Wednesday, 29 October 2014

Re: [wanabidii] Fwd: RE;MWIGULU;MABADILIKO NI MATENDO

Binafsi huwa sishabikii mtu kwa kutegemea kupata faida binafsi,bali ni katika kuangalia kuwa kama taifa tupate kiongozi bora....ushauri wako kuhusu mwigulu ni sahihi lkn ngoja nikuambie kitu,mwigulu kwa hulka yake yeye ni mtendaji na hufanya kila unachomtuma kwa uaminifu....alitumwa na chama akafanya alichokifanya nanyi mwakijua,ametumwa wizarani nanyi mwajua atafanya...na sasa muangalie utendaji wake na kisha muone kama hastahili urais

.

'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ngupula,
mimi sishabikii mtu kwa sababu sitafaidika na chochote kwa ushabiki wang kwa mtu au kundifulani la urais. Ninachtamani kukiona ni mwelekeo mzuri wa nchi yetu, kupata kiongozi anayefikiria kutondoa kwenye upofu wa fikira hata tunajigeuza matonya. Lakini angalizo kwangu kwa Mwigulu ni kuondoa mawazo ya kukiona chama kwanzanchi baadae, aionenchi kwanza chama baadae kama alivyojaribu kwa kipindi hiki kifupi. Tunahitaji muda kumpima asije kuwa kama alivyokuwa kamanda wa mapambano ya ufisadi alivyoaminiwa sana lakini kumbe hana kitu ameshuka ghafla.


On Wednesday, October 22, 2014 1:13 AM, 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Aksante dadangu  kwa comment nzuri....nakubaliana  nawe ni ngumu sana kumpata kiongoz wa aina ya sokoine au nyerere kwa sasa......hawa walikuwa ni wazalendo,wenye utu na ubinadamu usiopimika..
...nafikir hata hao wanaomfananisha ni indication kuwa wananchi kwa sasa wamechoka  kwa usanii wa viongoz na wanataka tija kwa matendo yenye kulenga mabadiliko...ni kweli dada,mabadiliko ni mfumo.....haya sasa mfumo ndio huo ushapigwa chini.....tunafanyaje sasa..tukikaa chini na kulalamika haitosaidia....tunashika kuti linaloshikika na kusonga mbele kwa matumaini tukijua mungu yupo

'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Tena muacheni  kabisa  Sokoine wetu apunzike kwa amani. Nilivyomjua  Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa  Jamhuri ya Tanzania, hakuna hata kiongozi mmoja wa kisiasa hapa nchini  katika hizi siasa za kusaka pesa  na vyeo hata kama ni kwa kuiba mchana kweupe au kuuwa wananchi wasio na hatia  kwa silaha za moto  wakiwa kwenye kusanyiko halali kisheria anayeweza kulinganishwa  na Edward Morine Sokoine. Wanaotafuta nafasi za madaraka na ulaji waendelee kufanya usanii  wao  kwa sababu Wabongo  tuko very cheap, wasahaulifu na hatufanyi utafiti wala uchambuzi kubaini yaliyo nyuma ya pazia.  Mbona  mzalendo Jaji Joseph Warioba  amefanya kitu (Rasimu ya Katiba) kuweka misingi ya kuleta mabadiliko endelevu kuwezesha kila  tunaoyechagua awajibike kuepusha matumizi machafu ya fedha za umma  ameishia kutukanwa na kubezwa? Si wote hawa wanatoka chama hicho hicho? Ataletaje mabadiliko wakati hakuna mifumo ya  kuwajibisha? Nijuavyo mimi  mtu hata kama awe karibu na malaika kama hakuna mifumo ya kumwajibisha umma utalizwa tu.    Itoshe tu kusema  hakuna miongoni mwa viongozi tulionao  sasa mwenye sifa za    Sokoine aliyekufa katika ajali ya kutatanisha akitokea Dodoma Bungeni. We acha kabisa, utu, uzalendo  na sifa za utumishi wa umma alizokuwa nazo Edward Moringe Sokoine ni adimu sana. 

Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

On Tuesday, October 21, 2014 6:46 AM, 'allan lawa' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

ndugu zangu,

mie si shabiki wa siasa. siyo sawa wala sahihi kumlinganisha Mwigulu na Sokoine. Sokoine alikuwa kitu kingine na hapana mfano wake hadi sasa. Yawezekana anayejaribu kumlinganisha huyu muungwana na Sokoine hakupata kumjua Sokoine au anafanya upotoshaji wa makusudi kwa maslahi ya kisiasa.

On Monday, 20 October 2014, 0:24, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Mtu anayeweza kumlinganisha Mwigulu na Sokoine nitasema bila kuuma maneno kuwa hamjui Sokoine. Au kurahisisha mambo Hamjui Mwigulu
--------------------------------------------
On Sat, 10/18/14, 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:<

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment