Sunday, 18 November 2012

Re: [wanabidii] TATIZO LA WANAUME SURUALI LINAZIDI KUONGEZEKA

Asante sana Abdalah Hamis kwa kutuelimisha, mara nyingi watu tunafikiri kwamba elimu ya maana ni ile ya kujua vitu kama kanuni za uchumi, hesabu, accounts nk. Kumbe tunaziacha elimu za maana na zinazogusa maisha yetu ya kila siku kama hiyo hapo uliyotupa. Kwa mara nyingine nasema asante na uendelee na bidii ya kutupanua kimawazo na kivitendo

2012/11/17 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>

Jinzi Ya Kulimaliza Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume

Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume. Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani.

Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni KUKOSA MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOSA KABISA NGUVU, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume, ingawa na wanawake wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo hili.

Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha kuwa, sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo bila hata kutumia vidonge wala dawa za miti shamba.

Ingawa Matabibu wanataja magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi, umri mkubwa kuwa ndiyo chanzo cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume, lakini imebainika kuwa idadi kubwa ya wanaume wanaofika hospitalini kutafuta nguvu za kiume hawana magonjwa hayo

Huu ni ushahidi kuwa wanaokabiliwa na janga hili wamebeba tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kimawazo zaidi kuliko hali halisi. Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini kuwa, wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na kwamba wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.
Katika hali ya kawaida kila mwanadamu ameumbwa kwa njinsi yake na inapotokea kushabihiana basi ni bahati, lakini mara nyingi usawa hupatikana kwa mmoja kujifunza au kusaidiwa kufikia kiwango cha mtu anayemuhitaji kuwa nae katika maisha hasa ya kimapenzi. Jambo hili wataalamu wanasema kuwa miili iko tayari kutii mafunzo na kubadilisha tabia zake kulingana na utashi wa mhusika.

Tatizo kubwa lililopo kwa wapenzi wengi wanaolalamikia upungufu wa nguvu ni kwamba maisha yao wanayachezea kwenye viwanja vya wenzao wanaokutana nao katika vijiwe na sehemu za kazi. Usikivu wa mazungumzo toka kwa wanaume wengine wenye uwezo wa kwenda mara nne hadi saba katika tendo au wanatumia dakika arobaini kufika kileleni umewafanya wanaume wengi kujihisi tu kuwa wao wanakasoro eti kwa kuwa huishia mara mbili au moja katika kufanya tendo.

Dhana ya kujiona ni mwenye kasoro inapojengeka akilini mwa mwanaume, huchipua hofu na hatimaye kumfanya ashindwe kabisa kusisimka anapofikiria au kukutana na mwanamke. Matokeo ya hangaiko la akili hushusha uwezo wa mwili na kumuongoza mtu kwenye kuwaza ugonjwa kisha kukimbilia hospitali au kwa waganga kutafuta tiba ya ugongwa ambao kimsingi hanao.

Lakini ukweli uko wazi kwamba kukimbilia kutafuta uwezo wa kufanya mapenzi mara sita au saba hakumfanyi mwanaume awe mlinganifu mwenye kusifiwa na wanawake wengi, kwani si wanawake wote wana uwezo wa kufanya mapezi kwa raundi hizo na si wote wanapenda kutumia takika 30 kucheza mpira wa kikubwa, wengine hukinai mapema na huona kero kuwa na wanaume ving'ang'anizi wenye sifa za kuganda wanapopewa.

Kwa kufahamu haya utagundua kuwa kukimbilia kutafuta tiba ya kumudu kwenda mara saba ni jitihada mfu kabisa zisizohitajika katika maisha ya mwanaume hasa ukizingatia kwamba wenye uwezo wa kufanya mapenzi mara nyingi hawakuzaliwa hivyo, bali walijizoeza kupitia mazingira ya malezi na makuzi yao. Maana hawezi kuwa mzoefu wa raundi mvulana aliyelelewa katika mafundisho ya kukatazwa ngono na kulindwa hadi akakakua.

Kadhalika hawi hodari wa kimapenzi msichana aliyefundishwa kujitunza, yote yatakayofuata kwa mvulana au msichana humea baada ya kupandwa na tabia chipukizi za ukubwani. Kwa msingi huo mwanaume anajukumu la kuutengeneza mwili wake uwe katika staili aitakayo. Ndiyo maana kuna wengine hawamudu kulala bila kufanya ngono, hii ikiwa na maana kuwa wamejizoeza tu, si kwamba wameumbwa na nguvu hizo.

Labda ili kufikia kilele cha somo hili ni vema tukalejea matatizo matatu niliyosema hapo juu ili tujue ni jinsi gani tunaweza kuepukana nayo bila hata kumeza vidonge na tukawa wanaume wa mbegu kama wengi wenu mjuavyo. Kwa kuanza tuzungumzie Kukosa msisimko. Hapa tunatakiwa kuajitambua sisi wenyewe kwanza, tukijua historia na mazingira yetu ya kimapenzi.
Kwa wanaume ambao wamebanwa sana kikazi na hufanya mapenzi mara moja moja, hukabiliwa na tatizo la kukosa msisimko kwa sababu miili yao imezoea. Sasa ili kuifanya ichangamke lazima waanze kuirejesha kwa kufanya mapenzi mara kwa mara na kwa raundi chache. Kisha wanatakiwa kufanya mazoezi na kula vyakula, vinywaji vyenye nguvu ili kujipa nguvu.
Pia kama mwanaume ameishi na mwanawake kwa muda mrefu na amekuwa na desturi ya kufanya mepenzi mara kwa mara katika mazingira yale yale anaweza kukumbwa na kasoro hiyo. Hivyo anashauriwa kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi, kupeana mahaba mapya, kuamsha mapenzi kwa kujaliana, pia kuondoa fikra zote zenye kukinaisha ikiwa sambamba na kuzingatia usafi wa mwili. Yakifanyika hayo mwili utaitikia taarifa ya akili na nguvu zitapatikana.
Kwa wanaoshindwa kurudia tendo wanatakiwa kufuata kanuni hizo hapo juu. Jambo kubwa ni suala la kuuzoeza mwili. Usiulazimishe kuanza mara moja kwenda mara nyingi wakati mapenzi yako yamekuwa ya kuiba mpaka baba alale na wakati mwingine muda wako wa kutoka kazini umebana na hivyo kukufanya ufanye mapenzi ya chap chap kila siku. Ukiwa mtu wa namna hii haiwezi ikatoke siku moja ghafla tu ukafanya mpenzi mara tatu bila kuchoka.
Pia inawezekana mwanaume akashindwa kurudia tendo si kwa sababu hana nguvu bali hapewi ushirikiano wa kutosha toka kwa mpenzi wake. Hivyo wakati wa kutafuta uwezo wa kwenda raundi nyingi ni vema usaidizi wa mwanamke ukatolewa, isitokee kupokea lawama tu za "huwezi, sijatosheka" kwani hizo ndizo zinazowafanya wanaume washindwe kabisa kwa hofu kuwa wanaaibika. Mawazo ya kuaibika yanapopewa kipaumbele huufanya uume kuzidi kusinyaa, kwa maana hiyo ni vema kuyatupilia mbali na kuacha kujihukumu.
Pia kuna hitilafu ya wakati wa kuridhishana, inaweza kutokea mwanamke akawa kamaliza raundi yake ya kwanza, wakati anaingia msisimko wa pili mwanaume anafika kileleni, kinachotokea ni mwanamke kumlazimisha mwanaume arudie tendo kwa muda mfupi tangu amalize, jambo ambalo ni vigumu. Sasa ikitokea mwanaume kachezewa na hana msisimko anapata hofu kuwa haweze, ikijengeka hivyo hata iweje jambo halitawezekana tena. Hivyo ni bora kupeana muda wa kupumzika kabla ya hatua ya pili ya mchezo.
Pale inapotokea hamasa ya kurudia haipo fikra za mwanaume zisipewe nafasi ya kushindwa kwani nyakati, mchoko, makujukumu, hofu za maisha na mambo kama hayo yanapokuja katika siku ya kustarehe ni wazi kuwa kiwango cha ufanyaji mapenzi kitakuwa chini na hali hii huwatokea wanaume wote, hata walio hodari wa kwenda raundi kumi kwa siku.
Sambamba na hilo wanawake wanashauriwa kutoonesha kujali pindi inapotokea hali hiyo, badala yake wawaambie wenzao kuwa siku hiyo inatosha hata kama hawajatosheka, lengo ni kuondoa hofu ambayo ndiyo msingi wa wanaume kuishiwa uwezo wa kufanya mapenzi. Hata hivyo maudhi, kufanya mapenzi na usiyempenda, msongo wa mawazo na kutokuaminiana huchangia kupoteza msisimko wa kuwa 'kidume'.

Ushauri wangu ni kwamba chochote ambacho unataka mwili wako ukifanye lazima uuzoeze. Ukizoea kuamka saa 12 asubuhi mwili utatii kanuni hiyo. Na ukizoea kufanya mapenzi kila siku mara mbili au tatu hali itakuwa hivyo. Mwisho katika sura hii ni vema wanaume na wanawake wakajifahamu kuwa uwezo wa kufanya mapezni unapungua kufuatana na umri isitokee mtu akakosa raha kisa hawezi kwenda mara nyingi kama zamani wakati anajua kabisa umri wake umekuwa mkubwa.

Jamani kutafuta nguvu za ujana zirudie uzeeni ni kujipa taabu ya bure. Firbath Bayi hawezi kutimua mbio kama alivyokuwa zamani! Ukiona umeingia kwenye utu uzima na mwili wako unaishiwa uwezo, kubaliana na hali. Lakini jambo la kushangaza siku hizi hata vikongwe wanapanga foleni kwa waganga kutafuta tiba ya kufanya mapenzi mara tatu kwa siku! Mapenzi yanataka uwezo wa akili na mwili tusishindane na uwezo asili tutapoteza muda na pesa bure.
Tatizo la mwisho ambalo nalo linatajwa kuwasumbua zaidi wanaume ni maumbile madogo ya uume. Wanaume wengi wamekuwa wakilalamika kuwa maumbile yao yanawazuia kuwapa dozi wapenzi wao. Lakini kama nilivyosema huko nyuma kwamba mapenzi hayana kanuni kwamba lazima mtu awe hivi ili amtosheleze mwenzake. Kinacholeta raha katika mapenzi ni hisia, hii ikiwa na maana kwamba mwanaume au mwanamke anaweza kufurahia mapenzi kwa kutomasana na kuhamasishana kwa viungo vingine vya mwili na kujikuta wameridhika hata bila ya kuingiliana.

Kwa maana hiyo wale ambao wanamaumbile madogo wanaweza kutafuta wanawake ambao nao wanamaumbile ya aina yao. Baadhi ya watalaam wanasema kwamba kwa kawaida umbile la nyeti za mtu linakwenda sambamba na urefu wa mwili wake. Kwa maana hiyo wanawake wafupi, ingawa si wote wanatajwa kuwa na nyeti zenye ukomo mfupi zaidi ya warefu na wembamba wa umbo.
Mbali na chaguo la mtu mwenye kuendena naye umbo, wanaume wenye kasoro hii wanatakiwa kujifunza sana michezo ya kimapenzi ambayo itawasaidia kuwafikisha kileleni wapenzi wao. Ni muhimu kwao kutumia sanaa na mitindo inayopunguza umbali na ukomo wa nyeti za kike.

Mwisho ni misingi ya tiba hii:

MOJA ni kuepuka hofu. Ikitokea siku moja umeshindwa katika tendo haina maana una kasoro, bali ni hali ya kawaida, hivyo usiingize huzuni na hofu utakuza tatizo. Hivyo kwa wale wenye tatizo hili wapunguze wasiwasi na wajiamini kuwa hawana tatizo.

PILI, nguvu za kiume zinahitaji mwili wenye nguvu, hivyo ni busara kula lishe bora na kufanya mazoezi yasiyokuwa makali sana.

TATU, kumfundisha mwanamke namna ya kukusisimua

NNE, kuepuka mawazo ya kuhuzunisha wakati wa tendo.

TANO, kupata muda wa kupumzisha mwili.

SITA, kuepukana na pupa, tumia muda usiopungua takika 20 kufanya romance.

SABA, kujiamini.

http://www.freeuscitizenship.info/2012/03/jinzi-ya-kulimaliza-tatizo-la-upungufu.html


2012/11/17 <gm26may@gmail.com>


Hayo mafuta ya Ubuyu wanayanywa au!?

Sample imefanyika kwa watu wangapi?

Please share the case study


Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: eva mushi <mushieva2000@yahoo.co.uk>
Date: Fri, 16 Nov 2012 13:03:30 +0000 (GMT)
Subject: Re: [wanabidii] TATIZO LA WANAUME SURUALI LINAZIDI KUONGEZEKA

Kwa muda mrefu nimepata kusikia pamoja na virutubisho vingi vya kuongeza nguvu za kiume mara nyingi nguvu za kike hazitajwi.Kuna wajasiriamali mkoani Mwanza wamegundua kuwa Mafuta ya Ubuyu ni dawa tosha kwa kuongeza nguvu za kike na za kiume.Mpo?????
 

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, 16 November 2012, 15:29
Subject: Re: [wanabidii] TATIZO LA WANAUME SURUALI LINAZIDI KUONGEZEKA
Ndugu wanabidiiHivi karibuni nilisoma kwenye gazeti moja kwamba siku hizi wapo akina mama wengi wenye tatizo la kupata watoto kwenye ndoa zao. Inawezekana kwa kiasi kikubwa tatizo si wao bali tatizo ni waume kama nimeielewa makala ya Rehema vizuri. Ingekuwa kula vyakula vinavyowafanya wanaume kuwa wanaume suruali vinaleta tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa baada ya kuwa na watoto, mimi ningemuunga mkono mia kwa mia ndugu Mbuba. Tatizo la wanaume suruali yawezekana lipo ata kwa vijana ambao hawajaoa wala kupata watoto. Kama tatizo hilo lipo ata kwa vijana na likaendelea kuwa kubwa ina maana mbele ya safari dunia itakuwa haina watu. Mbaya zaidi mbali na kusababisha umwanaume suruali ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini husababisha magonjwa mengi na hivyo uufanya mwili wa mtu kuwa dhaifu. Mtu wa namna hii hawezi kuzalisha vya kutosha na hivyo taifa litakuwa maskini. Nimejifunza maana nyingine kuhusu neno mwanaume suruali mimi nilijua ni mwanaume asiyekuwa mkakamavu au asiyekuwa na chochote kitu, kumbe ni mwanaume asiyeiweza shughuli? Kwa mtindo huo lazima wanaume suruali wapo wengi na ni watu wa makamo ya kati na wazee Ipo haja ya kueneza elimu hii ili jamii iendelee kuwa na sura ya jamii yenye ustawi. Elimu hii itaweza kutolewa vizuri baada ya kujua ukubwa wa tatizo kulinga na umri pamoja na jinsia kupitia njia za utafiti wa kisayansi
2012/11/16 Joseph Ludovick <josephludovick@gmail.com>
utafiti wangu na uzoefu umenionyesha kuwa wanawake ndo hawana nguvu za kike,au mimi ndo nina matatizo?

2012/11/16 <gm26may@gmail.com>

YahNa wale wachache wenye nguvu za kutosha watakuwa wana kazi kubwa kufidia maana wanawake wengi watakuwa wanahitaji huduma zaoHapo hujazingatia kuwa idadi ya wanawake ni kubwa mara 3 ya wanaume ( sijui na sensa ya mwaka huu itadhibitisha hilo)
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
Date: Fri, 16 Nov 2012 10:36:34 +0300
Subject: Re: [wanabidii] TATIZO LA WANAUME SURUALI LINAZIDI KUONGEZEKA

Duh MbubaHapa umemaliza kila kitu, ila ujue kwamba kama mmoja wa wanandoa akiwa na hilo tatizo maana yake atafungua mlango kwa mwenzake kutoka ndani ya ndoa japo kwa kuiba
2012/11/16 weston mbuba <matutetz@yahoo.com>
Rey,
Nadhani hii ni habari njema. Kama nguvu zinapungua ina maana uzinzi unapungua, UKIMWI utapungua, watoto wasotarajiwa watapungua, mfumuko wa wingi wa watu utapungua hivyo kuimarisha uchumi, watu kwenda nje ya ndoa kutapungua kama si kuisha kabisa, na hivyo kupunguza mifarakano katika ndoa, nk, nk, nk.
Hamna haja ya kuhangaikia utafutaji wa suluhu kwa jambo hili. --- On Thu, 11/15/12, Rehema Kikwete <rehemaki@gmail.com> wrote:

From: Rehema Kikwete <rehemaki@gmail.com>
Subject: [wanabidii] TATIZO LA WANAUME SURUALI LINAZIDI KUONGEZEKA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, November 15, 2012, 11:17 PM
KWA mujibu wa ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi yawanaume ambao wanakuwa wanaume suruali inazidi kuongezeka kwa kasihuku kukiwa hakuna dalili za kupungua kwa tatizo hilo.Sababu kubwa kwasasa ni kukua kwa matumizi ya vyakula vya viwandani. Vyakula hivi kwa bahati mbaya huwa vina kemikali nyingi.Hakuna shaka kwamba hata wewe umekuwa shahidi, kwa mfano maji mengiyanayouzwa siku hizi yamesafishwa kwa kemikali, juisi nyingihazijatengenezwa kwa matunda halisi, bali zimetokana na harufu ya matunda na kemikali.Ulaji usiofaa unaonekana kuwa ni mojawapo ya sababu kubwa za wanaumekwa wanawake kusumbuliwa na tatizo la nguvu au uwezo katika kushirikijambo hili.Ingawa tatizo la upungufu wa uwezo huo linaonekana zaidi kwa wanaume, hata wanawake nao wanasumbuliwa nalo, kwa maana ya kukosa hamu yakushiriki tendo la ndoa.Hata hivyo tiba ambayo wanaume wanaweza kutumia, ni ile ile ambayowanawake wanapaswa kuitumia, kwa maana ya kula aina fulani ya vyakulaili nao waweze kuwa sawasawa kama walivyo watu wengine.Wengine wanakula tu ili mradi tumbo limejaa, bila kuangalia hiki nakula kwa ajili ya kwenda kufanya nini katika mwili.Mafunzo mengi yametolewa kuhusu vyakula kuanzia shule za msingi hadisekondari na vyuo, kwamba mayai yanasaidia nini, vyakula vyenyekuongeza nguvu, wanga nk ni vipi. Lakini bado si wengi wanaojali walichofundishwa.Pombe inasaidia nini katika mwili? Sigara inasaidia nini katika mwili?Kahawa, soda na vyakula unavyotumia vina msaada gani mwilini? Ni mamboambayo unapaswa kuyajua.Ndugu yangu acha tabia ya kula tu vitu ili mradi unashiba. Unaharibu mwili wako, kwani baadhi ya vyakula vinachangia ugonjwa wakisukari au magonjwa mengine mwilini kama moyo au nguvu za kiumekupungua hasa vile vya jamii ya mafuta.Hata matumizi ya mafuta ya kula ni lazima kuwa nayo makini, kunabaadhi ya mafuta yanachangia mirija ya kupitisha damu katika mwilikuganda, matokeo yake damu haipiti vizuri, kitendo ambacho kinachangia mwili wa mwanadamu kuwa dhaifu.Wengi ni wazuri wa kusoma na kushukuru kwa mada nzuri, lakini hilosilo ninalotaka; ninachotaka ni kuona mtu anachukua hatua ili kuletamabadiliko.Viko vyakula maalumu vilivyotengenezwa tayari kwa ajili ya kuondoa tatizo la nguvu za kiume, lakini unaweza kujaribu kutumia baadhi yavyakula kama tangawizi vina msaada katika mwili.Kitaalam, tangawizi ni moja ya vyakula vinavyoweza kurejesha nguvu zakiume; Jinsi ya kufanya ni kwamba unaweza kuichemsha tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai asubuhi, mchana na jioni.NJIA NYINGINE YA KUFANYA:Unaweza pia kuchukua kitunguu saumu kisha changanya na asali pamoja nammea fulani unaitwa habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huo maratatu kwa siku.Ugali wa mtama asilia, mchuzi wa matembele, pweza, mrenda na maziwanavyo vina msaada katika mwili wa mwanadamu.Mambo yanayochangia kuwa na nguvu imara ni mawili nayo ni kula chakula bora pamoja, kupata mahitaji muhimu ya mwili na kisaikolojiaunahitajika uwe na amani.Ukiwa na hofu japo kidogo tu, au msongo wa mawazo hata mwanamke wakoafanyeje kukuliwaza ni ngumu kusisimka ipasavyo. Katika kushiriki jambo hili la ndoa, unapaswa kuwa katika mazingira namuda ambao unajisikia huru.Zaidi ya yote pendelea kunywa maziwa yaliyo changanywa na asalimbichi, kunywa maji mengi, punguza kula vitu vyenye sukari, na kula matunda, mboga za majani kwa wingi.Pendelea kufanya mazoezi ya viungo, jizoeshe kutembea kwa miguu aukutumia baiskeli angalau nusu saa kwa siku.Kama unakunywa pombe acha kabisa, punguza mawazo pale unapokuwa namatatizo, elewa kuwa matatizo ni sehemu ya maisha.http://rosemarymizizi.blogspot.com/-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Bariki G. Mwasaga,P.O. Box 3021,Dar es Salaam, Tanzania+255 754 812 387
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment