Hivi huyu Rais wa nchi anayetakiwa kujua kila cha jikoni ni kinyonga ambaye machio yake yanageuka mduara kuona pande zote au pweza mwenye mikono/mikia pande zote na macho kama kinyonga? Nini maana ya kuwa na Waziri, wakuu wa Mikoa, Wilaya; Mbunge, Diwania na watumishi wa ugani wa sekta mbali mbali pamoja na directorate zao na wahamasishaji? Mbona wabongo twapenda lawama hatuna zaidi ya negative orientation kwa kila kitu. Yaani kama ni mume na baba wa familia-ujue pini ya nepi ya mtoto inakaa wapi sio mama na housegirl kufahamu kiti na ujue mpaka kizoleo cha taka kwa muda huo kipo wapi. Si la kushangaza ukafika kijijini na Diwani au mbunge ukamuona naye anauliza maswali ambayo ni wajibu wake. ila, anafanya hivyo hapo kwa kupata/ili kupata sifa na ukaona watu wanamshangilia. Mfano ni ule wa -eneo letu mkoa huu una vijito/mito 50 inayoingia baharini lakini hakuna umwagiliaji-serikali inatufanyia nini? Kuna mazao yamejazana hapa hakuna soko-serikali inatufanyia nini? Muulize kama amekwisha kufika hata kwa bwana kilimo wakakaa na kupanga jinsi ya kuhamasisha wakulipa kujiunga kukodisha gari wakapeleke kwenye soko, wapate mkopo wa lorry la kati baadae special vehicle ya kusafirisha mazao yanayoharibika kama nyanya, kabishi etc. wapo wakulima wa Lushoto wafanyao hivyo. Kuhamasisha traditional irrigation system ambayo ipo TZ toka kilimo kianze duniani hadi leo. Hivi kweli Tibaijuka atapaka tu pekee kila kitu etc wengineo hawajui? Basi huko UN habitati alikotoka ni shirika la ajabu duniani. lakini hapa TZ, hata yale maeneo ya World Bank funded Sites and Services; Un-habitat SUDPF approach iliyopata sifa 1990s; NHC ya Mid 1970s; Squatter upgrading ya kuongeza barabara na kuweka umeme, EPM na ya sasa Community infrastrucural Upgrading Program (CIUP) Dar yote na Miji mingine ambayo CIUP hela la mkopo bank ya dunia na ni participatory na wanachangia na kuweka hela bank wenyewe-bado baada ya upgrading wanajaza takataka katika mitaro hiyo waliyogharimia na viosk kukaa barabarani na kufanya kinyume na bylaws waliotunga wenyewe. Kaione hii CIUP Manzese Uwanja wa Fisi, Manzese kwa Jongo. Pia kulikuwa na Mkopo wa worl bank wa sewerage rehabilitation, kuundwa kwa DSSD na sasa mipango shirikishi ya kuzoa takataka kwa kuupa madaraka Mtaa na wakazi kuunda CBO/NGO ya kuzoa taka (kujipa ajira na kuajiri vijana) na wakazi kulipia uzoaji taka-vimeshindikana!! Baadhi ya wananchi kuamka usiku kutupa viroba vya takataka barabarani ili asilipe 500/= kwa siku kutoka biashara yake. Kutoboa choo na mtaro kumwaga kinyesi na maji machafu ili asiite private sector tankers kunyonya uchafu ili asilipie. Yakifurika-serikali haitujali. Chandarua akipewa bure asipate matende na malaria-anafunikia mchicha na kuokotea chupa barabarani anajaza ndani ya chandarua ndio kibebeo! Ujenzi na uuzaji wa nyumba za NHC za bei nafuu mfano-Tabata, nenda kaangalie sasa uone kama ile design na makazi yapo ilivyotegemewa ili kutatua tatizo la nyumba kwa wasio uwezo. Zile nyumba za milion 3 sasa ni saluni za nywele, maduka, barabara zimezibwa wameweka vibanda yaani ni wazimu. Moto ukiwaka-hakuna pa kupita kuuzima. Na majengo kama hayo Mbezi beach na maeneo mengine wanakojenga kukopesha watumishi na raia-sheria iwe kali kwamba kama mtu akiziba njia, kubadili design na kuweka bar badala ya makazi; kuongeza majengo mengine mpaka maghorofa kwenye plot 100% kubadili site view na kufanya overload ya utilities-apigwe fine na vibomolewe kwa gharama zake. Ama sivyo-pamoja na effort zote za toka 1970 za NHC nyumba vyumba 6 na zile ndogo; juhudi za BRU-ARDHI; Habitat na SUDPF na sasa CIUP ya City Council na Halmashauri-hiyo Satellite Cities Ideology or Plan ni escape tu kutokana na kushindwa kushughulikia matatizo yaliyokuwa toka 1970 ya kutokuwajibika kwa wananchi (hasa kwa sasa) wanaoharibu city building and service plans na mfumo husika wa usimamiaji kushindwa kufanya kazi yake katika kusimamia mipango miji. Ni kama kukataa kufua nepi za mtoto kila wakati awekapo kinyesi na kutokumrekebisha atumie pot yake. Kwa vile anaweka kinyesi nguoni hivyo unamlala bila nguo na anashinda uchi kutwa-pamoja na risk zote unamwacha hivyo-escape usifue uchafu. Mh Tibaijuka sasa ameacha kubomoa majengo yaliyoziba njia, kubananisha au kujazwa ktk plot kinyume na city/area plot plan; kuwaondoa wa mabondeni wanaohamia kimakusudi anauza kariakoo ya NHC ya 60,000/= in 1974 sasa ni 1 billion anahamia Jangwani-Sunna, kigogo mkwajuni na Ilala-Baghdad, Mtoni Bondeni etc. Bila ya kuushughulikia -Uswahili na Swahili mentality ya Watanzania, hatutofika mbali. Tukitekeleza sheria-tutafika pazuri, kuogopana na visasi-tutabaki na kuwa kituko cha kucheka na hii E.A. Community ndio jamvi la wageni. TZ ni kuhama toka plan hii haijaisha au imevurugwa na kudandia ingine re-inventing the wheel always bila kutatua shina la tatizo. Ni mikopo na gharama kwa serikali na walipa kodi, ni mipango isiyo endelevu inaishia kati. Tutachekwa sana nchi jirani na nyinginezo, tutakuwa tukisifia miji na vijiji vya wenzetu kumbe nasi twaweza ila tu wa culture ya-haambiliki, tusiombenda ukweli. Hatuoni vibanzi vyetu machoni, hatujifunzi kutokana na makosa, daima ni kurudia makosa kutokana na mtazamo kuwa-daima mkosa si sisi ni wengineo nje ya sisi kwani sisi (wananchi) hatumo hatuhusiki. Kwa nini nchi hii Mungu asiizamishwe kisha kila kitu kije kipya yaani iundwe upya kuje na uzao mpya sio huu? --- On Tue, 28/5/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment