Monday, 12 December 2016

[wanabidii] Fw: TUUTAFAKARI UZALENDO WETU KAMA WATANZANIA KATIKA MIAKA 55 YA UHURU WETU



On Monday, December 12, 2016 6:58 PM, Fred Alphonce <fredrick197958@yahoo.com> wrote:


Tanganyika ilipata Uhuru kutoka kwa mikononi mwa ukoloni wa Mwingereza mwaka 1961 Disemba 9. Wiki jana sisi Watanzania tulikuwa na wakati mwingine wa kusheherekea kumbukumbu hii iliyofanikishwa na viogozi waasisi wa Taifa la Tanganyika huru na baadae kuwa Tanzania kufuatia muungano na visiwa vya Zanzibar.
Mwalimu Julius Nyerere aliongoza vuguvugu la ukombozi wa Tanganyika kutoka katika ukoloni weupe akishirikiana na watu wengi wakiwemo akina Rashid Kawawa, Job Lusinde, Oscar Kambona, Abdalah Fundikira na wengine wengi .
Wiki jana siku ya ijumaa tulifanya maadhimisho ya uhuru wetu, ikiwa ni miaka 55 ambapo tunakumbuka Sir Richard Turnbull ambae alikuwa gavana wa mwisho aliekabidhi serikali kwa Waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika wakati huo akiwa ni Mwl. Nyerere. Ni vema Watanzania kujitathmini kiwango chetu cha uzalendo kwa nchi yetu na ikiwa ni pamoja na kujivunia utaifa wetu.
Kwa upande mwingine ni vizuri tukawa na muda wa kutafakari kwa pamoja tafsiri ya uzalendo kwa Taifa letu ili tunapojitathmini tuko wapi ndani ya miaka hii 55, tujikague na kujipima kuona kama tafsiri tuliyonayo ina akisi hali halisi ya uzalendo kwetu sote.
Naomba kutoa tafsiri ya uzalendo kwa kuzingatia mambo yote ya msingi yanayohitajika katika dhana na tafsiri ya uzalendo kwa taifa letu.
Uzalendo ni kuipenda Tanzania, kufanya kila jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linakuwa ni sababu ya kuletea maendeleo endelevu, heshima, kuilinda dhidi ya maadui zake, kuhifadhi rasilimali (ikiwa ni mali asili) zake kwa faida ya kizazi cha sasa hali kadhalika kizazi kijacho.
Ili kuongeza "nyama", ya tafsiri hii, naomba kumnukuu Rais wa sasa wa Marekani Bwana Barack Obama aliwaambia jambo kubwa raia wa Mamerekani kuhusu uzalendo kwa nchi yao.
We, the People, recognize that we have responsibilities as well as rights; that our destinies are bound together; that a freedom which only asks what's in it for me, a freedom without a commitment to others, a freedom without love or charity or duty or patriotism, is unworthy of our founding ideals, and those who died in their defense… 
Naomba kuiweka nukuu ya Barack Obama katika muktadha wetu hapa Tanzania…"Sisi, watu wa Tanzania tuna majukumu hali kadhalika haki ambazo hatima yetu imefungwa kwa pamoja, huu ni uhuru ambao tu tunaomba kwa ajili yetu, uhuru pasipo kujitoa kwa ajili yaw engine, uhuru pasipo upendo au kuwajali wengine au uzalendo hauna misingi ya itikadi yetu na kwa wale waliokufa kuutetea uhuru huu".
Watanzania, hatuna budi kusimama kwa pamoja kuijenga nchi yetu kwa nguvu zetu zote. Tanzania yenye neema itawezekana tukiacha kulaumiana na kutupiana madongo kila uchao. Itawezekana pale ambapo kila mmoja atatimiza wajibu wake wa kuleta tofali, huyu akileta saruji, huyu akileta maji, mwingine mchanga, mwingine nondo, na kokoto ili kujenga Tanzania yenye neema kwetu na vizazi vijavyo.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wajalie hekima na busara viongozi wetu kutuongoza ili kufikia ndoto ya Tanzania ya uhuru mbali na ujinga, maradhi na umasikini. 
Fred Matuja
fmatuja@hotmail.com


 
Fred 
MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
Change is Essence to maturation 


0 comments:

Post a Comment