mawazo ya huyu kijana ni mazuri. Tukipoata rais mwenye mwelekeo. akayakusanya mawazo kama haya na ya watanzania wengine. Akaunda serikali namifumo ya kuyafanyia kazi nchi inaweza kusonga mbele. Narudia-(1)Tukipata rais mwenye mwelekeo. (2) Akachanganya mawazo haya na mengine mengi mazuri. Unaona january anasema sera ya CCO. maana yake sera zipo. Kisichokuwepo ni hicho nilichokitaja.
--------------------------------------------
On Mon, 2/2/15, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] JANUARY MAKAMBA NA TATIZO LA AJIRA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, February 2, 2015, 4:48 PM
MAKAMBA
NA TATIZO LA AJIRA."Ni
changamoto gani kubwa zinawakabili
vijana wa Tanzania? Wanasiasa wengi
wamekuwa wakisema watamaliza tatizo
la ajira nchini. Kuna mawazo gani mapya
kutoka kwa viongozi wa kizazi kipya ya
kumaliza tatizo hili?"Tatizo
la ajira lipo kwa vijana wa mijini na vijijini, vijana
waliopata bahati ya
kupata elimu ya juu na hata ambao wameishia la saba au
kidato cha nne. Ukiwa
umesoma, ajira tatizo, ukiwa haujasoma ajira pia
tatizo.Kwa
mujibu wa takwimu za Serikali, inakadiriwa kwamba wapo
Watanzania
milioni 23 kwenye soko la ajira – kwa maana ya watu wenye
umri na uwezo
wa kufanya kazi. Hawa ni watu wengi sana. Na kila mwaka
wanaingia vijana
900,000 kwenye soko la ajira. Hawa ni wengi sana.Moja
ya sera za msingi za CCM ni kuwawezesha wananchi kiuchumi
ili waweze kumiliki na kuendesha uchumi wa nchi yao na
waweze
kunufaika na uchumi unaokua. Katika kufanya hivyo, lazima
wawe na
maarifa ya kisasa kwa kuwa tupo kwenye mazingira ya uchumi
wa
kisasa.Yapo
mambo ambayo Serikali imekuwa inafanya kumaliza tatizo la
ajira. Mimi
nitajaribu kuongelea mambo mapya ya kuongezea zaidi ya yale
tunayofanya
sasa.Kwanza
kabisa, ni muhimu kubadilisha mtazamo na kuondokana na
dhana ya ajira au dhana ya kuajiriwa. Tuchukue dhana mpya ya
kipato.
Kimsingi watu hawatafuti ajira bali wanatafuta kipato cha
kujiendeleza
January Makamba akiwa amezungukwa na vijana wa Bodaboda
akiwasikiliza shida zao.kimaisha.
Kuajiriwa ni moja tu ya njia ya kutafuta kipato. Tukiwa na
dhana ya kipato itaweza kutusaidia kupanua wigo wa mawazo na
fikra
kuhusu mambo tunayoweza kuyafanya.Sasa,
nini tufanye kumaliza hili tatizo?
Kwanza, kupatikana kwa fursa za vipato kwa wananchi kuna
uhusiano wa
moja kwa moja na kunawiri kwa uchumi wa taifa, kuongezeka
kwa shughuli
za uzalishaji mali na uwekezaji wa sekta binafsi katika
shughuli zinahusisha
watu wengi, uwekezaji wa Serikali kwenye miradi mikubwa, na
kuwepo kwa
mazingira rahisi na mazuri ya kuanzisha na kufanya biashara.
Kwa hiyo haya
mambo lazima tuyafanye kwa uthabiti na kwa dhamira ya dhati
kabisa.Pili,
Serikali imekuwa na mipango mizuri ya kuwezesha yote haya
lakini
kumekuwa na nidhamu ndogo katika utekelezaji na ufuatiliaji.
Tatizo la kipato
kwa wananchi linahitaji mkakati mahsusi, mkakati mkubwa na
wa haraka
– mkakati ambao utaweka nidhamu na wajibu wa kisheria kwa
wahusika
kuutekeleza.Suala
la ajira linahitaji msukumo na hatua za kimapinduzi, na sio
maneno
tu ya kurudia kauli kwamba ni bomu bila kutoa ufumbuzi.
Pamoja na hatua hizi nilizozitaja awali napendekeza hatua
nyingine mahsusi
za kumaliza tatizo la ajira na kuweka chachu mpya ya ukuaji
wa uchumi:
Bunge lipitishe Muswada Maalum, Muswada wa Matumizi kwa
Uwezeshaji Kiuchumi kwa Vijana, ambao utakuwa ni sheria
maalum
ya matumizi ya shilingi trilioni 3.6 kwa ajili ya mkakati wa
miaka mitatu
wa kupanua ajira kwa kuchochea shughuli za uzalishaji mali
na uchumi
au Jobs Bill kwa lugha nyingine.Mwaka
2009, ulipotokea mdororo wa uchumi na wanunuzi wa pamba
kukaribia
kufilisika Rais Kikwete alionyesha ujasiri na kupeleka
Bungeni Mpango
Mahsusi wa kiasi cha shilingi trilioni 1.7 kuokoa zao la
pamba na mabenki
yaliyowakopesha wanunuzi wa pamba. Sasa ni wakati wa
kutengeneza
Muswada na Mpango Mahsusi na wa hatua kubwa zaidi ya ile ya
2009 kwa
ajili ya kukabiliana na tatizo la ajira.
Kwa kifupi, Muswada huu, utatenga fedha na kuweka utaratibu
kwa maeneo
muhimu yafuatayo:Kwanza,
kuwezesha kujengwa na kufufuliwa kwa viwanda 11 vya nguo
nchini.
Huko nyuma tulishawahi kuwa na viwanda vingi vya nguo. Sasa
hivi havizidi
vitano. Sekta ndogo ya viwanda vya nguo ndio inayoajiri watu
wengi zaidi lakini
pia ndio itakayotoa soko la uhakika la zao la pamba. Kwa
sasa, ni asilimia 30 tu
ya pamba yetu ndio inayotumika nchini. Fedha hizi zitatumika
kama dhamana
kwa makampuni binafsi hapa nchini kukopa kwa ajili ya ujenzi
wa viwanda
vipya 11. Hatua nyingine ya kuchukua hapa ni hatua ya kikodi
na kiushuru ili
kuwezesha viwanda hivi kukabiliana na ushindani wa kanga,
vitenge, mitumba
na vitambaa vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi.Sera
za kukuza viwanda vilivyo na uwezo wa kuajiri watu wengi –
kama
vya nguo- na vyenye kuzalisha bidhaa za matumizi ya wengi
ndani ya
nchi na zile za kuuza nje zitawekewa kipaumbele.Pili,
fedha hizi zitatumika kama mkopo na dhamana ya mkopo kwa
yoyote
anayetaka kuanzisha kiwanda au viwanda vya kusindika au
kuongeza thamni
ya mazao ya kilimo – ikiwemo zao la korosho ambalo
ubanguaji wake unaajiri
watu wengi.Mtu
yoyote atakayeamua kuanzisha kiwanda cha kuongeza thamani
ya mazao ya kilimo, kitakachoajiri watu kuanzia kumi, hasa
maeneo ya
vijijini, atapendelewa na Serikali na kusaidiwa kuharakisha
uwekezaji
huo na atapewa nafuu ya kodi.Tatu,
shughuli za ujenzi wa nyumba zinaajiri watu wengi. Kwa hiyo
sehemu ya
fedha hizi zitatumika kuwezesha uanzishwaji wa makampuni
madogo na ya kati
ya ujenzi wa nyumba lakini pia kuanzisha miradi mingi na
mikubwa ya ujenzi
wa nyumba bora za makazi na biashara kwa maeneo ya mijini na
vijijini. Tuna
mahitaji makubwa ya nyumba na tuna mahitaji makubwa ya
ajira. Tukijenga
nyumba nyingi kila siku kama wendawazimu tutamaliza matatizo
mawili kwa
mpigo. Sambamba na hili, ujenzi wa viwanda vya vifaa ya
ujenzi, kama vile
viwanda vya nondo, mabati, simenti, vigae, vioo, ili
kupunguza gharama za
ujenzi wa nyumba pia ni muhimu.Lakini
sote tunajua kwamba ujenzi wa miundombinu mikubwa, hasa ya
usafirishaji ni njia mojawapo ya kuongeza chachu katika
uchumi na kuongeza
ajira. Kwa hiyo jitihada za makusudi ni muhimu ziwepo
kuongeza kasi na ukubwa
wa miradi ya miundombinu nchini ambayo itaajiri vijana wengi
zaidi na kuingiza
fedha nyingi zaidi kwenye mzunguko wa uchumi, hasa pale
tutakapohakikisha
kwamba wajenzi wa miradi hii ni makampuni ya ndani
yatakayohifadhi na
kuwekeza fedha hizo hapa ndani.Nne,
kwa kushirikiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Muswada huu
utaanzisha mfuko mkubwa kwa ajili ya kutoa dhamana na mikopo
kwa
wajasiriamali wadogo kwa masharti nafuu kuliko mabenki au
mifuko
mingineyo iliyopo hapa nchini.Wajasiriamali
watakaopewa upendeleo ni wale wanaofanya shughuli za
uzalishaji mali hasa kilimo, uvuvi, mifugo na shughuli za
biashara zinazotoa ajira
kwa watu wengine. Mfuko huu utaendeshwa kwa uwazi na weledi
mkubwa,
ikiwemo njia ya kutoa mtaji kwa kuchukua hisa kwenye baadhi
ya biashara
hizi za kati na baadaye kuzirudisha hisa hizo kwa masharti
nafuu pale biashara
hizi zinapokuwa zimeinuka. Lengo ni kurahisisha na
kuharakisha upatikanaji
wa mitaji.Tano,
Muswada huu utaweka sharti kwamba asilimia si chini ya 30
ya
thamani ya manunuzi Serikalini na kwenye taasisi za umma
yatatengewa
kwa ajili ya makampuni yanayomilikiwa na vijana wasiozidi
umri wa
miaka 40 na wanawake – ili mradi makampuni hayo yawe na
uhai
usiopungua miaka miwili na yawe yameajiri pia watu
wengine.Sita,
Muswada huu utarasimisha shughuli za sanaa – ikiwemo
sinema, muziki
na kazi zote za ubunifu– na kutenga fedha kwa ajili ya
maendeleo ya tasnia
hii, ikiwemo kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wazalishaji,
waendeshaji
na wasanii wenyewe kwenye kuendeleza ubunifu na kuzalisha,
kutangaza na
kuuza kazi mpya kwa njia za kisasa.Saba,
kwa wale wanaohitaji kuajiriwa, tutaweka vituo vya kutoa
mafunzo ya
namna ya kuomba na kufanya usaili wa kazi – lakini pia
tunaweza kutumia
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, yaani FDCs, kama vituo vya
kupata na kujenga
maarifa mapya kwa muda mfupi kuhusu mbinu na ushauri wa
kukabiliana na
soko la ajira na fursa zilizopo za kujiajiri.Nane,
kwa biashara kubwa na viwanda vilivyopo sasa, Muswada
utaweka
motisha kwa yoyote ambaye ataweza kuongeza ajira mpya 50 au
zaidi kwa
mwaka, sio vibarua wa muda mfupi bali ajira kamili, kwa
kupunguziwa kodi za
mishahara, yaani payroll taxes; na kwa waajiri ambao ni
kampuni mpya ndogo,
yaani SMEs, motisha wa kupunguziwa kodi hizi kwa kila kazi
mpya tano au
zaidi kwa mwaka.Ukweli
hapa ni kwamba kunawiri kwa uchumi hakutokani na kodi
inayokusanywa na Serikali bali kunatokana na kipato na uwezo
wa
manunuzi walionao wananchi na kipato cha wafanyabiashara
kuweza
kukuza biashara zao na kutoa ajira nyingi zaidi.Tisa,
Muswada utatenga fedha za kuweka mazingira ya ujenzi wa vyuo
vya
ufundi, kwa kushirikiana na sekta binafsi, kwenye kila
wilaya hapa nchini ili
wanafunzi ambao hawajapata fursa ya kuendelea na kidato cha
kwanza au
kidato cha sita au vyuo vya ualimu wapate mafunzo mbalimbali
mahsusi ya
ufundi stadi na taaluma zinazohitajika kwenye soko la ajira
na kwenye uchumi
kwa ujumla. Takwimu zinaonyesha kwamba asilimia kubwa ya
wahitimu wa
vyuo vya ufundi hujiajiri.Tutakapokuwa
na Chuo cha Ufundi kikubwa na chenye hadhi katika
kila Wilaya tutatengeneza kundi kubwa la vijana ambao
watakuwa
na maarifa na stadi za kutengeneza maisha yao na watakuwa
tayari
kujiajiri.Na
utaratibu unaweza kuwekwa kwamba yoyote atakayemaliza Chuo
cha
Ufundi, kama alisomea ufundi-seremala basi siku ya mahafali
anakabidhiwa
vifaa vya kuanzia kazi, au mkopo au vocha ya kumuwezesha
kununua vifaa
hivyo. Uwezo wa kufanya hivi tunao.Kumi,
Muswada huu utatenga fedha kwa ajili ya kuweka katika kila
wilaya vituo
vya mafunzo ya maarifa mapya katika shughuli zinazoajiri
watu wengi – kilimo,
uvuvi na ufugaji – na maarifa ya uendeshaji biashara ili
vijana wanaofanya
shughuli hizi waweze kuzifanya kwa tija na wapate manufaa.
Kwa kuanzia,
tunaweza kuanza kwa kutumia vyuo vilivyopo vya Maendeleo ya
Jamii (FDCs)
ambavyo havitumiki kama inavyopaswa.Kumi
na moja, Muswada huu utaweka kanuni zitakazoainisha kiwango
cha
chini cha thamani ya manunuzi yanayofanywa na wawekezaji
wakubwa, hasa
katika sekta za mawasiliano, madini na mafuta na gesi,
kufanywa hapa nchini
na kutoka kwa makampuni ya hapa nchini.Kumi
na mbili, Muswada utaanzisha Mamlaka ya Ujasiriamali Mdogo
na wa
Kati (Small and Medium Enterprises Authority). Mamlaka hii
kubwa, ambayo
itaanzishwa kisheria, itachukua na kuunganisha baadhi ya
majukumu ya Baraza
la Uwezeshaji la Taifa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda
Vidogo (SIDO) na
itakuwa na jukumu la kusimamia na kuratibu maendeleo ya
kampuni changa
na biashara ndogo nchini. Kote duniani, biashara za kampuni
ndogo na za kati
ndio injini ya uchumi wa nchi.Hapa
kwetu asilimia karibu 90 ya biashara zote
nchini ni biashara ndogo na za kati, ambazo zinaajiri watu
wasiozidi wawili.
Wajasiriliamali Wadogo na wa Kati wana changamoto mahsusi,
zikiwemo za
masuala ya kodi, urasimishaji, masuala ya vibali, leseni,
mitaji, elimu ya biashara,
na uelewa wa fursa zilizopo. Changamoto hizi zikitatuliwa
basi mchango wa
biashara hizi kwa uchumi na utatuzi wa ajira utakuwa mkubwa.
Kwa mujibu
wa takwimu za Benki ya Dunia, asilimia 20 tu ya biashara na
kampuni ndogo
zikiongeza mfanyakazi mmoja kwa mwaka, ajira 400,000
zitazalishwa. Je
asilimia 80 za biashara hizi zikiongeza watu watatu kwa
mwaka? Tutakuwa
tumemaliza tatizo la ajira. Lakini, ili hili litokee, lazima
tuwe na taasisi madhubuti
kama hii Mamlaka ninayopendekeza, ambayo itashughulika na
ustawi wa
biashara na makampuni madogo na ya kati.Katika
kusaidia biashara na makampuni madogo na ya kati, Mamlaka
ya
Ujasiriamali Mdogo na wa Kati inaweza kupewa majukumu
yafuatayo: kwanza,
kusimamia utekelezaji wa sharti jipya la kisheria la
asilimia 30 ya manunuzi
ya Serikali yapewe kwa kampuni ndogo na za kati
zinazomilikiwa na vijana
na wanawake wenye uwezo; pili, kuyajengea uwezo wa weledi wa
kibiashara
makampuni madogo na ya kati kuwania zabuni; tatu, kusimamia
uharakishaji
wa malipo kutoka Serikalini kwa wazabuni wadogo na wa kati
ambao biashara
zao hudhoofika na hata kampuni kufa pale Serikali
inapochelewa kuwalipa;
na, nne, kujenga uwezo wa makampuni na biashara ndogo na za
kati kumudu
na kuweza kutumia nyenzo za kisasa za biashara ikiwemo
mifumo ya kisasa
ya mahesabu.Mwisho,
sheria hii itaweka taasisi na mifumo madhubuti ya
kuhakikisha kwamba
malengo ya fedha hizi yanatimia na kila mtu anatimiza wajibu
wake.Labda
nimalizie kwa kusema kwamba katika haya niliyoyasema kuna
ambayo
yanafanyika kwa kiasi fulani. Msingi wa mapendekezo yangu ni
kwamba,kwanza:
sasa tuyafanye kwa msukumo mkubwa zaidi na utaratibu wa
dharura;
pili, tuweke rasilimali-fedha za kutosha kwa ajili ya
kufanya kuliko kuwa na
mipango mizuri bila kuwa na fedha; tatu, badala ya kuwa na
mipango na mikakati
tu, basi kuweka sheria itakayolazimisha na kuweka wajibu wa
kutekeleza
mipango na mikakati hii. Lakini mwisho, kuunganisha yale
mazuri ya sasa na
haya mapya ili kuwa na mwendelezo utakaowezesha utekelezaji
wa haraka
bila kufumua kila kitu.Tukifanya haya yote kwa nidhamu
kubwa, tutawakomboa
watu wengi katika maisha ya mashaka kuhusu kipato na ustawi
wao.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment