Thursday 29 October 2015

Re: [wanabidii] Sumaye Na Kisa Cha Mchimba Kisima..!

Maggid,
Hata Sauli alibadilika baada ya kuwanyanyasa na kuwaua wakristo akageuka kuwa muumin wa ajabu na mchango wake katika kueneza injili duniani hauna mfano.
em

2015-10-29 14:21 GMT-04:00 Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>:
Mwalimu wangu Ananilea, 

Ahsante, lakini, bahati njema kwangu ni kuwa nimeishi kuweza kufuatilia siasa za nchi yetu kwa kushuhudia na kusoma vitabuni. Fredrick Sumaye si mgeni kwangu. Kudhani kuwa Sumaye ataweza kuleta mabadiliko ni kujitia upofu. Si Sumaye huyu, kwenye uchaguzi mmoja wa ndani wa CCM mwaka 1998 ndiye aliyehalalisha takrima pale mgombwa aliposhusha  ' takrima' kwa wajumbe wa mkutano . Fredrick Sumaye alifungua mkutano ule akiwa PM, na kwa vile mgombea alikuwa ' mtu wake; , Fredrick Sumaye akatutamkia watanzania kuwa ' takrima' si rushwa ni ukarimu tu wa Kiafrika! Na pale Kilimanjaro Sumaye huyo huyo alipata kuwaambia wafanyabiashara waliokuwa wamepeperusha bendera zao za upinzani kuwa wakitaka mambo yao yawanyokee, waende CCM!
Maggid

2015-10-29 11:02 GMT-07:00 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Maggid,
Haitapita miaka mingi pia kuona wale wote walioikataa Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi wakijutia maamuzi yao.

Mara nyingi viongozi hujitambua wakishaondoka madarakani  na kuishi maisha magumu wanayoishi wananchi.

Hivyo usimlaumu Fredrick Sumaye kwa kuondoka CCM, maana CCM ni chama cha siasa siyo Tanzania ambayo ni mama yake na  mama yetu sote.

Kadhalika unaposema Sumaye ameshindwa  kwenye uchaguzi huu sijui uanatafsirije ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu 2015.

Posti yangu moja hapa nimesema  walioshindwa katika uchaguzi wa mwaka huu ni Mamilioni ya Watanzania waliokuwa wanatamani mabadiliko ili waweze kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni yao. Lengo kupata serikali inayowajibika kwa wananchi--kuondoa pengo kubwa la kipato kati ya watawala wanaojitajirisha kufuru kwa fedha na mali za Tanzania ili hali mamilioni ya Watanzania wakibaki mafukara.

Hivyo, kumsodoa Sumaye kwa vile tu aliungana na UKAWA waliokuwa wanapigania maslahi ya Mamilioni ya Watanzania wanaotamani nchi  yao kuwa na Katiba mpya ni ushabiki wa kivyama ambao hauna tija kwa maslahikwa Tanzania na Watanzania wengi. Ni muhimu utambue kuwa maslahi ya Watanzania walio wengi ni muhimu kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja au chama cha siasa.

Na ni mtu  mwenye upeo mdogo wa uchambuzi wa masuala ya siasa na maendeleo ya nchi yetu ndiye peke yake  atakayethubutu kuwanyooshea vidole wanaCCM walioondoka kwenye chama hicho kwa lengo la kuchochea mabadiliko. Hii ni kwa sababu nchi haiwezi kupata maendeleo bila watu kuwa na fikra tofauti. Tafakari.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 10/29/15, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Sumaye Na Kisa Cha Mchimba Kisima..!
 To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, Wanazuoni@yahoogroups.com
 Date: Thursday, October 29, 2015, 6:25 PM

 Ndugu
 zangu,Fredrick
 Tluway Sumaye ni mmoja wa walioshindwa sana kwenye uchaguzi
 mkuu wa mwaka huu.Ni heri ya Lowassa na Kingunge
 kulikoni Sumaye. Nilibaki nikimshangaa Sumaye aliposimama
 majukwaani na kuiponda CCM huku akilaumu pia Katiba
 inayovikandamiza vyama pinzani.Katika uchaguzi wa mwaka huu yumkini wapiga kura
 wamewaadhibu watu wa aina ya Sumaye na kuwaonyesha, kuwa wao
 wapiga kura si wajinga.Nilimshangaa Sumaye na Kingunge kusimama majukwaani na
 kulaumu mfumo ambao wao walishiriki kuujenga na kuulinda.
 Kwa Sumaye na Kingunge wanapolaumu Tume ya Uchaguzi na
 Katiba ya Nchi ya mwaka 1977 wanasahau, kuwa wao wakiwa
 madarakani walikuwa na nafasi ya kuweka mazingira ya
 kufanyiwa mabadiliko.Ona
 Fredrick Sumaye, ukiacha mapendekezo ya Jaji Francis Nyalali
 ya mwaka 1992 ambayo yaliainisha sheria 40 kandamizi, na
 hata Sumaye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu mwaka 1995, sheria
 hizo 40 kandamizi alizikuta, hakufanya lolote.Mwaka 1998, Ben Mkapa aliunda Tume
 ya Jaji Kissanga iliyomkuta Sumaye akiwa Waziri Mkuu. White
 Paper ile ya Jaji Kissanga, mbali ya mambo mengine,
 ilipendekea pia Rais achaguliwe kwa kupata 50 plus asilimia
 za kura zote. Ikapendekeza pia Serikali tatu katika muundo
 wa Muungano. Nakumbuka pale Diamond Jubilee Hall, Ben Mkapa
 akiongea na wazee wa darisalaam aliinanga ripoti ya Jaji
 Kissanga akidai pia haikufuata adidu za rejea. Sumaye
 alikuwepo kama Waziri Mkuu, alikuwa na nafasi ya kuweka
 mazingira ya kurekebishwa kwa sheria hizo, lakini, wakati
 huo, alikaa kimya.Sumaye
 alikuwa bize akichimba kisima ambacho leo ameingia
 mwenyewe.Niwe mkweli kwa nchi
 yangu, Fredrick Sumaye wa leo, kama alitaka mabadiliko ya
 kweli, alipaswa kuendelea kubaki CCM na kuifanya kazi hiyo
 ndani ya CCM- kama ' Born Again Sumaye' . Angelikuwa
 na jukwaa pana zaidi na angeaminika zaidi.Ni dhahiri, kuwa matokeo ya leo
 yamemtumbikiza Fredrick Sumaye kwenye kisima alichokichimba
 mwenyewe. Inasikitisha.Ni
 mtazamo wangu.Maggid, 
 0754 678 252
 Iringa.

 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

0 comments:

Post a Comment