Nyakwana, soma mtiririko wa kesi ilivyoendeshwa unagalie kama kuna uzingatiwaji wa haki za kibinadamu, hyuo mtuhumiwa kwanini alinyimwa dhamana siku ya kwanza? kwanini alihukumiwa katika mazingira hayo? tena akiwa mwenyewe(hata kama sheria haispecify mahala pa kutolea hukumu na nani awepo au asiwepo)
Tujadili hilo
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
P"By faithfulness we are collected and wound up into unity within ourselves, whereas we had been scattered abroad in multiplicity"Saint Augustine (354-430) Theologian
From: Jones Nyakwana <jonesn1478@yahoo.co.uk>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com; "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>; "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>; "wanakenya@googlegroups.com" <wanakenya@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, July 17, 2012 1:28 PM
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko ] MWANAHARAKATI MBEYA AFUNGWA MWAKA MMOJA NA NUSU
--
Unacholalamikia ni hukumu au nini?
--- On Tue, 17/7/12, deogratius temba <deojkt@yahoo.com> wrote:
From: deogratius temba <deojkt@yahoo.com>
Subject: [Mabadiliko ] MWANAHARAKATI MBEYA AFUNGWA MWAKA MMOJA NA NUSU
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "wanakenya@googlegroups.com" <wanakenya@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 17 July, 2012, 11:16
--Mwanaharakati Mbeya afungwa mwaka mmoja na nusuMwanaharakati mwenzetu ngazi ya jamii aitwaye Frora Mathias, ambaye ni mtetezi wa haki za wanawake na makundi mengine yaliyoko pembezoni, yuko Gereza la Luanda Mkoani Mbeya tangu Ijumaa tarehe 13 Julai 2012 kwa kesi ya kupotea kwa fedha za SACCOS.Flora Mathias ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ifiga kata ya Ijombe, wilaya ya Mbeya Vijijini ni Mhasibu wa kikundi cha JUHUDI SACCOS kata ya Ijombe, na amefanya kazi kama muhasibu wa SACCOS hiyo kwa miaka 7. Kwa mujibu wa Flora, siku ya Alhamisi tarehe 29 Juni 2012 alipokuwa anapeleka fedha za SACCOS benki kiasi cha shilingi milioni tano (Sh. 5,000,000/=) tu, muda wa saa nne asubuhi, aliposhuka kutoka kwenye basi alilosafiria alikutana na mtu ambaye alimsalimia. Baada ya hapo hakumbuki chochote kilichotokea ila alijikuta yuko katika kichaka eneo la makaburini saa kumi jioni akiwa hana fedha zote alizokuwa nazo awali. Alipoona hivyo Flora alirudi kijijini kwake na kutoa taarifa kwa wanakikundi wenzake.Baada ya hapo Flora aliitwa ofisini kwa Mtendaji wa Kata ya Ijombe, Bwana Mpoki Kajange ambaye aliamuru Flora akamatwe na mgambo na kupelekwa moja kwa moja mahakamani (mahakama ya mwanzo ya Uyole). Hakimu wa mahakama hiyo aliandika maelezo ya Flora na kuamuru apelekwe rumande gereza la Luanda na hakuruhusu dhamana. Mtendaji wa kata ya Ijombe alikataa kutoa barua ya dhamana akidai yeye ndiye aliyemshtaki Flora, hivyo alishauri wakatafute barua ya dhamana kutoka kata nyingine. Flora alikaa rumande kuanzia tarehe 29 Juni hadi alipopelekwa mahakamani tarehe 3 Julai 2012 na kupata dhamana kwa masharti ya kupeleka sh. milioni mbili na laki tano (2,500,000)=/ ifikapo siku ambayo alipangiwa kurudi tena mahakamani yaani tarehe 12 Julai 2012.Baada ya Flora kutoka nje kwa dhamana alidai kuwa akiwa mahakamani siku alipokamatwa alishuhudia Mtendaji wa Kata ya Ijombe akimpa HAKIMU fedha. Wanakikundi wa SACCOS walimweleza Flora kuwa Mtendaji aliwadai wampe shilingi laki mbili (sh. 200,000/=) kwa ajili ya kufungua kesi mahakama ya mwanzo Uyole. Hata hivyo Flora, waliamua kupeleka suala hili TAKUKURU Mbeya.Siku ya Alhamisi tarehe 12/07/2012 Flora akiwa na msaidizi wa sheria toka ofisi ya Haki za Binadamu na wanakikundi wa Juhudi SACCOS, walifika mahakamani saa mbili asubuhi na kusubiri mpaka saa nane mchana, ndipo karani wa mahakama alipowajulisha kuwa hakimu hakuwepo hivyo warudi tena siku ya Jumatano tarehe 18 Julai 2012. Waliondoka na walipofika kituo cha basi yule karani aliwakimbilia na kuwajulisha kuwa hakimu alikuwa amefika hivyo warudi mahakamani. Baada ya kushauriana waliamua kutorudi kwani hata mshtaki (Mtendaji wa Kata) alikuwa ameshaondoka.Ilipofika saa moja usiku siku hiyohiyo Flora alipigiwa simu na karani wa mahakama na kujulishwa kwamba kesho yake tarehe 13/07/2012 alitakiwa afike mahakamani. Walipofika mahakamani asubuhi walisubiri na ilipofika saa saba mchana hakimu alisoma mashtaka na kumhukumu Flora kwenda jela mwaka mmoja na nusu na kumtaka akitoka alipe fedha za kikundi zilizopotea.--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------"By faithfulness we are collected and wound up into unity within ourselves, whereas we had been scattered abroad in multiplicity" Saint Augustine (354-430) Theologian Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'. Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako. This years motto: 'WALK THE TALK' For more options, visit this group at: http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment