Tuesday, 17 July 2012

Re: [wanabidii] MWANAHARAKATI MBEYA AFUNGWA MWAKA MMOJA NA NUSU

Kaka Temba hii kesi ilikua na muda gani tangu kukamatwa kwa Flora,
kusomwa awali hadi hukumu ya kesi. Je hakimu alitumia kifungu kipi
kumhukumu Flora, na je Kulikua na mashaidi wowote katika kesi
hii?Flora alipewa muda wa kufanya utetezi?Ni kifungu gani ambacho
hakimu alikitumia kumhukumu Flora mwaka mmoja na akirudi alipe hilo
deni? Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanazungukua kichwani maana
naona kuna uonevu mkubwa aliofanyiwa Flora na kuwepo kwa mazingira ya
rushwa. Ifikie hatua wanaharakati tujaribu kujenga nguvu za pamoja ili
kumtetea huyu dada na ikiwezekana kesi hii iwe ya mfano kwa viongozi
wa kijiji wanaojifanya miungu watu. Mwezi mmoja uliopita alitokea
Mtendaji wa kijiji aliempiga mama mjamzito huko Kilolo Iringa hadi
kupoteza maisha.Sasa tukiendelea kuwachekea hawa viongozi wa vijiji
wanaweza kuifikisha nchi hii kubaya maana kuna watu wachache ndani ya
system wanaowabeba.
huyu dada ni mmoja kati ya wanaharakati waliojaribu kuibua ubadhirifu
wa aina mbali mbali katika kata yake sasa kuna baadhi ya watu
wanamchukia kwasababu anafichua uovu na siri zao. Kwahiyo tunaitaji
kumsaidia na kukata rufaa ili huyu dada aweze kuwa huru na kuendeleza
mapambano.

Badi Darusi,
Executive Secretary,
KYWDP.

On 7/17/12, deogratius temba <deojkt@yahoo.com> wrote:
>
> Mwanaharakati Mbeya afungwa mwaka mmoja na nusu
>
> Mwanaharakati
> mwenzetu ngazi ya jamii aitwaye Frora Mathias, ambaye ni mtetezi
> wa haki za wanawake na makundi mengine yaliyoko
> pembezoni, yuko Gereza la Luanda Mkoani Mbeya tangu Ijumaa tarehe 13 Julai
> 2012 kwa kesi ya kupotea kwa fedha za SACCOS.
>
> Flora
> Mathias ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ifiga
> kata ya Ijombe, wilaya ya Mbeya Vijijini ni Mhasibu wa kikundi cha
> JUHUDI SACCOS kata ya Ijombe,
> na amefanya kazi kama muhasibu wa SACCOS hiyo kwa miaka 7. Kwa mujibu wa
> Flora,
> siku ya Alhamisi tarehe 29 Juni 2012 alipokuwa anapeleka fedha za SACCOS
> benki kiasi
> cha shilingi milioni tano (Sh. 5,000,000/=) tu, muda wa saa nne asubuhi,
> aliposhuka kutoka kwenye basi alilosafiria alikutana na mtu ambaye
> alimsalimia.
> Baada ya hapo hakumbuki chochote kilichotokea ila alijikuta yuko katika
> kichaka
> eneo la makaburini saa kumi jioni akiwa hana fedha zote alizokuwa nazo
> awali. Alipoona hivyo Flora alirudi kijijini kwake na kutoa taarifa kwa
> wanakikundi wenzake.
>
> Baada ya hapo Flora
> aliitwa ofisini kwa Mtendaji wa Kata ya Ijombe, Bwana Mpoki Kajange ambaye
> aliamuru Flora akamatwe na mgambo na
> kupelekwa moja kwa moja mahakamani (mahakama ya mwanzo ya Uyole). Hakimu wa
> mahakama hiyo aliandika maelezo ya Flora na kuamuru apelekwe rumande gereza
> la Luanda na hakuruhusu dhamana.
> Mtendaji wa kata ya Ijombe alikataa kutoa barua ya dhamana akidai yeye
> ndiye
> aliyemshtaki Flora, hivyo alishauri wakatafute barua ya dhamana kutoka kata
> nyingine. Flora alikaa rumande kuanzia tarehe 29 Juni hadi
> alipopelekwa mahakamani tarehe 3 Julai 2012 na kupata dhamana kwa masharti
> ya
> kupeleka sh. milioni mbili na laki tano (2,500,000)=/ ifikapo siku ambayo
> alipangiwa kurudi tena mahakamani yaani tarehe 12 Julai 2012.
>
> Baada
> ya Flora kutoka nje kwa dhamana alidai kuwa akiwa mahakamani siku
> alipokamatwa
> alishuhudia Mtendaji wa Kata ya Ijombe akimpa HAKIMU fedha. Wanakikundi wa
> SACCOS
> walimweleza Flora kuwa Mtendaji aliwadai wampe shilingi laki mbili (sh.
> 200,000/=) kwa ajili ya kufungua kesi mahakama ya mwanzo Uyole. Hata hivyo
> Flora, waliamua kupeleka suala hili
> TAKUKURU Mbeya.
>
> Siku
> ya Alhamisi tarehe 12/07/2012 Flora akiwa na msaidizi wa sheria toka ofisi
> ya
> Haki za Binadamu na wanakikundi wa Juhudi SACCOS, walifika mahakamani saa
> mbili
> asubuhi na kusubiri mpaka saa nane mchana, ndipo karani wa mahakama
> alipowajulisha kuwa hakimu hakuwepo hivyo warudi tena siku ya Jumatano
> tarehe 18
> Julai 2012. Waliondoka na walipofika kituo cha basi yule karani
> aliwakimbilia
> na kuwajulisha kuwa hakimu alikuwa amefika hivyo warudi mahakamani. Baada
> ya
> kushauriana waliamua kutorudi kwani hata mshtaki (Mtendaji wa Kata) alikuwa
> ameshaondoka.
>
> Ilipofika
> saa moja usiku siku hiyohiyo Flora alipigiwa simu na karani wa mahakama na
> kujulishwa kwamba kesho yake tarehe 13/07/2012 alitakiwa afike mahakamani.
> Walipofika
> mahakamani asubuhi walisubiri na ilipofika saa saba mchana hakimu alisoma
> mashtaka na kumhukumu Flora
> kwenda jela mwaka mmoja na nusu na kumtaka akitoka alipe fedha za kikundi
> zilizopotea.
>
> --------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
>
>
> "By faithfulness we are collected and wound up into unity within ourselves,
> whereas we had been scattered abroad in multiplicity"
> Saint Augustine (354-430) Theologian
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment