Tuesday, 10 July 2012

Re: [wanabidii] RE: UDHALILISHWAJI WA WAISLAM NA VYOMBO VYA DOLA VYA TANZANIA/2-3-4

Bwana Bakari,
Mifano uliyorejea ni mizuri lakini huoni kwamba tukikubali hizi chokochoko za udini tutaruddi kule kwa Iran na Iraq?
   Tusikubali kuuza nchi yetu kwa vishawishi ya maisha bora hawa mataifa makubwa ni kama shetani wanapandikiza chuki tutengane WAUZE SILAHA.
"TUJENGE NCHI YETU"

God created men in LOVE ,let us live with LOVE


--- On Mon, 7/9/12, method francis ngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: method francis ngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] RE: UDHALILISHWAJI WA WAISLAM NA VYOMBO VYA DOLA VYA TANZANIA/2-3-4
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, July 9, 2012, 9:16 AM

Ndugu Bakari Mohamed umenena.
Ni kweli kabisa ukitaka kuielewa vizuri hoja iliyo mbele yetu ni vyema ukachambua historia both at international level and national level. Ila binafsi ningeomba tuanzie historia ya babu zetu kabla ya ujio wa waarabu na wamissionari (ambao ndio walioleta hizo dini tunazobishania) pengine watu
waliovig'ang'anizi na kutaka kutulazimisha kufuata imani zao  wataelewa vizuri zaidi. Historia iache ibaki kama historia lakini pia ndugu Bakari kwa sasa sidhani kama tunahitaji kuelewa sana juu ya yafuatayo:
1.Uislam na Waislam walipewa nafasi gani kijamii, kisiasa na kiuchumi;
2.Uislam na Waislam walichukuliwaje na serikali; Uislam na Waislam walishiriki vipi kwenye harakati za maisha ya kila siku;
3.Uislam na Waislam waliingilianaje na taasisi za kidini na kisiasa!


Nafikiri inajulikana kwamba jamii ya waislamu huko nyuma haikujihusisha sana na elimu iliyokuwa ikitolewa na wamissionari kama ilivyokuwa kwa watu wengine ambao awali hawakujiunga na uislamu, wajerumani waliwatumia waarabu wakati wa utawala wao. Ni wazi kwamba kama jamii ya waislamu haikuwa na wasomi wengi kupewa nafasi nyingi kwa wakati huo. Lakini swali ni je hayo mambo yako hivyo hadi leo? Kama siyo ya nini kujadili hoja hizo kwa sasa?

Haya mambo ni vyema tuyaangalie kihistoria lakini pia tuyaangalia kwa ualisia wake kwa sasa bila kuvaa miwani ya rangi fulani itakayotuzuia kuzingatia ushauri uliotoa kwa maneno POUR VIVER ENSEMBLE ACCEPTONS NOS DIFFERENCE!  MARIDHIANO, UVUMILIVU WA KIDINI, UPENDO WA KWELI NA NIA NJEMA. Nimependa zaidi umaliziaji wako. Watu tuache kulalama tu kila kukicha, hivi serikali ni nani? Ni sisi tunaoiweka serikali na hivyo lolote tunaloona ni kinyume na matarajio basi tutafute ufumbuzi mapema iwezekanavyo. Maana siku hizi ata baadhi ya watu wameanza kutumia dini zao ili kupata public support, mimi nasema viongozi wa kidini wanaokubali kuhusishwa kwenye mipango hiyo hawatufai kabisa. Sis tunayo nafasi kubwa kuweza kurekebisha kasoro zozote zilizoanzishwa na wageni na baadaye kushikiriwa na baadhi yetu kwa kuegemea zaidi kwenye imani zao. While observing your rights observe others rights too. Kwa pamoja tutaweza
2012/7/9 Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
Hamis,

Pengine na wengine wote, udhalimu hauna dini, kuna mambo mengi yanayoweza sababisha mtu ukatendewa udhalimu pasipo hatia.

Kijana wetu mwanfunzi wa Chuo Kikuu Kisanji aliuawa na polisi siku ya wapendanao, wakadai nijambazi wakati walimkuta na girlfriend wake pamoja na rafiki zake. Ni kijana wa Kikristu lakini alidhulumiwa uhai wake pasipo hatia.

Tupige vita udhalimu wa polisi pamoja kama Watanzania tutashinda, kwani hawa wanakuwa na motives zao za kimaslahi na wala sio zakidini, tukijipofusha kwa dini tutasambaratika, watatumaliza.

Felix

2012/7/9 Bakari Maligwa Mohamed <maligwa1968@yahoo.com>
...Wanabidii!
 
Kama falsafa; Uislam ni kama nyumba (au mwili). Umejengwa kwa mtofali matano: (1) Imani ya Hapana Mungu Isipokuwa Mungu Mmoja na Mtume Muhammad [Rehena na Amani Juu Yake] ni Mjumbe Wake; (2) Swala [Salat] Tano za Kila Siku; (3) Kufunga [Swaum] Mwezi wa Ramadhan Siku 29 au 30; (4) Zakat [Matoleo ya Mali]; na (5) Kuzuru (Hija) Nyumba Takatifu [Makka]....kwa ujumla, "matofali" haya matano yanaunganishwa pamoja kwa (kama mfano na au mithili yake) saruji, mchanga, kokoto, mawe, na mchanganyiko wa maji kama ulivyoridhia Uislam kwa mafundisho ya falsafa ya Uislam kama mfumo kamili wa maisha ya watu wanaotakiwa kuwa "WAISLAM".
 
Sasa; suala hapa ni Uislam na Waislam! Uislam ni mfumo; na Waislam ni watu wanaotakiwa waishi kwa mujibu wa mfumo huo! Si mara zote watu wanaojinasibu na Uislam wanaishi kwa mujibu wa utashi wa Uislam, kama ilivyo kwa dini nyingine. Kama watu (wawe Waislam, Wapagani, au....) huwa na uchaguzi katika mambo ya dini. Na kuna dini (kama njia) inayochukuliwa "adui" na dini nyingine na hata kuwafanya watu hao wa dini nyingine kama "maadui"...na hapa ndipo panapokuja "dhana" ya kuwa: WATU FULANI NI ADUI (kwa utmbulisho wao)...na hivyo ndivyo wanapotangaza watu hao (wa dini fulani) kuwa ni "MAADUI" kwa mujibu wa utashi wa wale wanaotangaza. Inapotokezea hali kama hiyo ndivyo unavyoweza kudhani kuwa ni "mtu hatari" kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na wale wanaokutafuta kwa dhana ileile ya "hadhari" juu yako!
 
Uislam tangu mwaka 1948; baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kuundwa kwa taifa la Israeli ulitangazwa kuwa adui na vyanzo vya kimamlaka mbalimbali hadi sasa. Kutoka kuanzishwa kwa harakati za Wapalestina zilizochochewa na Vita vya Mashariki ya Kati baina ya 1948 na 1975 kati ya Waarabu na Waislraeli kumekuwapo na "agenda" mahsusi ya kuwatangaza baadhi ya Waislam wanaosemekana kuwa na "SIASA-KALI" na kuwapa majina ya "UGAIDI" ili kwa nembo (chapa) hiyo waweze kuwekwa kwenye "kilengeo" cha kushughulikiwa. Mwaka 1990, enzi za Bush (Baba) na wakati wa Vita vya Ghuba (I)...ilitangazwa kuwa, "Baada ya Ukomunisti ni Uislam." Hili lilikuwa tangazo la vita vya moja kwa moja dhidi ya Uislam kama mfumo na kwa jinsi hiyo, Waislam walikuwa wametangaziwa vita popote walipo na kwa vyovyote viwavyo...lazima washughulikiwe popote walipo. Ukiachilia mbali tangazo la vita kwa Waislam na Uislam lilitolewa Tanzania (rejea: Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1955 hadi 1985 cha Dakta John Sivalon M. M).
 
Ukiachilia mbali mambo madogomadogo yanayoweza kuandikwa kwa kalamu ya mkaa (penseli), yapo mambo makubwa yanayoweza kuandikwa kwa wino wa damu (ya wahanga) waliyodhalilishwa na mfumo unaoitwa wa mapambano dhidi ya UGAIDI kama nembo ya Waswahili (hususan Kiswahili cha kwetu Morogoro) kwamba, "KUMKOMA NYANI GILADI." Wapo watu wenye itikadi na falsafa ya Uislam wanakomolewa kwa sababu tu ya Uislam wao (narudia kwa msisitizo, wapo watu; si watu wote). Kwa jinsi hiyo, kama utasoma na kurejea vema historia ya Ujenzi wa Uislam Duniani ukilinganishwa na dini nyingine zenye dla zinazoilinda na kuitetea Istraeli (kuanzia 1948 hadi sasa) utagundua kwamba vita dhidi ya Uislam na Waislam ni vita endelevu inayopiganwa kwenye nyanja zote za maisha ya kiuchumi, kijamii na kisiasa...na wanaofanya kazi hiyo ni taasisi za kimaatifa zenye mafungamano na aidha Marekani, Uingereza au Israeli yenyewe kwa kuutumia Umoja wa Mataifa (UM) kama "mhuri" wa kuhalilisha vita hivyo.
 
Huu si wakati wa kurejea maandiko mepesi na yasiyokuwa na taathira ya "kisomi." Lazima ubukuzi mnene na wa kisomi ufanywe juu ya kwa nini Uislam na Waislam waonekane "tishio" na wawekwe kwenye "kilengeo" na hata kufanyiwa vitendo vya kibaguzi? Ipo haja ya wazi na itakayozingatia uhuru, haki, uadilifu na insafu katika kutafuta UKWELI na UHAKIKA juu ya madai ya Waislam dhidi ya udhalilishwaji unaodhaniwa kufanywa na watu wasiyetafuta HAKI SAWA mbele ya jamii ya watu mchanganyiko wa kimataifa, kitaifa na kijamii (kwa sehemu ya jamii tunamoishi kama watu wa sehemu moja). Kwa ujumla, hata kama UGAIDI (kama mfano) hauchagui dini, rangi wala kabila (la gaidi): watu wote duniani wana sura ya ugaidi wa aina na jinsi yao! Huu ni ukweli muafaka kwa kuwa kama vitendo vya kuuwa watu wasiyekuwa na hatia havifanywi na wale wanaojiita Waislam (wenye itikadi kali au siasa-kali kama wanavyojiita na/au kuitwa) bali hufanywa na watu wenye malengo yao [rejea mauaji yaliyokuwa yakifanywa na Wakatoliki wa Ireland ya Kaskazini dhidi ya Waprotestanti na kinyume chake; Mauwaji yaliyokuwa yakifanywa na magaidi wa ETA; mauwaji yliyokuwa na yanayofanywa na magaidi wa FARC; mauwaji yaliyokuwa yakifanywa na yanayofanywa na Mafia Gang; Mauwaji yaliyokuwa na yanayofanywa na Magenge ya Wauza Dawa ya Kulevya - Latino Amerika; na mauwaji yaliyofanywa na Anders Breivik wa Norway)...hii ni mifano tu!
 
Uislam, kama nilivyoandika hapo mwanzo; ni mfumo! Na ndani ya mfumo mna watu wanaoonekana kuwa ni sehemu ya mfumo huo. Hivyo, si vema kudhani kwamba kila Muislam ni "gaidi" na kila penye UGAIDI kuna Uislam! Hii ni dhana mbaya na potofu kwa vile ndio inayojenga "chuki" na kupalilia "sintofahamu" na "songombingo" za siasa ya dunia kuelekea kwenye mtafaruku wa kidini. Tazama; wakati huu dunia ikikodolea macho vurugu za uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan kwa takriban mwongo mmoja sasa na hata kumuua Usama (Osama) bin Laden, bado dunia haijaambiwa kwamba ni nani alimtengeneza Usama (Osama) na kwa nini alitengenezwa! Hii ni ajabu ya dunia. Hata pale ilipodhaniwa kwamba Iraq ni kitisho cha dunia kwa kuwa ilisadikiwa inamiliki silaha za maangamizi (WMD)...na dunia kutangaziwa hivyo na Tony Blair akitiwa munda na George Bush (Mtoto) dunia yote iliaminishwa hivyo na Iraqi ikavamiwa, kupigwa kijeshi na kuuawa kwa watu wengi pamoja na kukamatwa kwa Saddam Hussayn (Al-Tikrit)...yote haya yalikuwa ni matokeo ya vita vya chuki dhidi ya "uongo" unaoenezwa na Marekani na Uingereza dhidi ya Uislam na Waislam (kwa vile wanaouawa nchini Iraqi na Afghanista ni Waislam wengi kuliko dini nyingine).
 
Sasa, wote ni mashahidi; munda na "ngoma ya vita" inapigwa dhidi ya Iran! Nchi ya Iran inafahamika kwamba ni nchi iliyoingia kwenye mgogoro na Marekani na Uingereza tangu mwaka 1979 baada ya Mapinduzi ya Kiislam. Uislam wa Iran ndio "kilengeo" cha mataifa (wastakabari) wa dunia kwa sasa...wanapiga nara ya vita kwa kisingizio (pretext) cha kwamba Jamhuri ya Kiislam ya Iran ina mipango ya utengenezaji wa zana za kivita za "TONORADI" au maarufu kama "nyukilia"...ngoma zilezile zilizopigwa "Enzi za Saddam Hussayn" ndizo zinazopigwa sasa kwa Iran. Angalia, japokuwa si vema kufukua "maiti" za watu waliyokufa...hivi; Saddam Hussayn si ndiye yuleyule aliyetumiwa na Marekani wakati wa Vita vya Iran-Iraq vya miaka minane? Si walewale Marekani na Uingereza waliyekuwa wakimpatia Saddam silaha za kemikali (chemical weapons) alizotumia kuwaua Wairan zaidi ya milioni moja?! Huu ni nini? Au kwa kuwa waliyeuawa ni Wairani?
 
Sasa turejee kwenye mukhtadha wa maisha ya Uislam na Waislam wa Tanzania na jinsi wanavyochukuliwa! Kwa kuwa si wengi wanaopenda kusoma sana; nawaomba tuwe tunasoma sana (hii ni pamoja na andiko hili, kwa kuwa najua ni refu na linaweza likawafanya baadhi ya WANABIDII kuacha kulisoma kwa sababu ya uvivu tu wa kusoma)...vitabu vya historia vimeandika mengi na si tu kwa sababu vimeandikwa na Waislam (pekee) bali pia vipo vilivyoandikwa na Wakristo na hata wasiyokuwa kati ya hao. Tazama kitabu cha Dakta Sivalon (1992), tazama kitabu cha Andrew Coulson (1976), tazama vitabu vya wanahistoria wanaotegemewa waliyeandika historia ya Tanganyika (au Tanzania) juu ya ulinganifu wa dini na jamii ya watu wa Tanganyika na au Tanzania kisha angalia taathira ya Uislam na Waislam katika vipindi tofauti vya utawala wa kihistoria; yaani (1a) Utawala wa Wajerumani (1b) Utawala wa Waingereza (2a) Utawala wa Nyerere [1961 hadi 1985] (2b) Utawala wa Mzee Rukhsa - ali Mwinyi [1985 hadi 1995] (3a) Utawala wa Ben Mkapa [1995 hadi 2005] na (3b) Utawala wa Jakaya Khalfan Mrisho [2005 hadi sasa]...katika kuviangalia vipindi hivi tumia nukta hizi: Uislam na Waislam walipewa nafasi gani kijamii, kisiasa na kiuchumi; Uislam na Waislam walichukuliwaje na serikali; Uislam na Waislam walishiriki vipi kwenye harakati za maisha ya kila siku; na Uislam na Waislam waliingilianaje na taasisi za kidini na kisiasa!
 
Mwisho, Tanzania ni nchi ya watu; na watu hao ndio wanaoweza kujenga mustakabali murua wa maendeleo ya watu na vitu kwa utashi wa kanuni kuu ya kimaumbile: UPENDO, UVUMILIVU (WA KIDINI) na MSHIKAMANO WA DHANA NZURI BAINA YA WATU WENYE MITAZAMO NA FALSAFA MBALIMBALI JUU YA SIASA, UCHUMI NA JAMII. Kamwe hatuwezi kuendelea na mtazamo "hasi" dhidi ya watu na au mifumo yao ya maisha. Na tukifanya hivyo, kuna dalili ya kusambaratika kwa UHURU, UMOJA na AMANI yetu vitu ambavyo ni tunu isiyoweza kubadilishwa na kitu chochote na kwa gharama yoyote iwayo. Napenda kuwaasa ndugu zangu (wanabidii na wengine watakaopata fursa ya kuusoma waraka huu) kwamba: Wafaransa wana msemo wa zamani (japokuwa na sehemu ya Wafaransa mamboleo wameanza ubaguzi wa kishenzi) kwamba, "MNAPOTAKA KUISHI PAMOJA MZIKUBALI TOFAUTI ZENU" yaani, POUR VIVER ENSEMBLE ACCEPTONS NOS DIFFERENCE!
 
Mwenyezi Mungu Mtukufu Atubariki sote kwa pamoja...
Pamoja tunaweza kujenga jamii ya watu walio sawa na huru kwa kuzingatia MARIDHIANO, UVUMILIVU WA KIDINI, UPENDO WA KWELI NA NIA NJEMA...tusijenge mashobo kwa kisingizio cha nguvu za kimamlaka katika kuwatweza nguvu watu wengine kwa vile udhalimu hulipwa na yule aliyeumba kike na kiume na akajaalia baina ya jinsi hizo marejeo yake kwenye udongo!
 
Nawasilisha. 
 
Bakari M Mohamed, BBA [PLM], CPSP [T], MSc (PSCM), Reg. PSP (AU 0005)
  1. Lecturer in Procurement and Supply Chain Management
  2. Procurement and Supply Chain Auditor
  3. Procurement and Supply Chain Specialist, Consultant, Researcher and Trainer in Procurement Contracts Management
  4. Doctor of Alternative Medicines [DAM] & Natural Healing Therapist
Department of Procurement and Logistics Management
Mzumbe University Box 6 Tel (Office): + 255 23 2604381/3/4
Mobile      : + 255 713 593347
MZUMBE, Tanzania.

From: godfred mbanyi <mbanyibg@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, July 9, 2012 11:55 AM
Subject: Re: [wanabidii] RE: UDHALILISHWAJI WA WAISLAM NA VYOMBO VYA DOLA VYA TANZANIA/2-3-4
Bw. Hamis,pole sana kwa mkasa uliokupata!
Kwa kweli inasikitisha unapokuwa raia mwema halafu unashikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma mbaya kama hiyo!
Lakini,mimi siamini kama dini yako ndiyo iliyosababisha yote hayo, la hasha, nadhani kulikuwa na wrong identity!!
Mara nyingi makosa kama hayo hutokea, si unakumbuka sakata la kijana wa Mzee Mengi hapo uwanja wa ndege?
 
Halafu ndugu Hamis, mimi mwenyewe mwaka 2002 nikiwa safarini kwenda chuo kikuu cha Mzumbe , niliponea chupu chupu kuuawa na watu wakinifananisha na jambazi sugu aliyekuwa na kundi la majambazi wanaotumia silaha za moto huko Kigoma!
 
Kipigo nilichopata kwa sekunde kama kumi tu, kilitosha kunitoa damu na kuvimba uso mzima! Niliokolewa na waalimu wa shule moja ya msingi waliokuwa wananifahamu!
Baadae waliomba msamaha kwangu na kwa wazazi, nikaendelea na safari yangu kwenda masomoni!
Mpaka leo naamini wale watu wakiongozwa na viongozi wao wa kijiji, walinifananisha-wrong identitty! Sidhani na wala siamini kuwa ukristo wangu ulichangia kutaka kuuawa kinyama siku ile!
 
Pamoja na yote hayo, nakuomba uwasamehe bure waliokusababishia usumbufu huo!
Na nakusihi, uondoe notion kuwa yaliyotokea ni kwa kuwaa ni mwislamu!! Kwani Muislamu hana haki kuishi Tanzania? Mimi nadhani hii itaakuwa si sahihi na itapotosha sana, kwani hata kwenye jamhuri za kidini, bado watu wa imani nyingine wanaishi, tena kwa amani na kuthaminiwa!!
 
Mwl Mbanyi
 
--- On Mon, 7/9/12, Salim Himidi <bwanatosha@hotmail.com> wrote:

From: Salim Himidi <bwanatosha@hotmail.com>
Subject: [wanabidii] RE: UDHALILISHWAJI WA WAISLAM NA VYOMBO VYA DOLA VYA TANZANIA/2-3-4
To: "Wanabidii Jukwa la Uhariri" <wanabidii@googlegroups.com>, matinyi@hotmail.com, rugambwa@hotmail.com
Cc: ezekielmassanja@gmail.com, gm26may@gmail.com, "Mkereketwa WANABIDII" <denis.matanda@gmail.com>, "Salim H. HIMIDI" <bwanatosha@hotmail.com>, "Abdalah Hamis Mzalendo/Znz" <hamisznz@gmail.com>, "Mohamed Said Tanga" <mohamedsaid54@gmail.com>
Date: Monday, July 9, 2012, 12:07 AM

Ndugu Rugambwa,
As Mao Dze Doung would have said:
"Let A Hundred Flowers Bloom,
Let A Hundred Schools Of Thoughts Contend"
Truth is neither black nor white, it's always in between.
Waswahili wamesema: YASEMWAO YAPO, AU YANAKUJA!
Na hapa ninakunukuu:
"Huwezi pata suluhu, ila tuendelee kujadiliana"
Ahsante sana,
Bwanatosha
> From: rugambwa@hotmail.com> Date: Mon, 9 Jul 2012 04:30:42 +0000> > Ndugu Matinyi,> Nakubaliana na wewe tuna shida sisi kama nchi, nimesema deep down tu wabaguzi, wadini nk. Hatusemi tu.> > Pia nadhani hii mijadala ya dini ina taabu kidogo, kwa sababu, kuna upande mmoja unatumia reasoning ya kawaida na mwingine unatumia imani.> > Huwezi pata suluhu, ila tuendelee kujadiliana.> > Sisi kuishi pamoja kama wakristu, waislamu, wanaoaminu dini za kijadi ambazo ndo za kweli (maana hizi za kiislamu na kikristu tumeletewa na wageni)> .> Tunavyoishi sasa ni jambo la kujivunia sana, tusilete mizozo na migogoro ya kidini maana huwa haiishi ikisha anza.> > Kwenye reasoning; we have a science ya logic labda ndo wanaitumia watu wanao wa- profile waislamu kwenye mambo ya ugaidi. Which I strongly believe is very unfair, totally unfair.> > Here is the known two premises:> (a) uislamu sio ugaidi> (b) kila gaidi ni muislamu tena mwenye misimamo mikali na watoa mihadhara.> > Kwahiyo, yalompata huyo bwana alokamatwa Airport sidhani kama ni mistaken identity, ni kweli wali mtuhumu kwa kuangalia mihadhara yake, safari zake nk. Hiyo inaruhisiwa kwenye upelelezi. Na amekubali hawa jamdhuru na kum treat vibaya.> > Huko marekani watu weusi huwa ndo suspect wa kwanza kwenye uhalifu maana asilimia kubwa huwa ndio wanahusika na uhalifu na ndo wamejaa magereza.> > Unaweza hoji mfumo, huo ni mjadala mwingine.> > Mimi nilisha wahi kubadili passport iliyokuwa na visa za Israel ili nikaruhusiwe kuingia Iran. Kwa kazio niliyokuwa naenda kufanya walisema nisingeruhusiwa sio kufanya kazi hata kukanyaga mle : kisa nina visa tu ya Israel.> > Na likewise, nilipoenda Israel nilikuwa na visa za Pakistani na Algeria, usumbufu nilioupata tena sio wakati wa kuingia humo bali kutoka hapo Tel Aviv ulikuwa balaa.> > Majaabu!> Kwahiyo nafahamu jinsi haya mambo yalivyo stereo typed and so badly handled.> > Jumatatu njema.> LR> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.> > -----Original Message-----> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>> Date: Sun, 8 Jul 2012 18:02:12 > > 1. Dkt. Salmin alipokuwa rais wa Zanzibar alimfukuza sheikh mmoja kule visiwani na kumwambia aende Bara. Salmin ni mkristo?> 2. Mzee Mohamed alipokutwa kuwa hana madawa ya kulevya aliombwa radhi na kuachiwa. Kumbe hapo alishabadili dini na kuwa mkristo hapo hapo uwanjani?> 3. Nyerere alimweka ndani James Mapalala, na wengineo wengi wenye majina ya kibiblia. Kumbe hawa walikuwa waislamu?> 4. Kiongozi mmoja wa Simba alitiwa matatazi kuhusu mihadarati na majina yake yalikuwa ya kikristo. Kumbe naye alikuwa mwislamu?> 5. Juzi juzi Kikwete aliwatangazia watu kwamba wamewakamata maaskofu wakiwa na madawa na maaskofu wenzao wakamwamba awataje. Kumbe nao waislamu?> 6. Akina Bryson, Bomani, Kahama, Munanka na wale wazee wa Kilimanjaro na Meru waliofanya juhudi za uhuru kumbe wote walikuwa waislamu? > 7. Wakurya waliouawa na Wajerumani mpaka damu yao ikatengeneza kijito kwenye eneo la Busweta, enzi hizo za miaka ya 1800 mwishoni, kumbe nao walikuwa waislamu?> 8. Waliopigania uhuru kwenye mataifa yote jirani zetu ya Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Msumbiji, Zambia, Malawi, n.k. walikuwa waislamu?> 9. Kumbe juhudi zote za Tanzania kupigania uhuru wa mataifa mengine ya Afrika ziliongozwa na waislamu?> 10. Kumbe juhudi zote za Nyerere kuwapigania Wapalestina haki yao na kuwaacha Wayahudi na Marekani yao zilibuniwa na waislamu?> 11. Kumbe uhusiano mzuri wa Tanzania na mataifa ya Waarabu duniani ni kwa sababu Nyerere alikuwa mwislamu?> 12. Baba yake Kikwete alichagua kuwa DC wa wakoloni badala ya kupigania uhuru wa nchi yetu. Kumbe hakuwa mwislamu?>  > > > > ----------------> From: ezekielmassanja@gmail.com> Date: Sun, 8 Jul 2012 11:48:19 +0000> Ukivaa miwani ya rangi ya njano dunia yote itakuwa ya rangi ya njano. Ukiivua utaiona dunia katika rangi zake sawa sawa.> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom> ----------------> > From: gm26may@gmail.com > Date: Sun, 8 Jul 2012 11:12:40 +0000> > Hata Dr Steven Ulimboka angekuwa Mwislam wangeweza kurelate. Case yake na Udini> > Mungu Tusaidie tuondakane na tongotongo hizi za Udin> Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network> ----------------> > From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> > Date: Sun, 8 Jul 2012 13:43:40 +0300> Tumesoma humo kwenye maelezo lakini siamini kwenye conclusion kuwa hiyo issue ilimtokea yeye kwa kuwa ni muislamu. Kama walitaka kumbambikia nini sasa walishindwa? Kwangu mimi hiyo ni genuine case ya mistaken identity.> Wale wafanyabiashara wa madini mungu awalaze pema peponi; hivi kutakuwa na hoja akitokea mtu akasema eti janga lile liliwakumba kwa kuwa walikuwa wakristu?> Tuacheni kuingiza udini kwenye kila kitu!> > On 8 Jul 2012 13:27, "Salim Himidi" <bwanatosha@hotmail.com> > wrote:> > > Ahsenteni, kwa maelezo ya mtu aliyeona madhila, kwa nafsi yake, na kuamua kutueleza.> Uzuri wa huriya ya maoni na fikira ni kusaidiana tujenge muelewano bora na kutambua> ya KWELI na ya UZUSHI.> Kuzuia mazungumzo sio dawa ya kutoa UTATA.> KIZA huondoshwa na MWENGE!> Bwanatosha> > > > > Date: Sun, 8 Jul 2012 02:33:07 -0700> > From: hamisznz@gmail.com <mailto:hamisznz@gmail.com> > > > > > Utangulizi> > > > Sheikh wa kwanza kudhalilishwa na serikali ya Tanzania alikuwa Mufti> > wa Tanzania kwa wakati ule Sheikh Hassan bin Amir ambae kwa amri> > iliyotolewa na Julius Nyerere alikamatwa nyumbani kwake usiku wa> > manane akiwa kavaa khanga tu na akachukuliwa hivyo hivyo hadi uwanja> > wa ndege na kurejeshwa "kwao" Zanzibar. Kisa cha yeye kufukuzwa Bara> > ni kirefu na kwa sasa hapa si mahali pake kueleza. Nimekiweka kisa cha> > Sheikh Hassan bin Amir mwanzo kwa kuwa kina nafasi ya pekee katika> > historia ya Waislam na mapambano yao na serikali toka uhuru upatikane> > mwaka 1961. Lakini mwaka wa 1964 masheikh wengi waliwekwa kizuizini> > kwa amri ya Nyerere hiki nacho ni kisa kingine kinachohitaji wakati> > maalum kuhadithiwa. Baada ya haya ndipo kwa mara ya kwanza moto wa> > makumbi ukajitokeza juu na Waislam wakapambana na serikali katika> > mitaa ya Dar es Salaam mwaka 1993 na mabomu ya machozi na risasi> > zikapigwa. Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza kufanywa na> > Waislam baada ya uhuru. Hili lilikuwa sakata la kuvunjwa mabucha ya> > nguruwe. Damu ya Waislam ilimwagika. Masheikh kumi na moja wa Wilaya> > ya Kinondoni walikamatwa pasi na adabu usiku wa manane majumbani mwao,> > wakapigwa pingu na kutupwa katika malendrova ya polisi kama majambazi.> > Lakini haya yote si kitu tokeo lililotokea siku ya Jumatano tarehe 4> > Julai lilifurtu ada. Sheikh Nurdin Kishki akiwa na ugeni wa masheikh> > wenzake kutoka Yemen ndani yao akiwapo Mufti wa Yemen walivamiwa na> > askari waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia wakiwa njiani wakitokea> > Tanga na wakagaragazwa chini huku wakionyeshwa mitutu ya bunduki. Hii> > ilikuwa habari kubwa lakini vyombo vyote vya habari kama ilivyo ada> > kwa mambo yanayowahusu Waislam vyombo vyote muhimu vilipuuza stori> > hii.> > > > Baada ya utangulizi huu naeleza kisa kilichonifika mikononi mwa vyombo> > vya dola miaka sita iliyopita:> > > > Mkasa Wangu wa Kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere, Dar es> > Salaam Mwaka 2006> > > > Mohamed Said> > > > "Mwaka 2006 Radio Tehran walipendekeza jina langu rehekwa Wizara ya> > Mambo ya Nje Iran wanialike katika hawli ya Imam Khomeni. Sababu ya ya> > mie kualikwa ni kuwa mara kwa mara nilikuwa nikifanya mahojiano na> > Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili kuhusu siasa za Tanzania hususan> > wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 na ikatokea kuwa yale mahojiano> > yangu yakawa yanapendwa na wasikizaji wa Afrika ya Mashariki na Kati> > na sehemu za Emirati. Nilkwenda Iran na waalikwa walikuwa kutoka dunia> > nzima na wa kila aina, waandishi, wahadhiri wa vyuo vikuu, wasomi wa> > kawaida, mawaziri wa serikali kutoka nchi tofauti na watu wengine> > wengi. Msafara wetu wa wageni kwenda mahali ulikuwa ni msururu wa> > mabasi zaidi ya kumi yakisindikizwa na kimulimuli cha polisi. Kutoka> > Tanzania nilikuwapo mimi pamoja na waandishi kutoka Daily News na> > Kituo Cha TV cha Channel Ten. Nikiwa Tehran niliingia studio za Radio> > Tehran Idhaa ya Kiswahili na tukafanya mahojiano na mtangazaji wao> > mashuuri Abdulfataa Mussa na wenzake na vilevile kurekodi vipindi> > vingi kuhusu hali ya Waislam Tanzania.> > > > Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates> > iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani> > walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu> > kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli> > za kunishughulikia zilipoaanza. Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa> > namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi> > yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia> > kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni> > kurekebisha mitambo. Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa> > wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri> > na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule> > afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu> > wa usalama. Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa> > harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa> > kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia> > kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.> > > > Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa> > usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko> > chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi> > nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha> > kuwa yawezekana wamefananisha majina. Niliwaambia huenda Mohamed Said> > muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa> > kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na> > wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu> > na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa> > hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa. Wakaniamuru sasa tutoke twende> > nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika> > mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika> > lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa> > haraka huku nikosoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika> > nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu.> > Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza> > kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari> > zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya> > kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike> > na shari yangu.> > > > Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa> > sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo> > yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka mizigo> > ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama. Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa> > kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha> > kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu> > nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa> > zilizowafikia. Wakasema, "Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni> > msafirisha madawa ya kulevya." Nikawauiza, "Baada ya kupata taarifa> > hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?" Wakasema, "Ndiyo maana> > leo tumekukamata." Nikawaambia, "Si kweli kama kwa sababu mie> > nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na> > kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni "Mzungu wa> > Unga" kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya."> > Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na> > serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata> > mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali> > ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda> > sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi> > nini katika hii safari ya Iran? Niliwaeleza kuwa miezi michache> > iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano> > umefadhiliwa na serikali ya Amerika na wamenipa na tiketi toka Dar es> > Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha. "Mbona> > hamkunikamata wakati ule?" Ikawa swali na jibu swali. Nikafungua> > mlango mwingine nikawaambia, "Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata> > Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam> > sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyanyasa> > Muislam?" Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa> > naponzwa na dini yangu.> > > > Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali> > kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na> > yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu> > kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole> > nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu.> > Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya> > kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile> > katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule.> > Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo> > maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa. Nikakataa kujisaidia> > pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo> > chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote> > ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa> > chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.> > > > Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya> > katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende> > nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha> > madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na "audio cassette"> > nilzokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini> > naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini.> > Nikawauliza, "Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa> > Tanzania? Maana mimi hata nyumbani kwangu hii leo mkifika nina vitabu> > vya Khomeni na wanafalsafa wengine kama Karl Marx ambao nimesomeshwa> > pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam." Sasa hapo ikaja kejeli. "Ala wewe> > mtu wa Kariakoo lakini umefika hadi Chuo Kikuu!" Sikujibu kitu. Awali> > waliponitia mbarani waliniuliza kwetu na nikawaeleza kuwa nimezaliwa> > Kariakoo.> > > > Hawakunipa jibu kuhusu kuingiza vitabu na cassette za Khomeni. Ikawa> > sasa kama vile wameishiwa maswali. Nikaona kuwa sasa ni zamu yangu> > nami kuwapiga maswali. Yule aliekuwa akinihoji nikamwambia, "Mimi wewe> > nakufahamu vizuri sana kwa sababu ukicheza mpira Simba Sports Club na> > mie ni mpenzi wa club hiyo toka utoto wangu wakati huo ikiitwa> > Sunderland na mmoja wa baba zangu alikuwa mchezaji marufu wa club hiyo> > katika miaka ya 1950 akafiikia hadi kucheza Kombe la Gossage."> > Nilihisi amepata mfadhaiko kidogo akanambia,"Unanifananisha yule> > aliekuwa akicheza Simba ni ndugu yangu." Alikuwa anasema uongo lakini> > mie nikamkubalia. Hapo nikajua kuwa nishampata sasa hana nguvu tena ya> > kuuliza maswali. Kusema uongo ni dalili ya kujihami. Nikamrushia> > kombora lingine, "Sasa tuhuma za madawa ya kulevya zimekwisha tuko> > katika kwa nini naingiza vitabu vya Khomeni nchini?" Akanijibu> > kinyonge, "Tumeridhika huna madawa." Kufika hapa tukawa tumemaliza> > mahojiano.> > > > Wakati huo sasa ni usiku wa manane na nishapeleka SMS kwa sahib yangu> > mmoja bingwa wa mambo ya mtandao wa kompyuta kumjulisha kuwa> > nimekamatwa uwanja wa ndege kwa tuhuma za uongo za kuvusha mihadarati> > na yeye ile kuipata tu ule ujumbe wangu akaifahamisha dunia kuwa> > nimekamatwa uwanja wa ndege nikitokea mkutanoni Iran na> > nimebambikiziwa tuhuma za kuingiza nchini mihadarati. Waliponitia> > mbaroni tu walinionya kuhusu kutumia simu yangu ya mkononi lakini> > bahati nzuri hawakuninya'ganya. Aliyenipa onyo hili alikuwa mkuu wa> > kituo cha polisi cha uwanja wa ndege. Huyu rafiki yangu akawa> > kanisaidia sana maana hadi kumekucha wapenzi wangu wote ndani na nje> > ya nchi pamoja na vyombo vya habari vinavyonifahamu walikuwa na> > taarifa za kukamatwa kwangu. (Kwa kipindi takriban miaka ishirini> > nyuma kwa nyakati fofauti nimekuwa nikifanya mahojiano na radio zote> > muhimu kama, BBC, VOA, Sauti ya Ujerumani, Sauti ya Iran nk.).> > > > Nikawaomba wale watu wa Usalama waniachie basi nende zangu kulala> > nyumbani nirudi hapo kesho asubuhi kwa kuwa sikuwa nimebeba madawa ya> > kulevya. Wakaniambia, "Itabidi tukulaze hapa hadi asubuhi wakubwa wetu> > watupe amri ya kukuachia. Maana amri ya kukukakamata wewe imetoka> > juu." [IMG]file:///C:/Users/MOHAME~1/AppData/Local/Temp/> > msohtmlclip1/01/clip_image001.gif[/IMG]Sasa hapo ikawa nimelipata> > jingine. Kumbe wauza unga hawakamatwi hadi amri itoke juu. Sasa kama> > amri haikutoka ndiyo muuza unga atapita aingize sumu zake mitaani?> > Hili likazidi kunidhihirishia kuwa kukamatwa kwangu hakukuwa na> > uhusiano wowote na vita dhidi ya mihadarati bali ni vita vile vile> > vikongwe dhidi ya Uislam.> > > > Nikawa pale usiku kucha. Sasa wakati niko pale wakidhani nimelala.> > Wakawa wenyewe kwa wenyewe wanazungumza kuhusu hii 'operation' neno> > walilotumia ni kuwa 'leo tume-dial wrong number.' Wakawa wanasema,> > "Huyu bwana mbona hakuelekea kama muuza unga tena huyu mtu bwana> > kasoma kweli kweli" Wanadhani mie nimelala kumbe ni macho> > nawasikiliza. (Vipi utalala katikati ya michongoma?). We umeona jinsi> > alivyokuwa akijibu na kuchambua mambo." Hilo ndilo likawa gumzo lao> > wakinisifia kwa ufasaha na mantiki lakini wakizungumza kwa sauti ya> > chini kabisa. Hapa ikanidhihirikia kuwa hawa vijana walikuwa> > wanatimiza wajibu wao wa kazi tu lakini kiini khasa cha kukamatwa> > kwangu hawakuwa wanakifahamu.> > > > > > Walionikamata walikuwa vijana kama wanne na wote walijitambulisha kwa> > majina ya Kiislam. Nilijua ni waongo kwa kuwa Muislam anonekana katika> > uso na katika matumizi ya lugha. Lakini yule mchezaji wa Simba ni> > Muislam na yeye ndiye aliekuwa mkubwa pale akiongoza ile shughuli yote> > tena kwa kujidai na kujifaharisha sana. Kisa kile kile cha mtumwa> > anelimishwa na yule anefanya kazi za ndani nyumbani kwa bwana. Ila> > kitu kimoja lazima nikiri. Wale vijana walikaa na mimi kwa wema na> > hawakunibughudhi hata kidogo. Hata nilipokuwa nakwenda msalani kijana> > alienisindikiza alinitaka radhi akasema, "Nakusindikiza kwa sababu ni> > sheria lakini sisi tunakustahi kwa hiyo utuwie radhi kwa kukufuta hadi> > msalani."> > > > Asubuhi wakubwa wakaja kazini lakini hakuna alienikabili. Walikuwa> > wakinichungulia kutoka mlangoni kama simba ndani ya kizimba kwenye> > zoo, nami nikawa najifanya siwaoni. Ndipo akaja mkubwa mmoja tena> > akaniita kwa jina langu na kwa heshima na bashasha sana, "Bwana> > Mohamed tuwie radhi sana pamekuwa na makosa kidogo tuwie radhi sasa> > hivi tutakuruhusu uende nyumbani. " Akatoka nje akawa akipiga simu.> > Kisha akarudi ndani akaamrisha nibebewe mizigo yangu na gari la polisi> > linirudishe nyumbani. Kistaarabu kabisa nikakataa gari ile huku> > nikifanya maskhara kuwa naogopa gari ya polisi asijepiga simu akasema> > mrudisheni huyo mtuhumiwa. Ofisi nzima ikacheka. Hapo ndipo wale> > wakamataji wangu wa usiku wakabeba mizigo yangu nami nafuata nyuma> > tunatoka nje ya uwanja.[> > Kilichobaki sasa ni kueleza sababu ya mimi kukamatwa. Mwaka wa 2006> > Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria kilifanya kongamano la kimataifa hapo> > chuoni kwao kuzungumza kuhusu Ugaidi katika Afrika ya Mashariki na> > Maendeleo ya Afrika (Conference on Islam, Terrorism and African> > Development). Mimi ninlitoa mada iliyokuwa na anuani hii: Terrorism in> > East Africa the Tanzanian Experience. Katika mada hii nilijikita> > mahsusi katika kuisema Marekani kwa udhalimu wao duniani. Nikaeleza> > kuwa huo udhalimu wao ndiyo unaopelekea wao kuchukiwa dunia nzima.> > Hapa ningependa kufahamisha kuwa mkutano huu wafadhili wakubwa> > walikuwa Iran na Marekani. Saudi Arabia ilikataa kuchangia mkutano> > ule. Wakati nasema maneno haya ya kuwakanyaga wenyewe Waamerika wapo> > hapo mkutanoni.> > > > Baada ya kuwalani Waamerika sasa nikaigeukia serikali ya Tanzania na> > kuishutumu vikali kwa kupitisha Sheria ya Ugaidi. Hapa nikaeleza kuwa> > Waamerika wasione kuwa Tanzania imepitisha sheria hiyo ya ugaidi kwa> > haraka kwa sababu Tanzania ina tatizo na ugaidi. Nikaeleza kuwa sheria> > hiyo imepitishwa kwa sababu Bunge la Tanzania limehodhiwa na Kanisa na> > kupitishwa kwa sheria hiyo hakuna uhusiano wowote na ugaidi ila> > Wakristo wamepata fursa ya bure ya kupambana na Uislam wakitumia> > serikali ya Marekani kama upawa wao wa kuopolea chinyango ya moto> > kwenye chungu kinachotokota. Nikauchekesha mkutano kwa kuwaambia kuwa> > Wamarekani wamefanywa wajinga na Kanisa kwa kuchonganishwa na Waislam> > wa Tanzania ambao hawana ugomvi nao asilani. Baada ya kusema hayo> > nikahitimisha kwa kueleza nguvu ya Waislam Tanzania, kwanza kwa wingi> > wao na kisha kwa historia yao iliyotukuka iliyodumu takriban miaka mia> > wakipambana na ukoloni wa Wajerumani kwa silaha (1905 1907), kisha> > ukoloni wa Waingereza (1929 1961) na kuhitimisha kwa kuleta uhuru na> > kuanzia 1961 hadi sasa wanapambana na nguvu ya kanisa katika kupiga> > vita Uislam.> > > > Kufikia hapa ukumbi ukawa umepata joto. Wanigeria wamesimama kutaka> > niwaeleze vipi Waislam watakuwa wamepigania uhuru kisha wako wengi> > nchini wanaruhusu wao kufanywa raia daraja la pili. Wakashangazwa kuwa> > hata historia ya mashujaa Waislam waliopigana Maji Maji na kunyongwa> > na wakoloni na mashujaa walipigania uhuru wa Tanganyika hawatajwi> > katika historia ya ukombozi. Nilitoa majibu kadri Allah> > alivyoniwezesha. Nakumbuka kitu kimoja walichosema wale ndugu zetu> > Wahausa. Walisema hali hiyo iliyoko kwenu haiwezekani kutokea Nigeria> > kwa kuwa hiyo itakuwa na sawa na kutangaza vita. Kisha> > wakanihakikishia kuwa sheria hiyo ya ugaidi haitapitishwa Nigeria hata> > siku moja.> > > > Wapashaji habari wangu wakajanieleza baadae ni hili hitimisho langu> > ndilo lililosababisha Wamarekani kuleta taarifa Dar es Salaam kutaka> > taarifa zangu za "ugaidi" ikawa sasa sababu imeptikana ya mimi> > kushughulikiwa na vyombo vya dola. Ndipo ikatengenezwa hadithi ya kuku> > jike na ng'ombe dume (cock and bull story) kuwa Mohamed Said ni Mzungu> > wa unga kwa hiyo akamatwe.> > > > Mkasa huu ulinifika miaka sita iliyopita lakini hadi leo kovu la mkasa> > ule limebaki katika pasi yangu. Sielewi pasi yangu inaonyesha nini> > inapotiwa katika compyuta baada ya mkasa huu kwani kama mara tatu> > husimamishwa kwa muda na kuombwa nitoe maelezo ya ziada kuhusu> > niendako kila nisafiripo nje ya Tanzania. Nimeshuhudia hali hii Uwanja> > wa Ndege Amsterdam na Detroit, Marekani. Berlin, Ujerumani niliambiwa> > mzigo wangu umepotea lakini hata kabla sijatoka uwanjani nikatafutwa> > na kukabidhiwa mzigo wangu na kwa hili sikuwa peke yangu nilikuwa na> > mwenzangu, jamaa wa Kiarabu kutoka Misri. Sijui kama mizigo yetu> > ilikuwa imebakishwa nyuma kwa upekuzi zaidi. Amsterdam, Uholanzi baada> > ya kupita sehemu zote muhimu za upekuzi wakati naelekea kituo cha> > mwisho niingie kwenye ndege inayoelekea Detroit, Marekani> > nikachopolewa kutoka kwenye mstari na nikawekwa pembeni peke yangu kwa> > usaili wa ziada. New York kadi yangu ya benki ilikataa kutoa fedha kwa> > siku nzima hadi siku ya pili. Nilikujafahamishwa baadae kuwa "system"> > ilikuwa inanichunguza kwanza. Ilikuwa siku ya pili baada ya kuonana na> > maofisa wa benki ndipo kadi yangu ikaanza kutoa fedha. Geneva, Uswisi> > kadi yangu ilikataa kutoa fedha katika mgahawa. Sikujua kama ni yale> > yale au haya yalikuwa mengine. Lakini pasi hii afisa wa uhamiaji wa> > Tanzania alipoiingiza kwenye compyuta yake alimwita mwenzake kuja> > kutazama kisha wakawa wanacheka. Waliona nini kwenye pasi yangu Allah> > ndiye ajuaye."> >
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment