Thursday, 25 June 2015

Re: [wanabidii] CCM imethibisha kuwa mgombea wake ndiye Rais wa Tanzania na hakuna mtu maarufu zaidi ndani ya chama hicho

Mtu mwenye haiba, mvumivu, atakayepambana vilivyo na ufisadi ni Wilbrod Slaa.
em

Sent from my iPhone

> On Jun 25, 2015, at 6:45 AM, "'Lesian Mollel' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Unaadika makala as if wewe ur odering cc au as if unaakilisha maoni ya watanzania ni kosa,et wananchi wanategemea cc kuteua.......wewe sema mimi nategemea cc au nec kuteua......usisemee watu
> La pili huwez kupelekea watu jitu zoba zoba lisilo na sera au poyoyo akiambiwa hutubia analia au anaishia kulaum au kulalamika au kusema majungu oooh fulani mwiz wa richmond....au anakusanya watu,ooor kaiba esrow u know am always loughing tena jamaa ni lisomi nguli kabisa
> Napenda kuona mtu mwenye haiba,mvumilivu,asieropoka ovyo na mwenye sera,anaetoa matumain mapya kwa taifa hili ambalo halina tena matumain,ajira vijana washakata tamaaa,kina mama hoi,vitoto viko tu vinatumikishwa kuuuza kahawa na karanga kwenye mabaa na kufanya kaz za kitumwa majumbani......no hope at all halafu unapewa mic unaanza kulaum badala ya kutuambia utatutoeaje hapaaaaaaaaaaaaaaaa
> Lesian
>
> 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
>>
>> Sera inaonekana kuwa-waache wajimalize wenyewe!! Unapokuwa huwezi kumwambia uwazi usiyemtaka, unamuwekea mazingira tata anajimaliza mwenyewe. Ona utitiri wa mpaka mtu wa std 7 anaruhusiwa kuchukua form. Ina maana, misingi na vigezo vya uchaguzi hakuna? Hata matangazo ya kazi yana vigezo wanaangika-uwe na degree ya accounting na ukiwa na uzoefu wa miaka kadhaa ni added advantage. Ina maana uzoefu lakini uwe na usomi wa suala hilo uweze kuwa na ufanisi kazini ukashauri na kuongoza masuala ya account kampuni isiende mrama. Unapoacha watu 36 kuchukua form ya Urais kitu kikubwa hiki kuna mchezo wa foriti-tunahoji-pamoja na kukomaa kwa demokrasia-kuna dosari ktk chama chetu. Nini hasa ni nia ya kuacha iwe hivi? Mungu atusaidie.
>>
>> --------------------------------------------
>> On Thu, 25/6/15, 'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>>
>> Subject: Re: [wanabidii] CCM imethibisha kuwa mgombea wake ndiye Rais wa Tanzania na hakuna mtu maarufu zaidi ndani ya chama hicho
>> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
>> Date: Thursday, 25 June, 2015, 10:03
>>
>> Nimeipenda hii maada, hisia
>> zangu zinanitumakuwa ndani ya ccm hakuna kiongozi na wao
>> wanalijua hili. Kama wangekuwa naye mmoja wangemsimamisha
>> kwa kauli moja lakini kwa vile hawana kila mmoja anataka
>> kujaribu bahati yake hata kama anajiona hatoshi.Hawaaminiani
>> wenyewe kwa wenyewe je sisi tutawaamini vipi? Pamoja na
>> demokrasia lakini ni aibu kwa hili wanalofanya
>>
>>
>> From: mngonge franco
>> <mngonge@gmail.com>
>> To:
>> "wanabidii@googlegroups.com"
>> <wanabidii@googlegroups.com>
>> Sent:
>> Thursday, June 25, 2015 9:24 AM
>> Subject: Re:
>> [wanabidii] CCM imethibisha kuwa mgombea wake ndiye Rais wa
>> Tanzania na hakuna mtu maarufu zaidi ndani ya chama hicho
>>
>> Kwa maneno haya "Hadi sasa, CCM ni chama
>> pekee ambacho kimeweza kubeba haiba na taswira
>> ya utaifa na Chama chenye hazina ya viongozi, demokrasia
>> pana na mifumo". Fikiri na jiulize mara mbili mbili,
>> bila shaka hizi ni feeling na mapenzi ya mwandishi wa makala
>> hiyo haina uhalisia wala data zozote.
>>
>> Watu kukaa kimya au kuhudhuria mikutano kuna
>> vitu wanavitafuta, kama ni mfuatiliaji wa mikutano ya Kinana
>> utagundua watu wengi huenda kwenye mikutano kulalamika siyo
>> kusifia chama kwamba kinafanya vizuri. Ni haiba gani chama
>> kimebeba? Ni aina gani ya hazina ya viongozi waliobebwa na
>> CCM? Power mongers au viongozi waadilifu? Ni demokrasia gani
>> pana? Think twice before raising such concerns. Wako
>> watanzania zaidi ya milioni 45 sijui mwandishi ana uhakika
>> gani kama watu wote wenye talent na uwezo wa kuongoza wako
>> ndani ya CCM. Mara nyingi kiongozi mzuri hakurupuki na
>> kujitangaza kwenye vyombo vya habari bali uonwa na watu na
>> kuombwa awaongoze. Namalizia kwa maneno" Kibaya
>> ujitembeza na kizuri chajiuza"
>>
>> 2015-06-24 21:09 GMT+03:00
>> 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
>>
>>
>> KWA zaidi
>> ya mwezi mmoja sasa, macho na masikio ya Watanzania yamekuwa
>> yakielekezwa kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambako pazia
>> la uchaguzi wa ndani ya Chama wa kumsaka mgombea urais
>> lilifunguliwa. Hadi sasa wagombea wasiopungua
>> 38wamejitokeza, baadhi wametangaza nia na wengine wamechukua
>> fomu bila kutangaza nia hadharani kama wengine.
>>
>>
>>
>> Mwitikio wa wananchi na vyombo vya habari umekuwa mkubwa
>> sana kiasi kwamba wananchi na vyombo vya habari ni kama
>> wamesahau kuwa kuna matukio mengine yanaendelea nchini,
>> ikiwamo Bunge la Bajeti mjini Dodoma, ambalo kwa kawaida,
>> huvuta msisimko kuliko tukio lolote lingine la kitaifa.
>>
>>
>>
>> Somo kubwa ninaloliona ni ule ukweli kuwa pamoja na mawaa
>> yake, bado Watanzania wengi, wenye vyama na wasio na vyama,
>> wanaitazama na kuitumainia CCM kwa uongozi wa nchi. Ukweli
>> huu unaakisi ile nasaha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius
>> Kambarage Nyerere kuwa "Rais wa nchi yetu anaweza kutoka
>> Chama chochote cha siasa, lakini Rais bora wa Tanzania
>> atatoka CCM".
>>
>>
>>
>> Hadi sasa, CCM ni chama pekee ambacho kimeweza kubeba haiba
>> na taswira ya utaifa na Chama chenye hazina ya viongozi,
>> demokrasia pana na mifumo. Pengine ndio sababu wananchi na
>> vyombo vya habari hawaonyeshi shauku hiyo hiyo kwa michakato
>> inayoendelea ndani ya vyama vya upinzani ikiwemo vile
>> vinavyounda Ukawa, maana vina wigo finyu wa demokrasia ya
>> ndani ya vyama hivyo na isitoshe wagombea wake ni wale wale
>> wa siku zote. Na wengine wanapoonesha nia huundiwa zengwe na
>> kufukuzwa.
>>
>>
>>
>> Jambo ambalo halina mjadala ni kuwa Watanzania wanahitaji
>> mabadiliko ambayo yatawatoa katika lindi la umasikini na
>> ufisadi. Pamekuwepo na chambuzi mbalimbali hapo nyuma
>> zikihitimisha kwamba kiu hiyo ya Watanzania ya mabadiliko
>> ilimaanisha kuchoshwa na CCM, ama kuitoa CCM madarakani.
>> Tofauti na chambuzi hizo, tunachokishuhudia ni wananchi
>> kuendelea kuamini mabadiliko haya yanaweza tu kutokea na
>> kuletwa na CCM na si nje ya CCM.
>>
>>
>>
>> Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba
>> mwaka jana yanatupa fundisho kubwa. Kwa matarajio ya
>> wapinzani, kufanyika kwa uchaguzi ule baada ya Bunge la
>> Katiba kukamilisha Katiba Inayopendekezwa tuliyoambiwa
>> imechukiza wananchi, na kufuatiwa na mjadala wa Bunge wa
>> sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, CCM ingeanguka katika
>> uchaguzi wa serikali za mitaa. Pamoja na yote hayo, CCM
>> ilipata asilimia 84 ya kura ikilinganishwa na wapinzani
>> waliopata 16.
>>
>>
>>
>> Ukiachana na picha ya jumla inayoonyesha kuwa asilimia za
>> ushindi kwa wapinzani zilipanda kutoka asilimia nne mwaka
>> 2009 hadi 16 mwaka 2014, ukifanya uchambuzi wa kina wa
>> maeneo waliyoshinda wapinzani, utaona kwa kiasi kikubwa,
>> pale wapinzani walipoongeza viti, ushindi wao ni matokeo
>> zaidi ya hujuma zilizosababiswa na teuzi za ndani za CCM
>> kuliko jitihada na mkakati wa ushindi wa upinzani.
>>
>> Ndio sababu kuna mtawanyiko wa viti walivyoshinda
>> wapinzani ndani ya kata, wilaya na mikoa ambao ukiujumlisha
>> haukupi uhakika wa kusema kata, jimbo au wilaya fulani
>> imechukuliwa na upinzani. Kwa kifupi, ushindi wa upinzani
>> hauonekani kuwa ushindi wa kimkakati.
>>
>>
>>
>> Kabla ya CCM kutangaza ratiba yake ya uchaguzi, kulikuwepo
>> na manung'uniko na lawama kutoka kwa wananchi tena wengi
>> wasio wanachama wa CCM kuhusu kuchelewa kutangazwa kwa
>> ratiba ya uchaguzi wa CCM. Binafsi, haikunishangaza sana
>> kutokana na ukweli kuwa, kwa ukubwa wake na dhamana yake,
>> CCM si ya wana CCM peke yao bali inamhusu kila Mtanzania.
>>
>> Ndio kusema, yale maneno ya Baba wa Taifa ya mwaka 1995 kuwa
>> CCM ikishatangaza mgombea ni kama imeshatangaza Rais wa nchi
>> yetu bado yangali mujarabu hadi sasa.
>>
>> Katika uhai wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alishauri
>> kutokana na ule uhalisia kwamba upinzani wetu bado ni
>> dhaifu, na kusababisha mgombea wa CCM ndiye awe Rais, ni
>> muhimu kwa mgombea urais CCM akajulikana mapema zaidi,
>> ikiwezekana mwaka mmoja.
>>
>> Aliamini kwa kufanya hivyo, wananchi wote, hasa wale
>> walio nje ya CCM watapata pia muda wa kutosha kumjua na
>> kumpima, maana ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kuwa Rais
>> wao. Utamaduni huu wa Chama kutangaza mgombea wake mwaka
>> mmoja hutumika pia na jirani zetu wa Msumbiji.
>>
>>
>>
>> Utaratibu huo wa kumtangaza mgombea wa Chama mapema zaidi
>> unasaidia kukilazimu Chama kuchagua mgombea muadilifu maana,
>> wananchi wanakuwa na muda mrefu wa kumjua tofauti na
>> utaratibu wa sasa ambapo hutangazwa muda mfupi na kuingia
>> katika Uchaguzi Mkuu. Salama pekee katika utaratibu wa sasa
>> uko katika uthabiti wa mifumo na vikao vya Chama katika
>> kuhakiki, kuchuja na kuchagua mgombea. Kwa lugha nyepesi,
>> tumewekeza matumaini na imani yetu kwa wajumbe wa CCM
>> wasiozidi 2,300 kutuchagulia Rais wa Tanzania, na sisi
>> kubaki na jukumu la kumthibitisha tu.
>>
>>
>>
>> Katika zama hizi ambazo tunasikia kuwa wajumbe wa vikao
>> hivyo hupata nafasi hizo kwa fedha, na hivyo pia kununulika
>> na wagombea kwa fedha, kuna shaka kuwa wale wasio waadilifu
>> wanaweza kununua njia yao ya kwenda Ikulu. Maana
>> unachotakiwa kufanya ni kuwanunua wajumbe wasiopungua 1,500
>> tu. Ni kwa sababu hii, kumekuwepo na hofu kubwa miongoni mwa
>> wananchi kwamba vikao vya Chama vinaweza kuteleza na
>> kuchagua mgombea urais kwa vishawishi vingine nje ya sifa za
>> mgombea, mahitaji ya wakati na mahitaji ya nchi.
>>
>>
>>
>> Hofu hiyo ya vikao vya Chama kutumika kupitisha wagombea
>> wasio wasafi imetulizwa na kauli ya Mwenyekiti wa CCM,
>> Jakaya Kikwete. Wana CCM wengi na wananchi wamefarijika na
>> kauli ya Mwenyekiti kuwa Chama na vikao vyake havitayumba
>> katika kumchagua mgombea wa urais wa CCM. Muhimu zaidi ni
>> pale aliposema kuwa CCM haina nafasi kwa yule anayenunua
>> uongozi kwa fedha, au yule ambaye mienendo, matendo na haiba
>> yake haviakisi uadilifu na anachukiza wapiga kura ambao
>> wengi wao si wana CCM.
>>
>> Kauli ile ilituliza mioyo ya wengi maana kulianza
>> kuwepo shaka ya kuwepo nafasi kubwa kwa wenye fedha chafu na
>> tuhuma za kifisadi kupitishwa, hasa kwa tambo zao za
>> kukiweka Chama mfukoni au kutaja idadi wa wajumbe ambao wapo
>> katika daftari lao la malipo.
>>
>>
>>
>> Kufunguliwa kwa pazia la uchaguzi wa ndani ya CCM kumefufua
>> matumaini mapya kwa Watanzania wote. Kujitokeza kwa
>> watangaza nia wengi tena waliosheheni sifa kumeondoa ile
>> hofu iliyokuwa imetanda kuwa yuko mtangaza nia mmoja ambaye
>> tayari amekwishashinda na amekuwa akisubiri tu kukamilisha
>> ratiba ya chama atangazwe. Maana tumeshuhudia wenyeviti wa
>> CCM na wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM
>> wakisimama nyuma ya kila mtangaza nia aliyejitokeza.
>>
>>
>>
>> Tunachokiona katika mchakato huu wa kutangaza nia ndani ya
>> CCM ni ushahidi kuwa hakuna mwenye hatimiliki ya kugombea
>> urais wala mwenye uhakika wa ushindi. Zaidi, tumeona kuwa
>> ndani ya CCM hakuna ukame wa viongozi wenye uwezo wa
>> kumrithi Rais Kikwete kama tulivyokuwa tunaaminishwa na
>> kikundi fulani. Hii inaendelea kudhihirisha ubora wa CCM
>> kama chama kilicho imara kushinda mtu na kuwa hakuna mwana
>> CCM maarufu kushinda Chama.
>>
>>
>>
>> Haitashangaza pia, kwa wingi huu wa waliojitokeza,
>> hapatakuwa na ugumu wa kupata wagombea walio safi zaidi.
>> Maana wingi wa watangaza nia unaondoa ile sababu ya kufumba
>> macho na kumpeleka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu mgombea hata
>> yule asiyefaa kwa kisingizio aidha cha uchache wa wagombea
>> wenye sifa, au uchache wa wagombea waliojitokeza. Wana CCM
>> na wananchi hawatarajii kuona mgombea mwenye madoa mengi
>> miongoni mwa wale watakaopita katika mchujo wa kwanza wa
>> Kamati Kuu, maana walio safi na wenye sifa wamejitokeza
>> wengi wa kutosha hadi sasa.
>>
>>
>>
>> Macho, masikio na mioyo ya Watanzania imeelekezwa CCM. Ni
>> matumaini ya Watanzania kuwa CCM haitawaangusha. Watanzania
>> wanatamani CCM iendelee kuwa madhubuti, maana wanaamini,
>> bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba.
>>
>>
>>
>> --
>>
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>>
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
>> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>>
>>
>> Disclaimer:
>>
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
>> for any legal consequences of his or her postings, and hence
>> statements and facts must be presented responsibly. Your
>> continued membership signifies that you agree to this
>> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
>> Guidelines.
>>
>> ---
>>
>> You received this message because you are subscribed to the
>> Google Groups "Wanabidii" group.
>>
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
>> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>>
>> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>> --
>>
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>>
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
>> kudhibitisha ukishatuma
>>
>>
>>
>> Disclaimer:
>>
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
>> for any legal consequences of his or her postings, and hence
>> statements and facts must be presented responsibly. Your
>> continued membership signifies that you agree to this
>> disclaimer and pledge to abide by our Rules and
>> Guidelines.
>>
>> ---
>>
>> You received this message because you are subscribed to the
>> Google Groups "Wanabidii" group.
>>
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
>> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>>
>> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>> --
>>
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>>
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>>
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
>> kudhibitisha ukishatuma
>>
>>
>>
>> Disclaimer:
>>
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
>> for any legal consequences of his or her postings, and hence
>> statements and facts must be presented responsibly. Your
>> continued membership signifies that you agree to this
>> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>> ---
>>
>> You received this message because you are subscribed to the
>> Google Groups "Wanabidii" group.
>>
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
>> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>>
>> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment