Thursday, 12 July 2012

Re: [wanabidii] TUWE MAKINI NA VIONGOZI WA DINI WA AINA HII.

Pole sana! Nadhani alitaka kutengeneza jina na hivyo akaamua kucheza
"pata potea" (get lost). Mimi viongozi wa dini wa namna hii huwa
siwapi nafasi ya kuwasikiliza wakihubiri au kuwaruhusu wanihubiri.
Nikiwaangalia baadhi ya viongozi wetu wa dini nakumbuka maneno ya faza
fulani alikuwa akitoa semina siku moja na kusema: "Unafanya kitu
kifanye na ukisimamie. " You shound't be a'big boy or grown up baby!"

On 7/12/12, BADI DARUSI <robadio8@gmail.com> wrote:
> Salaam kwenu Wanaharakati,
> Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
> kunijaalia afya njema na kuandika waraka huu.
> Napenda kutoa masikitiko yangu makubwa kwa huyu Kiongozi wa dini na
> katibu wa Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA) Sheikh Said
> Mwaipopo. Kiongozi huyu ameonyesha mapungufu makubwa sana na nawaomba
> Wanaharakati kutoka taasisi mbali mbali kuwa nae makini yeye na
> viongozi wengine wa dini wa aina hii. Nasema hivi kwasababu kiongozi
> huyu ndie alikua naonekana kuwa mstari wa mbele kutaka suluhu baina ya
> Serikali na Madaktari waliokua katika mgomo nchini. Kiongozi huyu
> pamoja na viongozi wengine wa madhebu mbali mbali ya Kikristo nchini
> waliitisha kikao cha pamoja na madakrari na Wanaharakati siku ya
> Jumamosi sawa na Tarehe 7/7/2012 katika Hotel ya Traventine Magomeni.
> Kiongozi huyu Bwana Said Mwaipopo alipata mda mrefu wa kuwasikiliza
> Madaktari na alionyesha kwa kiasi kikubwa kuguswa na yale waliokua
> wakiyasema. Kwa pamoja viongozi wa dini waliafikiana kuitisha kikao
> cha Suluhu pamoja na Serikali ili kuweza kumaliza mgogoro. Na aliahidi
> mbele ya waandishi wa habari kuwa kama Serikali ikikataa hoja ya
> kukutana na Madaktari basi watauachia Umma uamue. Sasa leo nasikitika
> kuona ndio amekua mstari wa mbele kwa kusema kuwa taasisi yake
> itawashtaki madaktari waliokua kwenye mgomo mara baada ya Mh. Rais
> (Ikulu) kukataa ombi la Viongozi wa dini la kukutana nao ili
> kusuluhisha mgogoro uliokuwepo. Lakini pia kiongozi huyu anaelewa
> fika mazingira halisi yaliowafanya madaktari wagome na yeye alikua
> mstari wa mbele kuwatetea na kuahidi upatanisho kati ya madaktari na
> Rais(Serikali). Je Viongozi wa Dini wa aina hii wanafaa kuwepo katika
> jamii yetu? Nawausia Taasisi mbali mbali za Kiraia kuwa makini na
> Viongozi wa aina hii kwani wanaweza wakawa ni sehemu ya kufitinisha
> kati ya serikali, madaktari na Taasisi za kutetea haki za binadamu.
> Kama ameweza kuyakana maazimio ya Pamoja kati yake na Viongozi wengine
> wa dini je atashindwa kukukana Mahakamani huku ushahidi wa Video na
> Tape record upo? Siku nyingine tukialikwa katika majukwaa ya namna hii
> tuwe makini maana dunia imekwisha na kila mtu anaangalia Tumbo lake tu
> badala ya Jamii.
>
> Mimi Badi Darusi,
> Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Jinsia.
>
>
> NAWAOMBA MSOME ALICHOKISEMA KIONGOZI HUYU HAPA CHINI
>
>
> Baraza La Habari La Kiislamu Kuwafungulia Kesi Mahakamani Madaktari
> Waliogoma
>
> Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA) limesema linakusudia
> kuwafungulia mashitaka Madaktari Mabingwa wote pamoja na Madaktari
> waliokuwepo kwenye Mafunzo kwa Vitendo (Interns) ambao walishiriki
> katika mgomo kwenye hospitali mbalimbali nchini na kusababisha
> wagonjwa kukosa huduma za matibabu huku wengine wakipoteza maisha yao.
>
> Hatua hiyo imefikiwa baada ya baraza hilo kukaa na Madaktari waliokua
> katika mgomo na kukubaliana kuwa waiombe radhi Serikali pamoja na
> wananchi kisha warudi kazini, lakini Madaktari hao wamekiuka
> makubaliano hayo na kuendelea na mgomo jambo lililoonyesha kwamba
> hawakuwa tayari kupata suluhu.
>
> Katibu wa BAHAKITA, Said Mwaipopo amesema wameshauriana na Wanasheria
> wao na kuamua kuwafungulia kesi ya mauaji Madaktari hao katika
> Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam tarehe 16 Julai
> 2012.
>
> Amesema, "kwa tukio zima jinsi lilivyokwenda, limeonyesha kwamba
> Madaktari hawataki wala hawana shida tena ya kurudi kazini kwa sababu
> ni wazi kwamba kuna mtu yuko nyuma yao wanaemtumikia. Sisi kama
> Watanzania, sehemu ya jamii tumekaa na Wataalamu wetu wa Sheria
> tumekubaliana kwamba Jumatatu tunakwenda kufungua kesi Mahakamani kwa
> Madaktari wote waliogoma wakati wamesomeshwa na kodi zetu na Serikali
> yetu imewasomesha, tutawafungulia kesi ya kusababisha mauaji pale
> Muhimbili, kwa hiyo tunachofanya hivi sasa ni kwenda pale Muhimbili
> kwa mganga mkuu kuchukua orodha ya watu waliopoteza maisha."
>
> "Sisi tuliingilia kati mgomo huu kwa nia njema ya kutapata suluhu kati
> ya madaktari na serikali…lakini baada ya taarifa zetu kutoka kwenye
> vyombo vya habari Ikulu ilitoa tamko la kukataa kukutana na sisi...
> ...lakini Ikulu walieleza vizuri kwamba hawajawahi kukataa kukutana na
> viongozi wa madaktari kwa maana hiyo basi serikali imeonekana dhahiri
> kutaka suluhu. Baada ya taarifa hizo sisi tuliwatafuta viongozi wa MAT
> ambao tuliwaeleza kwamba kutokana na taarifa hizo wao waombe msamaha
> kwa serikali na umma wa watanzania kwa kuendesha mgomo ambao
> umesababisha vifo. Lakini baada ya kuwaeleza hivyo hawa viongozi wa
> MAT hawakukubali…sisi kama viongozi ambao lengo letu ilikuwa kutafuta
> suluhu tukaona hawa vijana (madaktari) wana nia mbaya. Lakini sisi si
> kujitoa tu bali tutawafungulia mashtaka ya mauaji wote walioshiriki
> katika mgomo huo. Tutafanya hivyo ili fundisho kwa wengine ambao wana
> nia kama za madaktari wanaoendesha migomo.
>
> Kwa hiyo sisi tunaunga mkono kufikishwa mahakamani kwa Rais wao ni
> njia sahihi kabisa ya kurudisha nidhamu, lakini pia tunaunga mkono
> matamko yote yaliyotolewa na serikali dhidi ya madaktari,"alisema
> Mwaipopo.
>
> Akijibu hoja hizo, Katibu wa MAT, Dkt. Edwin Chitage amesema hawaogopi
> kufikishwa mahakamani na kwamba wao waliwapokea viongozi hao kwa nia
> njema wakiamini ni viongozi wa dini.
>
> "Kama wamesema watatufikishwa mahakamani wao waende halafu tutakutana
> nao…sisi tuliwapokea kwa nia njema kabisa kwa sababu walituomba
> wenyewe..lakini baada ya kikao cha Jumamosi siku ya Jumapili
> wakatupigia simu kuomba tukutane nao,sisi tulikutana nao lakini cha
> kushangaza walitueleza kwamba wamepigiwa simu na mtu wa Ikulu
> akiwataka kutuambia kwamba inabidi tuandike barua ya kuomba msamaha
> halafu tuwape wao ili waipeleke…sisi tulishangaa jambo hili… sisi
> hatutafanyi kazi hiyo," alisema Dkt.Chitage.
> Chanzo: http://www.wavuti.com
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment