Wednesday, 29 October 2014

Re: Re: [wanabidii] ZITTO KABWE - UKAWA NI WASAKA TONGE

Ushindani wa kweli kisiasa kwenye nchi ya Tanzania utakuwepo endapo nchi itakusudia kwa dhati kuwekeza kwenye elimu, la lengo la 'kuongeza kiwango cha uelewa wa watu wote;' na nchi kujiwekea mkakati wa dhati kufikia hapa.

Siasa zisizokuwa na mashiko zilizopo, zinatokana na uelewa duni wa wananchi. Nia ilikuwepo tangu uhuru, ila, katikati, ililega, na ililegezwa maksudi kwa manufaa ya kisiasa zaidi licha ya ukweli kuwa elimu ndio msingi wa afya, uchumi, na mazingira bora.

Nchi kama nchi, inatakiwa dira ya elimu iwe na viwango vya elimu inaavyovitaka raia wake wote wavifikie. Dira hii ilikuwepo, kuwa na wajuzi wa ngazi ya kati kwa ajili ya kuendeleza viwanda vyetu, ila siasa za ulimwengu zikiwemo za taasisi za fedha za ulimwengu, ziliivuruga, tena wakabadilisha sera ya kusaidia vyuo vikuu na badala yake wakaanza kusaidia elimu ya awali miaka ya 80 na 90. Katikati ya miaka ya 90, wakagundua, walivurunda, wakaanza tena taratibu hadi tulipo leo, hata hivyo, sio kwa sera za awali tena, wamekuwa wabahili kuliko!

Ila kimsingi, hakuna taifa litakalokufundishia watu wako maana kufanya hivyo ni kujitengenezea wapinzani wa kesho. Jukumu la kuelimisha watu, siku zote ni jukumu la nchi husika. Tanzania tunajaribu ila hatuna dira, dira iliyojificha ni kuhakikisha mafanikio ya kisiasa siku zote yanapatikana, na ili iwe hivyo, uelewa uwepo kwa wachache ambao kwa namna moja, ndio hao wachache wanatarajiwa kuwa viongozi, ila wengi, wawe na elimu kidogo sana itakayowasaidia wasife njaa 'mediocrity education', lakini sio elimu ya kuwafanya kuishi kama wapambanaji kwenye maisha, tunaweza kuiita, bora elimu, ambayo, ndipo tulipo.

Je, mtu aliyekuzwa na mfumo huu wa elimu tunategemea awe mwanasiasa wa namna gani?

Ifike mahali, viwango vya elimu ya viongozi wetu kunzia ngazi ya Wilaya hadi taifa isiwe chini ya digree moja, na kwa ngazi ya chini isiwe chini ya Kidato cha Sita; na kiwango cha chini cha mwananchi wa kawaida kiwe Kidato cha Nne, na darasa la saba, iwe ni kwa wachche. Kufanya hivi sio muujiza inawezekana. Ikifikia hapa, hata mtizamo na mustakabali wetu kisiasa utakuwa tofauti. Tukifikia hapo, mwetu Zito mnayemuona 'bonge la mwanasiasa' wakati huo atakuwa mtu wa kawaida sana tu kama wanavyomuona wanaojua nini maana ya kuelewa. Na bila kupindisha maneno, ni mtu wa kawaida tu au kwa maneno mengine, 'an average politician' kwa hivyo, tusiyumbishwe na maneno.

 

2014-10-29 11:12 GMT+03:00 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Uko right kiwasila... natamani ungekuwa mwandishi wa makala fulani gazetini...unaandika dada na hukosei hata spelling

'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Upinzani wa kweli nchi za Africa bado maana wapinzani wengi ni tonge kama chama tawala tu. Mtu akikosa cheo upinzani anahamia chama tawala au kuunda chama chake. ujue nia hapa ni tonge.

Kuna kumbukumbu  huko nyuma waliungana (1995) hisi sikumbuki uchaguzi wa kwanza au wa pili ila waliungana isipokuwa tamaa ya kila mmojawao kugombea Urais ikawasambaratisha. Tatizo ni mtu mwenye tamaa kuweza kukubali kuiacha ampe nafasi mwingine.

Wanawake nao corrupt kama wanaume. Nilisaidia kesi ya mama mmoja Mkomazi ya kuchukuliwa ardhi yake ambayo mume aligawiwa na kijiji enzi za ujamaa mashamba makubwa kuchukuliwa. Lakini sera ilipobadilika waliokuwa na cutomary land zilizochukuliwa na vijiji wakaanza kuzivamia kuzichukua. Vidhibiti vyote vya mume kupewa na barua za kijiji kumtetea vilikwama na shamba likachukuliwa na huyo mwenye uwezo, kabila moja, koo zinafahamiana. Kuliundwa NGO na mzungu volunteer ya kutetea wanawake hapo vijiji vya kata na alikarabati majumba ya zamani ya Kisiwani sisal Estate wakawa na ofisi nzuri ya NGO kuliko ya Kata. Nikivaa joho la msikilizaji na rafiki kumbe mpelelezi akina mama hao wa NGO waliotakiwa kumsaidia wakimshauri akubali kupokea hela toka huyo mtu ili afute kesi hatoshinda ana uwezo atamkomesha. Ilipofika mahakamani Afisa/karani mahakamani mtetezi wa masuala ya Jamii wa Idara ya Ustawi Jamii (mwanamke) alikuja kumfuata mama tulipokaa kuchukua kitu kidogo/hela ili amsaidie kusaka na file lake. Picha niliyoipata si nzuri. wanawake nao pamoja na matatizo wayapatayo-sio clean ni corrupt wana tamaa hata wale waliopo ktk siasa-rushwa nao inawatawala. Mtoto umleavyo...Wanawake wanatetea fisadi, jambazi, mbakaji. Wanaume corruption na tamaa ya kudumu madarakani pamoja na uzee ndio donda sugu.

Kama hatuwajibiki hata ndani ya familia, kudhulumu mali ya yatima; kumpora mfiwa (ke) mali za urithi na unashuhudia hata kwa msomi aliyepewa dhamana ya kusimamia mirathi-anadhulumu. Nani atatetea uchumi wa nchi? Tujitakase pande zote!!

Wanaungana kijijini wazee wa mila wanatoa ardhi kisiri na watu wa kijijini hapo wanawaogopa wao ni wengi, wazee wa mila ni wawili watatu tu unategemea nini? na hao wanaoingiza wahamiaji haram, wageni wenye bunduki na mabomu kuja kuuza wanaokutwa na garage yenye magari na pikipiki zilizoibiwa ndani ya kuta zao mume, mke na watoto wakibadilisha magari ya ufahari wakati wanajua wamiliki waliuawa yamo uwani kwao wanabadili rangi na namba; tunapopigia kura mafisadi na kuwatangaza wema kuficha uovu wao na kampeni zimeanza; tunapokuwa na matajiri ambao hawaungani kuunda makampuni international yakamiliki mali na kuendesha miradi ya kiuchumi ndani na nje ya nchi kama Dangote bali kugharimia Iftah, Miss Tanzania, Mpira, mlo wa kristmas kila mkoa-vijana bodaboda nguvu kazi zijazane mtaani-unategemea nani ataushika uchumi kama sio wageni wajao. Waungane wachukue mashamba ya mamlaka mbali mbali yanayoota magugu kwa sasa, wakajenge nyumba na godown na processing industries huko, walete wakufunzi wafunze vijana na watoe ajira kwa vijana, omba omba mtaani wakae huko wazuke mapambo yauzwe ndani na nje ya nchi. hata ulaya tunanunua nguo za kutoka nchi mbali mbali-vitenge, tie and dye; unga wa muhogo, mihogo na viazi vibichi, dagaa na samaki hongwe, papa, mbaazi etc vinatoka nje ya nchi hizo nasi Tanzania tunaweza. lakini tupo katika Soda na Juice za rangi maembe, machungwa, mananazi yanaoza vijijini. Nani ataushika uchumi kama sio wageni na makampuni ya kitapeli kununua mazao kwa bei ya kuwaibia wananchi. na makampuni hayo na madalali wao ni ya waafrika, watanzania; ni waume na ndugu zetu. Tunajila wenyewe.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
-----------------------
Fratern Kilasara
,

P. O. Box - (Home): 62810; or (Office): 65300
Dar es Salaam - Tanzania.
Telephone (Office): +255 (0)22 2700021/4 Ext No. 239; Fax: +255 (0)22 2775591
Mobile (Personal): +255 (0)715 40 41 53 or +255 (0)754 40 41 53
Emails: kilasara.fratern@gmail.com or kilasara.fratern@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment