HOUSE WIFE "MAMA WA NYUMBANI"
Haijalishi elimu, cheo, nafasi, uwezo, nguvu kiuchumi au heshima uliyonayo, haijalishi unaheshimiwa kiasi gani na ndugu au watu wa nyumbani kwako, bado itakuwa haujasimama katika nafasi yako ya kuwa mke bora kama hautojiweka katika nafasi ya kuwa "HOUSE WIFE" au mama wa nyumbani. Yamkini wewe ni kama wengi wanao tafsiri mama wa nyumbani "house wife" kama mke asiye na kazi, mke asiye na chakufanya, mke ambaye hakusoma, mke asiye na majukumu, kwa jina lingine labda utamuita golikipa, lakini tujaribu kuangalia kwa mtazamo wa pili kwamba "house wife" au mama wa nyumbani ni mke anayeijali nyumba yake, mwenye kuwajali waishio ndani yake, mwenye kujua hisia zao za huzuni na furaha, mwenye kuhakikisha wana tabasamu wakati wowote, kipaumbele chake ni kwa wale walioko chini ya dari yake na sio ajira yake wala miradi yake (hapa sisemi asiwe ameajiriwa wala asiwe ana miradi). Kwa mtazamo huu utaona kwamba, katika hali yeyote ile ya mafanikio ya kifedha, kinafasi, kikazi au kielimu, mke bora hana budi ku "qualify" nafasi yake ya kuwa "house wife" kwanza (simaanishi asifanye kazi au biashara, namaanisha utayari wake wa kubeba majukumu), na hayo mengine yatafuatia. Ni mtazamo tu na unaruhusiwa kurusha jiwe pale unapoona nimekosea –Chris Mauki
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment