaka 2014.

Kiburi na jeuri  ya watawala  wa  serikali  ya CCM  kukataa ushauri wa wananchi kutengeneza Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi  ili kupunguza pengo la utajiri kati ya watawala na wananchi  ndiyo sababu  ya  wananchi  kuikataa CCM hata kama CCM itafanya propaganda na ufisadi kuonyesha inapendwa.
 
Tena wananchi wanajua kuwa  Dr Magufuli  akichaguliwa  kuwa Rais  maana yake ni kwamba serikali ya  CCM kuendelea kuwa  madarakani na hivyo  ujambazi hautakwisha kwa kuuwa  majambazi.

Badala yake  amani ya nchi itawekwa rehani kwa sababu kwa polisi kuua majambazi—hasira ya  wananchi itaongezeka siyo  tu dhidi ya polisi bali dhidi ya kila chombo ambacho serikali  itakitumia  kudhibiti umma unaotamani madadiliko ya  mfumo wa uongozi unaowafanya wananchi kuwa maskini na kudhalilishwa na vyombo vinavyopaswa kuwalinda raia.

Kwa hiyo vema  CCM wakati huu wa kampeni  isijidanganye, iwe ni kwa  kutumia tafiti za kimkakati  ama propaganda nyingine zozote  kuwa wanakubalika kwa  mamilioni ya wananchi  wanaoteseka kwa umaskini na hivyo eti watashinda uchaguzi.

CCM  na mgombea wao wa Urais Dr Magufuli  wanapaswa kuwa na miwani  itakayowaelekeza kuona kuwa kitendo cha  wananchi wenye silaha (majambazi)  kuvamia kituo cha polisi na kuuwa polisi, ni ishara tosha ya amani kutoweka nchini –maana ni mwanzo wa vita kati ya wananchi na polisi—kati ya wananchi na serikali yao.

Hii ni ishara tosha kwamba wananchi wameichoka serikali ya CCM iwe inaongozwa na  Dr  Magufuli au  mwanamuziki maarufu  nchini  Diamond au mwana CCM yeyote mwingine atakayedhaniwa ni kivutio kwa wananchi.

Kadhalika CCM wanapaswa kufahamu kuwa kwa wananchi wengi kushabikia upinzani ni ishara nyingine tosha kwamba wananchi  wameichoka CCM na serikali yake. Hivyo suluhisho siyo kuuwa upinzani, bali nchi kuweka mfumo mpya wa utawala ambao misingi yake wananchi wamependekeza kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.

Kwa hiyo  kama kweli CCM  na serikali yake  wanaitakia mema Tanzania yetu ---hasa amani ya  kweli unaotokana na  wananchi wengi kuridhika  na maisha  badala ya viongozi peke yake kuwa matajiri wa kukufuru,  ni vema  na ni muhimu sana  wakaheshimu  maamuzi  ya  wananchi  watakayoyafanya  kupitia sanduku huru  la kura  hapo tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015. Mungu ibariki Tanzania.

Note: Ninaruhusu  yeyote mwenye kutaka kuisambaza, kuichapisha  Makala hii afanye hivyo. Lengo sote tushiriki kuijenga Tanzania yetu.



Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment