Wednesday, 15 March 2017

[wanabidii] ISHARA, MAAJABU, NA MIUJIZA IKO HAPA!

Na. Maj. Frank Materu – ACMTC TANZANIA
"Wakamjia mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwambia awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. Akajibu, akawaambia, [ Kukiwa jioni, mwasema, Kutakuwa na ishara; kwa maana mbingu ni nyekundu. Na asubuhi, mwasema, Leo tutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu, lakini, je! Ishara za zamani hizi, hamwezi kuzitambua?] Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha akaenda zake". Mt. 16: 1-4
Kwa muda mrefu sana , mrefu sana wanaume na wanawake wamelilia kujionyesha, kwa mapambo, kwa ishara, kwa maajabu, kwa miujiza, lakini hawajalia kwa ajili ya Mungu. HII NI KWAMBA, HAWAJATAMANI KUMJUA MUNGU, KUKAA NDANI YAKE, KUMSHIRIKI YEYE, LAKINI KIRAHISI TU WAMETAKA KUJIONYESHA. Wamechoka kumtafuta Mungu ili kuona maonyesho ya nguvu zake, sasa wamefanya kujionyesha wenyewe.
Kila mwaka wanachukiza zaidi katika kuweka manyesho yao ya kiburi, na katika maonyesho yao hadharani, katika upuuzi wao na katika ujinga wao. Mungu ataondoka kabisa katika burudani zao kwa maana amechoshwa na wana wa wanadamu.
"Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa. Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana". Mt. 23:38-39
Wale watakaompenda  Mungu, na kumtumikia Mungu, na kumjua Yeye jinsi alivyo, ni wale watakaokuwa wa toba na kubakia wa toba mbele zake. Mungu amechoshwa na wale watafutao tu ishara, kwa maana ni kizazi kiovu na potofu.
Wakati watu wasipotafuta kumpendeza Mungu, kumpenda Mungu, kumjua Mungu kama alivyo, kwa maana anawapa rehema za msamaha, kweli hawamstahili Mungu. Mungu amewapa wana wa wanadamu, ishara, maajabu, miujiza, wameyafanyia nini?
Hakuna kitu kabisa, isipokuwa kutafuta kujipatia kipato, kutafuta kupata kwa ajili yao wenyewe mapato ya aibu, na kuendelea katika mchezo wa kupata. KATIKA MCHAKATO HUO WAMEMCHEFUA MUNGU, KWA KIWANGO AMBACHO AMEJIONDOA MWENYEWE KWAO.
Mungu ameuondoa uwepo wake katikati yao, akiwaacha hao kama kakazi ya walioangamia. Maana yake ni kwamba, amewaachilia kwa nguvu za mapepo, kwa maana wameyapenda kuliko kumpenda Mungu. WAKATI MTU ATAKAPOMFUATA MUNGU KWA AJILI YA ISHARA, MAAJABU NA MIUJIZA, HAMJUI MUNGU. Anatafuta tu kujionyesha, na Mungu amechoshwa na hilo.
Kwa muda mrefu sana watu wanamtumikia Mungu ili tu kujionyesha, na hiyo hiyo ni ujinga mbele za Mungu. Mungu anawaita wale watakaojinyenyekeza wenyewe mbele zake na kutembea katika njia yake. Anawatafuta wale halisi, kuliko wale bandia.
Mungu anawatafuta wale wa kweli, kuliko wale wanafiki wanaojifanya. Unapoona kie ambacho wanaume na wanawake walichokifanya kwa vile vitu ambavyo Mungu aliviweka duniani, kuonyesha kuwa ndiye Mungu mwenye nguvu, wamevichafua na kuviharibu kabisa.
Ni kwa sababu walifikiria kuviiba, walifikiria kuuchukua utukufu kwa ajili yao wenyewe na walifikiria kujilimbikizia mali kwa kupitia Mungu. UONAPO UCHAFU, UFISADI, UOVU ULIOINGIA, UNAWEZA UKAONA NI KWA NINI MUNGU AMENAWA MIKONO KWA AJILI HIYO.
Hiyo ina maana kwamba huwaacha watu katika ujinga wao, katika upumbavu wao, katika giza lao na kwenda njia nyingine. Kwa  hiyo umsikiapo  anayetaka na kulazimisha kwamba Mungu aonyeshe miujiza, ishara na maajabu, tafakari hili. FIKIRIA JE, WANATAFUTA KUMJUA MUNGU, KUMPENDEZA MUNGU AU TU  WANATAKA KUUVUTA UMATI ILI KUJIPATIA KIPATO?
Kama kweli wapo katika dhana hiyo, basi Mungu hatawasikiliza. Kwanini Mungu aonyeshe nguvu za miujiza yake, kwanini aweke ishara zake wakati yote wanayotaka ni ili wao wajipatie fedha. MUNGU KATIKA SAA HII ANAONYESHA MIUJIZA , GHADHABU YAKE, HASIRA YAKE.
"Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Kwa maana shina moja la mabaya ya kila namna, ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi". 1 Tim. 6: 9-10
Watu wako mbali na kile Mungu anachokifanya katika kizazi hiki kiovu. Mara zote wanatazamia rehema, wakati wanashahili ghadhabu. SASA KAMA UKIANGALIA KILE KITU MUNGU ANACHOKIFANYA KWA WANA WA WANADAMU, NI WITO WA TOBA ILI WASIANGAMIE.
Lakini kama watu kwa kiburi chao watakataa kutubu, wanafanya nini? Hao ndio wale wanaojiweka wenyewe kustahili ghadhabu, hasira na hukumu ya Mungu. Kuna baadhi wanaolia kuona ishara, miujiza na maajabu yakirejea kama wanavyotaka.
Lakini ni wajinga, wapumbavu na bubu mbele za Mungu kwa maana hawatambui ni nini Mungu anachokifanya katika saa hii. Hii ina maana kwamba, wanatazama siku za nyuma, katika nyakati nyingine, na wanazitaka nyakati hizo.
Lakini ni wajinga kwa sababu hawaoni kwamba ni Mungu aliye Hai ambaye ana hasira sana ambapo ni lazima afunue ghadhabu yake. KADHALIKA WANASHINDWA KUONA KWAMBA KATIKATI YA GHADHABU YAKE,  NI YEYE MUNGU ALIYE HAI AMBAYE ANATOA WITO WA MAPINDUZI YA TOBA ILI WALE WENYE SIKIO LA KUSIKIA WATUBU, NA KUTEMBEA KIKAMILIFU KATIKA MUNGU.
"Tokea wakati huo Yesu aliamza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia". Mt. 4:17
Kwa muda mrefu mno wamekomaa katika uovu na dhambi zao, na wale wanaodai kuwa ni watoto wake ndiyo wa kulaumiwa. Kwa sababu wameweka  burudani na maonyesho ya wazi ya kiburi, wamejifanyia wenyewe ujinga na ndiyo, ndivyo wanavyopenda.
Wamejigaragaza wenyewe katika uharibifu wa kidunia, na wakati huo wote wanadai wanampendeza Mungu. Hawampendezi Mungu, wamtia Mungu kichefuchefu, kwa sababu mioyo yao iko mbali na Mungu.
USILILIE ISHARA, MAAJABU NA MIUJIZA BAKI UWE NA SHAUKU NA MUNGU. Ufikapo wakati muafaka na majira yake, Yeye ni Mungu wa miujiza na ataifunua kwa wale wamngojeao na kukesha kwa ajili yake. Wakati watu wanatafuta tu maonyesho ya kiburi na burudani wanatafuta bure.
Kwa maana Mungu aliye Hai amekifu, amechefushwa na kuchoshwa kabisa  kwa kile ambacho watu wanefaya katika jina lake. Kwa sababu ni Mungu aliye Hai anayetafuta  kila mahali duniani katika saa hii kwa watu wa kweli wa toba.
 Hii ina maana kwamba masalia ambao wataacha uovu wao na kutembea katika haki kwa sababu ni Mungu wanayetamani kumpendeza. HAO MASALIA WATATAMANI KUMJUA MUNGU, BILA KUJALISHA HUO MWENENDO UTAKUWAJE.
Kwa muda mrefu watu wamejitawala kutoka kwa Mungu, na kudhani wangeweza kutamtamkia Mungu. Hii ni kwamba wamekuwa wakubwa kidogo, wasimamizi na wafalme katika haki zao wenyewe. Wanadhani wanaweza kumtamkia Mungu ni kwa jinsi gani atakavyotembea, na ni lazima aruke na kufanya hivyo.
Ni kwa kiasi gani, ni kwa kiasi gani, ni kwa kiasi gani cha maumivu ambacho wanaume na wanawake wamemsababishia Mungu katika dunia hii. ZAIDI YA MWENYE DHAMBI WA KAWAIDA, NI WATU WAKE WENYEWE WALIOMUUMIZA YEYE.
Wanapinga, wanakataa kumruhusu Yeye awe na njia yake mwenyewe, na wanasisitiza na kukomaa katika njia yao wenyewe. Kile wanachokileta sio Roho wa Mungu, bali ni kazi za mapepo katikati yao. Ni kwa sababu wamekataa kumruhusu Mungu awe na njia yake mwenyewe.
Tunaishi katika nyakati ambazo wale wanaodai kuwa ni watoto wa Mungu wengi wao wako mbali na Yeye. Hawatatembea katika toba, wala kujiweka wenyewe kwa toba. Wala hawatamruhusu Mungu kuwa Mungu kwa maana kwamba atawale, amiliki na awe na njia yake.
Wakati wote watajifanya , wakijionyesha saa zote, wakitaka tu kila mara kuwa na njia yao wenyewe. Kitu hicho ni chukizo, sikitiko na aibu mbele za Mungu, kwa maana Mungu hajawaita watu kujionyesha ili waonekane na watu wengine. Wala  hakuwaita watu wasemwe vizuri, bali amewaita watu wamfuate.
Kama ukitazama jinsi inavyochukiza, mbele za Mungu, inasikitisha na aibu. WATU WOTE KILA MAHALI WANAOLITAJA JINA LAKE, WANAHITAJI TOBA KWA MUNGU. Ili wasiendelee katika bandia, unafiki na dhihaka na kudai kuwa ni Mungu. Lakini watembee kwa upole katika Mungu, wakiukomboa wakati, wakiishi katika MAPINDUZI YA TOBA.
 
Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam. Barua pepe: materufrank@yahoo.com

 
 
 
 
 

0 comments:

Post a Comment