Ndugu Markus Honorius ametusaidia, kwa ustadi wa nasaha zake, kuhusu yanaosemwa
juu ya sakata hii ya UDINI na hoja tunazopeana.
Pamoja na vitabu viwili anavyovitaja, vya magwiji wawili, Sheikh M. Said na Dr H. Ghassany,
nimeona bora nipendekeze kitabu cha tatu, kinachostahiki kusomwa na wale wanaotafuta
hoja ziada, kuhusu suala hili.
Kitabu hicho ni kile cha Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi, Rais wa zamani wa Zanzibar na aliekuwa
Makamo Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, alievushwa nyadhifa zake zote
za Serikali, Dola na CCM, kwa izara, mjini Dodoma, 1985, kwa shinikizo za J. K. Nyerere, katika
kampeni ya "uchafuzi wa hali ya hewa".
Kitabu hicho kinaitwa: "30 Years Of Storm", yaani juu ya siasa za "Muungano" na
UDINI, 1964-94.
Kila la kheri,
Bwanatosha
Date: Tue, 10 Jul 2012 06:06:12 -0700
From: lundunyasa@yahoo.com

| Kaka Matinyi, afadhali umeuliza maswlai ya msingi kabisa. Mimi ni msomaji mzuri wa vitabu vya MOHAMED SAID. Lakini huyu ni mwanazuoni ambaye MAWAZO YAKE YAMEKATA ROHO, haoni na hajui sababu za kutoona. Ninasoma maandikao yako na ninacho kitabu chake cha MAISHA YA ABDULWAHED SYKES: Pengine ni mambo ya kihistoria yanapaswa kuzingatia na tafiti zinapotujia ni wazi zinaleta mjadala. lakini UKAKASI ni kwamba anapotumia waumini wa dini ya KIISLAMU kufanikisha malengo yake. Anawatumia WAISLAMU kwa njia mbaya kabisa na kuwavisha GIZA badala ya mwanga. ni kama ambavyo mwanazuoni DK. HARRITH GHASSANY yupo huko New York, kwenye kitabu chake cha KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU kuna baadhi ya mambo ni uongo mtupu, mbali ya baadhi yake kuelezewa vema. Lakini wasiojua ukweli watavaa GIZA watadiriki kuvaa GIZA na kukata roho kwa mawazo yao. Ni hatari, MOHAMED SAID anadhani anafikiria kwa mkondo wake, anadhani wasomaji wake ni WAISLAMU tu. Mimi namsaidia, aache kuwapotosha watu kwa kuitumia dini ya KIISLAMU. Ni udhaifu wa kufikiri na katu hawezi kuwa BWANA WA BUSARA. sijui kitu gani kinamfanya ALINGANISHE samahani sio KUFANANANISHA, narudia ni KULINGANISHA kati ya waislamu na wakristo. huyu amelemaa kabisa. Nb; hapa ofisi kwetu waliopo juu yangu kimadaraka hawapatani hata kidogo. Ni waislamu haswaaaa. Lakini mie mtu wa tatu kutoka nafasi yao huwa natengeneza na kuwaonyesha njia ya kuishi katika tofauti zao. nilichogundua kuwa mmoja anatumia akili kama za MOHAMED SAID, uislamu, uislamu, uislamu. Lakini mwingine ni mwanajamii hajali sana dini ya mtu. Mie mkristu napata shida kuwafanya wawe sawa, lakini wanafanya kazi kama CHUI, kama kigezo cha Uislamu ni kupendana kwa mtazamo wa MOHAMED SAID --- On Sun, 7/8/12, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
|
0 comments:
Post a Comment