Thursday, 25 June 2015

Re: [wanabidii] Lowassa angeyafanya haya China?

Chama kizima ndio mzizi wa tatizo. Kama sivyo mbona wajumbe wote wana CCM katika Bunge Maalumu la Katiba walikataa Katiba ya Wananchi ambayo ililenga kudhibiti mfumo unaozalisha ufisadi na mafisadi? Kinachotakiwa kunyongwa ni chama kizima maana ndicho kimezalisha na kulea ufisadi na ufisadi unatumika kuzalisha viongozi mafisadi.

Kumbuka ufisadi wa shilingi bilioni 133 za EPA, Bilioni 222 za ujenzi wa Twin Tower BOT, Richmond bilioni 172 na hivi mwaka jana 2014 bilioni 306 za Tegeta escrow jumla fisadi hizi nne tu zilizo wazi (maana pengine ziko nyingine nyingi zimejificha) zimeyeyusha fedha za wananchi bilioni 833. Ni nchi gani duniani ambayo chama kinachotawala kinaweza kupoteza kifisadi fedha za umma nyingi kiasi hiki (zaidi ya dola milioni 416) na wananchama wake watoke hadharani bila soni kuomba tena kuongoza nchi kama siyo Tanzania peke yake?

Wanaoomba kwenda Ikulu kwani si baadhi yao walikuwa kwenye hiyo serikali iliyosababisha ufisadi huo wa kutisha katika kipindi cha miaka 10?

Hivyo kwa mtazamo wangu, chama kizima ndicho kinakumbatia ufisadi na ndicho kinastahili kunyongwa kupitia SANDUKU HURU LA KURA. Siyo sahihi wala haki kumtwisha mgombea mmoja tu kapu la samaki wabovu (UFISADI) na adhabu ya kunyongwa wakati wote kama chama wananufaika na mfumo huo wa kifisadi.

Mbona baadhi yawagombea wanawake na wanaume walikuwa ni Wabunge wa CCM katika Bunge Maalum la Katiba na walikataa Katiba Mpya ya wananchi ambayo ingedhibiti ufisadi wa kimfumo na wa kitaasi ambao unafanya viongozi wakishachaguliwa waishi peponi kwa fedha za umma na tena wengine bila kufanya kazi yoyote zaidi ya kulala bungeni au kujinafasi na safari za Ikulu wakati wananchi wengi wakiishi kama wako jehanamu ya moto katika nchi moja iliyojaa utajiri wa kila aina? Kwani anayekumbatia mfumo wa kifisadi na naye ni fisadi tu maana kuwepo kwake madarakani kumetokana na ufisadi wa kitaasisi?

Sisi wananchi HATUDANGANYIKI. kinachotakiwa kunyongwa kupitia sanduku la kura ni chama maana ndicho mzizi wa ufisadi. Hata baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliiona hatari hii ya ufisadi wa kutisha na kusema bila CCM kupasuka ufisadi utaendelea kuisumbua nchi yetu. Kwa mtazamo wangu tunajaribu kufunika kapu lenye samaki mbali mbali waliooza kwa kulipulizia pafumu ambayo ni kumnyooshea kidole samaki mmoja tu kwamba ndiye pekee kaoza. Huu ni unafiki na ukiachwa uendelee utaitesa nchi saaaaaaaaaaaaaana.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 6/25/15, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Lowassa angeyafanya haya China?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, June 25, 2015, 3:19 PM


Hii Kali
sana. Sina la Kusema. Nimefungwa mdomo. Mlongaji kamaliza.
Kazi kwenu wapiga KURA mpate KULA.

--------------------------------------------
On Thu, 25/6/15, 'mpombe mtalika' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Subject:
[wanabidii] Lowassa angeyafanya haya China?

To: "Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 25 June, 2015, 14:04

Na Navaya ole Ndaskoi

PHILEMON Ndesamburo, Mbunge
wa Moshi Mjini, ni miongoni mwa
wabunge
walioijadili Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge
iliyochunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha
Umeme wa
Dharura ulioipa ushindi Richmond
LLC ya Houston, Marekani
2006,
iliyosababisha, aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa,
kujiuzulu.


Ndesamburo aliliambia Bunge, "…nchi za wenzetu kama
za
China, wahujumu wa namna hii si kwamba
wanajadiliwa,
wananyongwa
hadharani."Mafisadi wananyongwa China. China
ilimhukumu kunyongwa Liu Han Februari 2015.
Han alikuwa na
shilingi trilioni 10. Gazeti
la Telegraph la Uingereza la
Februari 9,
2015 liliripoti kuwa Han alikamatwa 2013 na

kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.
Opereshini Fox Hunt; maana yake ni operesheni
Kamata Mbweha,
ni maarufu sana nchini
China.

Kamata Mbweha
imefanikisha kukamatwa watuhumiwa wa ufisadi
680 waliokimbilia Marekani, Canada, Australia
na kwingineko.
Walirudishwa China kujibu
mashitaka ya ufisadi.
Waliopatikana na
hatia tayari wamekwishakunyongwa. China

haitaki porojo.

Dk.
Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati, aliwasilisha
taarifa ya Richmond bungeni Februari 6, 2008.
Kamati
ilimtuhumu Lowassa, pamoja na mambo
mengine, kuvunja sheria
kwa kushinikiza
Tanesco kupokonywa jukumu la kutafuta

kampuni ya kufua umeme.Waziri wa Nishati na Madini,
alimwandikia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Julai
13, 2006,
kuwa, "Nimezungumza tena na
Waziri Mkuu (Lowassa) leo, juu
ya bei ya
mitambo ya Aggreko. Msimamo (wa Lowassa) ni ule
ule niliokueleza awali na
ameagiza…achukuliwe
Richmond."

Februari 7 2008 Spika,
Samuel Sitta, alimpa Lowassa nafasi
ya
kujitetea. Lowassa alikuwa na saa zaidi ya 14 kujipanga
kujibu. Badala ya kijitetea Lowassa
alijiuzulu. Alifahamu
kuwa asingeweza
kuwababaisha kisanii wabunge makini kama

akina Mwakyembe?

Lowassa
anadai kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond. Si
kweli. Magazeti yalianika bayana kashfa hiyo.
Lowassa anadai
kuwa alitaka kuvunja mkataba
wa Richmond akiwaeleza wenzake
"kuhusu
habari za magazeti." Alihisi mambo yamemkalia
vibaya siyo?

Lowassa, na wapambe wake, anajitahidi
kujionyesha kuwa yeye
ni mtu wa uamuzi
mgumu. Anatamani umma uamini kuwa Jakaya

Kikwete ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kuvunja mkataba wa
Richmond. Alipoona kuwa Kikwete havunji
mkataba kwa nini
hakujiuzulu? Mtu wa
"uamuzi mgumu" asingesubiri Kamati

Teule ianike uozo wa kashfa ili kujiuzulu.


Jitihada za Lowassa kujinasua katika
kashfa ya Richmond
iliyotia taifa hasara ya
zaidi ya shilingi milioni 152 kwa
siku kwa
miaka miwili zitagonga mwamba. Anadai alionewa.
Wakuonewa Lowassa? Wajumbe wa kamati hiyo wako
hai. Wabunge
waliokuwa wakali wa CCM wakati
huo kama Christopher Sendeka,
Lucas
Selelii, James Lembeli, Anna Malecela mpo? Dk. Slaa na
wapinzani wenzake waliokuwa bungeni Februari 6
na 7, 2008
watanyamaza?


Vita ya Richmond ina wapiganaji wengi.
Hivyo acha niandike
mambo mengine muhimu.
Kwanza, uadilifu wa Lowassa unatiliwa
shaka
na watu wengi. Septemba 15, 2007 pale Mwembe Yanga,
Temeke, Dar es Salaam na kwa ujasiri mkubwa
Dk. Slaa
alimtaja Lowassa katika orodha
aliyoita ya "mafisadi."
Na kwa jinsi
Lowassa anavyotamani kuwa rais, japo kwa saa
chache tu, angekimbilia mahakamani kama
angekuwa msafi.
Hakudiriki!

Wahariri wa baadhi ya vyombo
vya habari waliokutana na
Lowassa Dodoma
hivi karibuni nao pia waliutilia shaka na

kuhoji utajiri wake. Lowassa aliwajibu kuwa eti ana
"ng'ombe kati ya 800 na 1,000. Kwetu
Umasaini unapokuwa
kiongozi unapewa
ng'ombe ili usipate taabu kwa ajili ya

kuwakarimu wageni wanapokuja." Huu ni uongo. Hakuna
kitu
kama hicho Maasaini.


Lowassa anadiriki kuwakashifu wazalendo
wanaopinga wizi wa
mali za umma. Alisema,
"...kudanganya watu kwamba nikiwa

masikini ndiyo nafaa kuwa kiongozi ni ujinga." Hili ni
tusi la nguoni kwa wanaopambana na ufisadi.
Utajiri usio na
maelezo ni batili. Hakuna
anayewachukia matajiri waliopata
fedha zao
kwa juhudi na njia halali, wanaolipa kodi na
hawajawahi kupora ofisi za umma.
Bilionea Philemon Ndesamburo, kwa mfano, ni
kipenzi cha
watu. Hakuna anayeutilia shaka
utajiri wake. Anamiliki hadi
chopa.
Bilionea mwingine anayeheshimika ni Dk. Reginald
Mengi.

 
Mengi anamiliki hadi vyombo vya habari. Haiwezekani
kuwaorodhesha hapa matajiri wasafi Tanzania.
Ni wengi sana.
Nani mwenye mgogoro nao?
Pili, kinyume cha majigambo yake na
wapambe
wake kuwa eti ni mchapa kazi na mwenye kuchukua
uamuzi mgumu Lowassa ni adui mkubwa wa sheria
na utawala
bora.

Gazeti la Mwananchi la Mei 26, 2015 lilimnukuu
Lowassa
akiuelezea uviziaji wake wenye
shaka, "Chini ya uongozi wa
Rais
(Benjamin) Mkapa tukagundua hawa jamaa (City Water) ni
matapeli...tulifanya kikao saa tisa alasiri,
tukachukua
kibali cha kumkamata yule Mzungu
wa City Water na
tukamfukuza akaondoka siku
hiyo hiyo kwa ndege kurudi kwao,
tulifanya
saa tisa alasiri ili asiende mahakamani kupata
zuio, kwa hiyo tulivizia muda huo ili asije
kwenda kupata
zuio." Huo ni uviziaji wa
kimafia. Mzungu huyo hakupewa
haki ya asili
ya kusikilizwa. Si ajabu walimvizia asije

akafungua mkoba wa mabaya.

Tatu, Lowassa alikuwa kinara wa mtandao wa
uliomwingiza
Kikwete madarakani mwaka 2005.
Kikwete aliposhinda alimteua
Lowassa kuwa
Waziri Mkuu; kuthibitisha majigambo ya Lowassa
kuwa yeye na Kikwete "hawakukutana
barabarani."
Waliuhadaa umma kwa maneno
matamu kama vile "ari mpya,"
"nguvu
mpya," "kasi mpya" na porojo nyingine kama
"maisha bora kwa kila Mtanzania." Ni wazi
kuwa ahadi za
Kikwete zimebaki hivyo;
ahadi. Shilingi imeporomoka. Gharama
ya
maisha imepanda.

Lowassa
asivyojali hayo leo anajipitisha badala ya kuomba
radhi kwa kuudanganya umma.

Nne, baadhi ya waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo
vya
habari, wanajitahidi kumsafisha sana
Lowassa, lakini
Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, anawaonya Watanzania
dhidi
ya genge hili, "Hao wanaomtaka Lowassa ni wale
wanaojua watanufaika binafsi (Lowassa akiwa
Rais)."

Mwisho, ni
rahisi samaki kuishi nchi kavu kuliko Lowassa
kuhamia vyama vya upinzani hasa vile
vinavyounda Ukawa.
Kwanza, hadiriki! Pili,
hatakiwi kule. Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa
Chadema, ameshasema Lowassa "hafai kuongoza
Tanzania." Profesa Ibrahim Lipumba,
Mwenyekiti CUF, nae
amekaririwa mara kadhaa
akisema kuwa "Lowassa ni
msanii."

CCM, kwa vyovyote vile,
haina sababu ya kumwonea haya
achilia mbali
kumwogopa Lowassa.

Raia
Mwema
Toleo la 411
24 Jun
2015

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com

Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed to the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails

from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit

https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment