Wednesday, 28 June 2017

[wanabidii] TTCL YAWAKUMBUKA WAHITAJI

[caption id="attachment_80035" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-80035" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/06/e22d3898-9d12-4943-92a4-bf1c15720a3b.jpg" alt="" width="800" height="533" /> Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thom Mushi (kushoto) kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, akikabidhi msaada wa Vyakula, Vinywaji na mahitaji mengine ya nyumbani kwa wawakilishi mbalimbali wa vituo vya New Life Orphanage home cha Boko na Kituo cha Sifa Group Foundation cha Vikawe Bondeni vyote vya jijini Dar es Salaam.[/caption]

&nbsp;

[caption id="attachment_80031" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-80031" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/06/7a81450e-07aa-4047-8d92-65729b61d6fd.jpg" alt="" width="800" height="533" /> Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thom Mushi (wa kwanza kulia) kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, akikabidhi msaada wa Vyakula, Vinywaji na mahitaji mengine ya nyumbani kwa wawakilishi mbalimbali wa vituo vya New Life Orphanage home cha Boko na Kituo cha Sifa Group Foundation cha Vikawe Bondeni vyote vya jijini Dar es Salaam.[/caption]

&nbsp;

[caption id="attachment_80032" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-80032" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/06/028baf62-163a-4549-ab47-985815519610.jpg" alt="" width="800" height="533" /> Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thom Mushi (kushoto) kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, akikabidhi msaada wa Vyakula, Vinywaji na mahitaji mengine ya nyumbani kwa wawakilishi mbalimbali wa vituo vya New Life Orphanage home cha Boko na Kituo cha Sifa Group Foundation cha Vikawe Bondeni vyote vya jijini Dar es Salaam.[/caption]

&nbsp;

<strong>KAMPUNI</strong> ya Simu Tanzania TTCL imetoa msaada wa Vyakula, Vinywaji na mahitaji mengine ya nyumbani ili kuwawezesha Watoto katika Vituo vya Yatima na Waishio katika Mazingira magumu kusherehekea Siku kuu ya Eid.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Meneja Uhusiano wa TTCL Ndg Nicodemus Thom Mushi amesema, TTCL inathamini sana makundi yenye mahitaji maalumu kama Yatima ndio maana mara zote imekuwa mstari wa mbele kuwasaidia kadiri uwezo wa Kampuni unavyoruhusu.

"Nawaomba mpokee salamu za Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndg Waziri Kindamba, anawasalimu na kuwatakia kila la kheri katika kukamilisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani na sherehe njema za Eid. Watoto wanaopata malezi katika vituo vyenu wana haki sawa na watoto wenye wazazi na wanaoishi na familia zao. Kwa ushiriano mwema kati yetu, tutawezesha Watoto hawa kukua salama na kua Raia wema wa nchi yetu na nguzo muhimu ya maendeleo ya Taifa letu" amesema ndugu Mushi.

&nbsp;

[caption id="attachment_80033" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-80033" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/06/c2ab1802-db92-4913-b72a-7881c72ef4c9.jpg" alt="" width="800" height="556" /> Picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thom Mushi mara baada ya makabidhiano ya msaada wa Vyakula, Vinywaji na mahitaji mengine ya nyumbani kwa wawakilishi wa vituo vya New Life Orphanage home cha Boko na Kituo cha Sifa Group Foundation cha Vikawe Bondeni vyote vya jijini Dar es Salaam.[/caption]

&nbsp;

[caption id="attachment_80034" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-80034" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2017/06/c09f19a7-cd35-466d-be08-90cd502d582d.jpg" alt="" width="800" height="564" /> Picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thom Mushi mara baada ya makabidhiano ya msaada wa Vyakula, Vinywaji na mahitaji mengine ya nyumbani kwa wawakilishi wa vituo vya New Life Orphanage home cha Boko na Kituo cha Sifa Group Foundation cha Vikawe Bondeni vyote vya jijini Dar es Salaam.[/caption]

&nbsp;

Akishukuru kwa Niaba ya Vikundi vilivyopokea msaada, Mkuu wa Kituo cha New Life Orphanage home cha Boko Dawasa Bi Mwanaisha Magambo amesema, Kituo chake chenye watoto 132 kitafaidika sana na msaada huu wa TTCL uliowafikia wakiwa wamekata tamaa kwa kutopata msaada wowote katika sherehe hizi. Nawaombea kwa Mungu, Kampuni hii idumu, mfanikiwe katika malengo yenu yote.

Msaada huu ni mkubwa, hatukuutarajia na tulikuwa tumekata tamaa kwa kuwa maombi yetu yote hayakupata majibu kutoka kwa Wafadhili wetu. Mmetushika mkono kipindi tulichowahitaji hasa, Mungu awabariki sana TTCL, msichoke kusaidia kundi hili la watoto lenye mahitaji makubwa ya msaada hasa wa chakula na vifaa vya Elimu.

Msaada wa TTCL umetolewa kwa vikundi Viwili vya New Life Orphanage Home (Watoto 132) na Kituo cha Sifa Group Foundation cha Vikawe Bondeni chenye watoto 50. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Mchele kg 300, Unga wa mahindi kilo 300, Unga wa Ngano kg 200, Sukari kg 200, Maharage kg 200, Mafuta Ndoo 6, Mbuzi 2, Soda katoni 40, Maji Katoni 40, Juice Katoni 80 na Viungo mbalimbali vya chakula na vifaa vya nyumbani kama mafuta ya kujipaka na Sabuni.

--
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment