Mama nkya mbona nyinyi na Ngos zetu za kupiga pesa hamuachi kuombaomba tena kwa huko huko inakoomba serikali au ndio nyani haoni kundule?
On Jun 26, 2015 4:11 AM, "fatma_elia via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
-- Warioba kwenye chama kubwa nahisi hata hiyo fomu hatapewa
Tuwashawishi hawa wengine ambao hawajamtaja mgombea wao wazungumze na huyu mzee ili tumpe miaka mitano tu ya kutunyooshea nchi kisha uchaguzi unaofuata watakuwa wamesoma na wanaweza kuwa na Candidate mzuri sana wa kumpokea kijiti
It is just a dream
Fatma
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
-----Original Message-----
From: "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 25 Jun 2015 14:41:12
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Tuwaulize wawania urais maswali magumu
Ndugu yangu, ukitaja Warioba si unataja mmoja wa wananchi. Ni nani katika chama hicho mwenye nia ya kuwasikiliza wananchi? Si ungewaona kwenye Bunge la Katiba?
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Thu, 6/25/15, 'fhkipamila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Tuwaulize wawania urais maswali magumu
To: "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, June 25, 2015, 9:16 PM
Ananilea dadangu mbona unasita
kutamka kuwa anayetufaa kwa sasa ni warioba
SENT FROM ALCATEL ONETOUCH TABLET
'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>Na zaidi tunahitaji Rais mwenye aliyeamua
mwenyewe na kwa dhati kabisa anaona uongozi wake
unaweza kutoa mchango mkubwa kwa nchi. Maana
yake awe ni mtu mwenye maono, utashi, mchapa kazi,
hekima, asiye mbinafsi na zaidi mwenye ujasiri wa
kusimamia serikali yake iwajibike kwa wananchi na siyo
kuwakandamiza na kuwaumiza kwa kutumia jeshi la polisi
wanapodai haki ya afya, elimu, barabara na ajira yenye staha
zinazotokana na utajiri wa nchi yetu na wala siyo kuomba
omba kwa wafadhili ambao nao wanakwapua mali zatu.
>
>Mtu anaweza kuwa msafi lakini moga wa kupigania haki za
wanyonge. Moga wa kufanya maamuzi mpaka amuulize
aliyemsukuma kugombea hiyo nafasi. Si mnakumbuka
Rais Kikwete awali alionekana kama vile alikuwa na
dhamira kusimamia upatikanaji wa Katiba Mpya
iliyotokana na maoni ya wananchi lakini mwishoni alikosa
ujasiri huo baada ya kuvutwa na chama chake maana Katiba ya
wananchi ingeondoa ufisadi unaokinufaisha chama chake?
Alikosa sifa moja tu--ujasiri
akaitumbukiza nchi kwenye mpasuko na zaidi
kachelewesha mabadiliko chanya --rasilimali za nchi
kunufaisha wananchi.
>
>Hivyo mgombea anaweza kuonekana ana sifa ya usafi
lakini akaogopa kubomoa mfumo unaofukarisha na kutesa
wananchi walio wengi huku wakitajirika watawala wachache.
>
>Sidhani kwamba kwa wananchi hoja ni mtu
anatoka Tanganyika au Zanzibar,Kusini au mashariki,
maana hoja siyo upande wa nchi atokako mtu katika
jamhuri yetu, bali ni mtu mweye uwezo na nia kiasi gani ya
kujitoa kuongoza nchi ili wananchi wengi wanufaike na
rasilimali za nchi na wasiwe wananyanyaswa na na kuteswa
wanapodai uwajibikaji wa serikali. Kuendelea
kufanya Ikulu kuwa sehemu ya majaribio ya
uongozi kutaendelea kutaigharimu nchi na
wananchi.
>Ananilea Nkya
> E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
>
>--------------------------------------------
>On Thu, 6/25/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>
> Subject: [wanabidii] Tuwaulize wawania urais maswali
magumu
> To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Thursday, June 25, 2015, 12:15 PM
>
> Evarist Chahali
>
> Ninaomba pia kutumia fursa hii kuwatakia ndugu zangu
> Waislamu mfungo mwema wa mwezi Mtukukufu wa Ramadhan.
>
> Katika makala ya hii nitaendelea kuzungumzia
> kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika
> baadaye mwaka huu. Na zaidi nitaelemea katika nafasi
ya
> urais, hususan mchakato unaoendelea ndani ya chama
tawala,
> CCM, ambapo hadi wakati ninaandaa makala hii, makada 37
wa
> chama hicho wameshajitokeza kuomba ridhaa ya chama
hicho
> kuwapitisha kuwania nafasi hiyo.
>
> Lakini kabda sijaingia kwa undani, pengine ni muhimu
> tukumbushane kuwa wakati idadi ya makada 37 (ambayo
huenda
> ikaongezeka) ni ya kihistoria, suala la kushtua zaidi
ni
> ukweli kwamba miongoni mwao ni pamoja na Makamu wa
Rais,
> Waziri Mkuu na mawaziri kamili saba, bila kujumuisha
manaibu
> waziri.
>
> Nimekumbushia suala hili kwa sababu ni vigumu kufahamu
> serikali yetu muda huu inaendeshwaje, hasa ikizingatiwa
kuwa
> Rais Jakaya Kikwete nae amekuwa katika safari za mara
kwa
> mara nje ya nchi (wakati ninaandika makala hii yupo
nchini
> India).
>
> Ukiondoa Makamu wa Rais, ambaye anakuwa kaimu Rais
wakati
> Rais anapokuwa nje, licha ya majukumu ya kiwaziri,
Waziri
> Mkuu na hao mawaziri wengine pia ni wabunge. Katika
hili ni
> vigumu kufahamu wanamudu vipi kugawa muda wao kwa
majukumu
> yao ya kiserikali, kiubunge na hayo ya kuwania
kuteuliwa
> kuwania nafasi ya Urais.
>
> Hata hivyo, si vigumu kudhani kwamba kwa muda huu,
akili na
> nguvu kubwa kwa makada wote waliotangaza nia zitakuwa
> zimeelekezwa kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Kwa
kiasi
> gani hilo linaathiri utumishi wao kwa umma, ni vigumu
kwa
> sisi wengine kufahamu.
>
> Nikirejea kwenye suala la makada wa CCM kutangaza nia
zao
> kuwania urais, jina lililosikika zaidi wiki iliyopita
> lilikuwa la Jaji Mkuu wa zamani, Augustino Ramadhan.
Japo
> jina lake lilishawahi kutajwa huko nyuma kama mmoja wa
watu
> 'wanaoweza kuokoa jahazi,' lakini kwa kiasi
kikubwa
> habari zilizosikika huko nyuma zilionekana kama tetesi
tu
> pasi uthibitisho.
>
> Angalau mara mbili, gazeti hili la Raia Mwema lilibeba
> habari zilizohusu uwezekano wa Jaji Ramadhani kugombea
urais
> kwa tiketi ya CCM.
>
> Binafsi, kwanza ninaheshimu uamuzi wa Jaji Ramadhani
kwani
> ni haki yake ya Kikatiba kuchukua uamuzi huo. Hata
hivyo,
> tayari kuna baadhi ya wananchi walioshtushwa kumsikia
Jaji
> huyo akielezea kuwa amekuwa mwanachama wa CCM tangu
miaka ya
> sitini.
>
> Kwanza ninadhani alipitwa tu kutoa kauli hiyo kwa
sababu CCM
> iliundwa mwaka 1977 baada ya TANU na ASP kuungana.
Kwahiyo,
> hakukuwa na CCM miaka ya sitini.
> Jaji huyo alieleza kuwa alijiondoa CCM mwaka 1992
kufuatia
> mabadiliko ya sheria, ambapo mfumo wa vyama vingi
> uliruhusiwa na hiyo kupelekea watumishi wa umma
kutoruhusiwa
> kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
>
> Japo Jaji Ramadhan anasema alijiondoa CCM wakati huo,
kuna
> wanaokwenda mbali zaidi na kutaka uthibitisho katika
suala
> hilo. Sote tunaijua Tanzania yetu, na kwa hakika
> tunawafahamu vema viongozi na wanasiasa wetu. Ni kwa
mantiki
> hiyo, kuna wanaotaka uthibitisho kuwa kweli Jaji huyo
> alijiondoa CCM na kutokuwa mwanachama wa chama chochote
cha
> siasa katika utumishi wake, ikiwa ni pamoja na Ujaji
Mkuu.
>
> Na kauli hiyo ya uana-CCM wake, kwa namna flani,
imerejesha
> tena suala la hukumu iliyotolewa na Jaji huyo kwa
> kushirikiana na majiji wengine dhidi ya kesi ya
Mchungaji
> Christopher Mtikila aliyetaka mahakama itamke kuwa
sheria
> inayozuwia mgombea binafsi ni kinyume cha Katiba.
> Pasi kuingiza kiundani katika kesi na hukumu hiyo,
binafsi
> ninaichukulia hukumu hiyo kuwa moja ya hiba (legacies)
kuu
> za utumishi wa Jaji Ramadhani.
>
> Kwa baadhi yetu tunadhani Jaji huyo angebaki shujaa
kwa
> demokrasia kwa sababu mfumo wa sasa unaolazimisha
wawania
> nafasi mbalimbali za uongozi ikiwa pamoja na urais
kuwa
> wanachama wa vyama vya siasa unatupunja fursa ya
kupata
> viongozi wa kisiasa wazalendo lakini wasiotaka
kujihusisha
> na vyama vya siasa.
>
> Hata hivyo, ili kumtendea haki, ni muhimu kutambua
kuwa
> hukumu hiyo haikuwa maamuzi binafsi ya Jaji Ramadhani
bali
> licha ya kuwahusisha majaji wengine pia, ilikuwa ni ya
> kisheria na sio hisia binafsi.
> Lakini kwangu, licha ya dalili zinazoonekana wazi kuwa
kana
> kwamba CCM imeshapata mgombea wake urais kufuatia
uamuzi wa
> Jaji Ramdhan kutangaza nia, nina wasiwasi kidogo
kuhusu
> ufanisi wake.
> Kubwa zaidi ni ukweli kwamba Idara ya Mahakama, ambayo
licha
> ya Jaji Ramadhan kuitumikia muda mrefu bali pia aliwahi
kuwa
> mkuu wake kwa maana ya ujaji mkuu, imeendelea kuwa moja
ya
> taasisi sugu kwa rushwa.
>
> Takribani kila ripoti inayotolewa kuhusu tatizo
la rushwa
> katika taasisi mbalimbali za serikali nchini mwetu,
Idara ya
> Mahakama haikosekani, na tena ikishika nafasi za juu.
> Mara baada ya kuchukua fomu kuomba CCM imteue kuwania
Urais,
> Jaji Ramadhan aliwaambia waandishi wa habari kuwa
atatumia
> uzefu wake kupambana na ufisadi. Swali la msingi:
uzoefu
> upi? Huohuo ulioshindwa ukiondoa Idara ya Mahakama
katika
> orodha ya taasisi zinazoongoza kwa rushwa?
>
> Kwa upande mwingine, Jaji Ramadhan alikuwa mjumbe wa
'Tume
> ya Warioba' iliyokusanya maoni kuhusu mabadiliko ya
> Katiba. Sote twakumbuka yaliyomsibu Jaji Joseph Warioba
na
> baadhi ya wasaidizi wake kupigania sio tu kazi nzuri
> iliyofanywa na tume yao bali pia mustakabali wa Katiba
> mpya.
> Kwanini Jaji Ramadhani amekuwa kimya sana katika suala
hilo?
> Je ukimya wake ulitokana na kufahamu kuwa siku moja
angeomba
> kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM?
>
> Na katika hilohilo, kwa vile mapendekezo ya Tume hiyo
> iliyomshirikisha Jaji Ramadhani yalikuwa muungano
wenye
> muundo wa serikali tatu, je kwa vile CCM ambayo jaji
huyo
> anaiomba ridhaa ya kumteua awe mgombea wake ina msimamo
wa
> serikali mbili kama ilivyo sasa, hilo si tatizo
angalau
> kimsimamo na kimtizamo?
>
> Hadi muda huu, Jaji Ramadhani ni Rais wa Mahakama ya
Afrika
> kuhusu haki za binadamu. Sihitaji kuorodhesha matukio
lukuki
> ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania
lakini
> miongoni mwa matukio makubwa ni pamoja na ukatili
unaofanywa
> na Jeshi la Polisi na rushwa (naam, rushwa sio tu adui
wa
> haki bali pia inachangia ukiukwaji mkubwa wa haki za
> binadamu).
> Je Jaji Ramadhani amekuwa wapi wakati ukiukwaji wa haki
za
> binadamu ukiendelea kushamiri na kuwa kama
umehalalishwa na
> Katiba yetu? Ni nani anaweza kusimama hadharani na
kuwaambia
>
>
> Watanzania kuwa 'Urais wa Jaji Ramdhani katika
Mahakama ya
> Haki za Binadamu Afrika umechangia hili na lile katika
> kutetea au kudumisha haki za binadamu nchini
Tanzania'?
> Niwe mkweli, binafsi ninamwona Jaji Ramadhani kama
Rais
> Kikwete alipojitambulisha mwaka 2005 kuwania urais na
> hatimaye kushindwa nafasi hiyo.
>
> Alionekana mtu mwadilifu, aliyeitumikia nchi kwa muda
mrefu,
> na pengine kubwa zaidi, msafi (asiye na kashfa). Sifa
hizo
> zinalingana na tunazosikia kuhusu Jaji Ramadhan. Je,
kwa
> mfano, kuwa msafi ni sawa na kuwa na uwezo wa kuongoza
> nchi?
>
> Lakini la mwisho kuhusu kada huyo ni taarifa za awali
kuwa
> amekuwa akiombwa na baadhi ya wana-CCM kuwania nafasi
ya
> urais (kuna wanaodai kuwa ndio mtu pekee anayeweza
kumudu
> 'kumzuia' Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa
asiingie
> Ikulu, na wengine wanasema Jaji huyo ndio 'msafi
zaidi'
> kuliko makada wengine wanazowania nafasi hiyo).
>
> Swali la msingi: je hao waliomwomba (kama ni kweli)
> hawafanyi hivyo kwa maslahi yao binafsi? Na je,
kumwomba
> huko (kama ni kweli) hakutopelekea urais wa Jaji
Ramadhan
> (iwapo atashinda) ukaishia kuwa kama 'deni la kwa
> wanamtandao' lilivyouandama utawala wa Rais Kikwete?
> Nimalizie makala hii kwa kuwakumbusha tena Watanzania
> wenzangu kuwa ni muhimu tujiulize na kuwauliza wawania
urais
> maswali magumu ili tusije kuishia kujiulaumu huko
mbeleni.
>
> Nchi yetu ipo katika wakati mgumu; umasini wa
kupindukia
> huku ufisadi ukizidi kuimarika, uhaba mkubwa wa
uzalendo,
> utovu mkubwa wa maadili ya uongozi ikiwa na pamoja na
uhuni
> katika matumizi ya fedha za umma, shilingi inayporomoka
kama
> ipo kwenye mashindano ya marathoni na kadhalika.
>
> Tunahitaji rais ambaye si tu anajua matatizo yetu bali
pia
> ana uzalendo na uwezo wa kukabiliana nayo. Hatuhitaji
Rais
> msafi lakini mwoga wa kupambana na maharamia
wanaoibomoa
> nchi yetu kila kukicha.
> Hatuhitaji mtu anayeahidi kupambana na rushwa ilhali
hana
> mfano japo mmoja wa jinsi alivyowahi kupambana na
rushwa.
>
> chanzo raia mwema
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and
hence
> statements and facts must be presented responsibly.
Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to
the
> Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit
> https://groups.google.com/d/optout.
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility for any legal consequences of his or her
postings, and hence statements and facts must be presented
responsibly. Your continued membership signifies that you
agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules
and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to
the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment