Katiba ya chama imeeleza wazi kuwa mwanachama yeyote atakaye enda mahakamani kwa shauri lolote dhidi ya chama na mahakama ikaamua kinyume na matarajio ya mshitaki, mwanachama atavuliwa uanachama Mara moja, hicho ndicho kilichofanyika. Hapa pana ubaya gani?
Kwa msomi kama ZZK hakuliona hili? Kama aliliona kwa nini asichukue hatua ya kuondoa madai yake mahakamani ili wayamalize nje ya mahakama? Na je angeshinda kesi yake leo hii tungekuwa tunasemaje au ndo tungeona viongozi wa CHADEMA ovyo!!!
Sheria/Katiba zinatungwa kwa ajili ya kutuadabisha na kututaka tukae katika mstari mnyoofu.
Tunapojiunga na vyama viwe vya siasa au kijamii ni vyema tukasoma na kuzielewa katiba husika ili kuepuka matatizo kama haya mbele ya safari mhusika anapokuwa hafuati katiba hiyo.
Ninasikitika kumkosa Zitto lakini kwa kuwa utashi wake ndio uliomfikisha hapo basi hapana jinsi.
Hakuna mahali ninapoona CDM wamekwenda kinyume cha katiba yao. Ninawapa heko na ninawashauri utaratibu huu uendelee kwa ila anayekwenda kinyume na taratibu waliOkubaliana bila kujali nafasi ya mtu yeyote ndani chama. Nje ya hapo kila mtu atafanya anavyotaka ama kwa kutumiwa ama kwa utashi wake na matokeo yake mvurugano ndani ya vyama.
Huu uwe ni utaratibu endelevu kwa vyama vyote hasa vya ipinzani ili kuondoa mapandikizi.
Pole sana mdogo wangu ZZK, Naamini utapata tu lango la kutokea ili uendelee kutoa mchango wako kwa taiga letu huku ukizingatia utamaduni na taratibu za huko unakoenda.
ABM
From: 'Adam Adam' via Wanabidii
Sent: 3/11/2015 8:17
To: wanabidii@googlegroups.com; Hildegarda Kiwasila khildegarda@yahoo.co.uk [Wanazuoni]
Subject: Re: [Wanazuoni] Re: [wanabidii] Kufukuzwa Kwa Zitto Chadema:Nimepokea Taarifa Kwa Masikitiko..
Natamani CHADEMA wengeweka ama kutumia busara mbadala katika suala hili. Gharama ya suala hili itakuwa kubwa kwa demokrasia nchini.
Hapo sasa jimbo la Zitto Kabwe litachukuliwa na CCM au chama kingine ili kulipiza kisasi kuikomoa Chadema. Hii imetokea pia kwa CCM kupoteza uongozi ktk serikali ya Mtaa katika Mitaa mbalimbali kwa kuweka viongozi au wagombea uongozi ambao hawakutakiwa na wananchi. Hivyo wana CCM wakaamua kumpigia kiongozi mwingine yeyote wa chama kingine chochote kuikomoa CCM na vijambo vyake ingawaje wanakipenda chama chao walifanya hivyo ili viongozi wake wabadilike wazingatie wanachama wao/raia wanataka nini ktk eneo lao na wanamtaka nani wampendae. Tukiwasikia wapiga kura wakisema hivi wakitoka kupiga Kura-Tumewakomoa, tumempigia CUF, Chadema eti wamemuweka fulani ambaye kura za awali hakushinda, hatumtaki mla rushwa, hatumtaki mbona huyu si mkazi wa mtaa huu hatumjui....Haya ya Mh Zitto-ni mazito; chuki binafsi na umimi zitatumaliza. Hapa CCM itavuna Jembe. Kama budi aendelee na wadhifa wake bungeni jee haitowezekana kuwa mbunge wa kuteuliwa na JK haraka sana? Hapa
sasa Chadema imeruka tope la kinyesi Jangwani Mtaa wa Sunna na kuangukia katika tope la mchanganyiko kinyesi cha nguruwe, mbuzi na ng'ombe Tandale kwa Mtogole.
--------------------------------------------
On Wed, 11/3/15, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Kufukuzwa Kwa Zitto Chadema: Nimepokea Taarifa Kwa Masikitiko..
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, Wanazuoni@yahoogroups.com
Date: Wednesday, 11 March, 2015, 6:28
Nimepokea
kwa masikitiko taarifa kuwa ndugu yangu Zitto Kabwe
amefukuzwa kwenye chama cha Chadema. Ni habari ya
kusikitisha unapotafakari demokrasia tunayojitahidi
kuijenga.Zitto
amekuwa mwanachama wa Chadema tangu akiwa kijana mdogo.
Mwenyekiti wa chama hicho , Freeman Mbowe, amenukuliwa mara
kadhaa akikumbushia jinsi alivyoshirikiana na Zitto
kuhamasisha vijana wengine waliokuwa vyuoni kujiunga na
Chadema.Kwenye
siasa za vyama kuna kutofautiana kifikra na kimitazamo. Na
mara
nyingine migongano huwa inahusu kugombania nafasi za
uongozi. Haya ni mambo ya kawaida kwa chama cha siasa.
Hayapaswi kuwa sababu za viongozi wa vyama kuwafukuza
wanachama.Kwenye siasa tofauti humalizwa
kwa hoja, kwenye vikao. Na anayekiuka taratibu za chama
kumfukuza kwenye chama ni adhabu kubwa na kali kama ya kifo.
Maana, anayejiunga na chama hufanya hivyo kwa mapenzi.
Anapokosea anaweza kuonywa au kuadhibiwa, lakini, kufukuzwa
kwa misingi ya kutofautiana kifikra na kimitazano si hulka
njema.Zitto Kabwe ni
mwanasiasa kijana na mahiri. Chadema ilipaswa imvumilie na
ishindane nae kwa hoja, lakini, si kumtupa nje kwa staili
tuliyoishuhudia.Chadema, kama
chama cha siasa, isijiandalie mazingira ya wanachama wake
kuwa na hofu ya kufukuzwa pindi wanapotofautiana na viongozi
wa juu. Itapoteza kisiasa.Na
hili la Zitto Kabwe linatukumbusha kile ambacho binafsi
nimeandika mara kadhaa, juu ya udhaifu kwenye Katiba yetu.
Kwamba Mbunge aliyechaguliwa na Wananchi anaishi kwa hofu ya
rungu la chama.Kwamba leo
Wananchi wa Kigoma Kaskazini wanampoteza Mbunge wao
waliyemchagua kwa maamuzi ya Chama anachotoka Mbunge wao.
Haya ni mapungufu makubwa. Wananchi hapaswi kuadhibiwa kwa
maamuzi ya vyama.Nachukua
fursa hii kumtakia kila la heri ndugu yangu Zitto Kabwe,
nikimuasa asikate tamaa, akipata fursa nyingine, aendelee na
siasa na hususan uongozi wa uwakilishi wa wananchi. Aendelee
kuwa sauti ya wasio na sauti, popote pale.Maggid Mjengwa,Dar Es Salaam.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and st
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment