screen-shot kutoka kwenye tovuti ambayo ni chanzo cha habari husika |
Nami nimeisoma mistari michache na kutafuta chanzo chake ambacho kinaonesha habari yenyewe iliandikwa mwezi uliopita, haipo kwenye vyombo vikubwa vya habari (yaani vyombo rasmi vilivyosajiliwa na vinavyoaminiwa kwa habari zake - registered and authentic) lakini tayari leo blogu kadhaa zinazomilikiwa na Watanzania zimeanza kuisambaza kama ilivyo.
Habari hiyo iliyochapishwa na tovuti moja inadai kuwa yupo mgonjwa nchini
Marekani katika jimbo la Georgia mwenye asili ya Tanzania ambaye amegundulika kuwa mgonjwa wa pili kuugua ugonjwa unaosababishwa na virusi hatari wa Ebola.
Habari hiyo ambayo inasema mgonjwa huyo aligundulika kuugua Ebola baada ya kurudi kutoka nchi yake ya asili, Tanzania, na kupelekwa katikahotpiali ya Grady Memorial, ni ya mzaha na haipaswi kuchukuliwa kwa makini kwani mwishoni kabisa kwa tovuti hiyo pameandikwa, "NewsBuzzDaily.com is a combination of real shocking news and satire news. Please note that articles written on this site are for entertainment and satirical purposes only."
Maneno hayo yanajieleza wazi na kumfahamisha yeyote anayesoma habari za tovuti hiyo kuwa taarifa zake ni za mzaha na burudani .
Mara kwa mara tunaendelea kukumbushwa kuwa makini kwa kuchunguza habari, taarifa na maandiko ili kupembua ukweli dhidi ya uongo na kuacha kusambaza habari ambazo zinaweza kusababisha mtafaruku katika jamii usio na sababu hata kidogo.
Tafadhali ukikutana na habari hiyo, ipuuze.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment