Tuesday, 20 November 2012

Re: [wanabidii] RE: CCM WAMEANZA KUIGA SERA ZA CHADEMA.

Mngonge, tatizo sio kulipa ada tu pia jinsi ya kulipa hiyo ada ni tatizo, mtoto anaenda NMB bank saa kumi na mbili asubuhi anakaa kwenye foleni hadi saa kumi jioni, utakuta katika kaunta tano za nmb ni mbili tu zenye wahudumu (tellers) nao muda wote wanaongea na simu! ukienda kwa meneja nae anaongea na simu tu ukimuuliza kwanini huduma hakuna unajibiwa kuwa mtangao uko down. Ukijiuliza kwa nini ada zilipiwe nmb tu wakati tunajua huduma zao hazikidhi mahitaji unashangaa.
 
Lakini tukijiuliza mangula ambaye ana wiki moja tu kazini na amekuwa nje ya system kwa miaka saba hiyo work plan kaiandaa lini? je amepata consaltation ya kutosha juu ya kile anachotaka kukifanya? Tangu BMW atoke ofisini secretariet imebadilika mara tatu yaani ile ya Makamba Mukama na sasa Kinana nidhahiri mambo mengi yamebadilika sana.
 
Wakati kilo ya nyama inafika shs 6500 bado wafugaji wanaambiwa wapunguze mifugo! sote tunajua ili uone maisha ya mtanzania yako nafuu basi angalau aweze kupata kijimnofu cha nyama ya ng'ombe. Mchele sasa ni shs 2800 kilo, sote tunajua watoto wetu hasa wa mjini asipopata mchele basi nyumbani hapaeleweki sasa hii team imeshajipanga kuwaeleza wananchi juu ya hili? BMW alituacha kilo ya mchele ni shs 240 na nyama 650 sasa kumetokea nini hadi hii hali inatukumba! naamini ngombe wetu hawatumii diesel ni nyasi tu nazo wanakula bure machungani!
 
Gill David, usiamini sana kuwa CDM wanayo tiba ya ufisadi, ni hao cdm wametumia mil 22 kumlipa diamond na masanja wakati wamasai waliomtoa jasho BW Bush kule arusha wakiambulia mil 1! Walimwandalia JK mlo pale hotelini wakati wakijua alikuwa na posho yake ya safari. Kama show moja ya Diamond inaingiza mil 80 na alikuwepo kwanini hiyo dhima isingekuwa na kiingilio na kila mtu akanunua bia yake na kujilipia msosi hizo mil 87 si zingerudi na faida juu!


 
2012/11/20 mngonge <mngonge@gmail.com>
Siku zote mtu mwongo hakumbuki alichokwishasema, hawa jamaa ni wababaishaji na ndo maana kila wanachofikiri kitawasaidia kuwadanya wapiga kura wanakirukia. Bila shaka katika zunguka yao wamegundua wananchi hawana uwezo wa kusomesha watoto wao ili kupata kura zao ni bora kuwadanganya kwa staili hiyo.

Swali ni je kwani tatizo walilonalo wadanganyika ni uwezo wa kutolipia elimu tu?  Nafikiri tunayo matatizo mengi hasa yanayotokana na umaskini, kwa sababu ya umaskini tunakosa huduma bora za afya, chakula, usafiri ata hiyo elimu.

Kusoma bure sawa je ubora wa elimu uko vipi? Naomba niseme kwamba tatizo letu kubwa ni umaskini, watuwekee mikakati ya kuboresha uchumi ili tuweze kujinasua na matatizo hayo


2012/11/20 GILL DAVID <gilldavidk@yahoo.co.uk>

Katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Novemba 10, 2010 katika Kata ya Mchangimbore katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, nawakumbusha Watanzania wote na tegeni macho na masikio yenu, Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa alisema nanukuu "Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure" na kwamba lazima wananchi wachangie. Narudia tena "Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure" na kwamba lazima wananchi wachangie. Kaeni sawa maana narudia tena "Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure" na kwamba lazima wananchi wachangie.

Naendelea kunukuu usemi wa Mwenyekiti wa CCM Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete "Nimebahatika kukaa serikalini muda mrefu hiyo sera ya bure tulijaribu na ikatushinda na wakati huo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, tulikaa naye tukaona hilo haliwezekani tukaamua tubadilishe sasa nawashangaa wenzetu wanawadanganya eti watatoa Elimu bure." Mbona nyie wote mlisomeshwa bure mnachopinga ni kitu gani jamani nyie vihiyo wa CCM.

Kwa upande wake Dk Slaa akiwa mjini Arusha katika moja ya mikutano yake alisema kwamba CCM walikuwa wakipinga sera ya elimu bure hadi sekondari kutokana na kulea Wezi, Wabadhirifu na kuthamini anasa kuliko maendeleo kwa wananchi. Leo hii wameona maji yamezidi unga, Watanzania wamejua na kushuhudia wanaibiwa Kodi zao, Madini yao, Wanyama wao, Misitu yao, Samaki wao, Ardhi yao, Ndugu Nape Mnauye anataka kudanganya umma wa Watanzania tena wasomi kuliko yeye kuwa eti "ELIMU BURE" ni sera ya chama chake cha CCM. Hivi huwaga nyie CCM mnapotoa matamshi yenu huwa hamrudii kuzisoma hotuba zenu mliziwahi kutoa kwa Watanzania.

 

CCM mkitaka msimame kwenye majukwaa hapa Tanzania na watu wawaamini sasa hivi kama wanavyoweaamini CHADEMA inabidi mrudishe kwanza mali za umma mlizikwiba, fedha za umma mlizoficha ulaya, mfute mikataba ya hovyo kabisa ya madini mliyowekeana na wawekezaji, muwatoe Wazungu wote mliowamilikisha ardhi ya Watanzania, Muwafukuze wawekezaji wote mliowapa vitalu vya kuua na kuuza wanyam wetu, na mrudishe elimu ya Watanzania iwe sawa kwa wote. Kwa kifupi mkubali kuwa masikini kama walivyo Watanzania.

 

Kusema kweli nyie CCM sasa hivi kushindana na CHADEMA ni ndoto za Alinacha au Abunuasi. Watanzania hawana imani na nyie tena. Kama kwenye uchaguzi wenu tu wa chama mnatumia mabilioni kuhonga nani anawaamini tena kuwakabidhi nchi. Kama mnawavunjia watu nyumba zao na kuwaacha wanalala nje nani tena ana imani na nyie. Kama mnawauzia hata wagonjwa wa ukimwi dawa bandia nani ana imani na nyie tena. Kama fedha za misaada ndizo mnaingiza kwenye uchaguzi na kuzitumia kwa rushwa nani tena anawaamini. Anayeiamini CCM sasa hivi ana kasoro za akili. Aende akapime Mirembe.

 

Mwisho na kila Mtanzania anielewe. CCM wakitaka Watanzania wawaamini warudishe mali zote za umma wanazomiliki na wahakikishe wanajitoa kwenye biashara wanazofanya na wawekezaji. Viongozi wa CCM ndio wauza mafuta, Viongozi wa CCM ndio wenye Mabenki, Viongozi wa CCM ndio wenye mahoteli makubwa makubwa, Viongozi wa CCM ndio wenye mashamba makubwa makubwa, Viongozi wa CCM ndio wenye mashamba ya mifugo, Viongozi wa CCM ndio wenye makampuni ya kuagiza magari, Viongozi wa CCM ndio wenye viwanda vikubwa vikubwa. Viongozi wa CCM ndio waliowadanganya Watanzania kuwa Serekali haiwezi kufanya biashara ili wafanye wao. Wakadiriki kuviua viwanda vyote nchini kikiwepo cha Matairi kule Arusha. Mimi nilishangaa. Magari yalivyo mengi Tanzania unadiriki kukiua kiwanda uagize tairi Kenya.

 

Eee Uwiiiiiii, narudia tena Watanzania Eeeeee Uwiiiiiiii Rushwa, Rushwa, Rushwa haitatoka Tanzania bila kukitoa chama tawala cha CCM madarakani. Misaada inakuja toka nje haiwafikii Watanzania kisa eti wanakiimarisha chama kishinde uchaguzi mwaka 2015. CCM wako madarakani kuhakikisha wanashinda kwenye chaguzi mbalimbali lakini sio kuhudumia Watanzania. Mimi nawaambia CCM sasa hivi Tanzania hakuna mjinga. Tena mahali mliharibu kuwekana nyie na wake zenu, na watoto wenu madarakani. CHADEMA tunawapa kura za "NDIO" mwaka 2015 nchi nzima na zungukeni kuwaamsha Watanzania wanaosubiri kupata maisha bora wakiwa ndani ya CCM. Msibishane majukwaani wala bungeni na hawa wajinga tangazeni sera zenu muwakomboe Watanzania kama alivyofanya Kamanda Robert Mugabe wa Zimbabwe. Ukitegemea kupata maisha bora ukiwa chini ya utawala wa CCM utasubiri sana. Tunawasubiri majukwaani tuwazomeeee!!

Mkereketwa

Galliard David

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment