Thursday, 11 June 2015

Re: [wanabidii] huyu ndiye pinda anayeutaka urais wa Tanzania

Mbona wanazidi kuongezeka? NEC itakuwa na utata kuchagua. Kwa sasa tunahitaji Rais zaidi ya Kagame dictator wa hali ya juu. Pia, Waziri Mkuu awe mkali asiye mwoga. Kutokana na kuwa, TZ ina kila kiyu nchini lakini hata extension staff hawafanyi kazi. Yupo kijijini hana mobilization yoyote, ana hair saloon, duka la dawa, dula la mitumba, bodaboda au bajaji anauza mchele hafanyi kazi ipasavyo. Mwingine anakaa Tarafani sio Katani eti nyumba za umeme hakuna ambapo kwa wazazi wake kijijini ukerewe au msolwa nyumba yao hovyo na wala hana maji, choo bora wala umeme. Vijijini aliko unakuta kuna nyumba nzuri za kupanga, kodi shs 5-10 kwa mwezi na wengine wana solar wanaonyesha video au taa za betri. Hawa wanataka PMO dictator aziambie wizara zifukuze wafanyakazi wasioishi katika maeneo yao bali wanakaa miji midogo au ya wilaya kwa visingizio mbali mbali.

Inawezekana kuboresha kilimo, nyumba, ufugaji kama extension staff watatiziza wajibu wao. Ukifika wewe mgeni kwa wiki moja ukawezesha kuhamasisha wanakijiji na kujenga choo cha shule ukajitolea kuchoresha design na kuilipia na kikajengeka hata darasa-utaona ile hela uliyojitolea inaingizwa ktk bajeti ya kijiji au kata wanadai warejeshewe; viongozi (M/Kiti kijiji, Diwani, Mbunge) wanatumia kuonyesha hiyo kama ndio mradi wao walioufanikisha-WIZI MTUPU na UZANDIKI. Tupo tupo tu tumebweteka.

Aje PMO na Rais wake wawezeshe kujengwa nyumba za police, FFU, JWTZ askari wake wasikae mitaani bali ktk nyumba za kambi. Hii itawezesha ufanisi wa kazi zao na kuwalinda. Askari hawezi kupambana na majambazi, kukimbizana na kubotana na wafanyabiashasha waliovamia eneo, au boda boda waliofanya vurugu halafu akarudi kukaa ktk nyumba ya kupanga mtaani manzese au eneo la uraiani. Anamkamataje mtoto kibaka, jambazi ambaye baba yake ni land lord wake? Kisha-arudi kulala hapo? Ni wazi atauawa. Nyumba zile za wakoloni za railway, police za vibanda ambazo paa zake za bati au vigae zimeshikiliwa na matofari juu ya paa, zinavuja, vyoo vimelala upande havifai kutumika; sare zao za kuvaa zinawabana na viatu vimelala upande-hakuna ufanisi hapa ni kufanikisha rushwa kutokana na frustration za kazi na maisha magumu. Mtumieni Mr Mchechu awajengee nyumba bora, kuwawekea canteen ya kula na kunywa kwa apendae ili waache kunywa pombe na raia na kuwa kundi moja bar na uniform
zao. Wawe na maduka yao ya bei rahisi na marufuku yeye kununua jumla akauze gengeni. PMO an Rais atakayerudisha JKT kuanzia baada ya kumaliza sekondari na kuhakikisha wanalima yale matuta ya kilometa moja kwa mkono na trekta ili tuwape vijana utambuzi na kupenda kilimo sio kuona bodaboda tu na kuuza vyupi vya mitumba, vipochi ndio ajira, kujenga ari ya utanzania kuipenda nchi sio kufurahia ujambazi na maandamano. Viongozi wasionyeshe huruma kwa kulia hadharani bali kuweza pia kuwabana watendaji na kuhakikisha wahalifu kesi zao hazichukui miaka.

Mzazi/mlezi anabaka mwanae kisha ndugu wanamuwekea dhamana na kumtoa au kukataa kufika mahakamani kutoa ushahidi; mzazi anashiriki albino ambae ni mwanae/ndugu kukatwa viungo au kuuawa halafu kesi ichukue karne inakuwaje? Mume anamwagia maji ya moto mkewe kisha ukoo upo kesi inasuasua; bibi mlezi/mama, baba anamchoma moto mtoto, anamfungia ndani ya box ndugu wanajua kuwa mtoto wa mwenzao kafichwa ndani hawamuoni ije mpaka jirani ndio wafichue siri-kamata hao ndugu wa karibu, mke na mume funda ili masuala haya yaishe. Boresha vituo vya ustawi wa jamii na malezi ya watoto yatima hao waliobaki wakalelewe. Idara ya Social Welfare na vyuo vyake, vituo vyake vifufuliwe-vimekufa hata taasisi za kulea wazee zipo kama mabanda ya Mbwa-WHY na PMO mwenye huruma yupo au alikuwepo? Vituo vya kulea wenye UKOMA ndio balaa-Why???? Tuna JKT, JWZ, NHC kwa nini nyumba zisiwe bora, magodoro, vyoo na kuna vyandarua vya bure? Kwa nini JKT, Magereza isilime mashamba yao na ya
mamlaka nyingine wakalisha vituo vya yatima, wazee na wenye ukoma? SIKIELEWI!! Halafu mtu anajitokeza kuwa mgombea Urais! Kama asemavyo Mzava hapa-atuonyeshe alichokifanya katika miaka 40 alipokuwa madarakani!! Nami ninatangaza nia kumbe ninaweza kuchaguliwa bila ya kuwa na nilichokifanya!! Watu wanauza nyumba Kariakoo, Ilala na kuhamia Jangwani, Mchikichini maji ya kinyesi mpaka juu ya paa-PMO, Mkuu wa Wilaya, Mbunge, Diwani WAPO. Viwanja mijini mfano Dar, Moro etc vilipimwa tena kwa mkopo wa wahisani. Mkaanzisha centre for housing studies, Vyuo vya ardhi, Idara za upimaji na ramani (baadae Nyerere centre for climate change, centre za taarifa za Ardhi) lakini bado miji inavamiwa, maeneo yaliyopimwa watu wanazidisha kuvuka mipaka ya viwanja, kufunga njia, maeneo wazi yanajengwa, kuweha garages, parking za magari binafsi au bajaji, kila nyumba ina bar na watu wazima kukojoa hovyo watoto wanaona-miji imekuwa makorokoro kinyaa-PMO na waziri wake
wanaangalia na Idara husika.

Wananchi wakipewa ardhi pa usalama wanauza na kurudi ambako nyumba hazijabomolewa. wanavamia misitu na mbuga za hifadhi-tunaangalia. Kiwanda kinamwaga maji machafu Local GVt inaangalia. NEMC ipo, vyuo vya maofisa wa mazingira na wizara ya mazingira na degree za mazingira na wasomi wake-USIMBOMOLEE huyo mwache-order fro above. Kama ni uwaziri Mkuu sasa Apewe Mh LUKUVI ili tule kisago cha uhakika kila kona tuweze kuvuka hapa pa USIASA tulipokwama. Tunataka utendaji tuliouona. Hati za ardhi ziwe na muhuru wa non-transferable without permission from Lands Dept-ili kuzuia uuzaji holela wa ardhi wafanyao ndugu zetu kisha kuhamia maeneo hatarishi na maisha kuendelea kuwa mabaya na kutesa watoto wakati hela wamechezea (milioni mia + kisha unahamia mashimo ya machimbo ya mawe, mchanga, matopeni kando ya mito, wetlands). Tunamheshimu Mh Pinda kwa yote aliyofanya lakini Urais-tunahitaji dikteta zaidi ya Kagame yeye mpole!! Watanzania tunahitaji kusukumwa sasa kwa
bakora. Ila usiasa utaleta maandamano na mapigano wakati issue inaonekana. Vyama vingi maana yake sio kupinga hata mazuri nao upinzani waonyeshe pia waliyofanya mazuri sio migomo na kashfa na lawama tu wakati kwano hujafanya kitu ila unakula bata, mikufu minene ya dhahabu ya bei ya mamilioni, ulaya kufanya manunuzi kijijini watu wanashinda wanalewa gongo na bangi mpaka ndoa zinavunja!!??

--------------------------------------------
On Fri, 12/6/15, 'mohamed mnzava' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] huyu ndiye pinda anayeutaka urais wa Tanzania
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, 12 June, 2015, 7:02

Hapa
tumepata taarifa za mtu ambaye yaonekana wazi kuwa amebebwa
na Taifa hili kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40 ya maisha
yake . . .  . .
Jambo la
msingi la kujiuliza ni kuwa Je katika miaka zaidi ya 40 ya
kuwepo katika nafasi za juu za madaraka yeye kwa
binafsi AMEFANYA MAMBO GANI YA MSINGI NA FAIDA aidha katika
kutatua matatizo SUGU yaliyopo kwa mtanzania wa kawaida? . .
. .  haswa katikaKupunguza
UMASIKINI, UJINGA, MARADHI NA UBADHIRIFU NA
RUSHWA?
Yeyote
ambaye anajipendekeza kutaka apewe dhamana ya uongozi ni
lazima tumuulize na atupatie majibu ya Tija zake katika
kutatua MATATIZO SUGU ya mtanzania wa
kawaida.
Bila
kutupatia majibu hayo ni dhahiri kuwa HANA jipya, ni
yuleyule
Aidha
AHADI alizotoa katika Bunge na nje ya bunge bado
hajazitekelezwa. Mifano:
  -
Kuzuia mauaji ya maalbino   -
Kuondoa au kupunguza matumizi ya magari ya kifahari kwa
watendaji wa serikali nk. 







On Friday, June 12,
2015 1:09 AM, 'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:



Mizengo Pinda alizaliwa
Agosti 12, 1948 mkoani Rukwa (atafikisha miaka 67 Agosti
mwaka huu). Pinda ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tangu mwaka 2008.Wazazi wa Mizengo Pinda wote
walikuwa wakulima kwa hiyo kijana pia alifuata nyayo hizo
huku akifanya jitihada kubwa kwenye masomo yake na
kufanikiwa kuhitimu shule ya msingi na sekondari, akifaulu
vizuri kila alikopita.

Baada ya masomo yake ya sekondari, Pinda
alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea Shahada ya
Sheria (LLB) mwaka 1971 hadi 1974. Baada ya kuhitimu,
alijiunga katika utumishi kwenye Wizara ya Sheria akiwa
Mwanasheria wa Serikali na alikaa katika utumishi huo tangu
mwaka 1974 hadi 1978.Mwaka 1978, alifanya kazi akiwa
"Ofisa Usalama wa Taifa" akiwa Ikulu hadi mwaka 1982,


Rais wakati huo, Mwalimu
Julius Nyerere alipomteua kuwa katibu wake binafsi (Katibu
wa Rais) nafasi aliyoishikilia hadi mwaka 1985.
Baada ya Mwalimu Nyerere kung'atuka na
kuikabidhi nchi kwa Ali Hassan Mwinyi, Pinda alitakiwa
kubaki kuendelea kumsaidia Mzee Mwinyi na alikubali wito
huo. Akaendelea kuitumikia Ikulu chini ya utawala wa Mwinyi
hadi mwaka 1992.

Mnamo
mwaka 1995, Pinda alijaribu kugombea ubunge katika Jimbo la
Mpanda Mashariki lakini alishindwa katika hatua ya kura za
maoni na ikampasa kurejea kwenye kazi yake ya awali
Ikulu.
Baada ya Mkapa kuteuliwa kurithi
Ikulu mwaka 1995, alimteua Pinda kuwa karani wa Baraza la
Mawaziri. Wadhifa alioushikilia kuanzia mwaka 1996 hadi
2000. Pinda amemuoa Tunu na wamepata watoto wanne; Janet,
Jenifer, Hardwick na Narusi.

MBIO ZA UBUNGE
Mwaka 2000,
Pinda aliachana na utumishi ndani ya Serikali na Ikulu
akajitupa jimboni Katavi kusaka ubunge kwa mara nyingine,
safari hii alipita ndani ya kura za maoni za CCM akafanikiwa
kuwashinda wapinzani na kuwa mbunge. Nyota ya Pinda ilizidi
kung'ara mwaka 2001, pale Rais Mkapa alipomteua kuwa Naibu
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
akifanya kazi chini ya waziri wake, Brigedia Jenerali Hassan
Ngwilizi, hadi mwaka 2005. Mwaka 2005, Pinda aliwashinda
Sebastian Bedastus wa TLP na Albert Damian wa CUF na
kuchaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Katavi na
aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa waziri kamili wa Tamisemi.


Bahati ya Pinda kisiasa
iliruka angani wakati wa "ajali ya kisiasa" ya Edward
Lowassa iliyoacha nafasi ya uwaziri mkuu wazi kutokana na
kashfa ya Richmond, Rais Kikwete alimteua Pinda kuwa Waziri
Mkuu. Jimboni Katavi mwaka 2010, Mizengo Pinda alishinda
uchaguzi kwa "kupita bila kupingwa" na aliteuliwa tena
na Rais Kikwete kushika wadhifa wa Waziri Mkuu hadi sasa.

MBIO ZA URAIS
Pinda ni mwanasiasa aliyeamua kwa dhati
kuachana na mambo ya ubunge na kujitosa miguu miwili kwenye
kinyang'anyiro cha urais. Wanasiasa wengi hujaribu
kugombea urais huku wakiwa wanautaka ubunge, hutupa ndoano
kwenye urais lakini wanapiga hesabu za ubunge ikiwa watakosa
ridhaa ya uteuzi, hawa ni aina ya watu ambao huamini kuwa
wanapaswa kusalia madarakani kwa njia yoyote ile, Pinda si
mmoja wao.

Hivi
ninapoandika, Pinda amekwishawaaga wana Katavi tangu mwaka
jana na amekuwa akijiweka hadharani na kuendelea na mikakati
ya chini kwa chini ya kuingia Ikulu.
Hata
hivyo, kutangaza nia kwake kumekuwa na maoni tofauti kutoka
kwa wananchi hasa ikizingatiwa kuwa wengi wanamfahamu vizuri
kwa uimara na udhaifu wake na kila mmoja ana sababu yake.
Oktoba, 2014 akiwa nchini Uingereza alieleza
kuwa amejitokeza kugombea urais ili pamoja na wenzake
walioanza harakati, Watanzania wapate muda wa kuwapima.

Mwandishi wa BBC alipomhoji
kama na yeye ni miongoni mwa watu wanaotaka kuvaa viatu vya
Kikwete alisema, "… umesikia kama nimo? … basi
tukubali hilo na yeye Waziri Mkuu yumo. Hao wote
waliojitokeza pamoja na Waziri Mkuu aliyejitokeza ni katika
jitihada za kusema hebu Watanzania nitazameni je, mnaona
nafaa au hapana?"

NGUVU
YAKE
Pinda ana nguvu ya asili, ni kiongozi
mtulivu na msikivu. Mawaziri wakuu wengi waliopita hapa
nchini si watu wa 'chapchap', Pinda yuko tofauti,
ukimpigia simu muda wowote ambao yuko karibu nayo atapokea
na atakusikiliza nini unasema, atakushauri hatua zipi
zichukuliwe au atakuomba muda afuatilie suala husika kwa
mawaziri wake. Mara nyingi husikiliza zaidi kuliko kuongea,
hii ni sifa muhimu mno kwa kiongozi yeyote yule anayehitaji
madaraka makubwa.

Jambo la
pili linalompa nguvu ni kutojikweza. Pinda si mtu wa makuu
wala mbwembwe, ni mtu asiyejikweza na kila mara anaishi
maisha ya kawaida tofauti na mawaziri wakuu wengi duniani na
hata baadhi ya waliopita hapa Tanzania. Yeye mwenyewe
hujiita "mtoto wa mkulima" na aina ya maisha anayoishi
yanafanana na "ukulima".

Jambo la tatu ni "usafi wa kisiasa".
Ukiondoa kashfa ya Escrow ambayo almanusura imuondoe katika
wadhifa alionao hivi sasa, Pinda hakuwahi kutuhumiwa
kuhusika na ubadhirifu wowote ule serikalini. Hata Escrow
kwa kiasi kikubwa tuhuma zilimwendea kwa sababu tu ya nafasi
yake ya Waziri Mkuu lakini si kwa sababu alishiriki kukwapua
fedha hizo.
Pinda ana nguvu ya asili ndani
ya CCM, kwa sababu ni waziri mkuu anayemaliza muda wake,
siyo jambo la ajabu kuwa ana watu wengi wanaomuunga mkono
ndani ya chama hicho.

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment