Pamoja na mapungufu yote yatakayokuwa yanatokana na katiba bado mtu
mwenyewe ana uwezo wa kujisimamia na kufanya mambo watu wakakubali.
Naungana na ndugu Matanda aliyeuliza swali kwamba je mbona Sokoine
alitumia katiba hiyo hiyo na akafanya vitu watu tukamkubali?
Mtu ukipewa nafasi ya uwaziri mkuu kisiasa umependelewa sana maana ni
nafasi ya kutenda watu wakashuhudia uwezo wako kiutendaji. Ukiachia
mbali Sokoine ata Mh. Lyatonga Mrema aliweza kunguruma na akasikika
kwamba yupo, wakati wa enzi zake mimi nilikuwa vijijini lakini
alianzisha utaratibu wa kutembelea maeneo mbalimbali majambazi
wakatetemeka, wanaume waliokuwa wanawapiga wake zao bila sababu nao
wakaanza kutetemeka kwa kumuogopa Mrema. Jambo ambalo halijajitokeza
kwa huyu mheshimiwa.
Uongozi ni kipaji wapo viongozi wengi hapa kwetu tunawaita viongozi tu
kwa sababu wamepewa kukalia kiti hicho lakini hawana sifa na wala
hawana uwezo kiuongozi. Kwa nchi kama Tanzania kionozi lazima awe na
uwezo wa kukemea na watu wamsikie kwa kuonyesha mabadiliko
yanayotakiwa.
Ninaamini wapo watanzania wengi tu ambao wana uwezo mkubwa wa kuongoza
ila hawajapewa nafasi ili tuweza kuwapima na kuwatambua kwamba ni
viongozi bora badala yake tunabaki kuwaangalia hawa ambao wana nafasi
ya kujitangaza. Je ni wangapi tunafikiri rais ajaye ni mtu anayeweza
kutoka ata nje ya kundi la CCM? najua wapo watakaosema haiwezekani
lakini pia tupo tunaosema in awezekana.
Kiongozi yeyote aliyekwishapewa madaraka makubwa kama waziri mkuu au
mawaziri wengine wanayo nafasi kubwa kujitangaza na kuonyesha uwezo
wao na wakakubalika kwa wapiga kura kuliko mtu mwingine aliye nje ya
kundi hilo. Kama mtu amepewa nafasi kama hiyo na akashindwa kuonyesha
uwezo hakuna sababu ya kusingizia katiba tatizo ni uwezo mdogo
kiungozi
On Sun, Nov 18, 2012 at 7:17 AM, Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com> wrote:
> I guess even the one who started this thread has the answer to his question.
> MPK is very weak when it comes to decision making.
>
> I think his leadership helm is confined to his family level, beyond that
> mnamuonea.
>
> Lutinwa
>
> Sent from Samsung Tab 10.1
>
> On Nov 18, 2012 2:35 AM, "Chambi Chachage" <chambi78@yahoo.com> wrote:
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment