Friday, 12 June 2015

Re: [wanabidii] huyu ndio bernard membe usiyemjua

Haaaaaaaaaa!

Sent from my iPhone

> On Jun 12, 2015, at 20:54, 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Tumechoka kuwafikiria watu wa kawaida kwenye nafasi kubwa kama za urais...huyu ataishia kuwa mzururaji tu...sioni uwezo wake wowote kwenye nafasi kubwa kama urais...Ngupula
>
> 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
>>
>>
>> Bernard Kamillius Membe alizaliwa Novemba 9, 1953 katika Kijiji cha Rondo-Chiponda, Wilaya ya Lindi Vijijini, akiwa ni mtoto wa pili katika familia ya watoto saba wa mzee Kamillius Anton Ntanchile na mama Cecilia John Membe. Membe alifunga ndoa ya Kikristo na Dorcas Richard Masanche mwaka 1986, na wamejaliwa kupata watoto watatu-wawili wa kiume na mmoja wa kike.
>>
>> Membe tunaweza kusema alizaliwa na kukulia katika hali ya maisha ya Mtanzania wa kawaida aliyezaliwa kijijini. Alizaliwa katika kijiji ambacho maji ilikuwa shida na hivyo kulazimika kutembea kilometa nyingi kufuata maji; hali hiyo ikifanya kuoga mara moja tu kwa wiki-siku ya Jumamosi.
>> Hapakuwa na hospitali na kwa hivyo uhai ulitegemea zaidi kudra za Mwenyezi Mungu na hekima na akili za wazazi na wazee wengine kijijini. Kimsingi haya ndiyo maisha ambayo Watanzania wengi tumekulia, hasa katika miaka ambayo Membe alizaliwa.
>>
>> Baba yake Membe alikuwa mwindaji aliyelazimika kuwa hivyo. Akiwa bado mtoto mdogo miaka kama mitano hivi, wakiwa shambani, Kamillius Anton Ntanchile alishuhudia simba akimnyatia na kisha kumdaka mama yake na kutokomea naye, na walikuja kupata baadhi tu ya viungo vya mwili wake.
>>
>> Tangu wakati huo Kamillius akawa na ndoto ya kumiliki bunduki na kuwa mwindaji. Na kweli alipokuwa mkubwa alifanikiwa kumiliki bunduki na kuwa mwindaji maarufu, na baadaye kuiambukiza familia yake kuwa familia ya wawindaji.
>> Kwa hivyo, kwa maneno ya siku hizi katika siasa za Tanzania unaweza kumwita Membe kuwa ni mtoto wa mwindaji!
>>
>> Baba yake Membe alifariki dunia mwaka 1987 kwa ajali ya kulipukiwa na bunduki pajani akiwa katika harakati zake za uwindaji. Kutokana na kutokuwa na huduma za afya karibu, Kamillius alikaa masaa kumi bila huduma yeyote na hivyo alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi. Kwa maelezo ya Membe, hii ndiyo hali iliyomchochea kupigania uwepo wa hospitali ya Wilaya katika Jimbo lake la uchaguzi.
>>
>> Elimu
>> Kwa kiasi kikubwa, Membe amefuata mtiririko wa kawaida katika kusoma kwake, kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu. Elimu ya msingi alisoma katika Shule ya Msingi Rondo-Chiponda (1962-1968).
>> Utaona kwamba aliingia shule akiwa na umri mkubwa kidogo, kama miaka kumi hivi, badala ya miaka saba, ambao ndio umri wa kawaida wa kuanza shule Tanzania.
>> Hii nayo ni hali ya kawaida kwa Watanzania walio wengi tuliozaliwa vijijini. Shule ya sekondari alisomea katika seminari ya Namupa (1969-1972), na baadaye akajiunga na Itaga Seminari Tabora kwa kidato cha tano na sita (1973-1974).
>>
>> Pengine jambo moja ambalo wengi hatukulijua kabla ni kwamba Membe alipata kusomea upadri kwa miezi kadhaa kabla ya kujiunga na Itaga Seminari. Kwa mujibu wa Paul Maokola, rafikiye Membe wa siku nyingi na ambaye kwa sasa ni mtaalamu wa uchumi na meneja miradi ya maendeleo wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa vijana 11 waliopata wito wa kusomea upadri na hivyo walichaguliwa kujiunga na Seminari Kuu ya Peramiho, Songea.
>>
>> Hata hivyo, baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka Membe alikuwa ni miongoni mwa vijana watatu waliofaulu vizuri sana. Kwa sababu hii aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mtwara wakati huo, (sasa marehemu) Maurus Libaba, aliamua kuwahamishia Itaga Seminari, ambayo ilikuwa ni seminari pekee ya Kikatoliki iliyokuwa na masomo ya kidato cha tano na sita.
>>
>> Baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 1974, Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria kwa muda wa mwaka mmoja. Wakati huo huo palitolewa Azimio la Musoma lililotaka watu wote waliomaliza kidato cha sita kufanya kazi miaka miwili kabla ya kujiunga na masomo ya chuo kikuu.
>>
>> Alipomaliza kutumikia Jeshi la Kujenga Taifa, Membe hakurudi tena kuendelea na kusomea upadri kwa kile ambacho rafiki yake Maokola anaeleza kwamba alipata wito mwingine wenye masharti nafuu ya kutumikia ulimwengu.
>>
>> Aidha, Membe hakujiunga moja kwa moja na chuo kikuu hata baada ya kumaliza miaka miwili ya utumishi wa lazima. Ni kwa sababu hii utaona kwamba alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1981/82 badala ya mwaka 1979 kama ilivyokuwa kwa rafiki yake Paul Maokola, akisomea shahada ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma, maarufu Mlimani kama PSPA.
>> Kuna sababu kubwa mbili ambazo zinaweza kuwa zilimchelewesha Membe kujiunga na chuo kikuu mapema.
>>
>> Sababu ya kwanza ni kwamba tayari alishaajiriwa kufanya kazi Ofisi ya Rais na ilikuwa ni lazima apate kibali (clearance) ili kwenda masomoni.
>>
>> Sababu ya pili ni matokeo yake ya kidato cha sita. Ukiangalia kwa makini matokeo yake ya Kidato cha Sita, ambayo ni 'S' mbili na 'E' moja, utaona kwamba pengine kwa matokeo haya asingepata nafasi moja kwa moja ya kujiunga na masomo ya chuo kikuu, ukizingatia kwamba kwa wakati huo nafasi katika elimu ya juu zilikuwa finyu.
>> Hali hii inathibitishwa na ukweli kwamba Membe aliingia Chuo Kikuu kwa kufanya mtihani unaoitwa �
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment