Tuesday, 10 July 2012

Re: [wanabidii] Watanzania waache Kuuza Ardhi Hovyo

Budi wananchi wafundishwe wasiuze ardhi. wapo wauzao kwa gharama kubwa, wanapata fedha, hawafanyi cha maana, wanalewa, wanaoa zaidi, wanavaa maguo, mwisho wanajenga mabondeni na mabarabarani. wengine wanauza bila kujali watoto au maisha ya wazazi wao wazee.
 
Wapo waliouza maeneo ya Makongo, Changanyikeni, Salasala n.k kuanzia 1970 hadi sasa ambao sasa wanajenga kando ya barabara wamemaliza kuuza hata pale walipokuwa wanaishi (nyumba yao).
 
Wengine walihama wakasema wanarudi kwao, baada ya muda wakaonekana wamerudi wanaponda mawe kunduchi. Wengine wameuza maekari mfano Salasala wamehamia ktk mashimo ya kunduchi wanaishi ndani ya maji mvua ikinyesha. Wameuza kariakoo millioni 800 na sasa ni bilioni moja. wamegawana warith mtu milioni 100 au 50. amefanya sherehe za ubatizo, arusi dansi za aina, hakwenda mkuranga akanunue ardhi alime, anunue badaji na hiyo 100,000,000/= au million 50, amehamia Sunna (magomeni-jangwani) au Hananasif bondeni, Baghdad (Below Ilala Mchikichini nea Yanga area)au kigogo bondeni. Mvua ya mafuriko imemzoa hela amemaliza na sasa yupo huko walikopimiwa katika hema. Njia ya Bagamoyo-Msata kumeuzwa kiasi kwamba nanasi sasa litafika 5,000/= Ni Bar za vileo unaziona zimesimama kando walikonunua kila baada ya plot 3 bar. Mashamba ya mananasi yataondoka, mikoroso na minazi. Mabonde ya mpunga ya Ruvu na irrigation system iliyopo yatageuka mashamba ya majumba. Hakieleweki kwa nini mabwana ardhi wanapima viwanja vya nyumba katika mabonde ya maji ya kulipa mpunga Ruvu basin na kwingineko. Maeneo hayo yangeendelea kilimwa mpunga sio kulima na kupanda 'nyumba'. Ni wazi malaria na hydrocele na matende yataongezeka. Utaziona nyumba zimezungukwa na maji. Hebu waende Ulaya wakaone wenzao wanafanyanye kule kwenye cities zenye mashamba pia. Mpango uwepo hiyo ardhi ilimwe sio nyumba majini. Mabonde la Kilimo yaheshimiwe yasijae mifugo wala nyumba.Ipigwe marufuku kuweka garage, godowns au nyumba za makazi unless zitajengwa kupitisha maji chini zio kuzuia na kufanya yafyurike yatokako, kwingine, kuweka maradhi au kubomoa majumba. Architects na land planners wapo kulikoni kinachoendelea. Administrators wapo, Diwani na MPs-kuwaje watu wanahamia kujenga next to Oxidation ponds ambapo wanabeba maradhi zaidi. Mtu anafyeka mikoko anajaza mchanga anaachiwa mpaka jengo linakamilika lije kubomolewa baadae. Ni hapo aanzapo kujenga na afisa aliyetoa vibali na land inspector aliyethimitisha washughulikiwe-potelea mbali kisasi cha kumgecha mtu anayetimiza wajibu wake. Inachosha hii bongo vitu kufanyika holela. Utaona maeneo ya NHC, Sites and Services Sinza, Tegeta, tangi bovu yalipimwa, barabara, mabomba ya maji. maeneo ya umma-hayapo, kote kumezibwa viosk, vibanda bila ya kujali hatari ya moto. Moto ukitokea kutokana na shughuli za matumizi mikaa, mapishi, oveload ya umeme na matatizo mengine-hakuna njia ya kupita magari ya zima moto kuifikia nyumba. Tunaona watu wanavyopoteza mali, tunaendelea kujenga na kuziba feeder roads. Hatujifunzi, hatuambiliki, hatushauriki.

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, 10 July 2012, 10:52
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania waache Kuuza Ardhi Hovyo

Sikuelewi kaka!
Wewe unadhani kuna mtu angependa kuuza ardhi yake kama ana option nyingine? Mimi kuna mashamba nimenunua njia ya bagamoyo na kila baada ya miezi miwili wauzaji wananipigia niende nikanunue kakipande kengine ambako nako wameamua kukauza na hiyo inafanyika kwa ajili ya umaskini uliokithiri na sio ujinga!!!!!

2012/7/10 Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
Ndugu zangu

Imetokea tabia na utamaduni wa watanzania kushiriki kuuza ardhi za watanzania wenzao hovyo na kiholela bila kufuata taratibu maalumu hata pale wanapofuata taratibu basi wanatumia hongo ili kuhakikisha maslahi yao yanatekelezwa yale ya kuuza ardhi hovyo kwa kiwango kikubwa .

Nimetembelea maeneo ya bagamoyo na msata siku chache zilizopita nimeona halikubadilika sana kwa maeneo mengi kuuzwa kwa watu wasioeleweka baada ya barabara hiyo kuanza kukamilika kwa kiwango kikubwa , sio bagamoyo tu , sehemu nyingi zinazojengwa barabara na miundombinu mengine ardhi inauzwa kwa kiwango kikubwa bila ofisi za vijiji kuwa na taarifa za uuzwaji wa ardhi hizo .

Huko tunapoenda watoto wetu wanaweza kukosa viwanjya vya kuchezea , kukosa viwanja vya kujenga shule na zahanati au hata sehemu za kufanya huduma nyingine za kijamii kama tutaendelea kuuzwaji huu wa ardhi kiholela .
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


0 comments:

Post a Comment