Thursday, 29 October 2015

[wanabidii] RE: [Wanazuoni] Uchaguzi Umekwisha, Turudi Kwa Wananchi.. [1 Attachment]

Nguvu zetu  za uanaharakati na uzalendo wetu ambao tunadai kuwa nao, tuvihamishie kwenye uhamasishaji kwa wananchi ili kila mmoja awajibike kwa nafasi yake kulitumikia taifa. Hatuwezi kutatua matatizo kwa kulalamika kila wakati. Tujiulize! Iwapo kila msomi atatumia fani yake kulalamika, ni watu gani wengine wenye sifa kulikp zetu, watafanya na kutekeleza majukumu? Ni uzembe na matumizi mabaya ya elimu zetu yanayoweza kuendeleza hali mbaya ya nchi yetu. Ni utovu wa nidhamu kwa wananchi wenzetu iwapo tutaendelea kuitumia elimu yetu kuilamu serikali.

..........................................................................
"Ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa kimya".

Baba Nouman,
Bongonyika, East Africa

From: Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com [Wanazuoni]
Sent: ‎29/‎10/‎2015 10:01
To: mabadilikotanzania; wanabidii; Wanazuoni@yahoogroups.com
Subject: [Wanazuoni] Uchaguzi Umekwisha, Turudi Kwa Wananchi.. [1 Attachment]

 
[Attachment(s) from Maggid Mjengwa included below]


Ndugu zangu,

Wakati wowote kuanzia sasa Tume Ya Uchaguzi inatarajiwa kumtangaza John Pombe Magufuli kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano. 
Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umefutwa, ni doa, na CCM na CUF Zanzibar hawana namna yeyote isipokuwa kuitafuta meza ya mazungumzo. Uchaguzi Zanzibar lazima ufanyike, tena haraka.
Tukisubiri hayo, maisha ya kisiasa yanaendelea. Na kazi ya kuijenga nchi kwa kufanya kazi lazima ifanyike. 
Kwa vingozi na tunaoshiriki kazi za kijamii tuna lazima pia ya kurudi kwa Wananchi, hususan wa vijijini, kutia shime na kushiriki wenyewe kwenye kuijenga nchi yetu. Kwa kufanya kazi.

Maggid, 
Iringa.

__._,_.___

Attachment(s) from Maggid Mjengwa | View attachments on the web

1 of 1 Photo(s)


Posted by: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)

Check out the automatic photo album with 1 photo(s) from this topic.
0.jpg


.

__,_._,___

0 comments:

Post a Comment