Thursday, 1 October 2015

Re: [wanabidii] Ugomvi wa Lowassa na Kikwete wawapumbaza Watanzania

Makala hii ni danganya toto. Hakuna ugonvi kati ya Kikwete na Lowassa. Huko ni kumpaka Kikwete kuwa ana chuki na LOwassa kama mlivyompaka Lowassa kwamba ni fisadi wa Richmond. Ni siasa nyepesi za maji taka, ambazo hazina nafasi Tanzania.

Kinachopiganiwa ni kitu kizito. Ni CCM iliyochafuka kwa ufisadi mfano EPA, Richmond na Tegeta Escrow ibaki madarakani ili kikundi cha watawala wachache kiendelee kujitajirisha kifisadi kwa fedha na mali za nchi huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanachama wa kawaida wanaCCM wakibaki katika mafuriko ya umaskini. Mwenye kuandika makala hii atambua kuwa fumbo mfumbie mjinga mwerevu analing'amua.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 10/1/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Ugomvi wa Lowassa na Kikwete wawapumbaza Watanzania
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "Mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 1, 2015, 1:11 PM








NIANZE makala haya kwa kusahihisha eneo moja dogo
katika makala
yangu ya wiki iliyopita iliyokuwa imebeba kichwa cha habari
kisemacho;
Hapa Kazi Tu, tutarajie nini? kwa lengo la kuweka kumbukumbu
sawa.



Katika makala hayo, kuna eneo niliandika: "Mwalimu
aling'atuka na
kukabidhi nchi hii kwa Mzee Mwinyi mwaka 1985, akiiacha
thamani ya
Shilingi ya Tanzania ikiwa juu, huku noti kubwa ya fedha za
Tanzania
ikiwa ni noti ya Sh 2,000 tu, sarafu ya senti tano (5) ikiwa
na thamani
ya kununua kitu dukani, noti ya Sh 100, maarufu mijini kwa
jina la Masai
kama inavyoitwa leo Msimbazi noti ya Sh 10,000 ikiwa na
thamani ya hali
ya juu pia.



"Ndani ya miaka mitano ya kwanza tu ya Mzee Mwinyi,
Tanzania
ikashuhudia anguko kubwa la viwanda, mashirika na kampuni za
umma.
Mfumuko wa bei ukapanda kwa kasi, Tanzania ikashahudia
serikali
ikiingiza noti ya Sh 5,000 kama moja ya mkakati wa kudhibiti
mfumuko huo
wa bei, kabla ya kuingizwa kwa noti ya Sh 10,000 katika
awamu ya pili
na ya mwisho ya miaka yake mingine mitano."



Usahihi ni kwamba Mzee Mwinyi alikabidhiwa nchi hii mwaka
1985, noti
kubwa ya fedha za Tanzania ikiwa ni noti ya Sh 100 na si Sh
2,000 kama
nilivyoeleza katika makala ile ya wiki iliyopita.



Baadhi ya wasomaji wangu wenye kumbukumbu nzuri
wamenikumbusha kwamba
wakati Baba wa Taifa anang'atuka uongozi wa taifa hili na
kumkabidhi
Mzee Mwinyi mwaka 1985, taifa lilikuwa na noti nne tu za Sh
5.00, Sh
10.00, Sh 20.00 na Sh 100, ambapo katika mwaka wake wa
mwisho huo wa
1985, noti ya Sh 5.00 iliondolewa na badala yake ikaletwa
sarafu ya Sh
5.00, maarufu wakati ule kwa jina la Gwala au Dala (dola),
ikiwa na
alama ya trekta, ishara ya nchi inayotegemea uchumi wa
kilimo cha
kisasa.



Sarafu hiyo ya Sh 5.00 au Gwala au Dala, ilikuwa sawa na
dola moja ya
Kimarekani, ndiyo maana vijana wa mijini wakaiita Dala,
wakiwa na maana
ya dola, lakini pia Sh 5.00 hiyo ndiyo iliyokuwa bei ya
nauli kwa mtu
mmoja kwenye mabasi ya mijini, na ndicho kisa cha mabasi
hayo ya mijini
kuitwa daladala kwa sababu ya nauli yake hiyo ya wakati
ule.



Kwa upande wa sarafu, wenye kumbukumbu sahihi
wamenikumbusha kwamba
Mwalimu aliacha sarafu tano tu, kwa maana ya sarafu ya senti
5.00
iliyokuwa na alama ya samaki, sarafu za senti 10 iliyokuwa
na alama ya
pundamilia, sarafu ya senti 20 iliyokuwa na alama ya ndege
aina ya
mbuni, sarafu ya senti 50 au thumani, iliyokuwa na alama ya
sungura na
Shilingi moja iliyokuwa na alama ya Mwenge.



Kwa mujibu wa wasomaji wangu hao wenye kumbukumbu bado za
tangu wakati
ule, takriban miaka 30 iliyopita, bei ya kinywaji baridi
aina ya soda,
ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi moja na thumuni (Sh 1.50)
katika karibu
maduka yote nchi nzima.



Nimekumbushwa pia na wasomaji wangu hao kwamba noti za
200, Sh 500,
1,000, 2,000 na 5,000 ziliingizwa na Serikali ya Mzee Mwinyi
katika
kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano tu, kati ya mwaka
1985 na
1990, wakati noti ya Sh 10,000 iliingia katika kipindi chake
cha pili
cha kati ya mwaka 1990 hadi 1995!



Sababu za kuongeza noti zenye thamani kubwa tano hizo
ndani ya miaka
yake hiyo mitano ya kwanza, zimetajwa kwamba ni kutokana na
hatua ya
serikali hiyo ya Mzee Mwinyi kukubali kutii na kutekeleza
masharti ya
Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa
Duniani (IMF),
yaliyotaka, pamoja na mambo mengine, kushushwa kwa thamani
ya Shilingi
ya Tanzania, jambo ambalo Baba wa Taifa alilipinga kwa nguvu
zake zote.



Nichukue fursa hii kuwaomba radhi wasomaji wangu wote kwa
upungufu huo
wa kumbukumbu za kitakwimu kuhusiana na sarafu na noti
katika kipindi
kile cha taifa hili kutoka mikononi mwa Mwalimu kwenda
mikononi mwa Mzee
Mwinyi.

Mada ya leo imebebwa na maneno; ugomvi wa Lowassa na Kikwete
wawapumbaza Watanzania.



Hili nimelipata sehemu fulani kwenye kijiwe cha mijadala ya
kisiasa,
inayojadili hali ya kisiasa ndani ya nchi hii, hasa katika
kipindi hiki
cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.



Kijiwe hicho ni maarufu kwa kahawa na michezo ya bao na
karata.
Kinapatikana wilayani Kinondoni, katika Jimbo la Kawe. Mzee
mmoja wa
makamo, baada ya kusikiliza ubishi wa kisiasa juu ya nani
zaidi kati ya
mgombea wa CCM, Dk John Pombe Magufuli na mgombea wa
Chadema, Edward
Lowassa, aliinuka kutoka kwenye benchi alilokuwa amekalia na
kutamka:



"Ninyi wote hapo ni wajinga tu. Mngekuwa mnafahamu kuwa
mnachokishabikia kwa sasa ni ugomvi binafsi wa madaraka kati
ya Mkwere
na Mmasai, msingepoteza muda wenu kumjadili Lowassa."



Katika kutoa ufafanuzi wake juu ya kauli yake hiyo, Mzee
huyo anasema
Lowassa ana hasira sana na Kikwete, hasa baada ya Mwenyekiti
huyo wa CCM
kuzuia jina lake lisifikishwe hata ndani ya kikao cha
Kamati Kuu mjini
Dodoma ili lijadiliwe na wajumbe wa kikao hicho na hatimaye
wajumbe
wenyewe waamue hatima yake.



Anasema hasira hizo zinazotokana na kitendo hicho cha Rais
Kikwete,
cha kutumia nguvu nyingi kuzuia jina la Lowassa kufikishwa
katika vikao
vya uamuzi vya chama chake, ndizo zilizomwongezea ghadhabu
na chuki
zaidi Lowassa, hivyo kuachana na CCM na kuhamia Chadema ili
tu
kumuonyesha Rais na

Mwenyekiti Kikwete, ni nani zaidi katika siasa za nchi hii
kati yao hao wawili.



Kwa mujibu wa Mzee huyo, tukio lile la Dodoma la jina la
Lowassa
kushindwa kufikishwa ndani ya vikao vikuu vya uamuzi vya
Chama, lilikuwa
ni tukio la tatu kwa mwanasiasa huyo kutoshwa na swahiba
wake mkuu
huyo, Rais Kikwete, jambo lililompandisha hasira Lowassa,
hivyo kuamua
potelea mbali, liwalo na liwe!



Binafsi, nakubaliana na hoja hizo za Mzee huyo. Watanzania
tumejikuta
hapa tulipo sasa, kutokana na kukumbwa na upepo wa ugomvi wa
madaraka wa
watu hawa wawili; Rais Kikwete na Lowassa, si kitu
kingine!



Kwa haiba na heshima aliyokuwa nayo Lowassa ndani ya CCM,
chama
kilichomlea na kumjenga kisiasa hadi kumfikisha hapo alipo,
isingekuwa
kazi rahisi kwa mbunge huyu wa Monduli kuchukua uamuzi mgumu
huo
alioufanya wa kuamua kuachana na chama chake hicho na
kujiunga na
Chadema, chama ambacho kwa karibu miongo miwili, viongozi
wake walikuwa
wakimchafua na kumdhalilisha mbele ya jamii ya
Watanzania.



Binafsi, naamini hata uamuzi wa Waziri Mkuu Mstaafu,
Frederick Sumaye,
wa kuamua kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na upinzani,
hautokani na
chuki na kukerwa na hatua ya chama hicho kukata jina lake
katika mbio
zake za urais mwaka huu mjini Dodoma, bali ni chuki na
hasira dhidi ya
Rais na Mwenyekiti Kikwete.



Nitaeleza. Imesemwa na bado inaendelea kusemwa kwamba
Lowassa na Rais
Kikwete ni marafiki wakubwa. Ni kutokana na urafiki huo,
uliowafanya
wawili hao, mwanzoni mwa miaka ya 2000 waingie katika
makubaliano ya
kirafiki ya kuachiana awamu za utawala wa nchi hii kwa
kuungana mkono na
kuunganisha nguvu zao za kisiasa.



Ni makubaliano hayo ya kirafiki kati ya wawili hao,
yalishuhudiwa bila
shaka na wapambe wao wa karibu, ndiyo yaliyomhakikishia na
kumwaminisha
Lowassa kwamba baada ya Rais Kikwete, yeye ndiye angekuwa
mrithi wake,
Rais wa Awamu ya Tano ya uongozi wa taifa hili.



Katikati kujiamini huko kwa Lowassa, kunakotokana na
makubaliano hayo
ya kirafiki, ya yeye kumwachia na kumuunga mkono rafiki yake
2005 ili
itakapofika mwaka 2015 achukue yeye nafasi kwa kuungwa mkono
pia na
rafiki yake huyo, ndiko kulikompa jeuri hadi kufikia
kukiambia chama
chake kwamba ndani yake hakuna yeyote mwenye uthubutu wowote
wa kukata
jina lake.



Lowassa hakutegemea kabisa kuona Rais na Mwenyekiti
Kikwete anayejua
makubaliano yao hayo, anaweza akamgeuka na kuwa upande wa
wanachama
wenzao kina Samuel Sitta, Bernard Membe na wangineo
waliokuwa hawataki
kabisa kusikia jina la Lowassa likiteuliwa na chama chao
kuwa mgombea
urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.



Hatua hiyo ya Rais na Mwenyekiti Kikwete, kuongoza na
kusimamia
mikakati ya kuhakikisha jina la Lowassa halipitishwi na
chama chake kuwa
mgombea mteule wa urais, lilikuwa ni pigo la tatu na mwisho
kwa
mwanasiasa huyo lililotonesha madonda ya mapigo mengine
mawili ya huko
nyuma, ambayo nayo yalisimamiwa na rafiki yake huyo.



La kwanza lilikuwa ni lile la mwaka 2008, pale Lowassa
akiwa Waziri
Mkuu, alipojikuta akijiuzulu wadhifa wake huo katika
mazingira ya
fedheha, aibu na udhalili.



Naamini, kabla ya kupatwa na mkasa huo wa kujiuzulu,
Lowassa hakuwa
amewahi kukaa chini na kufikiria dhamana ya nafasi hiyo
aliyokuwa
amepewa ya kuwa waziri mkuu, wala hakuwahi kufikiria kuwa
ingeweza
kutokea akakwamia njiani kabla ya 2015 kwa sababu kuamini
katika dhana
ya 'ushakaji' na Rais Kikwete.



Lowassa alijiamini na kujawa na jeuri ya hali ya juu
katika utendaji
wake wa uwaziri mkuu, akijua kwamba hakuna yeyote, awe
mteuzi wake
mwenyewe Rais Kikwete au mwingine yeyote yule anayeweza
kumwondolea
uwaziri mkuu wake kwa sababu ya makubaliano yao ya kirafiki
ya wawili
hao.



Alijua, hata akifanya chochote kile kibaya kwa serikali
yao,
angefumbiwa macho tu na mamlaka yake ya uteuzi kutokana na
'ushikaji'
wao. Akasau kitu kimoja muhimu katika uongozi wa nchi.
Dhamana! Ni nani
kati ya Lowassa na Rais Kikwete mwenye dhamana na nchi hii
na mwenye
dhamana na serikali yao.



Lowassa akasahau kwamba mambo yakiharibika, atakayeulizwa
na kulaumiwa
na umma wa Watanzania ni mkuu wa nchi, si yeye. Imani yake
hiyo ya
'kiushikaji' ilimfikisha mahali akatenda kinyume hata
cha maelekezo ya
serikali kupitia vikao vya Baraza la Mawaziri, hasa
lilipokuja suala la
kupata mitambo ya kufua umeme wa dharura kwa njia sahihi na
salama kwa
Serikali.



Lowassa akasimama kidete, kwa kutumia mamlaka yake ya
uwaziri mkuu,
huku akijua fika kuwa mamlaka ya juu yake ni ya
'kishikaji' akahakikisha
kwamba bila Richmond, bora nchi iingie gizani kwa kukosa
umeme!
Alikataa ushauri wa Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma
(PPRA),
akakataa ushauri wa Bodi ya Zabuni ya Tanesco, akasema hapa
ni Richmond
tu!



Kwa hiyo, hata baada ya kupatwa na mkasa huo wa Richmond
baada ya
Bunge, kupitia Kamati Teule ya Dk Harrison Mwakyembe,
kumkalia kooni na
kumtaka ajitathimini na kujipima kama anastahili kuendelea
na uwaziri
mkuu wake huo, kwa vyovyote vile, Lowassa alitegemea kuwa
atalindwa,
atapiganiwa na kukingiwa kifua na Rais Kikwete. Haikuwa
hivyo, Rais
Kikwete alimtosa likawa pigo kuu la kwanza kwa Lowassa!



Pigo la pili kwa Lowassa lilikuwa lile la uamuzi wa chama
chake,
ukiongozwa na Rais na Mwenyekiti Kikwete na mitume 12 wa
CCM, waliokuwa
wakimtaka Lowassa na washirika wake wajivue gamba kwa
kujiondoa wenyewe
kwa hiyari yao ndani ya chama hicho, kutokana na kuandamwa
na tuhuma za
ufisadi kila kona.



Lowassa akawekwa kati. Kule viongozi wa Chadema, huku
viongozi wa CCM,
wakiongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye. Lowassa
akala ganzi, akajikausha huku akijenga hoja za utetezi ndani
ya vikao
vikuu vya chama chake akitegemea kuungwa mkono kwa kupata
utetezi wa
Rais na Mwenyekiti Kikwete ndani ya vikao vyao hivyo, lakini
haikuwa
hivyo!



Ni baada ya pigo hili la tatu mjini Dodoma, la Lowassa
kukatwa jina
lake katika mazingira yenye utata, ndipo hapo amefunguka
akili na
kubaini kwamba kumbe rafiki yake huyo alikwishampuuza na
kuvunja urafiki
wao pamoja na makubaliano yao yote ya kupeana utawala wa
nchi hii kama
mali yao.



Lowassa, baada ya kufunguka akili na kubaini hali hiyo,
ameamua
kumtangazia vita ya kisiasa Kikwete. Kuhakikisha anatumia
rasilimali
zake zote, kuing'oa CCM madarakani ikiwa mikononi mwa
Kikwete bado!



Kama ilivyo kwa Sumaye, mgomvi wa Lowassa si CCM, bali ni
Kikwete.
Ugomvi wa Kikwete na Sumaye, ulianza mwaka 2005 wakati wa
mchakato wa
kusaka mgombea mteule wa urais ndani ya chama hicho.



Kwa wenye kumbukumbu Sumaye alifikia hatua ya kumwambia
Kikwete kwamba
mtu yeyote anayetafuta urais kwa kuwaua washindani wake kwa
kalamu
(magazeti), akipata urais ataua kwa risasi!



Chuki ile ya Sumaye ya mwaka 2005 dhidi ya Kikwete, bado
anayo hadi
leo baada ya jina lake kukatwa mjini Dodoma chini ya
usimamizi wa Rais
na Mwenyekiti Kikwete, ndiyo maana waziri mkuu huyo mstaafu
ameamua,
katika hilo la 'kumshughulikia' Kikwete, azike tofauti
zake na misimamo
yake dhidi ya Lowassa na kuungana na Lowassa.



Hapo ndipo Tanzania imefikishwa, hapo ndipo CCM
imefikishwa, na zaidi,
hapo ndipo Watanzania walipofikishwa na wanasiasa hao
watatu. Hivi
ugomvi huo wa mafahari wawili hawa, Lowassa na Kikwete una
tija gani
yoyote kwa taifa hili, kiasi cha kuwavuta baadhi ya
Watanzania wenzetu
kujitoa akili na kumshabikia mtu mwenye hasira na chuki zake

aliyedhamiria kununua urais kwa gharama yoyote ili kuwakomoa
na kulipa
visasi kwa wagomvi wake?



Nihitimishe makala haya kwa kusema kwamba wote
wanaomshabikia Lowassa,
kama anavyoonya mzee yule wa kwenye kijiwe cha kahawa,
wameamua kununua
ugomvi usiokuwa wa kwao. Ni vema wakakumbuka kuwa siku zote
mwenye kisu
kikali, ndiye mwenye kula nyama. Katika ugomvi huu, Lowassa
ameshika
makali, yatamkata tu!



Chanzo Raia
Mwema



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "Re: [wanabidii] Ugomvi wa Lowassa na Kikwete wawapumbaza Watanzania"

Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU

Ndalo;
Exactly there you are.
Nimekuelewa vizuri na hiyo ndio ingekuwa maana halisi ya mabadiliko.
Haya ya sasa ni kubadili chupa tu.
 
Reuben



On Thursday, October 1, 2015 4:50 AM, mary ndaro <mary.ndaro2@gmail.com> wrote:


Natamani kungekuwa na mbadala kwenye haya mabadiliko...Mimi binafsi watu waliotumua mfumo mbovu kutufikisha hapa haijalishi wanaahamia wapi...hao sio jibu wala mabadiliko tunayoyataka. Nakubali wananchi wamechoka na mfumo mbovu Wa ccm lkn majibu sio cdm chini ya EL
On 10 Sep 2015 15:40, "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ndugu Kim,

Neno mabadiliko  katika muktadha wa uchaguzi  Tanzania mwaka  huu 2015 linatumika kumaanisha wananchi kuchagua  serikali mpya  tofauti na serikali ya CCM iliyoko madarakani ambayo ilikataa kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi.

Katiba Mpya itaweka misingi ya kuzuia serikali kuwa chanzo  ufisadi wa  fedha za umma, watawala kujitajirisha na kuwatajirisha  wawekezaji kutoka nje  kwa kutumia rasilimali za nchi yetu  huku mamilioni ya wananchi wakibaki masikini wa kutupa.

Mfano ufisadi wa   mwaka jana 2014 wa Tegeta escrow bilioni 306, ufisadi wa  Richmond bilioni 172 mwaka  2008 na ufisadi wa EPA bilioni 133 mwaka 2005 na hakuna aliyefikishwa mahakamani.

Mabadiliko ya  kupata serikali  inayoongoza na  vyama vingine tofauti na CCM  ikiandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ---Katiba hiyo  itaweka misingi  ambayo pamoja na mambomengine madaraka ya Rais yatapunguzwa—kuzuia Rais kuwa Mungu mtu.

Kadhalika madadiliko  yataweka mihimili  isiyoingiliana  ya utawala—serikali—bunge na mahakama HIvyo  serikali  ikifanya ufisadi kama ule wa Tegeta escrow na EPA  watawala hawatakwepa mkono wa sheria  kama walivyokwepa.

Kadhalika mabadiliko   yatazuia   watawala wachache  wakijitajirisha kwa kutumia fedha za wananchi  kujilipa mishahara mikubwa, mafao na marupurupu wakati  watumishi wengine wa umma madaktari, wauguzi, walimu, polisi na wananchi wengi wakibaki maskikini.

Pia Katiba Mpya  itaweka misingi mizuri  ya kuwepo usawa wa kijinsia katika uongozi hasa 50 kwa 50 wabunge wanawake na wanaume  majimboni badala ya hili changa la macho ambalo baadhi ya vyama vinajidai eti kwa kuweka wagombea wanawake ni usawa wa jinsia.

Je inawezekana kuwa  na usawa wa jinsia endelevu kama haijaandikwa kwenye Katiba ya nchi? Kama kweli serikali CCM walikuwa wanataka nchi iwe na usawa wa jinsia katika uongozi ni kwa nini waliikataa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ambayo ilikuwa imependekeza utaratibu mzuri kabisa wa kupata asilimia 50 kwa 50 ya wanawake na wanaume bungeni kutoka majimboni?

Hivyo mabadiliko  wanayoyataka wananchi wanaosumbuliwa na umaskini hapa nchini   wao wenyewe wananchi  wamejipanga kuweka msingi wake hapo hapo tarehe 25 Oktoba 2015 kwa  kuiondoa CCM madarakani   na kuweka  serikali ya vyama vinavyounda UKAWA (CUF, NCCR Mageuzi, CHADEMA  na NLD) ambavyo  vilipigania  Katiba Mpya inayotokana na  maoni ya wananchi na vimeahidi  kwamba  wakichaguliwa Katiba Mpya  ya wananchi itaandikwa.

Hivyo yeyote anatumia neno mabadiliko kwenye kampeni zake ajuwe  akichaguliwa atatimiza yaliyobebwa katika tafsiri hii.  Kinyume chake hayo siyo mabadiliko wanayoyataka wananchi.   Mungu ibariki Tanzania.


Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 9/10/15, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Date: Thursday, September 10, 2015, 2:45 PM

 Kwanza
 MABADILIKO ni nini?
  Tukisema TUNATAKA MABADILIKO, maana yake ni
 nini? ya wapi? kwenye nini? yatamgusa nani? yatatuchukua
 muda gani? yatatokea tokeaje?
 Mabadiliko yaweza kuwa baya kwenda zuri au zuri
 kwenda baya, dogo kuwa kubwa au kubwa kuwa dogo, nyembamba
 kuwa pana au....

 Its all about "different" "utofauti wa hiki
 kilichopo". nikikosea nisahihishwe. mie sio mtaalam wa
 lugha!!
 Mnazi awaye yeyote iwe wa Chama au mtu, aandike
 akituelezea vizuuri na kwa ufasaha jinsi watakavyoleta
 MABADILIKO nchini. i mean ameshawishikaje kuwa mnazi wa
 flani/chama flani kuamini watafanya MABADILIKO ndani ya kila
 mmoja wetu ili tukuamini na kukufuata popote ulipo!! Wanazi
 wote hapa mkae mkijua nyie ni mawakala wa HAO mnaowasemea!!
 kwa sababu sie hatumjui yule/wale vizur zaidi yako, umeamua
 kuwa agent wake/wao ina maana unayajua ya kwake/kwao! Latin
 proverb "if you host a guest, host his dog"
 Tukibaki kuainisha MAHITAJI YA NCHI na
 MTU/CHAMA chenye SULUHU yake bila kuijadili, kuchambua na
 kuitafakari SULUHU yenyewe kwa kina, hatuna tofauti na mtu
 anaeajiri bila vyeti na interview. Akiulizwa kwa nini? ati
 " ameahidi ataongezea kampuni faida ndani ya miaka
 5" ****!!! Its the question of HOW not WHO!!! WHO will
 come later to filter HOW!!
 Watanzania tumelogewa wapi??? tunashindwa na
 hesabu ndogo ambazo tunazifanya kwenye maisha ya kila
 siku!!!!!????? Mpaka inakera.



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


Read More :- "Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU"

[wanabidii] Magufuli atashinda lakini mabadiliko hayaepukiki

NIANZE kwa kuwaomba radhi wasomaji wangu kwamba sitaonekana tena katika safu hii kuanzia toleo lijalo hadi mwanzoni mwa Desemba mwaka huu.

Sababu yenyewe ni kwamba narejea kijijini kwangu wiki hii kwa ajili ya shughuli zangu za kilimo. Msimu wa kilimo utakapomalizika nitarejea tena Dar kuendelea na shughuli za uandishi wa habari.

Nimeona niyaweke wazi hayo kwa sababu kutoweka kwangu ghafla kwenye safu hii (bila maelezo) kunaweza kutafsiriwa vibaya mitandaoni. Uongo unaweza kutembezwa mitandaoni kwamba nimehongwa fedha ili nisiendelee kuandika kwenye safu hii hadi uchaguzi mkuu umalizike.

Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikiitumia safu hii kuweka msimamo wangu bila kificho kuhusu mgombea urais John Magufuli ambaye, kwa mtazamo wangu, naamini ndiye anayeweza kuaminika kukabidhiwa dhamana ya kuiendesha nchi yetu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Johnson Mwambo

Walio nje ya taaluma hii ya uandishi wa habari pengine walishangaa kuona mwandishi wa safu (Mbwambo) anamuunga mkono moja kwa moja mgombea urais wa CCM na kumkosoa wa Chadema. Hiyo ilikuwa tu katika kutekeleza wajibu wangu – yaani kuchangia katika juhudi za kuepusha nchi yetu isitawaliwe na mtu mwenye tuhuma za miaka mingi za ufisadi.

Napenda kuitumia fursa hii kuwafahamisha wasomaji wangu ya kwamba mwandishi wa safu kumuunga mkono mgombea fulani wa urais ni jambo la kawaida kabisa duniani katika taaluma hii. Wanafanya hivyo kule Uingereza, wanafanya hivyo kule Marekani, na hata hapa Afrika ni hivyo hivyo.

Gazeti au mwanasafu wa gazeti anaruhusiwa kabisa kuunga mkono mgombea fulani wa urais (endorse a candidate) ili mradi tu afanye hivyo wazi bila kificho, na wasomaji waelewe msimamo wa huyo mwanasafu au hilo gazeti tangu mwanzo kabisa.

Kwa mantiki hiyo, napenda pia nifafanue kwamba bodi ya wahariri ya gazeti la Raia Mwema haikupewa maagizo yoyote na wamiliki wa gazeti hili ya kumuunga mkono mgombea yeyote wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Na badala yake wahariri wetu wamepewa maelekezo ya kuwatendea haki wagombea wote kwa kuzingatia zile kanuni kuu za habari zinazofuatwa kote duniani.

Kwa ufupi, Raia Mwema halina rasmi mgombea urais wake – yaani haliku-endorse yeyote - awe Magufuli, Lowassa, Mama Anna Mghwira nk. Hata hivyo, kwa wanasafu wanaoandika maoni binafsi wa Raia Mwema, wao wana uhuru huo wa ku-endorse mgombea urais wanayemtaka. Na kama nilivyoeleza, hicho ni kitu cha kawaida kabisa katika tasnia yetu duniani.

Ni kwa sababu hiyo nimekuwa nikiitumia safu yangu hii ya Tafakuri Jadidi kuwaeleza Watanzania maoni yangu binafsi kwamba Edward Lowassa hafai kuwa rais wetu mpya kwa sababu, licha ya kuandamwa na kashfa za ufisadi kwa miaka 20, hana jipya ambalo hakuweza kulitenda katika miaka yake zaidi ya 20 ya uongozi serikalini.

Wakati huo ndio msimamo wangu binafsi, wanasafu wenzangu wengine nao wamekuwa wakitumia safu zao kwenye gazeti hili hili kuwahamasisha Watanzania wamkatae Magufuli na CCM yake na wamchague Lowassa. Narudia tena; yote hayo ni mambo ya kawaida kabisa katika uendeshaji wa magazeti duniani.

Baada ya ufafanuzi huo, niseme kwamba ninaondoka Dar es Salaam kurudi kijijini nikiwa na imani kuwa mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli ataibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Nisichokuwa na uhakika nacho ni ushindi wake utakuwa ni wa asilimia ngapi.

Matokeo ya utafiti wa hivi karibuni wa asasi za TWAWEZA na IPSOS (SYNOVATE) yanaweza yasiwe na usahihi wa asilimia 100, lakini ukweli ni kwamba yanaakisi ukweli wa mambo ulivyo na utakavyokuwa Oktoba 25.

Sina lengo la kurudia hoja nilizokuwa nikizitoa kwa zaidi ya mwezi mmoja katika safu hii zinazonifanya niamini kuwa Magufuli atambwaga Lowassa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Itakuwa ni kuwachosha tu bure kurudia hoja hizo.

Hata hivyo, jambo la msingi la kukumbuka ni kwamba CCM kimejiandaa mapema kwa uchaguzi huu kuliko Chadema, na kinaendesha kampeni zake kisayansi; ilhali Chadema ni mbwembwe
na usanii tu.

Hata uamuzi wa Chadema wa hivi karibuni wa kuongeza angani idadi ya helkopta za kampeni ni sehemu tu ya hizo mbwembwe. Kuna wakati kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kiliwahi kutumia helkopta tatu lakini kikaambulia ushindi kwenye kata tatu tu!

Vyovyote vile, ubashiri wangu ni kwamba Magufuli atashinda. Ubashiri wangu mwingine ni kwamba kuhamia kwa Lowassa katika Chadema na kampeni ya urais aliyoifanya hakutaleta mabadiliko makubwa kwa chama hicho kwa maana ya kuongeza viti vya ubunge.

Kwa hiyo, kwa upande wa Chadema, ujio wa Lowassa utakuwa umekidhoofisha tu chama hicho kiutendaji kiuliko kilivyokuwa huko nyuma. Baada ya Oktoba 25, hali ya Chadema itakuwa mbaya, na kama nilivyopata kusema awali, sitashangaa ACT Wazalendo kikiziba baadaye pengo la Chadema kama chama kikuu cha upinzani nchini. Ni suala la muda tu hilo kutokea.

Na hili linanikumbusha maneno ambayo (sina hakika na ukweli wake) niliyoambiwa hivi karibuni na swahiba mmoja wa karibu wa Lowassa kwamba mheshimiwa huyo alipoamua kujiunga na Chadema ili agombee urais alijua fika kwamba hatashinda urais huo kupitia chama hicho!
Kwa mujibu wa maelezo yake aliyodai kaambiwa na Lowassa mwenyewe, swahiba huyo anasema Lowassa aliamua kugombea urais kupitia Chadema ili 'kukiadhibu' chama hicho kwa kumchafua kwa zaidi ya miaka tisa kuwa ni fisadi mkubwa.

Lakini pia aliamua kugombea urais kupitia chama hicho ili kupata fursa maridhawa ya kulipiza kisasi kwa Rais Kikwete ambaye aliweka kando uswahiba wao na kumtosa wakati ule alipoandamwa na kashfa ya ufisadi ya Richmond kiasi cha kumlazimisha kujiuzulu uwaziri mkuu.

Swahiba huyo wa Lowassa aliniambia ya kwamba 'adhabu' ya kwanza kwa Chadema ni huo mparaganyo uliosababisha Katibu Mkuu wa chama hicho aliyeshiriki sana kukijenga, Dk. Slaa kujiuzulu nafasi yake. Si siri kwamba mpaka sasa Chadema kinapwaya kwa kumkosa mtu wa sampuli ya Dk. Slaa kukaimu nafasi hiyo.

Adhabu ya pili au tuseme pigo la pili la Lowassa kwa Chadema ni hilo la 'kuwalazimisha' kina Mbowe na Lissu ambao walikuwa vinara wa kumwita fisadi, kuyameza matapishi yao wenyewe kwa kumsafisha wakati wa kampeni za urais kuwa si fisadi.

Kwa mujibu wa swahiba huyo wa Lowassa, hakuna jambo linalomfurahisha mgombea urais huyo wa Chadema hivi sasa zaidi ya kuwaona Lissu na Mbowe wakihaha jukwaani kujaribu kuuaminisha umma kuwa walikosea kumwita Lowassa fisadi. Yaani anafurahi kuwaona wakimeza matapishi yao wenyewe!

Kwa mtazamo wake, hiyo ni adhabu kubwa kwa kina Mbowe na Lissu kwa sababu heshima yao, weledi wao, uungwana wao, uadilifu wao na uaminifu wao kwa wanachama wa Chadema sasa uko shakani kwa sababu ya 'kumeza' matapishi yao hayo.

Kwa maana hiyo, Lowassa anajiona 'kalipiza kisasi' kwa vinara hao wa Chadema waliomwita fisadi, na kwa Chadema yenyewe ambayo anaamini itasambaratika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25!

Kuhusu kulipiza kisasi kwa Kikwete, swahiba wake huyo alinieleza ya kuwa kwa kugombea urais kupitia Chadema, Lowassa amepata fursa maridhawa ya kulipiza kisasi kwa kumpaka matope Kikwete wakati wa kampeni kuwa utawala wake wa miaka 10 ulikuwa hovyo kabisa, na kwamba ndiye aliyemlazimisha kuutia saini mkataba wa kifisadi wa Richmond. Fursa hiyo asingeipata kwa kiwango anachopata hivi sasa wakati wa kampeni za urais.

Kama hayo aliyonieleza swahiba huyo wa Lowassa ni ya kweli, basi inamaanisha kuwa tangu mwanzo Lowassa alijua ya kuwa hatashinda urais kupitia Chadema, na alichokifanya, hivyo basi, ni kutafuta tu fursa ya kulipiza visasi kwa Chadema na Kikwete.

Bila shaka anafanya hivyo kwa sababu hana cha kupoteza. Sitashangaa baada ya Oktoba 25 akajirudia Monduli kustaafu kabisa mambo ya siasa; maana atakuwa amemaliza 'kuwashughulikia' waliomwita fisadi kwa miaka tisa.

Kwa hiyo, imani yangu ya tangu mwanzo kabisa kwamba Lowassa hana na hatakuwa na faida yoyote kubwa kwa Chadema baada ya Oktoba 25 imeimarishwa na kauli hiyo ya swahiba wake huyo.

Tukirejea kwa CCM, ni kweli kuwa Magufuli atashinda lakini mambo hayawezi kubakia vilevile katika chama hicho na katika uendeshaji wa serikali yake. Kwa maneno mengine, mageuzi hayataepukika baada ya Oktoba 25 labda kama CCM kinataka kuishia vilikoishia KANU cha Kenya na ZANU cha Zambia.

Kwa maneno mengine, kampeni zilizoendeshwa na zinazoendeshwa na Lowassa na Chadema yake, ni maandiko mengine ukutani ambayo CCM lazima itakuwa imeyaona na kuyasoma vyema kwa sababu ya ukubwa wa herufi zake! Itakuwa imeweza kuyasoma hata kama ina makengeza!
Na maandiko hayo ukutani yanasomekaje? Yanasomeka hivi: "Ni wakati wa mabadiliko. Tumeichoka CCM kiasi kwamba hata shetani tuko tayari kumpigia kura aingie Ikulu".

Huo ni ujumbe mzito na unaotisha, na ni chama-mfu tu cha kisiasa ndicho kinachoweza kuudharau ujumbe wa namna hiyo. Watu wakishafikia hatua ya kukata tamaa kimaisha kiasi cha kusema kwamba hata kama ni shetani wako tayari kumwingiza Ikulu, ni lazima CCM kijiulize; kulikoni?

Na ujumbe huo si mtupu (hollow). Ni ujumbe unaoendana na hali ambayo imekuwa ikionekana katika mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa – yaani maelfu ya vijana waliokata tamaa ya maisha hufurika katika mikutano yake kumsikiliza.

Hata hivyo, kitakachoikoa CCM na kumfanya Magufuli ashinde urais Oktoba 25 ni kwamba, tofauti na Chadema, chenyewe kina muundo na mtandao wa hadi ngazi za vijiji na kata uliokiwezesha kuhahakikisha kila mwanachama wake amejiandikisha kupiga kura na siku ya kupiga kura kuhakikisha anajitokeza kupiga kura.
 
Chadema hakina muundo huo, na pia hakina mtandao huo wa hadi ngazi ya vijiji na kata. Kwa hiyo, kinabakia tu na imani (potofu!) kuwa vijana wote wanaofurika kwa maelfu katika mikutano ya kampeni ya Lowassa wamejiandikisha kupiga kura - kumbe ukweli ni tofauti kabisa na huo. Kasoro hiyo ndio iliyomwangusha Dk. Slaa mwaka 2010, na ndio itamwangusha Lowassa Oktoba 25.

Lakini Chadema na ACT Wazalendo nk haviwezi kukubali kubakia na udhaifu huo huo kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020. Bila shaka navyo vitajitahidi kuweka ofisi na mitandao ya hadi ngazi za vijiji na kata, na hivyo uchaguzi mkuu mwingine wa mwaka 2020 unaweza kuleta matokeo tofauti kabisa na tutakayoyapata Oktoba 25 mwaka huu.

Na ndiyo maana nasema ya kwamba kama CCM kinataka bado kuendelea kukamata dola, ni lazima baada ya Oktoba 25 kifanye mageuzi makubwa yatakayoipa serikali yake mwelekeo mpya wa kutatua kero ambazo kwazo zilifanya vijana wafurike katika mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa wakiwa na mategemeo kwamba ndiye atakayetatua matatizo yao.

Yaani kama kama tatizo ni ajira, basi serikali ijayo ya CCM ni lazima ionekane kweli kweli ikitatua tatizo hilo. Kama tatizo ni maji, basi lazima liwe historia ifikapo mwaka 2020. Au kama tatizo ni kilimo duni na ukosefu wa masoko kwa wakulima, serikali ijayo ya CCM lazima ilitatue hilo kabla ya mwaka 2020. Na kama tatizo ni kutamalaki kwa ufisadi nchini, basi lazima janga hilo liwe limemalizwa ifikapo mwaka huo.

Vinginevyo, CCM kitakwenda na maji ifikapo 2020! Safari hii kitashinda uchaguzi kwa taabu, lakini safari ijayo kisipojirekebisha kitashindwa kiurahisi. Ndiyo maana naamini ya kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Lowassa ameisaidia/ataisaidia mno CCM kujiona kilivyo, na ndio sababu naamini kwamba baada ya Oktoba 25 'kitajivua gamba' lake la zamani.

Vyovyote vile, kwa kuwa hii ndiyo makala yangu ya mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, napenda nirudie kile ambacho nilikisema huko nyuma. Kitu hicho ni kwamba wagombea wote wawili wa urais – Lowassa na Magufuli wana mapungufu ya wazi.

Niliandika huko nyuma kwamba pamoja na wote kuwa na mapungufu makubwa kuna mmoja ambaye ni nafuu kidogo kuliko mwenzake (a lesser devil). Ombi langu ni lile lile: Kwa kuwa wote wana mapungufu makubwa tutajitakia balaa kama tutampa lesser devil wetu wingi wa wabunge wa chama chake bungeni. Yaani akivurunda tutakuwa hatuna njia ya kumdhibiti bungeni kwa sababu atakuwa na wingi wa wabunge.

Kwa hiyo, salama yetu ni kwamba yeyote tutakayempigia kura – awe Lowassa au Magufuli, tusimpigie kura mgombea ubunge wa chama chake. Kwa mfano, kama kura ya urais unampa Lowassa, basi kura ya ubunge mpe mgombea wa CCM au ACT Wazalendo. Na kama kura yako ya urais unampa Magufuli, basi kura ya ubunge kipe Chadema au ACT Wazalendo.

Kwa namna hiyo, tutajipa matumaini (japo kidogo) kwamba yeyote atakayeshinda urais kati ya hao wawili, Bunge litaweza kumdhibiti kama ataongoza nchi hovyo. Lakini kama akiwa na wingi wa wabunge wa chama chake bungeni (kama ilivyokuwa kwa CCM kwa miaka mingi), hatutaweza kumfunga 'gavana' hata kidogo kama akivurunda.

Na mwisho kabisa nawatakia uchaguzi mwema na wa amani Oktoba 25. Nikirejea Desemba nitaendelea kuandika makala za kumkosoa (kwa hoja) mtawala wetu mpya bila kujali ni Magufuli au Lowassa; maana hiyo ndiyo kazi niliyojitwisha katika fani hii ya uandishi wa habari.

Sikuingia katika fani hii ili kuwaremba na kuwasifu watawala wakiwa madarakani. Nitawasifuje watawala kama wanatekeleza kile ambacho wananchi walikitarajia wakati wanawapa kura zao?
Nimeingia katika fani hii kuwakosoa watawala wanapovurunda ili wasilale usingizi; ilhali wananchi wanateseka. Kazi hiyo nitaendelea nayo bila kujali rais mpya ni Magufuli au Lowassa.

Vyovyote vile, rais akichapa vyema kazi hakuna 'habari' hapo. 'Habari' ni pale rais anapokuwa mvivu, mlevi, legelege, fisadi nk. Kwenye taaluma yetu ya habari tuna msemo maarufu; mbwa akimng'ata binadamu hakuna habari. Habari ni binadamu akimng'ata mbwa.

Kwa maana hiyo, nitaendelea kuwakosoa watawala wetu, na sitajali ni Magufuli niliyempigia kura yangu au Lowassa. Nitamkosoa (kwa hoja) yeyote kati ya hao wawili atakayefanikiwa kuingia Ikulu Oktoba 25; maana hakuna 'habari' katika kumsifu. Tafakari.
Read More :- "[wanabidii] Magufuli atashinda lakini mabadiliko hayaepukiki"

[wanabidii] Ugomvi wa Lowassa na Kikwete wawapumbaza Watanzania

NIANZE makala haya kwa kusahihisha eneo moja dogo katika makala yangu ya wiki iliyopita iliyokuwa imebeba kichwa cha habari kisemacho; Hapa Kazi Tu, tutarajie nini? kwa lengo la kuweka kumbukumbu sawa.

Katika makala hayo, kuna eneo niliandika: "Mwalimu aling'atuka na kukabidhi nchi hii kwa Mzee Mwinyi mwaka 1985, akiiacha thamani ya Shilingi ya Tanzania ikiwa juu, huku noti kubwa ya fedha za Tanzania ikiwa ni noti ya Sh 2,000 tu, sarafu ya senti tano (5) ikiwa na thamani ya kununua kitu dukani, noti ya Sh 100, maarufu mijini kwa jina la Masai kama inavyoitwa leo Msimbazi noti ya Sh 10,000 ikiwa na thamani ya hali ya juu pia.

"Ndani ya miaka mitano ya kwanza tu ya Mzee Mwinyi, Tanzania ikashuhudia anguko kubwa la viwanda, mashirika na kampuni za umma. Mfumuko wa bei ukapanda kwa kasi, Tanzania ikashahudia serikali ikiingiza noti ya Sh 5,000 kama moja ya mkakati wa kudhibiti mfumuko huo wa bei, kabla ya kuingizwa kwa noti ya Sh 10,000 katika awamu ya pili na ya mwisho ya miaka yake mingine mitano."

Usahihi ni kwamba Mzee Mwinyi alikabidhiwa nchi hii mwaka 1985, noti kubwa ya fedha za Tanzania ikiwa ni noti ya Sh 100 na si Sh 2,000 kama nilivyoeleza katika makala ile ya wiki iliyopita.

Baadhi ya wasomaji wangu wenye kumbukumbu nzuri wamenikumbusha kwamba wakati Baba wa Taifa anang'atuka uongozi wa taifa hili na kumkabidhi Mzee Mwinyi mwaka 1985, taifa lilikuwa na noti nne tu za Sh 5.00, Sh 10.00, Sh 20.00 na Sh 100, ambapo katika mwaka wake wa mwisho huo wa 1985, noti ya Sh 5.00 iliondolewa na badala yake ikaletwa sarafu ya Sh 5.00, maarufu wakati ule kwa jina la Gwala au Dala (dola), ikiwa na alama ya trekta, ishara ya nchi inayotegemea uchumi wa kilimo cha kisasa.

Sarafu hiyo ya Sh 5.00 au Gwala au Dala, ilikuwa sawa na dola moja ya Kimarekani, ndiyo maana vijana wa mijini wakaiita Dala, wakiwa na maana ya dola, lakini pia Sh 5.00 hiyo ndiyo iliyokuwa bei ya nauli kwa mtu mmoja kwenye mabasi ya mijini, na ndicho kisa cha mabasi hayo ya mijini kuitwa daladala kwa sababu ya nauli yake hiyo ya wakati ule.

Kwa upande wa sarafu, wenye kumbukumbu sahihi wamenikumbusha kwamba Mwalimu aliacha sarafu tano tu, kwa maana ya sarafu ya senti 5.00 iliyokuwa na alama ya samaki, sarafu za senti 10 iliyokuwa na alama ya pundamilia, sarafu ya senti 20 iliyokuwa na alama ya ndege aina ya mbuni, sarafu ya senti 50 au thumani, iliyokuwa na alama ya sungura na Shilingi moja iliyokuwa na alama ya Mwenge.

Kwa mujibu wa wasomaji wangu hao wenye kumbukumbu bado za tangu wakati ule, takriban miaka 30 iliyopita, bei ya kinywaji baridi aina ya soda, ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi moja na thumuni (Sh 1.50) katika karibu maduka yote nchi nzima.

Nimekumbushwa pia na wasomaji wangu hao kwamba noti za 200, Sh 500, 1,000, 2,000 na 5,000 ziliingizwa na Serikali ya Mzee Mwinyi katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano tu, kati ya mwaka 1985 na 1990, wakati noti ya Sh 10,000 iliingia katika kipindi chake cha pili cha kati ya mwaka 1990 hadi 1995!

Sababu za kuongeza noti zenye thamani kubwa tano hizo ndani ya miaka yake hiyo mitano ya kwanza, zimetajwa kwamba ni kutokana na hatua ya serikali hiyo ya Mzee Mwinyi kukubali kutii na kutekeleza masharti ya Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa Duniani (IMF), yaliyotaka, pamoja na mambo mengine, kushushwa kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania, jambo ambalo Baba wa Taifa alilipinga kwa nguvu zake zote.

Nichukue fursa hii kuwaomba radhi wasomaji wangu wote kwa upungufu huo wa kumbukumbu za kitakwimu kuhusiana na sarafu na noti katika kipindi kile cha taifa hili kutoka mikononi mwa Mwalimu kwenda mikononi mwa Mzee Mwinyi.
Mada ya leo imebebwa na maneno; ugomvi wa Lowassa na Kikwete wawapumbaza Watanzania.

Hili nimelipata sehemu fulani kwenye kijiwe cha mijadala ya kisiasa, inayojadili hali ya kisiasa ndani ya nchi hii, hasa katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Kijiwe hicho ni maarufu kwa kahawa na michezo ya bao na karata. Kinapatikana wilayani Kinondoni, katika Jimbo la Kawe. Mzee mmoja wa makamo, baada ya kusikiliza ubishi wa kisiasa juu ya nani zaidi kati ya mgombea wa CCM, Dk John Pombe Magufuli na mgombea wa Chadema, Edward Lowassa, aliinuka kutoka kwenye benchi alilokuwa amekalia na kutamka:

"Ninyi wote hapo ni wajinga tu. Mngekuwa mnafahamu kuwa mnachokishabikia kwa sasa ni ugomvi binafsi wa madaraka kati ya Mkwere na Mmasai, msingepoteza muda wenu kumjadili Lowassa."

Katika kutoa ufafanuzi wake juu ya kauli yake hiyo, Mzee huyo anasema Lowassa ana hasira sana na Kikwete, hasa baada ya Mwenyekiti huyo wa CCM kuzuia jina lake lisifikishwe hata ndani ya kikao cha Kamati Kuu mjini Dodoma ili lijadiliwe na wajumbe wa kikao hicho na hatimaye wajumbe wenyewe waamue hatima yake.

Anasema hasira hizo zinazotokana na kitendo hicho cha Rais Kikwete, cha kutumia nguvu nyingi kuzuia jina la Lowassa kufikishwa katika vikao vya uamuzi vya chama chake, ndizo zilizomwongezea ghadhabu na chuki zaidi Lowassa, hivyo kuachana na CCM na kuhamia Chadema ili tu kumuonyesha Rais na
Mwenyekiti Kikwete, ni nani zaidi katika siasa za nchi hii kati yao hao wawili.

Kwa mujibu wa Mzee huyo, tukio lile la Dodoma la jina la Lowassa kushindwa kufikishwa ndani ya vikao vikuu vya uamuzi vya Chama, lilikuwa ni tukio la tatu kwa mwanasiasa huyo kutoshwa na swahiba wake mkuu huyo, Rais Kikwete, jambo lililompandisha hasira Lowassa, hivyo kuamua potelea mbali, liwalo na liwe!

Binafsi, nakubaliana na hoja hizo za Mzee huyo. Watanzania tumejikuta hapa tulipo sasa, kutokana na kukumbwa na upepo wa ugomvi wa madaraka wa watu hawa wawili; Rais Kikwete na Lowassa, si kitu kingine!

Kwa haiba na heshima aliyokuwa nayo Lowassa ndani ya CCM, chama kilichomlea na kumjenga kisiasa hadi kumfikisha hapo alipo, isingekuwa kazi rahisi kwa mbunge huyu wa Monduli kuchukua uamuzi mgumu huo alioufanya wa kuamua kuachana na chama chake hicho na kujiunga na Chadema, chama ambacho kwa karibu miongo miwili, viongozi wake walikuwa wakimchafua na kumdhalilisha mbele ya jamii ya Watanzania.

Binafsi, naamini hata uamuzi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, wa kuamua kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na upinzani, hautokani na chuki na kukerwa na hatua ya chama hicho kukata jina lake katika mbio zake za urais mwaka huu mjini Dodoma, bali ni chuki na hasira dhidi ya Rais na Mwenyekiti Kikwete.

Nitaeleza. Imesemwa na bado inaendelea kusemwa kwamba Lowassa na Rais Kikwete ni marafiki wakubwa. Ni kutokana na urafiki huo, uliowafanya wawili hao, mwanzoni mwa miaka ya 2000 waingie katika makubaliano ya kirafiki ya kuachiana awamu za utawala wa nchi hii kwa kuungana mkono na kuunganisha nguvu zao za kisiasa.

Ni makubaliano hayo ya kirafiki kati ya wawili hao, yalishuhudiwa bila shaka na wapambe wao wa karibu, ndiyo yaliyomhakikishia na kumwaminisha Lowassa kwamba baada ya Rais Kikwete, yeye ndiye angekuwa mrithi wake, Rais wa Awamu ya Tano ya uongozi wa taifa hili.

Katikati kujiamini huko kwa Lowassa, kunakotokana na makubaliano hayo ya kirafiki, ya yeye kumwachia na kumuunga mkono rafiki yake 2005 ili itakapofika mwaka 2015 achukue yeye nafasi kwa kuungwa mkono pia na rafiki yake huyo, ndiko kulikompa jeuri hadi kufikia kukiambia chama chake kwamba ndani yake hakuna yeyote mwenye uthubutu wowote wa kukata jina lake.

Lowassa hakutegemea kabisa kuona Rais na Mwenyekiti Kikwete anayejua makubaliano yao hayo, anaweza akamgeuka na kuwa upande wa wanachama wenzao kina Samuel Sitta, Bernard Membe na wangineo waliokuwa hawataki kabisa kusikia jina la Lowassa likiteuliwa na chama chao kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Hatua hiyo ya Rais na Mwenyekiti Kikwete, kuongoza na kusimamia mikakati ya kuhakikisha jina la Lowassa halipitishwi na chama chake kuwa mgombea mteule wa urais, lilikuwa ni pigo la tatu na mwisho kwa mwanasiasa huyo lililotonesha madonda ya mapigo mengine mawili ya huko nyuma, ambayo nayo yalisimamiwa na rafiki yake huyo.

La kwanza lilikuwa ni lile la mwaka 2008, pale Lowassa akiwa Waziri Mkuu, alipojikuta akijiuzulu wadhifa wake huo katika mazingira ya fedheha, aibu na udhalili.

Naamini, kabla ya kupatwa na mkasa huo wa kujiuzulu, Lowassa hakuwa amewahi kukaa chini na kufikiria dhamana ya nafasi hiyo aliyokuwa amepewa ya kuwa waziri mkuu, wala hakuwahi kufikiria kuwa ingeweza kutokea akakwamia njiani kabla ya 2015 kwa sababu kuamini katika dhana ya 'ushakaji' na Rais Kikwete.

Lowassa alijiamini na kujawa na jeuri ya hali ya juu katika utendaji wake wa uwaziri mkuu, akijua kwamba hakuna yeyote, awe mteuzi wake mwenyewe Rais Kikwete au mwingine yeyote yule anayeweza kumwondolea uwaziri mkuu wake kwa sababu ya makubaliano yao ya kirafiki ya wawili hao.

Alijua, hata akifanya chochote kile kibaya kwa serikali yao, angefumbiwa macho tu na mamlaka yake ya uteuzi kutokana na 'ushikaji' wao. Akasau kitu kimoja muhimu katika uongozi wa nchi. Dhamana! Ni nani kati ya Lowassa na Rais Kikwete mwenye dhamana na nchi hii na mwenye dhamana na serikali yao.

Lowassa akasahau kwamba mambo yakiharibika, atakayeulizwa na kulaumiwa na umma wa Watanzania ni mkuu wa nchi, si yeye. Imani yake hiyo ya 'kiushikaji' ilimfikisha mahali akatenda kinyume hata cha maelekezo ya serikali kupitia vikao vya Baraza la Mawaziri, hasa lilipokuja suala la kupata mitambo ya kufua umeme wa dharura kwa njia sahihi na salama kwa Serikali.

Lowassa akasimama kidete, kwa kutumia mamlaka yake ya uwaziri mkuu, huku akijua fika kuwa mamlaka ya juu yake ni ya 'kishikaji' akahakikisha kwamba bila Richmond, bora nchi iingie gizani kwa kukosa umeme! Alikataa ushauri wa Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma (PPRA), akakataa ushauri wa Bodi ya Zabuni ya Tanesco, akasema hapa ni Richmond tu!

Kwa hiyo, hata baada ya kupatwa na mkasa huo wa Richmond baada ya Bunge, kupitia Kamati Teule ya Dk Harrison Mwakyembe, kumkalia kooni na kumtaka ajitathimini na kujipima kama anastahili kuendelea na uwaziri mkuu wake huo, kwa vyovyote vile, Lowassa alitegemea kuwa atalindwa, atapiganiwa na kukingiwa kifua na Rais Kikwete. Haikuwa hivyo, Rais Kikwete alimtosa likawa pigo kuu la kwanza kwa Lowassa!

Pigo la pili kwa Lowassa lilikuwa lile la uamuzi wa chama chake, ukiongozwa na Rais na Mwenyekiti Kikwete na mitume 12 wa CCM, waliokuwa wakimtaka Lowassa na washirika wake wajivue gamba kwa kujiondoa wenyewe kwa hiyari yao ndani ya chama hicho, kutokana na kuandamwa na tuhuma za ufisadi kila kona.

Lowassa akawekwa kati. Kule viongozi wa Chadema, huku viongozi wa CCM, wakiongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Lowassa akala ganzi, akajikausha huku akijenga hoja za utetezi ndani ya vikao vikuu vya chama chake akitegemea kuungwa mkono kwa kupata utetezi wa Rais na Mwenyekiti Kikwete ndani ya vikao vyao hivyo, lakini haikuwa hivyo!

Ni baada ya pigo hili la tatu mjini Dodoma, la Lowassa kukatwa jina lake katika mazingira yenye utata, ndipo hapo amefunguka akili na kubaini kwamba kumbe rafiki yake huyo alikwishampuuza na kuvunja urafiki wao pamoja na makubaliano yao yote ya kupeana utawala wa nchi hii kama mali yao.

Lowassa, baada ya kufunguka akili na kubaini hali hiyo, ameamua kumtangazia vita ya kisiasa Kikwete. Kuhakikisha anatumia rasilimali zake zote, kuing'oa CCM madarakani ikiwa mikononi mwa Kikwete bado!

Kama ilivyo kwa Sumaye, mgomvi wa Lowassa si CCM, bali ni Kikwete. Ugomvi wa Kikwete na Sumaye, ulianza mwaka 2005 wakati wa mchakato wa kusaka mgombea mteule wa urais ndani ya chama hicho.

Kwa wenye kumbukumbu Sumaye alifikia hatua ya kumwambia Kikwete kwamba mtu yeyote anayetafuta urais kwa kuwaua washindani wake kwa kalamu (magazeti), akipata urais ataua kwa risasi!

Chuki ile ya Sumaye ya mwaka 2005 dhidi ya Kikwete, bado anayo hadi leo baada ya jina lake kukatwa mjini Dodoma chini ya usimamizi wa Rais na Mwenyekiti Kikwete, ndiyo maana waziri mkuu huyo mstaafu ameamua, katika hilo la 'kumshughulikia' Kikwete, azike tofauti zake na misimamo yake dhidi ya Lowassa na kuungana na Lowassa.

Hapo ndipo Tanzania imefikishwa, hapo ndipo CCM imefikishwa, na zaidi, hapo ndipo Watanzania walipofikishwa na wanasiasa hao watatu. Hivi ugomvi huo wa mafahari wawili hawa, Lowassa na Kikwete una tija gani yoyote kwa taifa hili, kiasi cha kuwavuta baadhi ya Watanzania wenzetu kujitoa akili na kumshabikia mtu mwenye hasira na chuki zake aliyedhamiria kununua urais kwa gharama yoyote ili kuwakomoa na kulipa visasi kwa wagomvi wake?

Nihitimishe makala haya kwa kusema kwamba wote wanaomshabikia Lowassa, kama anavyoonya mzee yule wa kwenye kijiwe cha kahawa, wameamua kununua ugomvi usiokuwa wa kwao. Ni vema wakakumbuka kuwa siku zote mwenye kisu kikali, ndiye mwenye kula nyama. Katika ugomvi huu, Lowassa ameshika makali, yatamkata tu!

Chanzo Raia Mwema
Read More :- "[wanabidii] Ugomvi wa Lowassa na Kikwete wawapumbaza Watanzania"

[wanabidii] New content updates

Dear Wanabidii Africa Mashariki,

The following new content has been been added to our website:

Press Releases


01/10/2015 - La Banque africaine de développement a approuvé, le 30 septembre, un don du Fonds africain de développement (FAD) en faveur de la Côte d'Ivoire, pour un montant total de 8,226 milliards CFA pour le financement du projet d'appui au renforcement de la compétitivité du secteur industriel (PARCSI).

Categories: Côte d'Ivoire, Partnerships


01/10/2015 - The African Development Bank Group (AfDB) fast-tracked a grant of US $16-million on Wednesday, September 30, to help clean up the poorest suburbs of the Zimbabwean capital. The first stage of the project will concentrate on removing the raw sewage currently spilled into residential areas and securing the water supply for the most vulnerable areas of Greater Harare, home to 2 million people.

Categories: Zimbabwe, Water Supply & Sanitation, Human Capital Development, Health, Gender, Zimbabwe Multi-Donor Trust Fund, Zimbabwe Multi-Donor Trust Fund


You have received this email because you subscribed to content updates of the African Development Bank.

Manage my account

African Development Bank Group
Immeuble du Centre de commerce International d'Abidjan CCIA
Avenue Jean-Paul II
01 BP 1387
Abidjan 01, Côte d'Ivoire
Phone: +225 20 26 10 20
Email: afdb@afdb.org

This is an automated message, please do not respond. For all enquiries please contact afdb@afdb.org.

© African Development Bank Group - All rights reserved

Read More :- "[wanabidii] New content updates"

Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU

Natamani kungekuwa na mbadala kwenye haya mabadiliko...Mimi binafsi watu waliotumua mfumo mbovu kutufikisha hapa haijalishi wanaahamia wapi...hao sio jibu wala mabadiliko tunayoyataka. Nakubali wananchi wamechoka na mfumo mbovu Wa ccm lkn majibu sio cdm chini ya EL

On 10 Sep 2015 15:40, "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ndugu Kim,

Neno mabadiliko  katika muktadha wa uchaguzi  Tanzania mwaka  huu 2015 linatumika kumaanisha wananchi kuchagua  serikali mpya  tofauti na serikali ya CCM iliyoko madarakani ambayo ilikataa kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi.

Katiba Mpya itaweka misingi ya kuzuia serikali kuwa chanzo  ufisadi wa  fedha za umma, watawala kujitajirisha na kuwatajirisha  wawekezaji kutoka nje  kwa kutumia rasilimali za nchi yetu  huku mamilioni ya wananchi wakibaki masikini wa kutupa.

Mfano ufisadi wa   mwaka jana 2014 wa Tegeta escrow bilioni 306, ufisadi wa  Richmond bilioni 172 mwaka  2008 na ufisadi wa EPA bilioni 133 mwaka 2005 na hakuna aliyefikishwa mahakamani.

Mabadiliko ya  kupata serikali  inayoongoza na  vyama vingine tofauti na CCM  ikiandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ---Katiba hiyo  itaweka misingi  ambayo pamoja na mambomengine madaraka ya Rais yatapunguzwa—kuzuia Rais kuwa Mungu mtu.

Kadhalika madadiliko  yataweka mihimili  isiyoingiliana  ya utawala—serikali—bunge na mahakama HIvyo  serikali  ikifanya ufisadi kama ule wa Tegeta escrow na EPA  watawala hawatakwepa mkono wa sheria  kama walivyokwepa.

Kadhalika mabadiliko   yatazuia   watawala wachache  wakijitajirisha kwa kutumia fedha za wananchi  kujilipa mishahara mikubwa, mafao na marupurupu wakati  watumishi wengine wa umma madaktari, wauguzi, walimu, polisi na wananchi wengi wakibaki maskikini.

Pia Katiba Mpya  itaweka misingi mizuri  ya kuwepo usawa wa kijinsia katika uongozi hasa 50 kwa 50 wabunge wanawake na wanaume  majimboni badala ya hili changa la macho ambalo baadhi ya vyama vinajidai eti kwa kuweka wagombea wanawake ni usawa wa jinsia.

Je inawezekana kuwa  na usawa wa jinsia endelevu kama haijaandikwa kwenye Katiba ya nchi? Kama kweli serikali CCM walikuwa wanataka nchi iwe na usawa wa jinsia katika uongozi ni kwa nini waliikataa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ambayo ilikuwa imependekeza utaratibu mzuri kabisa wa kupata asilimia 50 kwa 50 ya wanawake na wanaume bungeni kutoka majimboni?

Hivyo mabadiliko  wanayoyataka wananchi wanaosumbuliwa na umaskini hapa nchini   wao wenyewe wananchi  wamejipanga kuweka msingi wake hapo hapo tarehe 25 Oktoba 2015 kwa  kuiondoa CCM madarakani   na kuweka  serikali ya vyama vinavyounda UKAWA (CUF, NCCR Mageuzi, CHADEMA  na NLD) ambavyo  vilipigania  Katiba Mpya inayotokana na  maoni ya wananchi na vimeahidi  kwamba  wakichaguliwa Katiba Mpya  ya wananchi itaandikwa.

Hivyo yeyote anatumia neno mabadiliko kwenye kampeni zake ajuwe  akichaguliwa atatimiza yaliyobebwa katika tafsiri hii.  Kinyume chake hayo siyo mabadiliko wanayoyataka wananchi.   Mungu ibariki Tanzania.


Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 9/10/15, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Date: Thursday, September 10, 2015, 2:45 PM

 Kwanza
 MABADILIKO ni nini?
  Tukisema TUNATAKA MABADILIKO, maana yake ni
 nini? ya wapi? kwenye nini? yatamgusa nani? yatatuchukua
 muda gani? yatatokea tokeaje?
 Mabadiliko yaweza kuwa baya kwenda zuri au zuri
 kwenda baya, dogo kuwa kubwa au kubwa kuwa dogo, nyembamba
 kuwa pana au....

 Its all about "different" "utofauti wa hiki
 kilichopo". nikikosea nisahihishwe. mie sio mtaalam wa
 lugha!!
 Mnazi awaye yeyote iwe wa Chama au mtu, aandike
 akituelezea vizuuri na kwa ufasaha jinsi watakavyoleta
 MABADILIKO nchini. i mean ameshawishikaje kuwa mnazi wa
 flani/chama flani kuamini watafanya MABADILIKO ndani ya kila
 mmoja wetu ili tukuamini na kukufuata popote ulipo!! Wanazi
 wote hapa mkae mkijua nyie ni mawakala wa HAO mnaowasemea!!
 kwa sababu sie hatumjui yule/wale vizur zaidi yako, umeamua
 kuwa agent wake/wao ina maana unayajua ya kwake/kwao! Latin
 proverb "if you host a guest, host his dog"
 Tukibaki kuainisha MAHITAJI YA NCHI na
 MTU/CHAMA chenye SULUHU yake bila kuijadili, kuchambua na
 kuitafakari SULUHU yenyewe kwa kina, hatuna tofauti na mtu
 anaeajiri bila vyeti na interview. Akiulizwa kwa nini? ati
 " ameahidi ataongezea kampuni faida ndani ya miaka
 5" ****!!! Its the question of HOW not WHO!!! WHO will
 come later to filter HOW!!
 Watanzania tumelogewa wapi??? tunashindwa na
 hesabu ndogo ambazo tunazifanya kwenye maisha ya kila
 siku!!!!!????? Mpaka inakera.



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
 Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Read More :- "Re: [wanabidii] 2015: NI KURA YA MAAMUZI MAGUMU"