Mtu ambaye hajawahi kufika kusinu mika ya 1970s, 1980s, 1990s na 2000 hadi sasa anaweza akasema si uchochezi n i shida zao. na yule ambaye hajui maji ya mitambo ya Dar na umeme vinatoka wapi-anaweza akasema hivyo. Kwenda Mtwara kupitia Rufiji kwa gari ilichukua wiki in 1970 na kupitia Songea zaidi ya wiki. Labda upande Meli au ndege. Hata nyama ya kula kule ikipelekwea kwa ndege barabara hazikupitika kutokana na mtu Rufiji na eneo kubwa la mafuriko na milima ya Songea ya Lukumburu na utelezi. wanafunzi hasa wale wapya wa kwenda kusoma huko kulala njiani , njaa, ugeni-mimba zilikuwa njingi. Mpaka ikawa sheria form 1 waendao sekondaria wasichana Mangamba budi wapande ndege ay EA airways zamani kwa wale watokao dar na mikoa mingine ya mbali na kule ambao wangeanzia Dar safari yao kwa Bus la TTCompany. hali ya Mtwara na miradi iliyopo kabla hii ya Gas ni maendeleo mara dufu basi tu uzembe wetu waswahili wa kutokujituma. Lindi Town zamani ilikuwa imeendelea sasa ikiitwa PARIS. Maendeleo yakitokana na bandari, wahindi na waarabu hapo, secondary ya wasomi watanashati na majengo mazuri, barabara za lami. Fahamu shirika kubwa la maendeleo huko kusini ni Aga Khan Foundation lakini sasa kuna mashirika kibao na miradi ya value added crop products, ya health, vikoba, ufugaji mbuzi ng'ombe wa kisasa. Malori nenda rudi kutwa kusafirisha nazi, maembe etc. Ni wao wenyewe kugangamala, kuunda vikundi vya kuzalisha mali, vikampuni na kuchakalika. Power tiller za kulimia zinauzwa wilayani (milioni 6), Miradi ya Serikali ya Kilimo -DADPs; daraja refu la mkapa, bandari na daraja la msumbiji; miradi ya Mkuhumi na ya maji zamani ya Finnida walijitahidi. Mikorosho, miembe na minazi ndio usiseme bonde la Ruvuma na Rufiji linakutana. Bado tu irejeshwe meli ya abiria maana bandari kuu nyingine inajengwa Mafia kuunganisha, Rufiji, Kilwa kisiwani-Lindi-Mtwara. Kwa sasa Mafia ujenzi unachukua mchanga na kokoto Bagamoyo. huku mbali sana ukilinganisha na Kisiju ila bandari tatizo. Bandari zikiwa tayari mizigo na abiria kusafiri na biashara kama zamani wakati meli ya GVT ipo. Magereza ya huko Mtwara ni kilimo na ufugaji nao watapeta na kuweza hata kulima mimea ya kutengeneza dawa za vidonge na mazao ya kula maana usafiri upo na kuna chuo cha kilimo. Pia kusafirisha mazao na samaki nchi jirani. Mtu atakuwa anafika Mtwara kupitia Songea na Rufiji, Meli na Anga Efficiently na Mtalii anaunganisha Arusha-ZNZ-Mafia-Kilwa-Mikindani Mtwara. Nini kubomoa miundombinu ya hela za umma? Mipango ya serikali ni polepole nani alijua kama mwenge kutajengwa Viwanda na GVT offices (Cocacola, NECTA, Mawasilianoetc) au Mbezi tangibovu badala ya Puguroad na Posta? Nani alitegemea kuwa nchi hii itakuwa hata na private schools na universities wakati ilikuwa ni nUjamaa na GVt ownership? Ina maana tumebadilika kulingana na wakati na uchumi kidunia. Nao wa kusini wabadilike, kuna kila kitu wapo wamekalia na kulalia Almasi ya natural resources. Wasiiharibu. Badala yake-wazee wakae na vijana wao, wapange mikakati ya kuhakikisha wanajenga skills wafaidike. Kuna wazee wanajua kuzuka mazuria, magunia, kamba za makumbi ya mnazi; akina mama wanajua mikeka ya ukindu, makawa, vipepeo na mapambo kibao. Hiyo ni biashara kwa sasa makumbi wanayachoma moto tu. wasiuze ardhi kama wengineo, wajipande kupata haki waje kuwa wabia. Unachoma mahakama unaunguza hati na vidhibiti vyako vyote utakuja kuvipata wapi? Anayekuchochea na baada ya wewe kukamatwa au kuungua na kuumia-atakusaidiaje? Kama si uchochezi-uharibifu uliofanyika, mtu mwenye akili timamu asingefanya vile na si mara ya kwanza kufanya hivyo. Fikiria (na ushahidi ninao), hata mzazi kufungia mbuzi malishoni zisizagae kula mashamba ya wanafunzi shule ni tabu wanatishiana uchawi wakati wanafunzi wanakosa chakula ili wale mahudhurio na ufaulu uwe mzuri. Bwana mifugo anatishiwa asikimate kutoza faini na kuwafungia wasile mashamba. Hili wanalofanya-si ajabu, ni ufinyu wa fikra. --- On Tue, 28/5/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment