Friday, 18 April 2014

Re: [wanabidii] N/WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFUTA MALIPO,AZUIA BENKI KUWALIPA WALIOKIMBIA BUNGENI "UKAWA"

Watu jamii ya Mwigulu ndio wataipasua nchi hii maana inaonyesha hawajui maana ya utumishi wa umma. Yeye mwenyewe katika mchango wake amesama 'over his dead body ' (mpaka afe) hawezi kuafiki wazo tofauti na serikali mbili, na alishawatamkia bungeni akichangia kua kama wengine hawataki serikali mbili waondoke bungeni. Unaendaje kutunga katiba ya wengi huku ukiwa na msimamo wako usiotikisika?? Mwigulu anazani wao kama CCM wanaweza kutunga katiba peke yao?
On Friday, April 18, 2014 9:02 AM, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
TUKO KWENYE SHEREHE ZA KUKUMBUKA KIFO CHA MKOMBOZI WETU YESU KRISTO. " BABA MSAMEHE MWIGULU NCHEMBA MAANA HAJUI ATENDALO"  ISSUE NI KUPATIKANA KWA KATIBA YENYE KUKUBALIWA NA WANANCHI.


2014-04-18 0:29 GMT+03:00 Mwana CCM <mwanaccm2015@gmail.com>:
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba

Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf na
NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.

Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya hazina kinasema,Mwigulu Nchemba ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.20/04/2014.Pia ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.

Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu  kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile. 

Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe wakiojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato. Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.

Bunge la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment