Sunday, 5 October 2014

Re: [wanabidii] BURIANI UKAWA


Neatness,
Nakubaliana na wewe. Angelikuwa hajaokoka, isingelikuwa tatizo. Mtu akishasema, ameokoka, tayari ana kikomo, tayari ana miiko. Tunatakiwa kuwa mawe yaliyo hai. TUNATAKIWA KUWA BARUA ZILIZO HAI. – TUONEKANE NA KUSOMWA NA WATU WOTE. Kwa maneno mengine, tunatakiwa kumruhusu Kristo aumbike ndani mwetu – katika kiwango kile ambacho watu watatuangalia na kujua kwamba sisi ni wa kwake.
Sasa, je, hivyo si ndivyo Paulo alivyosema? "Nifuateni mimi kama nami ninavyomfuata Kristo." Kwa maneno mengine, "nimemruhusu Kristo anishughulikie, sasa na wewe mruhusu akushughulikie – ili uweze kusogezwa mbele katika kile Mungu anachotaka kwako."
      Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo Yesu amekuwa KIUMBE KIPYA; YA KALE YAMEPITA tazama YAMEKUWA MAPYA [2Kor.5:17]
Lakini mambo yale yaliyokuwa FAIDA kwangu, naliyahesabu kuwa HASARA kwa ajili ya Kristo. [Wafilipi 3:7] . Katika wokovu kuna faida na hasara. Mambo ya dunia inabidi kukubali kupata hasara, ili upate faida katika mambo ya mbinguni.
KUOKOKA NI GHARAMA. Wengi hawataweza. Yesu alisema, jitahidini kuingia katika ule mlango mwembamba,….maana wengi watajitahidi lakini hawataweza.
Dada Hapiness, mimi nami nimeokoka kama wewe, na kama binadamu hatujawa wakamilifu. Tunajikwaa katika mengi, na tunatubu na kugeuka. Ujumbe wako umefika, sasa kwa ajili ya Kristo, makala inayofuata naomba ionyeshe mabadiliko. Ubarikiwe na uwe baraka. Materu
 


On Sunday, October 5, 2014 6:40 PM, Neatness Msemo <nmuzeh@gmail.com> wrote:


Happy,
Mwandishi wa habari za mahakamani, unatisha.
Nimesikitika sana kwa jinsi unavyochanganya mambo.
Nimeona jinsi unavyohukumu wakati si kazi yako.Je nani anakulinda dada yangu kwani umeongea kana kwamba unajaribu luonyesha hisia zako ambacho si dhambi.
Lakini kama kweli wewe unasomea sheria naamin umeenda kinyume na maadili ya sheria na uandishi wa habari.
Kwani hupaswi kumshambulia mwingine bila kuwa na sheria inayokulinda kufanya hayo.
Kama unavyoandika habari kwa mtazamo wa kukilinda chama ndivyo wengine wanafanya kwa kulinda maslahi ya vyama vyao au utashi wao.hupaswi kuwashambulia na kibaya zaidi unatumia maneno ya biblia na kuwaita mashetani na kwamba wapo jehenam wewe mtotobona unachanganya mada.mchungaji wako nadhani inamwaibisha kwani wewe huna hata chembe ya ukristo.
Mtu anayemjua Mungu na kumfuata siku zote anakusanya pamoja na Kristo na sio kutawanya.maana alikuja kuokoa na sio kuwapeleka watu jehenamu.wanakwenda kwa kukosa maarifa.
Wewe unawaita watu wajinga .wapuuzi n.k nasikitika sana.wewe ni wa ndugu yao ibilisi kwani unawahukumu usiowajua na unavaa ngozi ya kondoo wakati wewe ni mbwamwitu.
Usijidanganye.chochote apandacho mtu  ndicho atakacho vuna.mimi sipingi kuonyesha utashi wako lakini usipitilize kwani neno linasema utatoa hesabu ya maneno yako na kwa kadiri ya neema uliyopewa kujua mema utatKwa kuyatolea hesabu.
Nijuavyo mimi kuhusu siasa najua ni mchezo mchafu na wengi huchafuana.sasa kama na wewe ni mwanasiasa sidhani kama hapa ni jukwaa lako.huwa tunapenda haki na ukweli.ninachokuomba ni kuwa kama nia yako ni kupata umaarufu ama una kitu unataka basi andika proposal uzipeleke au uzitume naamin itapata unalotakiwa.
Bahati mbaya niliyonayo labda utanielewa vibaya binti mzuri unayechipukia.kama mwanasheria.na mwana habari tumia kalamu yako vizuri.utafanikiwa.kwani hili tunalojaribu kuliongelea ni jambo linalohusu nchi na vizazi vijavyo.sasa kulifanyia mchezo  siku moja tutahukumiwa kwani kila jambo linanukuliwa.
Kanisa la Elishadai ni kanisa linaloheshimika usitake kuonyrsha kuwa mchungaji anakufundisheni kuandika maneno kama haya.kwani bibilia inasema tusinie yasiyotupasa kunia.kwanini ujifanye unajua kila kitu na unajiamini kama vile hakuna mtu anayejua zaidi yako hata kusikiliza ushauri hutaki ujue WeWe Hujajua kitu kabisa nadhani ungechukua muda kusoma unayoyaandika na kuyatathimini ungegundua kuwa bado wewe ni mtoto mdogo ambaye unatakiwa unywe maziwa yasiyoghoshiwa ili uukulie wokovu.kama kweli uko Elishadai kwani uko mbali na kweli huwezi kuwa unamjua Mungu na kisha ukamkataa kwa kupingana naye.kama kweli wewe ni kisima cha upendo kwanini unatoa maji machungu yanayo waumiza watu.
Maneno hayo hayo ungeweza kuyaleta vizuri tu kwa nini utimie mizaha na maneno yasiyofaa au yenye kumtuliza muhitaji.
Kutumia maneno kama marehemu wakati inajua ule ulikuwa muungano wa vyama au watu fulani sidhani kama inajenga kama mtu unayemwamini Mungu.umetumia kejeli chungu mzima ambazo hazikuwa za lazima.bado story yako ingependeza kama ungeiandika tu kama inavyowafaa watakatifu kwani hatupaswi kubadilika na kuwaweupe mahali fulani na kuwWeusi mahali pengine.soma Ufunuo wa Yohana 3 ujue ni wapi ulupoanguka na kutubu. Usihukumu usije ukahukumia.nimejaribu kukupa angalizo kama utasikia sawa la kama hutasikia naamin Mungu atasema nawe na namna nyingine.Paulo Mtume lwenye Warumi anasema mwingine anakula hiki mwingine analula hiki basi tunapaswa kuchukuliana na udhaifu wa kila mwingine.hata ikibidi kutokula kama kinamkwaza mwingine.Happy unawakwaza wengine acha mizaha katika mambo ya msingi ujue demokrasia inaruhusu kila mtu kutoa aliyonayo kwauhuru.kama CCM ilijipanga vizuri inaonyesha kukomaa kisiasa.lakini swali la kujiuliza je hao wengine je nao hawakujipanga?lakini je wanao uhuru uliowazi wa kufanya lama hao baba zetu.kama hawana usisifie tu kwani kama mwana sheria unajua hakuna haki.
Kama katiba imeisha kujadiliwa hakuna haja ya kushabikia kuwa wamefariki umoja bora ungesema kuwa umoja wao sasa umevunjika.kusema amezikwa ukawa je kiswahili sanifu ni kweli au unaharibu lugha.
Mwisho nakupongeza kwani unalijua vilivyo somo la propaganda za siasa naamin mwakani utafaa kwenda jimboni kwako unapotoka.angalizo kwenye kutoa maamuzi kama hutabadika hutafaa kuwa mbunge wala mkuu wa wilaya.
On Oct 5, 2014 9:42 AM, "Ireneus Kakuru Mushongi" <ireneuskakurumushongi@gmail.com> wrote:
We mtoto,
Juzi ulishea na sisi life progress ya kwako tukaona uko kwenye trend nzuri ya professionalism, tukakuencourage kukeep up kumbe unknowingly we never know you have a troubled mind.
Sasa unajaribu kutuprove wrong kwamba wewe si yule tuliyemfikiria alivyo.
Hatupingi wewe kuonyesha hisia zako za kisiasa ama ni njaa driven ili baadaye ufikirike katika tunu zao..  but this is too wrong!
Hii ni personal hatred unayoonyesha kwa kutumia kalamu yako but as well ni kinyume na taaluma ya sheria unayohangaika kuisoma kwa sababu inahitaji a critical thinker ambaye si wewe kwa akili hii.
Stop and think before allowing your pen to sail through a paper and place yourself on the other side then you will decide a way forward.
Njaa isikusumbue. Mgema akisifiwa..tembo hulitia maji.. this way you are distorting your image and professionalism.
I bet ungeanza kuandika riwaya uuze kwani una muda mzuri wa kutengeneza hadithi ili kuwafurahisha mashabiki wako...unless you are a propagandist wao.. ukamsaidie bwana mdogo yule majukwaani..unaonekana unapataka kwa nguvu. Kadi si unayo tayari?
Nimemaliza.. Ngambila balinsi... Kajungu malizia...
On Oct 4, 2014 8:05 PM, "Erick Maro" <rikmaro@gmail.com> wrote:
Maneno mengi kumbe zote Pumba.
On Oct 3, 2014 5:55 PM, "'jabir yunus' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Kwa hivo tulikuwa na marehemu UKAWA, ambaye tunaarifiwa kuwa amefariki dunia, siyo? Marehemu anafariki dunia!!!!

Duh, ama kweli, kazi ipo.

Jabir+
--------------------------------------------
On Fri, 10/3/14, 'ezekiel kunyaranyara' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: Re: [wanabidii] BURIANI UKAWA
 To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Friday, October 3, 2014, 3:21 PM

 Wanajamvi
 Si kila kitu kinaweza kuguswa kwenye Katiba.
 Mengine tena Mengi yataingizwa kwenye sharia zitakazotungwa
 na BUNGE. K.E.M.S.


      On Friday, 3 October
 2014, 10:47, Boniface Magessa <magessabm@gmail.com>
 wrote:


  Njaa ni mbaya sana...halafu huyu
 dada si yuko chini ya kituo cha sheria na haki za binadamu
 kinachomiliki university of bagamoyo!!!!napenda atambue kuwa
 mwajiri wake anapingana na yeye....kama sujakosea...
 On 3 Oct 2014 10:14,
 "Selemani Rehani" <srehani@hotmail.com>
 wrote:



 Domilia,
  
 Hongera kwa uvumilivu wako. Mimi nilipona anarudia rudia
 nikadelete wala sikusoma. Hongera kwa uvumilivu wako wa
 kusoma visivyosomeka.
  
 Date: Fri, 3 Oct 2014 00:11:20 -0700
 From: wanabidii@googlegroups.com
 Subject: Re: [wanabidii] BURIANI UKAWA
 To: wanabidii@googlegroups.com

 Dear Katabazi,

 Nimesoma
 ujumbe wako: jibu fupi ni hili:



 MAMBO
 YA MSINGI YANAYOKOSEKANA KWENYE KATIBA:1.0       
 Mfumo mbovu wa uongozi na utendaji serikalini na
 taasisi zake Tanzania bado     
 haujaguswa kwenye katiba......2.0     
 Nani atawadhibiti wanasiasa kwa kuweka ukomo wa ubunge?
 Wananchi wamenyimwa hiyo fursa ndani ya katiba
 "mpya".......

 3.0    
 Uwajibikaji na kutenganisha serikali, bunge na
 mahakama: kuharamisha mbunge kuwa waziri, 
 kusitisha teuzi lukuki za Rais........4.0 Idadi ya
 mawaziri kuwa 30 badala ya 15 ya mapendekezo ya wananchi.
 Kwa nini mawaziri 30? Ni wa nini? Kwa
 rasilmali gani tulizo nazo kubeba mzigo wote huo? Watafanya
 kazi gani?
 5.0 Idadi ya
 wabunge 390 ya nini badala ya 75 Bunge la Muungano? Ni wa
 nini?
 6.0    
 Kwa nini hakuna miiko ya uongozi iliyo inayotamkwa na
 Katiba, wakati tatizo kubwa la viongozi (ni wengi) TZ ni
 ukosefu wa maadili, uwajibikaji, uzalendo, uwazi
 nk.?7.0 Taifa la
 Tanzania linajivunia TUNU gani? Amani hakuna tena wala umoja
 - ni hadithi tu sasa hivi!


 8.0 Nani
 atashughulikia mambo ya Muungano, na yasiyo ya
 Muungano?

 Uwe mwangalifu
 Katabazi
 Domilia




      On Thursday, October 2, 2014
 11:43 PM, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
 wrote:




 BURIANI   UKAWA

 Na
 Happiness Katabazi
 HAPPINESS
 Katabazi nimepokea kwa  furaha  kifo Cha Marehemu
  Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kilichotokea jana
 saa nne asubuhi ya Oktoba 2 mwaka huu, jijini Dar es Salaam,
 kutokana na maradhi ya shinikizo la Damu (BP).
 Marehemu
 Ukawa alikumbwa na umauti Jana  wakati
  akitaka  kuingizwa Kwenye Gari akimbizwe hospitalini
 akatibiwe.
 Kwa
 mujibu wa mashuhuda  tukio Hilo,   walisema
  Marehemu Huyo   alikuwa ameketi kwenye
 Televisheni akifuatilia kikao cha Bunge Maalum la Katiba
 lilokuwa likiitimisha kazi yake mjini Dodoma, na ghafla
 Ukawa  Alipomuona na kumsikia Katibu wa Bunge la
 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Thomas Kashilila
 akitangaza matokeo ya kura zilizokuwa zimepigwa na wajumbe
 wa bunge hilo na kumsikia Dk.Kashilila akisema theluthi
 mbili ya Zanzibar imepatikana na kwamba Katiba
 iliyopendekezwa na Bunge imepitishwa kwa kupigiwa kura
 nyingi za ndiyo.
 Ndipo
 marehemu Ukawa hali yake ya kiafya ikabadilika ghafla na
 alianza Kulalamika  kuwa anajisikia vibaya anaomba
 apepewe  ili apate hewa kwani anaona Giza na anapumua
 kwa Shida sana.
 Jamaa
 waliokuwa wamekaa na Ukawa,walianza kumpepea huku wengine
 wakimfungua Vifungo Vya shati na Kumvua viatu na kumpepea na
 wengine wakitafuta Gari ili wamkimbize Hospitali , lakini
 wakati wakimtoa Ukawa ndani ya nyumba yake wampakize Kwenye
 Gari ,Ukawa aliwafia mikononi Kabla ya kapakizwa Kwenye Gari
 Hilo.
 Hata
 hivyo mashuhuda walisema waliukabidhi mwili wa Marehemu
 Ukawa hospitalini ', ukiwa Tayari wa baridi na Daktari
 na kwamba hadi marehemu huyo anakumbwa na umauti
 hakufanikiwa kupata nafasi ya kututubu dhambi
 zake.
 Na
 walisema kwa mujibu wa ripoti ya daktari ,Daktari amesema
  Chanzo Cha kifo Cha Ukawa  ni ugonjwa wa
 shinikizo la Damu lilompata baada ya kusikia tangazo kuwa
 Katiba iliyopendekezwa na Bunge imepitishwa  na
 theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar imepatikana maana
 Enzi za Uhai wake Marehemu Ukawa Aliaminisha umma Kuwa
 theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzinar
 haitapatikana.Marehumu Ukawa amekumbwa
  na aibu licha ni Marehemu.
 Msiba
 wa Marehemu Ukawa ulifanyika jana ile ile na mwili wake
 ukazikwa Kinondoni Mtaa wa Ufipa  yaani Makao Makuu ya
 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 Na
 waombolezaji walipata fursa ya Kuweka mashada  ya maua
  Kwenye Jeneza Hilo la Marehemu Ukawa , na Jana jioni
 ndugu wa Marehemu Ukawa walianza kuweka  tanga ndugu
 ambapo tanga ndugu hiyo ya siku Tatu inamalizika
 Kesho. 
 Waombolezaji
 walikuwa wakitoa sifa za Marehemu Kuwa Marehemu alikuwa ni
 mkorofi, Ana maneno makali, Mzushi Kwani alikuwa akijitapa
 ametumwa  na Watanzania Kumbe muongo maana  hata
 hajawahi kutoa orodha ya Majina ya Hao Watanzania
 waliomtuma,  mchonganishi,hakutaka Katiba
 iliyopendekezwa na Bunge ipatikane na alisusia vikao vya
 bunge akaamua kwenda kusiko julikana maana jimboni alikuwa
 haonekani,mbinguni haonekani.
 Marehemu
  Ukawa Enzi za Uhai wake alijiapiza na kuaminisha umma
 Kuwa ni lazima Bunge livunjwe Kwani
  theluthi mbili ya wajumbe wa Zanzibar
 haitapatikana.
  Lakini
 Jana theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar ilipatikana
  na Katiba iliyopendekezwa na Bunge ikapitishwa na
 Oktoba 8 Mwaka huu,   Bunge Hilo litamkabidhi Rais
 Jakaya Kikwete.  Ukawa ndiyo akajikuta amepatwa na
 ugonjwa wa BP  na kufariki Dunia ghafla bin vuu.Poleni
 sana Wafiwa.
 Marehemu
 Ukawa amefariki Kipindi Kizuri wakati Watanzania Wengi
 hatukuwa tukimuamini   tena na Kumuunga mkono mAana
 tulishambaini Ukawa ni kiongozi
  asiyeitakia Mema Tanzania ,alikuwa anaamasisha wananchi
 wavunje  Sheria za nchi na waandamane na wagome
  bila kikomo na Matokeo yake baadhi ya wafuasi wake
 walijaribu kuandamana lakini jeshi la polisi mikoa yote
 iliweza kuyasambaratisha maandamano Kabla hata
 hawajaandamana.
 Unapoizuzungumzia
 Ukawa ,hasa Unaizungumzia Chadema na CUF.  Lakini
  Katika Ukawa , Chadema ndiyo ilikuwa na Nguvu na sauti
 Kwani hapa Tanzania Bara ndiyo Chama Kikuu Cha upinzani na
 ndicho chenye wabunge wengi  kuliko CUF, NCCR- Mageuzi
 na ilikuwa Ikiungwa mkono na baadhi ya viongozi wa Taasisi
 za kidini.
 Wakati
 Bunge Maalum lililokuwa linafanyakazi yake kuliibuka vitendo
 Vya baadhi ya wajumbe toka kundi la Ukawa, CCMkutolea maneno
 yaliyofaa na niliwahi kukemea tabia hii kupitia Moja ya
 makala zangu.
 Lakini
 Marehemu UKAWA ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa wajumbe
 wa Bunge hilo yeye alidai ameshindwa kuimarisha vijembe
 hivyo na kwamba Akiamua kwenda kushitaki kwa wananchi Kuwa
 wajumbe wa Bunge Hilo toka CCM wamekuwa wakiwadhalilisha
 sana.
 Watanzania
 waliwasilikiliza na kuwapima na Mimi Nikiwa mmoja wao
 nilimsikiliza  Ukawa na kumuona Hana hoja   ya
 Msingi maana  Kama kutolewa lugha ya kejeli hata wao
 nao walikuwa wakiwatolea wenzao lugha za kejeli Cha Msingi
 wasisusie vikao Vya Bunge.
 Ushahidi
 wa kuthibitisha Kuwa nilimshauri Marehemu UKAWA kupitia
 makala yangu ya Agosti 3 Mwaka huu,iliyokuwa na kichwa Cha
 Habari kisemacho " Ukawa Rudini Bungeni", huo hapo
 ndani ya makala hiyo nilimshauri Marehemu Ukawa arudi ndani
 ya Bunge akatetee Katiba ya wananchi akiwa ndani ya Bunge,na
 kwamba kususia bunge siyo suluhisho na mwisho wa siku sisi
 tutamfananisha Ukawa ni sawa na 'kamanda
  aliyeama kambi vitani',Marehemu alinipuuza  Hadi
 Jana umauti wa ghafla ulimkuta na ameacha historia Mbaya na
 rekodi yake hapa nchini imeifadhiwa Kuwa Ukawa alikuwa Hana
 mapenzi Mema na nchi yake.
 Kifo
 hicho kilichomkuta Marehemu Ukawa Jana, ni Ishara Mbaya
 kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa
 Mwaka 2015 hasa kwa Chadema na CUF. 
 Hatua
 ya  Jana Bunge kupitisha Katiba iliyopendekeza ni wazi
 'kisaani' kimepinduliwa pinduu.
   
 Hakuna
 Cha Ukawa tena kusikilizwa na wananchi, wananchi wanachotaka
 sasa nikuiona na kuisoma Katiba iliyopendekezwa na Bunge
 walisomea wenyewe na wataalamu wawaelimishe kuhusu kilichopo
 ndani ya Katiba hiyo ya Bunge la Katiba na sisi wasomi wa
 Sheria nao HIvi sasa tuna shahuku  kubwa ya kuipata
 nakala hiyo ili tuweze kuisoma    na wahadhidhiri
 wa Sheria waweze kuwafundishia wanafunzi wao wa fani ya
 Sheria vyuoni.
 Hivyo
 ule Wimbo wa ' Rasimu ya Tume Warioba'.  HIvi
 sasa umechuja. Wimbo unaotamba sasa ni Wimbo wa '
  Katiba iliyopendekezwa na Bunge au Katiba ya Mzee Sugu
 ,Samuel Sitta'.
 Sasa
 kwakuwa Marehemu Ukawa alisusia Bunge Hilo na yeye Ukawa
 alikuwa Mtetezi wa rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ambayo
 Tayari ilishakufa tangu Jana na kuzaliwa Katiba
 iliyopendekezwa na Bunge, sijui sasa Marehemu Ukawa
 atafufuka aanze kuipinga Katiba iliyopendekezwa na
 Bunge?
 Jibu
 hawezi kufufuka tena kwasababu Ukawa yupo jehanamu kwa baba
 yake shetani na shetani Hana huwezo wa kumfufua
 Marehemu.
 Labda
 Ukawa Angekuwa ameenda mbinguni , Mungu angeweza kumfufua
 kwasababu Mungu Ana mamlaka ya kuumba, kuruhusu mtu
  afe na kufufua Katika wafu. Pole sana Marehemu
 Ukawa maana  hivi  sasa upo Katika ziwa la Moto
 jehanamu na umekuwa Kuni huko jehanamu.
 Na
 ndiyo basi tena ulilolitaka halikuwa tulia huko huko
 jehanamu uungue na Moto maana hayo ndiyo malipo ya sala za
 watu tulizokuwa  tu liloombea taifa,  Bunge Hilo
 limalize salama Kazi yake na wale wote wenye jicho la husuda
 ,wanaotaka kuleta machafuko
  ,Mungu  awashughulikie  ,sasa hiyo ndiyo Adhabu
 yako.
 Marehemu
 Ukawa Enzi za Uhai wake aliposusia vikao Vya Bunge Hilo,
 akajigeuza yeye ni mbunge wa Tanzania Kumbe siyo.
  Wakati
 Marehemu Ukawa analazimisha wananchi waamini Bunge lilikuwa
 linafanya ubakaji wa Demokrasia ya kuichakachua kinyume Cha
 Sheria Rais ya Warioba wakati akijua Kifungu Cha 25(2) Cha
 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2014.
 Chama
 Cha Mapinduzi kupitia Katibu Mkuu wake,Abdullaman Kinana na
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, walizidi kuchanja
 Mbuga kuimarisha Chama ' kustimleti' wanachama
 wake.Na wakati huo CCM kupitia wanachama wake wakawa
 wanakiwalisha  vyema Chama chao ndani ya Bunge Maalum
 la Katiba kwa njia ya Amani.
 Na
 kwa mtazamo wangu ,mbinu hiyo inayotumiwa na CCM kupitia kwa
 Kinana, Nape na waliokuwa wajumbe wa Bunge Maalum la
 Katiba,ni Moja ya kujisafishia njia ya kupata ushindi mzito
 wa CCM  Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na
 Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
 Wakati
 CCM imejiimarisha na kujijenga hivyo kimkakati, Siyo
 Chadema, CUF , NCCR Mageuzi Navyo kila Chama kwa wakati wake
 havifanyi  harakati za kustimuleti wanachama, zaidi
 Tunaona Chadema viongozi wake wanaowaamasisha wanachama wao
 waandae  maandamano haramu ambayo Jeshi la Polisi lime
 yapiga marufuku.
 Tunachokishuhudia
 ni kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo Vya upinzani kila
 mtu akijitafutia Umaarufu binafsi kwa Malengo yake binafsi
 ya kupata Ubunge au kutetea Kiti Cha Ubunge na wengine
 wabunge wa Ukawa nao wamenukuliwa
  wakisema wa kiombwa Kugombea urais, watagombea.
 Mbatia
 ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi yeye anadaiwa kuwa
 anataka Kugombea Ubunge jimbo la Vunjo.
 Viongozi
 wengine wa Ukawa nao Wanadaiwa Kuwa wanataka Kugombea urais
 hivyo akili zao na Nguvu za wanazielekeza  kwa jinsi ya
 kuwashika wajumbe watakaopitisha Majina Yao ndani ya vikao
 husika Vya vyama vyao na siyo kuvijenga kwanza vyama
  vyao na kuviandaa kupata ushindi Katika uchaguzi wa
 serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu Mwaka
 2015. 
 Na
 hapa ndipo vyama Vya upinzani hapa nchini vinapokosea na
 mwisho wa siku uchaguzi ulifanyika wakishindwa wanaanza
 kujitetea CCM imewaibia kura, Tume ya Uchaguzi wa Taifa,
 haipo Huru.
 Tafadhali
 sana Vyama Vya upinzani hatutataka tena kusikia utetezi huo
 Mara baada ya Uchaguzi wa serikali za mtaa, uchaguzi Mkuu
 kumalizika.Maana mmejimaliza wenyewe ,badala ya Kujenga
 vyama vyenu na kujiandaa kikamilifu na uchaguzi wa serikali
 za mitaa karibu Mwaka mzima sasa mmeupoteza kwa kuzungumzia
 Habari za Ukawa,Ukawa na mwisho wa siku
  hamjafanikiwa.
 Wakati
 wenzenu wa CCM walikuwa wakifanya mambo yote kwa wakati
 mmoja.Yaani CCM ilijigawa Makundi . Moja ya kundi Lao
 linaloongozwa na Kinana, Nape linazunguka mikoani kuimarisha
 Chama chao na kustimuleiti wachama wao na wengine kuingia
 ndani ya Bunge Maalum la Katiba kutunga Katika
 iliyopendekezwa.
 Ipo
 siku Chadema watakuja kukubaliana na Mimi Kuwa Huyo Mshauri
 anayewashauri viongozi wa juu watoe matamko ya kuamasisha
 wanachama wao washiriki maandamano yasiyo na Kibali ni
 Mshauri Mbaya sana ambaye ala
  Lengo  Moja baya sana la kuisambaratisha Chadema na
 Watanzania wameishaanza kuona Chadema ni Chama Cha Vurugu na
 Watanzania ni wapenda Amani.
 Mapema
 kabisa niliisa  Chadema Kuwa kijitambue Kuwa ni Chama
 Kikuu Cha upinzani na kina wabunge Wengi, na siyo vyama Vya
 upinzani vinapenda mafanikio hayo ya Chadema,Chadema
 haikunielewa ila ikalazimisha  urafiki na baadhi ya
 vyama Vya upinzani ambavyo vyama hivyo havina mvuto tena wa
 kisiasa hapa nchini ila vimeanza kusikika kupitia Marehemu
 Ukawa.
 Tangu
 Jana
  Katiba ilivyopitishwa na Bunge , wafuatiliaji wa mambo ya
 siasa wanaamini hiyo ni Ishara Mbaya  kwa Chadema na
 siyo Ukawa tena ambao ilikuwa Ikiundwa na CUF, NCCR
 Mageuzi.
 Wafuatiliaji
 Hao wameibuka na mtazamo huo Kwasababu ni wazi Chadema Ndio
 ilikuwa na sauti na wajumbe Wengi Kwenye Ukawa kuliko Vyama
 vingine. 
 Hivyo
 ni Ishara Mbaya Kwa Chadema Kuwa jaribio la kutaka
 kuandamana bila kukoma na kuvunja Sheria za nchi na
 limeshindikana, Njama Yao ya upotoshaji umma Kuhusu Kuwa
 Bunge Maalum la Katiba halipo
  Kuhalili na linafuja Fedha za wananchi, Theluthi mbili ya
 wajumbe wa Zanzibar haitatimia zimeshindwa vibaya sana na
 wameumbuka wao Chadema na Marehemu Ukawa.
 Nalipongeza  
 Bunge Hilo lilokuwa likiongozwa na 'Mzee Sugu au Mutu ya
 Danjeee'-  Samuel Tengeneza Sitta na Makamu wake
 Samia Suluhu. 
 Pia
 nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba
 iliyopendekezwa na Bunge, Mtemi Andrew Chenge na Aliyekuwa
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni , Profesa Costa Ricky Mahalu.
 Sitta, Chenge.Mahalu wote hawa
  ni wasomi wa Sheria tena siyo wa kubabaisha.
 Hongereni
 na timu yenu mmefanyakazi ambayo mmeandika historia na
 mmeacha alama Kwenu na  vizazi vyenu.
 Na
 kwa wale Ukawa  nao wameacha historia Mbaya ambayo siyo
 ya kupigiwa mfano ya kususia Bunge hilo na Mara kwa Mara
 wakawa wananukuliwa na vyombo Vya Habari wakiliombea dua
 mbaya Bunge Hilo Kuwa akidi haijatimia Mara Bunge
 litarejeshwa, Matokeo yake Bunge alikuhiishwa wala kuvunjwa
 na akidi ikatimia na Katiba iliyopendekezwa na Bunge
 imepatikana. Kweli dua la
  Kuku halimpati Mwewe.
 Na
 kwa wale wasomaji wa makala zangu watakumbuka Kuwa tangu
 mchakato wa Bunge Maalum la Katiba lianze kuandika Katiba
 hiyo, nilijiokeza kuandika makala zaidi ya Tatu na makala
 hii ya Leo ni ya nne.
 Makala
 ya kwanza niiliitoa Agosti  3 Mwaka huu, ilikuwa na
 kichwa Cha habai kisemacho: " Ukawa Rudini
 Bungeni'.  Makala pili il ilichapishwa Kwenye
 Gazeti la Rai  la Septemba  18   Mwaka huu,
 ambayo ilikuwa na kichwa Cha Habari " Freeman Mbowe,
 Dozedozee".  
 Makala
 ya tatu niliandika Septemba 22 mwaka huu,ilikuwa na kichw
 acha habari kisemacho 'Wanaolazimisha maandamano ni
 maajenti wa shetani". Makala ya nne  ilichapishwa
 Katika Gazeti la Rai la Septemba 25 Mwaka huu, ilikuwa
  na Kichwa Cha Habari : " Tuna Chui wa
 Karatasi,siyo waandamanaji. Na Leo naandika makala hii yenye
 kichwa Cha Habari kisemacho  ' Buriani
 Ukawa'.
 UKAWA
 ambao wengine ni wabunge wakati wa Kipindi kile Cha Bunge
 linaandaa Katiba iliyopendekezwa wakasusia Bunge. Hawakuweza
 kujulikana wapo
  Duniani au mbinguni! Maana majimboni Kwao walikuwa
 hawaonekani wala bungeni hawaonekani.
 Kwa
 kitendo historia hii iliyoandikwa Jana na Bunge akidi ya
 wajumbe kupatikana, Je Ukawa  hawaoni  hii ni aibu
 Na fedhea kwao?
 Kwa
 Sababu  ni Ukawa ndiyo alikuwa  akipayuka
  mitaani Kutaka Bunge Hilo livunjwe Kwani ni matumizi
 Mabaya ya madaraka na ufujwaji wa Fedha za walipa kodi kwa
 kitendo Cha Sitta kulazimisha Bunge liendelee wakati akijua
 wazi theluthi mbili ya Wajumbe toka Zanzibar
  haitapatikana.
 Marehemu
 UKAWA ambaye alikuwa akiitetea na hakutaka kabisa rasimu ya
 Tume ya Jaji Joseph Warioba isiguswe  wala kukosolewa
 wala kupunguzwa kitu chochote kile ili wakifahamu kifungu
 cha 25 (2) cha Sheria ya Mabadiliko Sura ya 8 kama
 ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2014 ,yanalipa madaraka
 Bunge Maalum la Katiba kuboresha rasmi ya Warioba au kuweka
 vitu vipya.
 Hadi
 Jana umauti unamkumta Marehemu Ukawa,alikuwa hajatubu
  dhambi zake   Mbele ya Watanzania ikiwemo dhambi
 ya kuchochea wananchi
  waandamane bila vibali vya Polisi, uongo na upotoshaji
 mkubwa kuhusu majukumu ya Bunge hilo, Marehemu  alikuwa
 akiwadanganya Watanzania Kuwa kura za kupitisha  Katiba
 iliyopendekezwa na Bunge hazitatosha Kwani theluthi mbili
 toka Zanzibar haitapatikana, hakuungama.
 Na
 kwakuwa hakuungama, aliendelea kushupaza shingo hadi umauti
 umemkuta , ni wazi Marehemu Ukawa amekwenda jehanamu ya Moto
 kwenda kuonana na baba yake Shetani Kwani Biblia in atuambia
 Shetani ni Baba wa Uongo, na Ukawa hapa Duniani alikuwa ni
 muongo,mchonganishi, mkorofi, aambiliki na hizo ni miongoni
 mwa sifa walizonazo wafuasi wa shetani. 
 Hivyo
 Ukawa alikuwa ni Ajenti wa shetani ambaye alikuwa anaenda
 kuona Katiba iliyopendekezwa na Bunge Hilo hazipatikani na
 Tanzania I naingia Kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe
 kwa kisingizio Cha mchakato wa Kuipata Katiba.
 Lakini
 Kwa Kuwa bado Mungu anaipenda Tanzania na watu wake
 wanaipenda Kwasababu kuna baadhi ya viongozi wa dini akiwemo
 kiongozi wa Kanisa la Elishadai  la Boko Basiaya,Dar es
 Salaam, Kanali Mstaafu ,Bruno Kinunda na waumini wake kila
 Ibada ya Jumapili tulikuwa  tunaanza ibada kwa
 kujitakasa dhambi zetu na kuliombea  taifa na mchakato
 na Bunge Maalum la Katiba lifanyekazi zake kwa Amani
  na utulivu na kweli Hilo limefanikiwa na Bunge Hilo
 kumaliza Kazi yake Jana kwa Amani .
 Hongera
 Lilokuwa Bunge Maalum la Katiba kwa kumaliza Kazi yake
  salama licha Bunge lilipitia Katika wakati mgumu wa
 kurushiwa vijembe na kuonekana linawasaliti Wananchi jambo
 ambalo Si la kweli .Binafsi nimefurahishwa na Hatua hiyo ya
 Bunge Hilo kutuletea Katiba iliyopendekezwa na
 Bunge.
 Wasomo
 wa Sheria tunasema Hatua inayofuata  ni Katiba hiyo
 kupelekwa Kwa wananchi ili wapigie kura ya ndiyo au
 Hapana. 
 Hivyo
 wananchi msipotoshwe ,kisheria bado Katiba mpya ya Jamhuri
 ya Muungano wa Tanzania haijapatikana.
 Tutulie,
 Tusikubali kushawishiwa na maajenti wachache  wa
 shetani kuingia mitaani kuanza kuipinga Katiba hiyo
 iliyopendekezwa na Bunge wakati bado hata haijatangazwa
 Katika Gazeti la Serikali ,na hatujaisoma na kuielewa na
 mambo gani mazuri na mabaya yapo ndani ya Katiba
 hiyo.
 Na
 ieleweke Kuwa kila Mtanzania mwenye umri wa kupiga kura
 Ndiyo ataruhusiwa kupiga kura ya ndiyo au Hapana kuhusu
 Katiba hiyo  Katiba hiyo.
 Tayari
 kuna watu wameanza kutoa maneno ya kejeli kuhusu upitishwaji
 wa Katiba hiyo,lakini wapingaji Hao hawana hoja zenye
 mashiko na Hakuna hata mmoja aliyeipata nakala na kuisoma na
 kuilewa. Wapingaji Hao ni sawa na Mfa Maji haishi
 kutapatapa.
 Ni
 wajinga na wapuuzi wachache ambao wao kila
  kitu kinachofanywa na serikali, Bunge wanapinga eti tu
 kwasababu Taasisi zao zinaendeshwa na wanapata ufadhili
 kutoka  kwa 'mwabana' zao huko nje ya nchi kwa
 Kigezo Kuwa wao ni wakosoaji wa kubwa  kila kitu
 kinachofanywa na serikali na ni Watetezi wa Haki za binadamu
 huku wakisahau Haki inaendana na wajibu.
 Wakati
 Bunge Maalum la Katiba lilipokuwa likifayakazi yake
 tulishuhudia Jaji Joseph Warioba baadhi ya Wanasheria ,
 wanaharakati ambao wamesoma somo la Katiba wanafahamu hatua
 za kutengenezwa kwa Katiba, wakitoa matamko ya kupotosha
 umma kuhusu mamlaka ya Bunge Hilo.
 Nao
 baadhi ya waandishi wa Habari ambao hata somo la Sheria la
 Katiba Hawajawahi kulisoma na hata hawafahamu Hatua
 zinazotakiwa zipitiwe wakati taifa husika linatengeneza
 Katiba yake.
 Waandishi
 hao baadhi  ambao wamepachikwa jina la 'Mavuvuzela
 ya Ukawa' , Katika Kipindi chote hicho hawakutaka
 kujifunza Hatua hizo na Matokeo yake wakajikuta wao
 wanaingia Kwenye Mkumbo wa kupelekeshwa na kuaminishwa uongo
 na marehemu Ukawa na kisha wakauchapisha  Kwenye vyombo
 Vya Habari. Nao wameumbuka Kama alivyoumbuka Marehemu Ukawa
 Jana.
 Historia
 ya maandishi Yao nayo itawahukumu kwasababu  baadhi ya
 waandishi nao walikuwa wakiandika  Bunge litavunjwa,
 Bunge limechakachua rasimu ya Warioba na kupuuza maoni
 ya wananchi bila Kuwa na ushahidi wa hayo.
 Na
 Mbaya zaidi baadhi ya Wanasheria na waandishi wa Habari
 walidiriki kupotosha umma kuhusu amri mbili tofauti
 zilizotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Katika
 Kesi ya Kuomba Bunge Maalum la Katiba lisimame ambayo
 imefunguliwa na Mwandishi wa Habari Saed
 Kubenea. 
 Ambapo
 Mahakama hiyo ilitoa amri ya kutupilia Mbali ombi la Kubenea
 na kuruhusu Bunge Hilo liendelee na Kazi yake.Kuna baadhi ya
 waandishi na Wanasheria baada ya Mimi kuandika Habari
 kupitia Mtandao wakinipa ya Kuwa Mahakama hiyo haijatoa amri
 hiyo ilihali ukweli ni kwamba Mahakama ilikuwa imetoa amri
 ya kulitupa ombi la Kubenea lilokuwa linataka Bunge
 lisimame. Kioja Cha aina yake.
 Aidha
 kwa makusudi Marehemu Ukawa na wafuasi na baadhi ya
 waandishi wa Habari waliamua kupotosha ukweli kupitia
 mitandao amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ya
 Septemba 25 Mwaka huu, Katika ombi dogo Na. 28/2014
 lilofunguliwa na Kubenea
  dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  ambapo Mahakama
 hiyo pamoja na mambo mengine ilisema Bunge Maalum la Katiba
 Lina madaraka ya kufanyia maboresho na kuongeza vitu Katika
 rasimu ya Tume ya Warioba kwa mujibu wa Kifungu ha 25(2) Cha
 Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka
 2014. 
 Sijui
 walikuwa na Lengo gani yarabi. Na wengine nao akiwemo
 Warioba alisema  hafahamu hiyo theluthi mbili ya
 Wajumbe toka Zanzibar itapatikana wapi  maana eti haipo
 na kwamba Sitta ,ni jeuri sana.
 Niitimishe
 Kwa Kusema
  Tanzania ni yetu sote ,hivyo sote Tushikamane kuilinda na
 kuijenga.Mchakato wa kuipata Katiba mpya isiwe Kigezo Cha
 kuisambaratisha Amani yetu.
 Tutumie
 majukwaa sahihi na wakati sahihi kuisoma Katiba
 iliyopendekezwa na Bunge.Na Kwa Kuwa Ukawa Tayari
 ameishafariki na kuzikwa na ile rasimu Tume ya Jaji Warioba,
 ni imaini Yale malumbano na uchonganishi wa kipuuzi
 hautakuwepo kabisa au utapungua sana.
 Labda
 Mzimu wa  Ukawa uibuke  na kuanza Kuzusha
  sokomoko, lakini kwakuwa Tayari Watanzania
 walishambaini
  Marehemu Ukawa ndiyo alikuwa Mzushi ,Kisarata Mtaa,
 kizabinazabina na aliwasaliti ,watajiuliza maswali
 haya;
 Je
 Mzimu  Ukawa  ulikuwa  ni miongoni mwa
 wajumbe waliyoshiriki kuitunga Katiba iliyopendekezwa na
 Bunge?
 Watajijibu
 Kuwa hakushiriki kwani alisusia bunge.Na Kama alisusia Bunge
 atawezaje kufahamu kwa kina ni njema ya Bunge la Katiba
 kutengeneza Katiba iliyopendekezwa?
 Watajijibu
 kuwa Mzimu wa Ukawa una nia ovu ya kutaka kuikwamisha kwa
 makusudi Katiba iliyopendekezwa na Bunge .
 Watanzania
 hawausikiliza Mzimu huo wa Marehemu Ukawa, wataupuuza
  na watamtimua Kwani anawezakuwaletea  matatizo ya
 kufunguliwa Kesi mahakamani na kupigwa virungu na Polisi na
 kulala selo Kama Marehemu Ukawa alivyowasabishia wa kapigwa
 virungu na Polisi na kufunguliwa Kesi za jinai mahakamani za
 makosa Kama kuingia kwa jinai, kufanya mkusanyiko
 haramu.
 Buriani
 Marehemu Ukawa ,hatutakuona tena.
 Chanzo: Facebook:
 Happy KatabaziBlog: www.katabazihappy.blogspot.com0716
 774494Oktoba
 3 Mwaka 2014.







 Sent from my iPad



 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.







 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment